Saturday, May 9, 2015

KONGAMANO LA KWAYA KANDA YA SHC.

KONGAMANO LA KWAYA KANDA YA SHC.

KWAYA 18 ZA MKOA WA MBEYA ZA UDHURIA KONGAMANO LA UIMBAJI LILILO FANYIKA HUKO IGANZO MAKAO MAKUU YA SHC JANA TAREHE 19/04/2015 KONGAMANO HILI LILIANDALIWA NA IDARA YA MZIKI KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA MAWASILIANO YA SHC.
HIKI NI KITUO CHA TATU SASA BAADA YA KUMALIZA KWAYA ZA MKOA WA KATAVI(27/03/2015) NA KWAYA ZA MKOA WA RUKWA (29/03/2015)
BADO VITUO VIWILI:
1. KITUO CHA MAFINGA KWA KWAYA ZA MKOA IRINGA NI TAREHE 29/04/2015
2. KITUO CHA MBINGA KWA KWAYA ZA MKOA WA RUVUMA NI TAREHE 27/04/2015
KUMBUKA KUJA NA WIMBO NAMBA 8 & 25 PIA NYIMBO ZAKO MBILI:
PIA ZINGATIA VIGEZO

PICHA MBALI MBALI ZA SEMINA YA UWAKILI GANGILONGA IRINGA.

                       PICHA MBALI MBALI ZA SEMINA YA UWAKILI GANGILONGA IRINGA.                        
Semina ya Uwakili ya Union Mission ya Kusini mwa Tanzania ambayo imeanza Tar. 19/02/2015 hadi Jumapili  Tar. 22/02/2015 Gangilonga, Iringa. Mnenaji mkuu ni Mkurugenzi wa Uwakili wa General Conference E. Punina. Semina hizo zimehudhuliwa na Wachungaji wa mitaa yote, Wazee wa Kanisa, na Wakuu wa Huduma za Uwakili kutoka makanisa ya Konferensi za SHC, SEC, na ECT.
Mkurugenzi wa Uwakili wa General Conference Pastor Erika Puni akifundisha juu uwakili unavyohusiana na uongofu.

Wana semina wakiwa makini katika kusikiliza kile kinachofundishwa.
MSIMAMO WA KANISA JUU YA NEMBO YAKE NA MAELEZO JUU YA KILE KINACHOWAKILISHWA.

