Saturday, July 15, 2017

MAGAZETI YA LEO JULAI 16,2017


Rr

Mitandao ya kijamii inaweza kusababisha magonjwa ya akili - Utafiti

Rorya · 2 days ago

Je, unapenda kufungua mitandao mbalimbali ya jamii kama Facebook, Tweeter, Instagram, Google Plus, Snapchat, LinkedIn, Youtube na mingineyo kila siku? 

Kama jibu ni ndiyo, basi uko hatarini kupata tatizo la msongo wa mawazo na wasiwasi. 

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi. 

Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi kubuniwa na kuboreshwa.

Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa

Rorya maendeleo 5 hours ago

Kipimo sahihi cha maendeleo na mafanikio ya biashara ni ukuaji wa biashara. Tunategemea biashara iwe inakua kadiri siku zinavyokwenda. Ukuaji wa biashara tunaouzungumzia ni kuongezeka kwa idadi ya watu inaowafikia, kuongezeka kwa mauzo, kupata faida kubwa na kuweza kufungua matawi zaidi ya biashara hiyo. 

Kukua kwa biashara ni ndoto ya kila mtu anayeingia kwenye biashara lakini ni wachache sana ambao wanaweza kukuza biashara zao. Wengi wamekuwa wanaendesha biashara zilizodumaa na wakati mwingine zinakufa kabisa. Hakuna bahati nzuri kwa wale ambao wanakuza biashara zao na wala hakuna bahati mbaya kwa wale wanaoshindwa kuzikuza. 

Tofauti pekee inaanzia kwenye maarifa waliyonayo watu kwenye ukuzaji wa biashara. 
Wale ambao wanakuza biashara zao wanajua vitu ambavyo wengine hawavijui. Kwa kuwa vitu hivi siyo siri bali ni maarifa ambayo kila mtu anaweza kuyapata na kuyatekeleza, leo tutakwenda kuangalia njia tano za uhakika za wewe kuweza kukuza biashara yako na kufikia ndoto zako za kibiashara. Jifunze njia hizi na zitumie kwenye biashara yako ili uweze kufika mbali. 

1. Tengeneza timu sahihi ya kibiashara.  
Kwanza kabisa ni vyema ukajua biashara haiwezi kukuzwa na mtu mmoja, wewe mwenyewe huwezi kufanya kila kitu ambacho biashara yako inataka kifanywe. Unahitaji kuwa na watu ambao watakusaidia kwenye biashara yako na watu hawa ni vyema ukawa umewaajiri. Hapa kwenye kuajiri kuna changamoto kubwa sana kwenye biashara nyingi. Wengi wamekuwa wakiajiri mtu ambaye yupo tayari kupokea mshahara kidogo bila ya kujali ataleta mchango gani kwenye biashara. 

Biashara ni kama timu ya mpira wa miguu, kadiri wachezaji wanavyoelewana vizuri na kusaidiana ndivyo timu inavyopata ushindi. Unahitaji kuwa na timu sahihi kwenye biashara yako. unahitaji kuajiri watu ambao wana uwezo na vipaji tofauti. Angalia ni maeneo gani muhimu ya biashara yako na ajiri watu ambao wanaweza kuyafanyia kazi maeneo hayo na kuleta majibu mazuri. Ajiri watu ambao wana vitu ambavyo wewe huna, hii itakunufaisha wewe kwa kukupa muda wa kufanyia kazi yale ambayo ni muhimu zaidi kwa biashara yako. 

2. Wekeza sehemu ya faida kwenye biashara yako.  
Watu wengi wanaoingia kwenye biashara wamekuwa wakifikiri kwamba biashara ikishaanza basi wao ni kuchuma faida na kuendesha maisha yao. Kwa njia hii wamekuwa wanatumia kila faida wanayoipata na hivyo kupelekea biashara kubaki pale ilipo au hata kurudi nyuma, yaani kupata hasara. Biashara haiwezi kukua kama hakuna uwekezaji endelevu kwenye biashara hiyo. 

