Barabara ya kutoka DODOMA kwenda iringa kukabidhiwa kulingana na kiwango cha ubora wa Hali ya juu
Saturday, June 20, 2015
LOWASSA LEO IRINGA MAPOKEZI NI ZAIDI YA RAIS.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli
amedhihirisha nguvu kubwa na utajiri wa watu aliyonao,
baada ya kupata mapokezi makubwa Mkoani
Iringa.Lowassa amewasili Iringa asubuhi hii akiongozana
na wabunge karibu wote wa mkoa wa Iringa,kwa ajali ya
Harambee ya ujenzi wa kanisa na Kituo Cha radio Cha
overcomers.viongozi wote wa Chama tawala Mkoani Iringa
na Serikali nzima imempokea Mh Lowassa.
Tuesday, June 16, 2015
DONALD RUN FOR US PRESIDENT
GREECE IS MISLEADING VOTERS
Juncker says Greece is 'misleading' voters over Greece has been warned it is running out of time Jean-Claude Juncker has accused the Greek government of misleading voters as Alexis Tsipras said its creditors were trying to "humiliate" the country. The European Commission president said the government had not told the truth about its bailout proposals. "I am blaming the Greeks [for telling] things to the Greek public which are not consistent with what I've told the Greek prime minister," Mr Juncker said. Mr Tsipras has said that the lenders wanted to raise VAT on electricity. Other Greek ministers have criticised suggestions to increase sales tax on medicines.
MSEVENI WA UGANDA KUCHIMA VIJEMBE
WASIRA KUDHAMINIWA IRINGA LEO.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasirra
amesema yupo tayari kumuunga mkono mgombea
yoyote atakayeteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)
kupeperusha bendera ya chama hicho katika
kinyang’anyiro cha urais Oktoba mwaka huu endapo
nafasi hiyo haitaangukia mikononi mwake.
Pamoja na ahadi hiyo, amesema hawezi kutoa jibu lolote
kwasasa kama atagombea tena au hatagombea ubunge
katika jimbo lake la Bunda kwasababu haijaingia katika
kinyang’anyiro hicho cha urais kwa ajili ya kushindwa.
Akizungumza na wanahabari kabla ya kukutana na
wadhamini wake zaidi ya 100 waliojitokeza kumdhamini
mjini Iringa jana, Wasira alisema; “ mimi ni mtu mwenye
uzoefu mkubwa wa kuongoza watanzania, kwahiyo nina
amini nina fursa kubwa zaidi ya kuwa mgombea.”
Akizungumzia idadi kubwa ya wana CCM wenzake
wanaojitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu, alisema
hashangazwi hata kidogo kwani CCM ina hazina ya
viongozi wengi wenye sifa za urais japokuwa katika hao
waliojitokeza hakuna anayemuhofia.
“Tofauti na wale wenzetu, wao wana mtu mmoja mmoja
tu katika vyama vyao, ukizungumza CUF utamtaja
Lipumba na vyama vingine ni hivyo hivyo; ni sasa tu
baada ya kuunganisha vyama vyao kupitia umoja usio
rasmi angalau unaweza kuona kama wako wengi, lakini
kiuhalisia ni wale wale wanaotegemewa na vyama vyao,”
alisema.
Alisema hali hiyo ni tofauti na kabisa na CCM na
akawasihi wagombea wenzake wasipende
kuzunngumzia majina ya watu kama anavyofanya yeye.
“Katika harakati zangu zote sipendi kuzungumzia majina
ya watu, tunazungumza hoja, tunazungumza uchumi,
umasikini, ufisadi, rushwa na mengineyo kama hoja,
hatuzungumzi ufisadi kwa kulenga watu,” alisema.
Alisema katika kinyang’anyiro hicho anayelenga watu
atakuwa anahukumu watu huku vitabu vitakatifu
vikiwakataza kuwahukumu wengine ili nao
wasijehukumiwa.
“Habari ya ufisadi na mafisadi ni msamiati ulioingizwa
na wapinzani wetu. Mimi kama Wasira sina majina ya
watu mfukoni mwangu ambao naweza kusema nikiingia
Ikulu nitawashughulikia,” alisema.
Alisema endapo atapata ridhaa hiyo, ufisadi na rushwa,
atavishughulikia kama hoja kwa ahadi ya kutovifumbia
macho kwasababu vyote vinaua nchi na kuwafanya watu
waone haki sio haki.