FALSAFA YA NEMBO
Nembo ina utambulisho na, kama unavyotambua, utambulisho ni chochote ambacho wewe au wengine wanachoweza kutengeneza ili kiwe. Kitambulisho hicho ni kitufulani ambacho kinatengenezwa kutokana na hadhi na wakati. Hata hivyo, kwa nembo ili iwe mali ya kundi maalumu, ni lazima ilindwe kisheria na kutambuliwa na hivyo ndivyo inavyotokea kuwa, nembo lazima iwe ya kipekee na yenye msimamo.
Mojawapo ya matatizo ambayo kanisa limekabiliana nayo kwa miaka mingi iliyopita, imekuwa ni kwamba kamwe halijawa na nembo yake ya kipekee na yenye msimamo; kwa uhakika kamwe hapajakuwa na makubaliano au utwaaji wa nembo kiofisi ya aina yeyote. Hatimaye michoro mingi wakilishi imekuwa inatumika kama nembo kwa vyombo mbalimbali vya kanisa kama vile malaika 3 na Dunia na tarumbeta. Tofauti hizi zote katika maeneo mbali mbali zimekuwa zikitumiwa na makundi ya kanisa na makundI mengineyo. Na kwa sababu hapakuwa na msimamo na hata ulindwaji wa kisheria, hatukuweza kuimiliki au kutawala kwa matumizi ya michoro hii dhidi ya watumiaji wengine. Kujibu (kutatua) tatizo hilo, ilitulazimu kutengeneza nembo ambayo ina upekee na msimamo madhubuti.
UUNDWAJI WA NEMBO (LOGO DEVELOPMENT).
Kwa kuwa tulikuwa tunaanza kuanzia chini (kwangua chini), tuliajiri Mtaalumu wa Kiadventista (mbunifu wa Kiadventista) na kutafiti mawazo ambayo yatawakilisha kanisa, utume wake, imani yake, na vilevile kuakisi ulimwengu wa leo katika hali ya mtizamo na hisia. Matokeo unayoyaona ni baada ya mchakato mzima (hatua zote) wa kawaida wa kanisa wa kamati nyingi za mara kwa mara, mapitio na kura za kanisa katika mkutano wa mashauri. (Jambo)Halikufanyika hewani, bali ni jambo la watu wengi kutoka duniani kote likijumuisha michango mbalimbali na uthibitishwaji.
Tumefikia lengo la kuwa na nembo inayolindwa kisheria ambayo ni alama ya utambulisho (trademark) ulimwenguni kote, sambamba na jina “Seventh Day Adventist” na sasa tunaweza kutawala matumizi yake na kutengeneza miongozo maalumu ya matumizi yake. Mojawapo ya sababu ya kuwa na muongozo ni kudumisha msimamo na kuhakikisha nembo inawakilisha ulimwenguni kanisa la Waadventista Wasabato na sio tu kitambulisho cha eneo fulani (kitambulisho cha kanisa moja). Msimamo wa rangi, mwonekano wake (sura yake), na viwango vya michoro mingine inathibitisha kwamba nembo inabakia kwa utambulikanaji wake kila mahali na kwa kiwango fulani cha ubora wake.
MAANA YA NEMBO
Baadhi ya watu wamelaumu kwamba uondoaji (kuachwa) kwa nembo ile ya “zamani” inawakilisha kuachana na kile tunachokiamini, ni miongoni mwa malaumu. Hakuna kinachoweza kuwa mbali na ukweli. Hatuakisi kutoka kwenye nembo yetu; nembo yetu inatuakisi sisi (tulivyo sisi), na ikiwa tupo sahihi kwa kile tunachokiamini, hicho ndicho nembo yetu itasimama kwacho (itawakilisha). {Nothing could be further from the truth. We don't reflect our logo; our logo reflects us, and if we are true to what we believe, that is what the logo will come to stand for}. Kwa uhalisi wa jambo hili nembo mpya kwa ukamilifu zaidi inawakilisha kwa mapana ya kile tunachokiamini. Inaanza na msingi wa Neno, wenye kiini cha Msalaba, njia ya Wokovu wetu; ikionesha miali mitatu inayozunguka Dunia, ikiwakilisha kwa pamoja Utatu Mtakatifu [ Baba, Mwana, Roho Mtakatifu] na vilevile ujumbe wa malaika watatu kwa ulimwengu wote. Na yote haya yameoneshwa kwa njia rahisi, na bado kwa usanifu na mtindo wa kisasa. MWISHO WA TAFSIRI.
“Huu uthibitisho wa kile kilicho halisi na sio kile kisicho halisi” na mch. Mwanga.
NI MSIMAMO WA KANISA LA WAADVENTISTA ULIMWENGUNI JUU YA NEMBO YAKE YA UTAMBULISHO ULIOTOLEWA NA GENERAL CONFERENCE DHIDI YA TAFSIRI POTOFU YA KILE AMBACHO SICHO HALISI.
ULITOLEWA NA
John Torres
Public Relations
World Headquarters
Seventh-day Adventist Church
Silver Spring, Maryland  USA
www.Adventist.org
NA KUTAFSIRIWA
PR. FILBERT JOSEPH MWANGA
IMEHARIRIWA NA
PR. LUPAKISYO MWAKOBELA MWAKASWESWE

PICHA ZA WANAWAKE WAZURI DUNIANI.

PATA PICHA ZA WANAWAKE WAZURI DUNIANI. 
KUMBUKA UZURI YAITAJI UMAKINI WAKUTOSHA KWANI CHANGAMOTO ZA MIRUZI YAWEZA KUKUCHANGANYA NA KUJIKUTA CHAGUO LAKO LINAKUA BATILI. 

