Thursday, September 17, 2015

Kutana na Anna katika kampeni za Act

Mama machachari katka chama cha act wazaleo yupo kwenye harakati za hapa na pale ili kukijulisha umma thamira ya kweli toka chama hicho juu ya maendeleo.

Wednesday, September 16, 2015

PATA JINALAKO HAPA TOKA TCU

MAJINA YAMETOKA KWA WAIOOMBA KUJIUNGA VYOO VIKUU

TCU MAJINA YA WALIOKOSA VYUO MWAKA 2015/16 HAYA HAPAA

TCU YATOA MAJINA YA WALIO KOSA AWAMU YA KWANZA MAJINA YANAPATKANA HAPA http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Group%20(I_L).pdf WAWEZA Wasilia nasi kwa Sim No 0768441610 kujua jinsi ya kutuma maombi ya pili.

WAZIRI SAADA MKUYA AZINDUA KAMPENI.....


Waziri wa fedha , Bi Saada Mkuya azindua kampeni

Mgombea ubunge jimbo la Welezo, Waziri wa Fedha , Bi Saada mkuya akimwaga sera katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni jimboni. mkutana ulifanyika jana uwanja wa KimaraMeza kuu ikimsikiliza kwa makini mgombea Ubunge wa jimbo la Weleze Bi Saada Mkuya(hayupo pichani) akijinadi na kumwaga sera. Mkutano huu pia ulihudhuriwa na mgombea uwakilishi wa jimbo hilo la Welezo, Hassan Hafidh (wa pili kulia waliokaa)Wanachama na wapenzi wa CCM kutoka jimbo la Welezo waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya jimbo la Welezo jana huko Uwanja wa Kimara wakimsikiliza kwa makini mgombea ubunge wa jimbo hilo Bi Saada Mkuya SalumWanachama na wapenzi wa CCM kutoka jimbo la Welezo waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya jimbo la Welezo jana huko Uwanja wa Kimara.Timu ya kampeni ya mgombea Ubunge wa jimbo la Welezo

ACT WAZALENDO JIMBO LA IRINGA WAZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE


ACT WAZALENDO JIMBO LA IRINGA WAZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE

 Viongozi  wa ACT  wazalendo Iringa  wakijiandaa kwa  wimbo  wa Taifa jukwaani wakati wa uzinduzi wa kampeni  zao kwenye uwanja wa Mwembetogwa jana  mjini Iringa jana
Mgombea ubunge  jimbo la Iringa mjini Chiku  Abwao  akiwahutubia  wananchi  katika  uzinduzi wa kampeni kwenye uwanja wa Mwembetogwa jana

Mgombea ubunge  jimbo la Iringa mjini Chiku  Abwao  akiwahutubia  wananchi  katika  uzinduzi wa kampeni kwenye uwanja wa Mwembetogwa jana
Msanii Baba  Revo  akiwa na Chiku Abwao

ACT WAZALENDO YAZINDUA KAMPENI ZAKE WILAYANI BAHI MKOANI DODOMA


ACT WAZALENDO YAZINDUA KAMPENI ZAKE WILAYANI BAHI MKOANI DODOMA

 Mgombea Mwenza wa chama cha ACT wazalendo Hamad Yusufu akizungumza na wakazi wa Mayamaya kata ya Zanka wilayani Bahi mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kuomba kura alipokuwa akimnadi Mgombea Urais wa chama hicho Anna Mghwila, mgombea ubunge wa jimbo hilo Eva Kaka na madiwani wa kata mbalimbali.  Mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Eva Kaka akimkabidhi fedha Mwalimu Joseph John mkazi wa Mayamaya kama kifuta machozi kutokana na mwalimu huyo kuunguliwa na majani kwa ajili ya malisho ya mifugo yake ambapo nyumba yake ilinusulika kuungua.
 Katibu wa Mipango na uchaguzi wa ACT Mkoa wa Dodoma, Alyoce Ambokile akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza katika mkutono huo wa kuomba kura katika kata ya Zanka Mgombea Udiwani kupitia chama hicho kata mojawapo ya wilayani Bahi Anthon Lyamunda akiongea jambo kwenye mkutano huo   Kaimu katibu  Witness Peter na Mweka hazina wake Ldya Molel wa ACT mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika wilaya ya Bahi mkoani DodomaViongozi wa ACT mkoa wa Dodoma wakipunga mikonoWamanchi wa eneo ilo wakifuatilaia kwa makini mkutano wa ACT
Vijimambo 

