Saturday, June 18, 2016

PICHA MBALIMBALI ZA MAKAMBI YA UNJILISTI MTAA WA KIHESA

KIPINDI CHA NDOA KATIKA MKUTANO WA MTAA WA KIHESA

Mama wa Ndoa katika ufunguzi wake
mama pamoja na Mzee uwagire wakitoa somo la ndoa
kumbuka watoto pia wapo katika maeneo haya
mwalimu wa watoto wakiwa katika darasa lao
hiiii siyoooooooo yakukosaaaaaaaaaa karibu sana katika Mukutano wetu....

UFUNGUZI WA MKUTANO WA WAIJILISTI NDANI YA MTAA WA KIHESA.....

 karibuni sana katika mkutano wa waijilisti ndani ya mtaa wa kihesa

hapo ni kwaya ya ngome wakimba katika ufunguzi wa mkutano

wapo makini sana kwaya ya ngome

mwl. wa kwaya ya ngome bw.Manoko 

washiriki makini katika mkutano makini 

bw.GILDAF katika kinanda siku ya kufungua mkutano




mzee wa kanisa la ngome mzee mtango pamoja na mzee uwagire pamoja na muhubiri mkuu katika mkutano katka ufunguzi wa mkutano 






mass kwaya wakiongozwa na bw.Manoko katika ufunguzi


karibuni katika mahubiri haya kwani Mungu pamoja na watumishi wake wapo hapa katika 

Friday, June 17, 2016

Hospitali ya Amana yaboresha huduma zake



*Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Hospitali ya Rufaa ya Amana Jijini Dar es Salaam imeboresha huduma za afya kwa kuweka mashine maalumu ya kutibu meno ijulikanayo kama (Ceramic dental machine) lengo ikiwa ni kuboresha huduma hizo katika hospitali za umma. Akiongea katika mahojiano kwa njia ya simu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bw.Meshack Simwela ameeleza kuwa kwa sasa wataweza pia kutoa huduma ya afya kwa viongozi wa serikali pamoja na wabunge kupitia wodi maalum iliyotengwa kwa ajili yao ili kupata huduma hiyo wanapokuwa jijini hapa. "Tunaishukuru sana Serikali yet... more »

KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA CHAFANYIKA MVOMERO MKOANI MOROGORO



New Picture (11)Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akihutubia wananachi wa mkoa wa Morogoro  waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Mkoa wa Morogoro katika shule ya Msingi Kigugu, wilaya ya Mvomero
New Picture (12)Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa na kulia ni Bibi Magreth wakipokea maelezo ya mratibu wa chanjo Mvomero kabla ya uzinduzi wa matone ya chanjo kwa watoto wa kata ya Kigugu wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika shule ya Msingi Kigugu Turiani mkoani Morogoro tarehe 16.6.2016.
New Picture (13)Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akikabidhi msaada wa vitabu vilivyotolewa na asasi ya MVIWATA wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na mkoa wa Morogoro katika shule ya Msingi Kigugu, wilayani Mvomero. Kushoto ni Mkuu wa wilya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa akifuatiwa na viongozi wa mradi wa MVIWATA na kijiji cha Kigugu (16.6.2016).
New Picture (14)Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba, wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Bibi Magareth Musai (kulia), na kushoto ni mwenyekiti wa asasi ya MVIWATA Bw. Mgweno wakiwa wamesimama mkabala na jiwe la msingi la maktaba ya Kata ya Kigugu lililozinduliwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika shule ya Msingi Kigugu Turiani, wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro tarehe 16.6.2016.
New Picture (15)Watoto wa Shule ya Msingi Kigugu wilaya ya Movomero, mkoani Morogoro wakiingia uwanjani kwa maandamano wakati wa kilelele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyohudhuriwa na wakazi wa mkoa wa Morogoro katika kijiji cha Kigugu Turiani, mkoani Morogoro, siku ya Tarehe 16.6.2016.
New Picture (16)Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Morogoro mtoto Aprinia M. Joseph, mwanafunzi wa (kidato cha IV) Shule ya Sekondari Mgulasi, akisoma risala ya watoto wa mkoa wa Morogoro kwa Mgeni rasmi Katibu Mkuu, wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Kinga (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani Morogoro yaliyofanyika katika kijiji cha Kigugu,wilaya ya  Mvomero, tarehe Juni 16, 2016.