“Katika kipindi hiki wana CCM lazima kazi yetu iwe ni
kuwaelimisha wananchi wakijue chama chetu na kujenga
umoja. Hatutakiwa kuzozana wenyewe kwa wenye, hiyo
itatupunguzia nguvu badala ya kutuimarisha, kumbukeni
Iringa mlivyohitilafiana mwaka 2010 na kupoteza jimbo
la Iringa Mjini kwa wapinzani,” alisema.
Alisema katika utawala wake atatilia mkazo kilimo cha
kisasa kwa kutumia zana za kisasa na kujenga viwanda
vya kisasa ili mazao yaweze kuongezewa thamani.
ZITTO KUZUNGUMZIA TAARIFA YA CAG
Tamko la Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ndg.
Zitto Kabwe kuhusu Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014
1) Taarifa nyingine ya CAG imetoka, kwa mujibu wa Katiba
ya JMT na kwa mujibu wa sheria za nchi. Taarifa hii
imechelewa kutolewa kulingana na mabadiliko ya Ratiba za
Bunge ambapo hapo awali taarifa ilikuwa ikitoka mwezi
Aprili na kuwezesha kuchangia katika mchakato wa Bajeti
ya nchi. Taarifa ya mwaka huu na ile ya mwaka Jana
imetoka wakati wa Bunge la Bajeti na hivyo Bajeti ya
Serikali haijazingatia hoja za ukaguzi ili kuboresha mfumo
wa matumizi ya fedha za umma. Ni vema utaratibu wa
zamani wa ripoti kutolewa mwezi Aprili urejewe ili
wabunge waweze kutumia ripoti hizo wakati wa kamati
katika kujadili makadirio ya Bajeti za Wizara mbalimbali.
2) Taarifa kama miaka iliyopita bado sio nzuri. Mapato
mengi ya Serikali bado yanapotea. Uk. 53 wa Taarifa
unaonyesha kuwa mizigo inayoingizwa nchini kupita
kwenda nchi jirani zinazotumia bandari zetu hubakia nchini
na kuingizwa sokoni hivyo kukwepa kodi. Mwaka
2013/2014 mizigo ya transit iliyobaki nchini kiudanganyifu
ilikuwa zaidi ya bidhaa 6000 kwa mujibu wa Taarifa ya
CAG. Hivyo kodi ya tshs 836 bilioni haikulipwa kwa mizigo
hiyo sawa sawa na 10% ya makusanyo yote ya kodi za
ndani. Tshs 836 bilioni ilipotea mwaka 2013/14 peke yake.
Wakati hili linatokea Serikali ipo ukata mkubwa na
kushindwa kuendesha miradi yake mbalimbali. Fedha
iliyokwepwa idara ya forodha peke yake inalipa Madeni
yote ya wakandarasi wa barabara wanaoidai TANROADS
na riba kulimbikizwa kila mwaka. Fedha hii ingelipa Madeni
yote ya mfuko wa PSPF wanayoidai Serikali. Fedha hizi
zingeweza kulipia miradi 2 mikubwa nchini ya BVR na
vitambulisho vya Taifa ambayo inasuasua kutokana na
ukata.
Natoa wito kwa CAG kwanza kuweka wazi orodha ya
bidhaa hizo zilizobakia nchini na kuingizwa nchini bila
kulipa kodi. Vile vile CAG aweke wazi wafanyabiashara
wote walioagiza bidhaa hizi na vyombo vya kiuchunguzi
vichukue hatua za kuwashtaki wafanya biashara hawa
mara moja.
Natoa wito kwa Kamati ya Bunge ya PAC kuwaita mara
moja maafisa wa TRA kujieleza mbele ya kamati kuhusu
suala hili na kuandaa taarifa maalumu bungeni ili kuanika
uoza huu unaopoteza mapato mengi sana ya Serikali.
3 ) CAG kaonyesha kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana
kitengo cha maafa cha ofisi ya Waziri Mkuu ambapo tshs
163 billioni za chakula cha maafa hazikukusanywa katika
kipindi cha miaka 5 iliyopita. Huu ni kama mrija wenye
wastani wa tshs 32 bilioni kuchotwa kwa kisingizio cha
chakula cha maafa kwa wananchi. Kwa malezo ya CAG ni
kwamba Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekula
fedha za chakula cha misaada. Maana hakuna uthibitisho
wa kuwa mahindi yaliyogawanywa na taarifa kutolewa na
Wakala wa Akiba ya Chakula (NFRA). Kitengo cha maafa
ofisi ya PM kimekuwa mrija wa wizi wa fedha za umma,
wizi ambao umekuwa ukifanyika bila ya kugunduliwa kwa
miaka 5 sasa. ACT Wazalendo inaisihi Kamati ya Bunge ya
PAC kufanya uchunguzi maalumu kwenye kashfa hii ya
tshs 163 bilioni katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Wakala wa
Hifadhi ya Chakula ( NFRA).