Tuchukulie biashara kama mfano wa ng’ombe, ng’ombe anapozaa ndama, unaweza kukamua maziwa na kuyatumia au kuyauza. Lakini pia ndama naye anataka maziwa ili aweze kukua, sasa kama utamsahau ndama na kufurahia maziwa, utashindwa kuendeleza ufugaji wako. Unatakiwa kuhakikisha ndama amepata sehemu yake ya maziwa na wewe ndiyo utumie maziwa yanayobaki. 

Wafanyabiashara wengi wamekuwa hawana mpango wa uwekezaji kwenye biashara zao, wanachofanya ni kununua vitu pale vinapoisha. Kwa njia hii biashara haiwezi kukua, biashara inakua pale sehemu ya faida inaporudi kwenye biashara kama uwekezaji. Na unafanya hivyo ukiwa unajua kabisa kwamba nimeongeza kiasi fulani kwenye mtaji na nimefanya hivyo kwa kununua kitu fulani ambacho hakikuwepo awali, au nimeongeza mzigo ambao nimekuwa nanunua. 

3. Kuwa tayari kubadilika.  
Tunaishi kwenye kipindi ambacho mabadiliko yanatokea kwa kasi sana, kila siku kuna vitu vipya vinakuja na vitu vya zamani vinakosa thamani. Kuna biashara ambazo zilikuwa maarufu miaka kumi iliyopita ila kwa sasa hazipo kabisa, na kwa kipindi hiko cha miaka kumi pia zimekuja biashara ambazo watu hawakuwahi kuzidhania. 

Mabadiliko yanatokea na yataendelea kutokea kila siku kwenye maisha na biashara zetu. Wale ambao wao tayari kwenda na mabadiliko wananufaika, wale ambao hawapo tayari wanaachwa nyuma na mabadiliko haya. 

Kila siku jifunze kuhusu biashara yako na biashara kwa ujumla, jua kinachoendelea kwenye ulimwengu wa biashara, jua mbinu mpya za ufanyaji wa biashara na angalia jinsi teknolojia mpya zinaathiri biashara yako. pale unapoona mabadiliko yanaathiri biashara yako usisite na wewe kubadilika. Kung’ang’ania kile ambacho umezoea kufanya kwenye biashara kutakuchelewesha kufika mbali kwenye biashara yako. 

KITABU; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.  

4. Toa huduma bora kabisa kwa wateja wako.  
Wateja ulionao ndiyo sababu biashara yako ipo, kama hakuna wateja hakuna biashara, haijalishi una bidhaa au huduma bora kiasi gani. Hivyo katika mipango yoyote ya kuikuza biashara yako, wateja lazima wawe kipaumbele cha kwanza. 

Wateja wako wanaweza kuwa mabalozi wazuri au wabaya wa biashara yako. Wateja wanaoridhika na huduma wanazozipata wanakuwa mabalozi wazuri na watakuletea wateja wengi zaidi. Lakini wale ambao hawaridhishwi watakuwa mabalozi wabaya kwa kutoa taarifa ambazo siyo sahihi kuhusu biashara yako. 

Ili kutoa huduma bora kwa wateja wako, wape ahadi kubwa halafu toa zaidi ya kile ambacho umeahidi. Na pia inapotokea mteja amepata changamoto kwenye biashara yako msaidie kuitatua. Kwa njia hii utatengeneza uhusiano mzuri na wateja wako kitu ambacho kitaiwezesha biashara yako kukua zaidi. 

5. Epuka hatari zisizo za lazima. 
Kwenye ulimwengu wa biashara, hatari ni kitu cha kawaida, kuna maamuzi mengi ya hatari ambayo unahitaji kufanya ambayo yanaweza kuleta faida kubwa kama yakifanikiwa. Lakini pia yakishindwa yanaleta hasara kubwa. Pamoja na kwamba biashara zipo kwenye mazingira ya hatari, bado siyo sahihi kuchukua kila hatari. Epuka zile hatari ambazo siyo za lazima kwenye biashara yako. 

Hapa unahitaji kufikiri vyema kabla ya kuchukua maamuzi. Na pia unahitaji kuilinda biashara yako dhidi ya hatari ambazo huwezi kuzizuia kwa kuikatia biashara hiyo bima. Kwa kuwa na bima una uhakika wa kuendelea na biashara hata kama kuna ajali iliyopelekea wewe kupoteza sehemu kubwa ya biashara yako.