Chama cha ACT WAZALENDO chazindua kampeni zake za Ubunge jimbo la Manyoni


Chama cha ACT WAZALENDO chazindua kampeni zake za Ubunge jimbo la Manyoni

SAM_0108
             
bahathi ya viongozi wa chama hicho mkoani hapo

baadhi ya wagombea ubunge wa chama cha ACT Wazalendo waliohudhuria mkutano wa uzinduzi katika jimbo la Manyoni-Singida.
Na, Jumbe Ismailly, Manyoni      
CHAMA Cha ACT Wazalendo wilaya ya Manyoni Mkoani Singida kimezindua kampeni za ubunge wa jimbo la Manyoni mashariki kwa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo,Muttee John Henry na kuwatisha watendaji wa idara ya afya wanaouza madawa kwenye vituo vya kutolea huduma na hivyo kusababisha wananchi kukosa huduma katika vituo vya kutolea huduma hizo.
Akiwahutubia wananchi wa mji wa Manyoni na vitongoji vyake,mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni mashariki kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo,Henry amesema vituo vingi vya kutolea huduma za afya vimekuwa vikikabiliwa na uhaba mkubwa wa madawa jambo linalowafanya wagonjwa wanaofuta huduma kutakiwa kwenda kununua dawa kwenye maduka ya madawa yaliyopo karibu na vituo hivyo.
Hata hivyo mgombea huyo alifafanua kwamba kutokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa dawa,ni asilimia sita tu ya watanzania ndiyo wanaonufaika na mfuko wa afya ya jamii (CHF),hali inayoonyesha bado kuna idadi kubwa ya watanzania wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma hizo za afya kwenye maeneo ya vijijini.
‘Ndugu zangu nchi hii asilimia sita tu ya wananchi wa Tanzania ndiyo wanaonufaika na mfuko wa afya ya jamii na asilimia 98 ya wakulima,wafugaji,bodaboda,mama lishe na wafanyakazi katika sekta isiyokuwa rasmi hawanufaiki na mfuko wa afya ya jamii(CHF)’’alifafanua Henry.
Kwa mujibu wa Henry,licha ya wananchi hao kupigania kuongeza uchumi kwa nguvu zote kwa kipindi cha miaka 35,wanapofikia umri wa miaka 60 huwa wamechoka na hivyo kujikuta wakisahaulika katika taifa lao walilolitumikia kwa kipindi kirefu katika maisha yao.
Aidha alisisitiza kwamba taifa linalowasahau wananchi waliolitumikia kwa miaka mingi ikilinganishwa na watumishi wa serikali ambao wanapostaafu hulipwa mafao yao ya kustaafu,hilo siyo taifa jema ambalo baba wa taifa alikuwa akijivunia.
Alisisitiza mgombea huyo kijana kwamba ni wakati muafaka sasa wa kuweka utaratibu wa kuwasaidia watanzania wanyonge  hao pale wanapochoka.
 Ili kukabiliana na hali hiyo ya ukosefu wa madawa kwenye vituo vya kutolea huduma,Henry alisema chama cha ACT Wazalendo kimetafakari sana na kuja na mpango mpya wa kuanzisha mfuko utakaowasaidia watanzania wanyonge.
“Najua fedha zetu tunazokusanya ni chache sana lakini mfuko wa wanyonge ambao utaweza kuhifadhi fedha kidogo kidogo ndiyo kimbilio la wanyonge wanaopata majanga ya kuugua basi wanapona kwa mfuko wa afya ya jamii”alifafanua.
Naye katibu wa Mkoa wa Chama Cha ACT Wazalendo,Lipu Loti Robert alisema idadi kubwa ya watendaji wamebainika kulihofia azimio la Arusha lililoachwa na baba wa taifa marehemu,Mwalimu Julius Nyerere na ndiyo maana waliamua kulivunja kwenye moja ya vikao vilivyofanyika Zanzibar.
Hata hivyo Roberti aliweka wazi kuwa ACT baada ya kubaini kutokuwepo kwa azimio la Arusha ndipo walipozindua azimio la Tabora ambalo lina mambo manne,ambayo ni pamoja na Hifadhi ya jamii,suala la uchumi shirikishi,sekta ya afya na sekta ya elimu.
SAM_0105katibu wa ACT Mkoa wa Singida,Bwana Lipu Loti Robert akifungua mkutano wa uzinduzi wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni mashariki.

Tuesday, September 15, 2015