SEREKALI KUMBUKENI YATIMA.

NIVEMA JAPO KWA KUJIKAZA TUKAWAJALI YATIMA.

nivema watu kama hawa wakapata japo nguvu toka serkalini ila wapo kimia sana waweza sema wapo ICT au wenda WAMELAZWA NJEE YA INCHI.
 ONGERA SANA  DADA MUNGU YUPO NAWE.
 WAAAAAAAAAAAAAOOOOOOOOOO
 HAKITO FARAJA KWA KIJANA WA KESHO

Tuesday, May 5, 2015

DANGOTE KUIBEBA ARSENAL

DANGOTE MAJANGA JUU YA TISHIO.
Aliko Dangote
Mtu tajiri barani Afrika Aliko Dangote amesema kuwa bado anataka kuinunua kilabu ya Arsenal licha ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2010 alipotaka kununua hisa za kilabu hiyo.
Bilionea huyo kutoka Nigeria ni tajiri mara nane ya alivyokuwa wakati alipojaribu kununua hisa za klabu hiyo na kwamba shabiki huyo wa Arsenal bado hajatupilia mbali ndoto yake ya kutaka kuinunua kilabu hiyo ya Landon Kazkazini.
''Bado nina matumaini kwamba siku moja nitainunua timu hiyo',' alisema Dangote mwenye umri wa miaka 58.''Naweza kuinunua bei ambayo wamiliki wake itakua vigumu kukataa'', huku akiongezea kuwa ''najua mpango wangu''.
Uwanja wa Emirates
La kushangaza ni kwamba Dangote ametaja hadharani kwamba Arsene Wenger anafaa kubadilisha mbinu yake akisema kuwa timu hiyo inahitaji mwelekeo mpya.
Dangote ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 ni tajiri zaidi ya Stan Kroenke ambaye anamiliki hisa nyingi katika kilabu hiyo na Bilionea raia wa Uzbek Alisher Usmanov ambao wamekuwa wakipigania udhibiti wa kilabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni.Afrika sasa twaweza toka kwa dangote.
Manny Pacquiao ameshutumiwa kwa kudanganya kuwa alikuwa akiumwa bega kabla ya pambano dhidi ya Floyd Mayweather. Pambano hilo lilipigwa Las Vegas, Marekani.

Monday, May 4, 2015

PATA PICHA ZA MIGOMO YA MADEREVA NA TUKIO ZIMA LA JANA.

PATA PICHA ZA MIGOMO YA MADEREVA NA TUKIO ZIMA LA JANA.

MAGARI YAKIWA UBUNGO BILA KUTOKA.
 MADEREVA WAKIWA NA BANGO LAO

Mgomo tena, Madereva wasema leo hakuna basi barabarani nchi nzima

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta.
Takribani siku 22 zikiwa zimepita tangu madereva wagome kutoa huduma za usafiri nchi nzima, leo wametangaza mgomo mwingine kutokana na ukimya dhidi ya madai yao kwa serikali.

Madereva hao jana walitoa tamko la kuwapo kwa mgomo huo kupitia vyama vyao, huku wakikanusha kwamba watagoma sambamba na kuandamana.

Walisema leo watakuwa kwenye ofisi zao za muungano wao zilizopo Ubungo, jijini Dar es Salaam na hawatatoa huduma za usafiri.

Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu wa Umoja wa Madereva na Chama cha Malori, Rashid Salehe, alisema, mgomo upo pale pale kwa madai kuwa bado kuna mambo ambayo yameendelea kuwa kikwazo kwao.

Alisema iwapo serikali haitatoa majibu ya kuridhisha, leo hawataingia barabarani kutoa huduma za usafiri.

Alisema jana walifanya mkutano wa madereva jijini Dar es Salaam huku ajenda kubwa ikihusu mgomo huo.

Alitaja baadhi ya sababu zinazowafanya wagome kwa mara nyingine kuwa ni serikali kutotekeleza madai yao likiwamo la kupewa ajira rasmi na waajiri wao.

