Saturday, July 23, 2016
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WANAWAKE WA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma ambapo aliwasihi kuendelea kudumisha umoja na mshikamano pamoja na kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi na kujiunga na Mabaraza mbali mbali ya kuwezesha wanawake.
Baadhi ya Wajumbe walishindwa kujizuia na kuamka kwa shangwe na vifijo.
Mke wa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ,wilaya ya Lindi Mama Salma Kikwete akizungumza na Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma .
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson akungumza kwenye mkutano uliowakutanisha Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akipokelewa na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku (Msukuma) mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Herman Kapufi mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ,Missana Mwishawa muda mfupi baada ya kuwasili katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo.
DK. JOHN POMBE MAGUFULI ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA CCM, AMCHAGUA TENA KINANA KUWA KATIBU MKUU
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM baada ya wajumbe hao Kumthibitisha kuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano Kwa kumpigia kura zote za ndiyo wajumbe waliopiga kura ni 2395 kura zilizoharibika ni 0 na Mwenyekiti Dk. John Pombe Magufuli ameshinda kwa kwa kupigiwa kura zote 2395, Lakini pia mwenyekiti huyo ameamua kuendelea na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Sekretarieti nzima iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa CCM.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uchaguzi uliopita na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza machache kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipokea ilani ya uchaguzi kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.
Viongozi wastaafu wakiwa katika mkutano huo kutoka kushoto ni Mzee John Samwel Malecela, Mzee Amani Abeid Karum, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Mohamed Gharib Bilal na Mzee Pius Msekwa.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Ndugu Agustino Mrema akiwasliana na wake wa viongozi wastaafu.
Baadhi ya wajumbe wakishangilia mara baada ya mkutano huo kumthibitisha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Mwanachama wa CHADEMA Mgana Msindai akiwapungia mkono wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM baada ya kurejea CCM alipotangaza rasmi kwenye mkutano mkuu huo.
Mgana Msindai akielekea jukwaani ili kutangaza nia yake ya kurejea CCM leo kwenye mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma.
Freddy Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wa chama cha CHADEMA akitangaza nia yake ya kurejea CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma leo.leo.
Taarifa kwa umma na waandishi wa habari
Ndugu waandishi wa habari kwanza tunawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa kuwaeleza Watanzania adhima yetu ya kwenda Dodoma, katika kuhakikisha BAVICHA tunaisimamia kauli Jeshi la Polisi na ya Mhe. Raisi, na kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote hadi mwaka 2020 tukianza na mkutano haramu wa CCM hapo tarehe 23 July 2016.
Tunaendelea na msimamo wetu kuamini mkutano huo sio halali,kwakuwa ni Mkusanyiko wa Kisiasa ambao Mhe. Raisi na Jeshi la Polisi waliikataa vinginevyo watoke hadharani kukanusha Agizo na msimamo wao ulioathiri tayari vyama vya upinzani vikiwemo CHADEMA na ACT kwa kuzuiwa kukutana.
Sisi BAVICHA tunaheshimi kauli ya Kiongozi wetu mkuu wa chama,aliyotuomba tusiende Dodoma, kauli hii imeipa nafuu kubwa CCM kwakuwa hawakuwa na ubavu wa kutuzuia tusizuie mkutano wao.
Tulijipanga kila kona ya nchi hii,na hata jeshi la Polisi lisingeweza kutuzuia katika kutekeleza azima yetu,ya kutaka haki na usawa wa Kidemokrasia katika nchi hii ya Kidemokrasia.
Sasa basi,baada ya M/kiti kutuomba vijana wake tusiende Dodoma, sasa tunaamua kuja na plan B,ambapo hatutaenda Dodoma lakini hatutaruhusu mkutano wa CCM ufanyike mpaka pale Serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za Kidemokrasia kwa kila chama,kufanya siasa maana hivi tunavyoongea CCM wao wanafanya mikutano ya hadahara na wengine wanazuiwa.
Tunayo taarifa ya Baadhi ya mawaziri na wabunge wa CCM wao wanafanya mikutano ya hadhara katika majimbo mbali mbali,na picha za matukio hayo tunazo kwa ushahidi hivyo tukashitaki wapi?
Tunazo taarifa za Wakuu wa wilaya wakifanya mikutano ya hadhara na wanachi,hivi kati ya mkuu wa wilaya na vyama vya siasa nani mwenye mamlaka ya kufanya siasa!??
Tunaomba Watanzania waone na wapaze sauiti jinsi nchi yao inavyoongozwa Kidikteta,na kukosa usawa.Leo Dodoma kumepelekwa Polisi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Singida,Dar es salaam na Iringa wakiwa na kila aina ya Vifaa vya kivita.
Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Polisi wengi wasio na Idadi wakiwa na silaha nzito za kivita wanaenda kulinda mkutano wa Kisiasa,hii haijawahi kutokea.
Mtakumbuka Polisi wamewahi kuzuia mikutano mingi sana ya CHADEMA kwa kigezo kutokea machafuko na hali ya usalama ni ndogo,lakini hii imekuwa tofauti sana kwa upande wa Ccm wao usalama ni mdogo sana kupita maelezo katika mkutano wao wa tarehe 23 July,lakini vimepelekwa mpaka vifaru vya jeshi kuimarisha usalama.