4) ACT Wazalendo inalitaka Bunge kuchukua stahiki dhidi
ya Wizara ya Ujenzi kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha kuwa
Wizara ilidanganya Bunge katika kupitisha Bajeti ya tshs
252 bilioni ambapo kati yake tshs 87 bilioni ziliibiwa au
matumizi yake kutoeleweka.
5) ACT Wazalendo inampongeza CAG kwa kuendelea na
zoezi la kisheria la kukagua mahesabu ya vyama vya siasa.
Hii inaweka misingi ya uwajibikaji kuanzia kwenye vyama
vya siasa, taasisi muhimu sana katika ujenzi wa
demokrasia. Vyama vya siasa vichukulie ripoti ya CAG
kama changamoto ya kutoa kwanza kibanzi kwenye
macho yao ili kuwa na ‘ moral standing’ ya kupambana
dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma nchini.
Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo

KIGOMA YAWAKA MOTO.
ACT WAZALENDO WAJA KWA MBWEMBWE KIGOMA. cha kipia cha act yaendelea na operesheni majimaji Mkoani KIGOMA na kupata wanachama wengi kuliko waliyo tarajia wapinzani wao
Monday, June 15, 2015
Chuo cha rucu iringa kuboresha majengo
Chuo kikuu cha RUCU IRINGA yaendelea na uboreshwaji wa majengo ili kuongeza ufansi katika elimu ya juu hapa tanzania.
Pata picha mbalimbali hapa
ACT YATIKISA GEITI
ACT WAZALENDO NI CHAMA KICHANGA SANA TANZANIA ILA MAKACHA SASA NI NAMBA TANO KWA UKUBWA NA KUFANYA WATU WENGI KUKIPENDA.
wanaichi wakiwa makini kusikiliza uongozi wa act geita
waki
Sunday, June 14, 2015
KIMENUKA- KIGOGO WA CCM AMLIPUA LOWASSA,AMWITA LOWASSA NI MWIZI ,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI.
KIMENUKA- KIGOGO WA CCM AMLIPUA LOWASSA,AMWITA LOWASSA NI MWIZI ,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI.
http://fullhabari.blogspot.com/2014/09/kimenuka-kigogo-wa-ccm-amlipua.html
majanga ndani ya ccm kwa sasa kila mtu na yake.
WAZIRI wa Zamani wa Serikali ya wamu ya tatu na Nne, wa CCM Dr. Anthony Diallo na Mwenyekiti wa sasa wa CCM Mkoa wa Mwanza. |
PICHANI NI WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU EDWARD LOWASSA |
1: Sijamtuma Mzee yeyote kwenda kwa Lowasa kwa sababu sio waziri mkuu tena na hata kama angekuwa bado waziri mkuu nisingeweza kumwambia mtu akaniombee vyeo kwa Lowassa. Hao wazee aliowataja wapo Mwanza na mnaweza kupata namba zao za simu na kuwauliza kama nilishawahi kufanya hivyo. Pili, mwaka 2003/4 haukuwa mwaka wa uchaguzi, ilikuwaje niende kuomba cheo wakati niliingia baraza la Mhe. Rais Mkapa 2001? Wakati huo Lowassa hakuwa waziri mkuu! Tatu, mwaka 2004 sijaonana na JK na Karamagi hajanishawishi kumuunga mkono JK mwaka 2005. Mimi ndiye niliyetumwa kumwambia Lowassa asigombee 2005 kwavile dhambi na tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mwalimu zilikuwa kwenye mioyo ya watanzania na asingeweza kupata kura za ushindi isipokuwa angempunguzia JK kura zake na wote kukosa. Karamagi tumekutana naye bungeni baada ya kuchaguliwa ubunge baada ya kifo cha Mhe. Kinyondo. Mimi nimezaliwa na kukua kwa kuzingatia nidhamu ya Kisukuma, sijalelewa kihuni kufika kumsema mtu kama JK. Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais! Mimi sijasema Lowassa alidhulumu CCM kupata hisa Vodacom, nilichosema CCM ilikuwa iwe mbia wa MTN, kampuni iliyonyimwa leseni wakijua fika kuwa ilikuwa ikisaidie chama, badala yake wakafanya njama kuvunja tume ya mawasiliano kihuni, na hapohapo wakaipatia vodacom leseni lowasa kwa kutumia watoto wake, alipata walikipata. Ushahidi kuhusu hili ni kampuni yake kupewa U-Super Dealer wa Vodacom ambayo uliwafanya wanufaike kwa kuuza simu nchi nzima.