“Msimamo wetu upo palepale kwamba kesho (leo) hatutaendesha magari..madereva wanaambiwa wezi, tunataka mikataba iboreshwe…tutakaa hapa hata ndani ya siku saba hadi serikali ije na kutoa majibu yanayoridhisha. Tunataka tupatiwe mikataba inayoeleweka na waajiri wetu mbele ya serikali,” alisema na kuongeza:

“Tumekaa katika kikao cha leo (jana) kwa ajili ya kuangalia maazimio ya kikao tulichokaa Aprili 29, mwaka huu…katika kikao hicho zaidi ya madereva 40 walisema hawana hela.”

TABOA WAIPA
ANGALIZO SERIKALI
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Enea Mrutu, alisema walipata taarifa zote kuhusu mgomo huo na kueleza kwamba wanaotangaza mgomo huo siyo madereva walioajiriwa.

Kwa mujibu wa Mrutu, madereva hao ndiyo waliosababisha magari yao kutoingia barabarani Aprili 11, mwaka huu na kuitaka serikali kuingilia kati suala hilo, vinginevyo leo magari hayataweza kuingia barabarani.

DARCOBOA: MGOMO
UWE WA HIARI
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk, alisema chama hicho kina taarifa kuhusu mgomo huo, lakini akaeleza kusikitishwa kwake kwa namna madereva wa vyombo vya usafiri wanavyowahusisha wao akisema hawahusiki.

Kutokana na hilo, Mabrouk aliomba mgomo huo usiwe wa lazima bali wa hiyari kwani si vyema kuwahusisha wao wanaohusika na daladala tena ndani ya mkoa na kupewa vitisho vya kupigwa mawe endapo gari lolote litakaidi agizo hilo.

“Serikali iangalie suala hili, kama kuna jambo lipo nyuma ya pazia basi liwekwe wazi….kama ni wa mikoani kwa nini wanatuhusisha sisi, tusitafute kuwasumubua wananchi,” alisema mwenyekiti huyo wa Tarcoboa.

SUMATRA: WANANCHI WATASUMBULIWA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra), Gilliard Ngewe, alisema, suala hilo lipo katika wizara husika na kwamba kufanyika kwa mgomo huo kutaathiri wananchi kutokana na kukosa huduma za usafiri.

Hata hivyo, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (pichani), bila mafanikio kutokana na simu yake kutopatikana, huku Naibu wake, Charles Tizeba, akisema: “Naomba mnitafute kesho..nipo msibani.”

NIPASHE pia lilimtafuta Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na Naibu wake, Makongoro Mahanga, lakini simu zao hazikuwa hewani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alikaririwa na vyombo vya habari juzi akisema amepokea ujumbe mfupi wa simu kwamba leo kuna mgomo.

Tishio la mgomo wa leo ni mwendelezo wa mgomo mwingine mkubwa ambao ulidumu kwa takribani saa saba kwa mabasi kutokuruhusiwa kutoka katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Ubungo, Aprili 11, mwaka huu.

Madai ya mgomo huo ambao ulileta adha kubwa kwa wananchi yalikuwa ni kupinga ucheleweshwaji wa malori kwenye mipaka hususani ya Tunduma ambako hukaa kwa zaidi ya siku 26 licha ya kulipiwa kila kitu bandarini.

Mengine ni kupinga sheria namba G 31 ya mwaka 2015 ambayo inazungumzia faini ya Sh. 300,000 au kifungo cha miezi 21 kwa madereva wanapofanya makosa barabarani. Pia kupinga madereva kutakiwa kwenda Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya kujinoa.

Madai mengine yalikuwa ni wamiliki wa magari kutowashirikisha madereva katika mikataba yao ya kazi.
Hata hivyo, mgomo huo ulisitishwa baada ya serikali kupitia kwa Waziri Kabaka kufuta sharti la kwenda chuoni kila baada ya miaka mitatu.

Pia aliahidi kulipatia ufumbuzi suala la mikataba yao katika kikao kilichotarajiwa kufanyika wiki iliyofuata.CHANZO: NIPASHE
Vijimambo
Read more