Hii ni double standard ya hali ya juu,inayooneshwa na jeshi la Polisi kwa vyama vya siasa na huwa mara nyingine tunasema Polisi wanatumika na Ccm na huu ni ushahidi wa kwanza mkubwa kabisa.
Polisi wa nchi hii wako radhi wao wafe lakini Ccm isiguswe na wapo radhi hata kuua wapinzani ili Ccm iendelee kuwa madarakani,uko wapi usawa wa Kidemokrasia??? Uko wapi weledi wa kiutendaji wa jeshi letu la Polisi?.
UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINADAMU.
Tokea BAVICHA tumatangaza kwenda Dodoma, majeshi yaliyopelekwa Dodoma kuisaidia Ccm yamekuwa yakifanya unyanyasaji mkubwa kwa raia,wamekuwa wakikamata wananchi hivyo na kuwaweka ndani bila kuwafungulia kesi,na jina la mtu aliyekamatwa tokea siku ya jumatano mpaka Leo hajafunguliwa kesi,wala kufikishwa Mahakamani na hata mawakili wanapoenda kujua hatima yake wanafukuzwa na Polisi.
Polisi wanaingia katika Nyumba vya kulala wageni usiku,kufanya ukaguzi,kinadada wanadhalilika kwakuwa wengine wanakutwa uchi wa mnyama na Polisi wa kiume,huu ni unyanyasaji mkubwa unaofanywa na jeshi la polisi Dodoma.
Sasa tunawaomba vijana wetu wote nchi nzima watulie na wasubirie maamuzi ya kikao kikubwa cha kamati ya Utendaji,kitakachokaa siku ya jumatano ya tarehe 20.07.2016 Kukutana na M/kiti wetu tukiwa tayari na Plan B ya kuipigania Demokrasia ya Taifa letu.
Imetolewa July 16
M/kiti BAVICHA Taifa

KAMATI KUU YA CHADEMA KUKUTANA KWA DHARURA DAR ES SALAAM
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), itakutana kwa dharura, jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, ambapo pamoja na masuala mengine, itapokea taarifa na kujadili hali ya siasa nchini.
Katika siku za hivi karibuni, taifa limekuwa likipitia katika majaribu makubwa, ikiwa ni pamoja na uvunjifu mkubwa wa sheria na taratibu za kuongoza nchi unaofanywa waziwazi na mamlaka za juu/viongozi waandamizi wa nchi kupitia kauli na matendo mbalimbali kiasi cha kuwashtua Watanzania ambao wangependa kuona nchi yao ikiendeshwa katika misingi ya uwajibikaji wa kisheria na demokrasia.
Katika kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24, mwaka huu, Kamati Kuu pia itapokea taarifa na kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu mipango mbalimbali inayoendelea ya kukipanga chama ili kiendelee kufanya shughuli zake kwa ufanisi hususani kinapokwenda kuimarisha misingi kuanzia ngazi ya kitongoji nchi nzima, kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.
Imetolewa Ijumaa, Julai 22, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA

RIPOTI YA 2014 KUHUSU UTAFITI WA UTUMIKISHWAJI WATOTO HADHARANI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi, (wapili kulia), akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika Julai 20, 2016 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014 katika uzinduzi wa matokeo hayo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Azfar Khan akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)
NA MWANDISHI WETU
UTUMIKISHWAJI wa Watoto bado ni tatizo kubwa nchini ambapo kati ya watoto watatu wenye umri wa miaka 5 - 17, mtoto mmoja anafanya kazi ambazo ni hatarishi katika maisha yake kiafya, kimwili na kisaikolojia.
Akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dkt. Abdallah Posi amesema tatizo la utumikishwaji wa watoto bado ni kubwa hapa nchini na hivyo ni wajibu wa jamii kuwekeza katika elimu badala ya kuwaajiri au kuwatumikisha watoto.
“Utumikishwaji wa watoto bado ni tatizo kubwa duniani kote si Tanzania pekee, kwani kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO), asilimia 11 ya watoto wote duniani (watoto milioni 264) wenye umri wa miaka 5 – 17 wanatumikishwa kwenye ajira za aina mbalimbali,” amesema Dkt. Posi.
Dkt. Posi amesema kwa mujibu wa ripoti ya utumikishwaji wa watoto Tanzania wa mwaka 2014/15, watoto wenye umri wa miaka 5 – 17, watoto milioni 4.2 ambao ni sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu umebainisha kuwa, watoto wanafanya kazi zaidi katika sekta za Kilimo, Misitu na Uvuvi ambazo zinaajiri asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi.
Dkt. Chuwa ameongeza kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao (asilimia 58.8) wa siku kujihudumia na usafi binafsi ambapo wasichana wameonekana kutumia asilimia 59.2 na wavulana hutumia asilimia 58.3 kujihudumia.
Aidha, shughuli za kujisomea kwa watoto ni asilimia 15.5 ambapo wavulana wanatumia muda mrefu zaidi kujisomea kwa asilimia 16.4 na wasichana hutumia asilimia 14.6 kujisomea
Subscribe to:
Posts (Atom)