Maradhi Ya Gesi Tumboni (Colic) Msokoto Wa Tumbo


Rorya maendeleo  8 hours ago

MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo 

Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya 

kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. 

Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo. 

TIBA:  
Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. 

Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. 

Njia Bora Za Asili Za Kukuza Nywele Zako Mambo Unayotakiwa Kuyafanya


Rorya maendeleo 

 hours ago

Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair,tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo.Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu. 

Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi.Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani?Zina tabia gani?Zinataka nini? 

1.Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda. 
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi.Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako.Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri.Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua. 

2.Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe. 
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri. 

3.Linda unyevu wa nywele zako 
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri. 

4.Zifahamu nywele zako 
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu.Unajuaje? 
Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi. 

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi. 
Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka. 

Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita. 
Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana. 
Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka. 

5.Mafuta ya Kupaka kichwani. 
Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele  aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia.Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana.Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree. 

6.Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana. 
Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako.Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana.sio kitana.Chanuo kubwa(wide toothed comb). 

7.Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue. 
Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu.Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka.Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda. 

8.Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo. Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi.Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24. 

Nafasi za kazi leo Julai 15


Rorya maendeleo Blog 1 hour ago


Bonyeza Links zifuatazo kusoma zaidi na kuapply: 

6 Job Opportunities at KP Recruiters, Sales Executives 

Job Opportunity at Heifer International, Communications Officer 

Job Opportunity at Melia Serengeti, Assistant Financial Controller 

Job Opportunity at Kilombero Sugar Company, Deadline is 21 July 2017 

Job Opportunity at GIZ, Advisor 

Job Opportunity at ALISTAR, Group Procurement Manager 

Job Opportunity at PCI, HR & Administration Manager 

Geographic Service Team (GST), Finance Administrator 

Job Opportunity at ABT Associate, Administrative Assistant 

Job Opportunity at NMB, Special Asset Management 

Job Opportunity at TIGO Tanzanian, Relations & Monitoring Officer

Unamjua binti aliyeongoza matokeo ya kidato cha sita?


Rorya maendeleo Blog1 hour ago

Sophia Juma, mwanafunzi wa St Marry’s Mazinde Juu ya Tanga ameibuka kidedea katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15, akishika namba moja kitaifa. 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa nafasi ya pili imeshikwa pia na msichana, Agatha Julius Ninga wa Tabora Girls. Wote walikuwa wakichukua masomo ya mchepuo wa Sayansi (PCB). 

Kadhalika taarifa hiyo imeeleza kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21). 

Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu. 

 Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385. 

“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11  umepanda  kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza; 

“Pia ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.” 

Shule zilizoongoza 

Katika matokeo hayo, Shule ya Wasichana ya Feza Girls ya Dar es Salaam imeibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili. 

Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys (Pwani) iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne. 

Shule nyingine  ni  Marian  Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza Boys (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi. 

Shule zilizoshika mkia 

Shule zilizoshika mkia ni Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja). Nyingine zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya) na Mlima Mbeya (Mbeya). 

Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja) na St Vicent(Tabora). 

Waliofutiwa matokeo 

Kadhalika taarifa ya Necta imeeleza kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu. 

Taarifa ya Dk Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea. 

Pamoja na hao kumi, watahiniwa wengine 15 hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo kutokana na  matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya mitihani hiyo. 

‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde. 

Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018. 

TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA (NECTA)

MATOKEO KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2017

MATOKEO YA DIPLOMA YA UALIMU (DSEE) 2017

MATOKEO YA CHETI CHA UALIMU (GATCE) 2017

Shule zilizoshika mkia matokeo ya kidato cha sita


Rorya maendeleo· 1 hour ago

Zanzibar.  Ni kilio na kicheko. Hivyo ndivyo tutakavyoweza kusema, kwani matokeo ya kidato cha sita, yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15 yamezitaja shule kumi zilizofanya vibaya na kushika mkia kitaifa. 

Shule hizo ni Kiembesamaki Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja). 