Kama wanasema Lowassa ni mzima, naomba akakimbie uwanja wa Taifa azunguke hata mara moja kama hataishia ICU. Na kama ni mzima, anatumia fedha za nchi kwenda kutibiwa nini ujerumani kila wakati au Ujerumani nako siku hizi kuna waganga wa kienyeji? Pili kwanini alikwenda kuombewa kwa Emmanuel Ministries huko Nigeria? Kampeni za Urais zinahitaji afya nzuri, sio mzaha kuweka mgonjwa akatufia kwenye jukwaa! Kuhusu tuhuma ya rushwa toka kwa Kimaro, nina hakika Kimaro bado yupo hai, na kama ni mkweli aseme ukweli. Kimaro ni rafiki yangu na nilimshawishi akawekeza hoteli ya Nyumbani sasa ni JB Belmonte, Mwanza. Sijachukua fedha ili nimpatie kitalu kwavile yeye sio mwindaji na sijasikia kuwa ana hiyo biashara. Ninachofahamu ana mahoteli na ndiyo biashara yake. Rais yupo kama alishaniita kunieleza hilo anaweza akasema, ni mkweli. Tuhuma za mimi kuhongwa na Kimaro alizianzisha Lowassa baada ya mimi kutaka kumuondoa Mkurugenzi wanyama pori wizara ya Maliasili. Mkurugenzi huyo alikuwa na mahusiano naye na baadae walikuja kuoza watoto wao. Hilo kila mtanzania analifahamu, na alimtetea sana abaki wizarani wakati huo. Lowassa yupo kwenye mtandao wa yote yanayosemwa kuhusu wanyama pori. Pia tuhuma za kumtapeli aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mhe Karume ndio nazisikia leo. Karume sijafika nyumbani kwake Zanzibar na wala hata alipokuwa Ikulu Zanzibar. Yupo na anaweza kuulizwa, ni mkweli atasema yaliyo kweli.
Huyo msichana anayesemekana nilimpa mimba, mhudumu wa Dodoma hotel, ndiyo namsikia leo, na kama yupo aniletee mtoto huyo kwani ndio nasikia kwenye watu wa Lowassa baada ya kuweweseka na machache tu tuliyoyaweka hadharani. Mwisho la kupewa fedha na mtuhumiwa wa IPTL nalo jipya simfahamu, labda Lowassa anamfahamu! Tatizo la huyu Lowassa, ni kupata URAIS, asipoupata sijui kama atabaki na afya ya kuridhisha. Anatuhumu watu tusiounga mkono jitihada zake tu, je wanaogombea watakuwa na hali gani mbele yake? Ushauri wa bure kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais hatopata.Kidumu Ccm kidumu chama tawala.
Burundi parliament approves two new members of electoral.
BUJUMBURA Burundi (Xinhua) -- Both chambers of the Burundian parliament have approved two new members of the National Independent Electoral Commission (CENI) who will replace two ladies resigned earlier this month.
The two new female members are Annonciate Niyonkuru and Alice Nijimbere, both Tutsi, replacing respectively of Spes-Caritas Ndironkeye who was the CENI Vice-President and Illuminata Ndabahagamye who was in charge of finance and administration.
At the National Assembly (lower chamber), the candidacies of the two were approved by 81 out of 82 MPs present at the plenary session, while at the Senate (upper chamber) 33 voted for them and 3 against.
“I am satisfied with the vote because the CENI is now going to be complete in accordance with Article 90 of the national constitution which provides that the CENI is composed of five commissioners from various political spheres and ethnic groups,” said Pascal Nyabenda, chairman of the ruling party, the National Council for the Defense of Democracy-Forces for the Defense of Democracy (CNDD-FDD).
Annonciate Niyonkuru, the future CENI Vice-President was the President of the first instance court of Ngozi in the northern province of Ngozi and Alice Nijimbere, the future commission in charge of finance and administration was working in the education sector at Matongo in the northern province of Kayanza.
On June 1, the two former members, both from the Union for National Progress, confirmed their resignation through separate letters sent to CENI President Pierre Claver Ndayicariye.
In their letters, they explained that “the prevailing political and security environment does not offer ideal conditions” for holding elections which are very important for the Burundian people.
With only three remaining commissioners, CENI could not make any decision as it required four out of its five commissioners to make decisions.
Burundi is to hold elections in June and July.
A new election schedule shows that legislative and communal polls will take place on June 29, the presidential election on July 15 and senatorial elections on July 24.