Nyingine zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya), Mlima Mbeya(Mbeya) 

 Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja na St Vicent(Tabora).

Tazama Matokeo ya Kidato cha sita hapa


Rorya maendeleo Blog.1 hour ago



Tazama Matoke ya Kidao cha Sita kwa kufuata link hizo hapo Chini 

==>>Bofya hapo chini Kuyatazama

1. Matokeo ACSEE

2. Matokeo Ualimu (DSSEE)

3. Matokeo Ualimu ( GATSE)

Ufugaji Wa Samaki Kwa Mtaji Mdogo


Rorya maendeleo Blog. May 23, 2017

Ndugu zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu, mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa Blogu ya WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi nikakubaliana na ombi hilo. 

Unaweza kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki, kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to get you anywhere’ GO BIG OR GO HOME. 

Ninachokiamini katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza. 

Ndugu zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu, mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa Blogu ya WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi nikakubaliana na ombi hilo. 

Unaweza kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki, kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to get you anywhere’ GO BIG OR GO HOME. 

Ninachokiamini katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza. 

Katika Makala yangu ya wiki hii ningependa kuwashirikisha kitu kidogo sana nacho ni UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO SANA… kipindi cha nyuma, nilikuwa nikiwaona watanzania wenzangu hasa huku Iringa, wakijishughulisha na ufugaji wa samaki, ni miaka miwili imepita sasa, lakini nilikuwa ‘bize’ na mambo yangu sikutaka kujifunza Zaidi kuhusu fursa hii. Mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka jana 2014 rafiki yangu Nicolaus Kulangwa, ambae huko nyuma alinifundisha kilimo cha Matango,alinipigia simu akinitaka nikataembelee mradi wake wa kufuga samaki. Nilienda kijini kalenga hapa Iringa. Nilichokiona nilianza kukifanyia kazi hapohapo na siku ileile. Wakati rafiki yangu akiwa na jumla ya mabwawa saba ya samaki aiana ya sato na pelege mimi ndio kwanza nilijutia muda ambao niliambiwa kuhusu fursa ile halafu nikazembea kuifanya. 

Kama tunavyofahamu, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya unachokifanya na kugusa jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo kwa mifugo mingine yeyote ile, kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili ufugaji wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa na hivyo kufikia malengo ya mfugaji huyo. Lakini kutokana na mazingira ya ufugaji wa huku Iringa hasa Kalenga, nitayataja mambo hayo kwa kifupi sana, mambo haya huenda yakatofautiana kutoka eneo moja la nchi hadi jingine, na kwa vile mimi sijasomea chuo cha ufugaji wa samaki, maelezo haya ni yale niliyoyapata kwa uzoefu tu, siyo ya kufundishwa chuo, mapungufu yatakayogundulika na ‘wasomi’ wataniandikia email ili nikawashirikishe wenzangu. 

Mambo hayo ni kama ifuatavyo: 
ENEO AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI.  Inasisitizwa kwamba, eneo hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu maji kupotea hovyo. Udongo wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa tifutifu ama udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti ama kuweka ‘kapeti gumu’ lisilo ruhusu maji kupotea. 

UPATIKANAJI WA MAJI,  wote tunafahamu kwamba samaki huiishi majini, maji ndiyo roho ya masaki, samaki ni maji na maji ni samaki. Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na maji ya kutoshana salama kwa kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji kwa ajili ya ufugaji wa samaki ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji ya ardhini hasa visima Kwa maeneo ya huku Iringa, tunabahati ya kuwa na mto Ruaha ambao maji yake yapo muda wote wa kipindi chote cha mwaka. Inashauriwa kwamba eneo hilo liwe salama ili kuwalinda samaki na mfugaji kwa ujumla. 

BWAWA.  Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija. 

MBEGU AMA VIFARANGA,  mfugaji wa samaki anashauriwa kutembelea maeneo ambayo wafugaji wakubwa wanazalisha vifaranga ili aweze kupata mbegu bora anayohitaji. Kwa wananaoishi Iringa na maeneo ya jirani, wanaweza kupata mbegu kwa bwana Nicolaus. 

UTUNZAJI WA BWAWA NA USAFI.  Ili mfugaji aweze kunufaika na miradi ya kufuga samaki ni lazima uafanye usafi wa kutosha ndani nan je ya bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu na viumbe wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge wasiweze kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja. 

ULISHAJI . Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji kula chakula kingi sana. Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza kuwa mara tatu kwa wiki ama Zaidi. 

AINA YA CHAKULA.  Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga zilizosagwa, unga wa mahindi, mabaki ya chakula kama ugali nk. 
Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo mengine ni kama vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia masoko, utaalamu nk. 

CHANGAMOTO KATIKA SAMAKI  ni magonjwa kama vile magonjwa ya samaki yapo mengi yakiwa nayasababishwa na vimelea vifuatavyo magonjwa yanayosababishwa na bakteria, magonjwa yanayosababishwa na virusi magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa yanayosababishwa na protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni. Chanagamoto nyingine ni kama vile, Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Iwapo bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa. 

UVUNAJI WA SAMAKI.  Hujudi za mfugaji ndio zinaweza kupelekea kuvuna samaki wa kutosha na kumletea faida kwa muda mfupi. Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea ubora wa chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8. Kuna watakao sema huu ni muda mrefu, ukiona ufugaji wa samaki wanatumia muda jaribu kingine. Ama endelea kukaa nyumbani kwako, ukiisubiri serikali na mashirika ya kijamii yakusaidie. 

 Nielezee kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi kwa watanzania na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za kiuchumi, na ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa, imesababisha watanzania wengi kuanza kuwa wabunifu na kuanza kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji. Kwa sasa mabwawa mengi yanapatikana katika mikoa sita yenye rasilimali nyingi kama Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma. Ufugaji wa samaki umeenea kote nchini. 

Kwa sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/ kwa huku Iringa na ukiuuzia bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/ kwa kilo. Hii ina maana kwamba ukiwa na kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni mbili na laki nane kila baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu tano? Utagundua kwamba adui wa mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo weka kichwani kwako.

Niseme wazi tu kwamba, ufugaji wa samaki, ni fursa nyingine ambayo ipo wazi kwa kila Mtanzania kuifanya, kuna watakao singizia mitaji, hali ya hewa nk,lakini ukweli ni kwamba bwawalangu dogo nilitumia pesa ndogo sana kulichimba ikiwa ni pamoja kununua vifaranga vya samaki. 

Tumekuwa watu wa kujiwekea mipaka ya mafanikio vichwani mwetu. Kumbuka kwamba ukishajiwekea mipaka ya mafaniko. Maisha yetu yataweza kubadilika iwapo tutabadilisha namna tunavyoyatazama mambo. Kwa mfano unaweza kuwa umejiwekea mipaka ya kimapato kwamba wewe mwisho wako ni kupata laki moja, mtazamo huo ukikaa kichwani basi ukiambiwa bwawa moja linaweza kukutolea shilingi milioni 25 kwa miezi sita, utakataa na hivyo fursa hiyo itakupita. 

Nilipokuwa nikisoma kitabu cha ‘THE TRUTH SHALL MAKE YOU RICH’ cha reallionaire mdogo kuliko wote Farrah Gray kwa sasa, nimejifunza kwamba, maisha yetu yanaweza kubadilika muda wowote na dakika yoyote iwapo tutajijengea Imani kwamba, maisha yanawezekana popote. Na kwa Tanzania hii ambapo kila mwananchi anaruhusiwa kulimiliki ardhi kwenye mkoa wowote umasikini litakuwa ni swala la kujitakia. 

Ninamalizia makala hii kwa kusema kwamba, kila saa katika maisha yetu ni fursa, makala hii pia ni fursa kwako na kwangu, kuna baadhi ya nchi duniani ambapo wananchi wake hawana bahati ya kukaa kwenye meza zao na kujifunza mambo haya. Kwawatakao penda kuja Iringa, kujifunza ufugaji wa samaki, tunawakaribisha sana. Nicolaus na mimi na wafugaji wengine watakusaidia kuapata elimu Zaidi yahii niliyoandika hapa.