Saturday, April 9, 2016

Mahakama yatengua ushindi wa Chadema

wananchi
Mahakama yatengua ushindi wa Chadema

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imetengua rasmi matokeo ya udiwani, Kata ya Boma Mbuzi wilayani

Moshi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imetengua rasmi matokeo ya udiwani, Kata ya Boma Mbuzi wilayani hapa yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema, Yudosi Tarimo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Hukumu hiyo imetokana na kesi ya kupinga ushindi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia CCM, Juma Raibu.

Hukumu hiyo iliyotolewa leo na Hakimu Mkazi, Pamela Meena ilisomwa na Hakimu Julieth Maole baada ya kusikiliza pande zote mbili na kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji.

Hakimu Maole alisema katika uchaguzi huo Tarimo alipata kura nyingi dhidi ya Raibu kwa tofauti ya kura moja.

Alisema katika vituo vinane vya kupigia kura vilivyokuwa katika kata hiyo, vilikuwa na tofauti ya matokeo ya udiwani wakati wa kuhesabiwa ikilinganishwa na idadi ya watu waliopiga kura.

ìKwa utofauti huo ulikuwapo ni wazi kwamba katika majumuisho ya kura yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema haukuwa wake kutokana na mgombea wa CCM kuweza kuithibitishia Mahakama,î alisema hakimu huyo.

Raibu alifungua kesi ya kupinga matokeo ya udiwani yaliyompa ushindi Tarimo wa kura 3,512 dhidi ya kura 3,511 alizopata yeye.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo kusomwa, Tarimo alisema hajaridhika na atawasiliana na wanasheria wake ili waweze kukata rufaa kwa madai kuwa, katika uamuzi wake hakimu hakuzingatia ushahidi muhimu aliouwasilisha.

Baada ya hukumu kutolewa mamia ya wafuasi wa CCM waliokuwa wamefurika nje ya Mahakama hiyo walishangilia ushindi wa mgombea wao.

Aliyempiga chenga Magufuli, anaswa TRA

Aliyempiga chenga Magufuli, anaswa TRA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemtia mbaroni mfanyabiashara aliyepiga chenga agizo la Rais
Mkurugenzi wa Elimu kwa WalipaKodi wa TRA,  Richard Kayombo akionyesha mifuko ya sukari ya viwanda vya hapa nchini inayotumika kuwekea sukari iliyoingizwa kinyemela kutoka nje ya nchi. Sukari hiyo imekamatwa katika ghala la kuhifadhia vyakula inayodhaniwa kuwa ni mali ya mfanyabiashara Barakat Salehe anayeishi katika kijiji cha Njia Nne wilayani Kilwa juzi. Picha na Saumu Mwalimu

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemtia mbaroni mfanyabiashara aliyepiga chenga agizo la Rais John Magufuli la kuzuia uingizaji sukari kutoka nje, badala yake akaamua kuingiza shehena ya bidhaa hiyo kwa njia ya magendo.

Mfanyabiashara huyo, Yusuph Barakati Saleh alikamatwa na TRA akidaiwa kumiliki mifuko 896 ya sukari iliyoingizwa nchini kupitia bandari bubu katika Kijiji cha Njianne, Kilwa mkoani Lindi.

Hatua hiyo imekuja takriban miezi miwili baada ya Rais Magufuli kutangaza kwamba hakuna vibali vitakavyotolewa kuruhusu uingizaji wa sukari, ili kuvilinda viwanda vya ndani.

Sukari hiyo iliyoingizwa nchini kutoka India na Brazil, ilikamatwa na timu ya doria ya TRA (Fast) usiku wa kuamkia Jumatano.

Timu ya Fast na Polisi ilibaini shehena hiyo ikiwa  imehifadhiwa katika ghala, sehemu ikiwa imebadilishwa vifungashio na kutumia mifuko yenye nembo za viwanda vya Kilombero, TPC na Mtibwa ili ionekane imezalishwa nchini na kuingizwa sokoni.

Pia ilikuwapo sukari ambayo haikuwa imefungwa kwenye mifuko, bali ilikuwa imerundikwa kwenye turubai ikionekana kulowa maji.

Mwandishi alishuhudia sehemu ya sukari hiyo ikitiririka maji ya rangi ya kahawia, na ilidaiwa kuwa maji hayo yamekuwa yakikusanywa na kuingizwa sokoni kama asali.

Pia katika eneo hilo zilikamatwa bidhaa nyingine ambazo ni katoni 223 za betri za redio aina ya Tiger, katoni 135 za hamira na katoni 48 za sabuni.

Katika ghala jingine ambalo inasadikiwa ndimo shughuli ya kubadilisha vifungashio hufanyika, vilibainika vifaa mbalimbali kama mashine ya kusaga, jenereta, mzani, malighafi za kutengenezea mifuko na mashine za kushonea mifuko hiyo.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema bidhaa hizo zilikamatwa na kikosi hicho cha Fast, ambacho hufanya doria maeneo mbalimbali na kukamata bidhaa za magendo kwa kushirikiana na polisi.

“Kazi hii imetokana na juhudi za wananchi wema ambao wametupa taarifa na kikosi chetu cha Fast kwa kushirikiana na polisi wamebaini kwamba vitu hivi viko hapa,” alisema Kayombo. Alisema ghala hilo liko chini ya ulinzi na mzigo wote ambao umekamatwa utataifishwa na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika.

Kayombo alisema pia ilikamatwa mifuko mitupu 2,000 yenye uwezo wa kujaza kilo 25 kila mmoja na mingine 36, 000 ya kilo 50 kila mmoja.

Alisema pia kuna mifuko 1,150 ya viwanda vya Tanzania iliyotumika ya kilo 25 kila mmoja, madumu matupu ya mafuta ya kula 609 ya lita 20 kila moja na mengine 310 ya ujazo wa lita 10 kila moja.

Akizungumzia athari za bidhaa hizo, Kayombo alisema kuwa ni pamoja na madhara ya kiafya kwa watumiajai na kwa uchumi kwa kuwa Serikali inapoteza mapato.

“Hatuwezi kuwa na uhakika wa ubora wa sukari hii maana itakuwa haijapita Shirika la Viwango (TBS), wala Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA),” alisema Kayombo.

Kayombo alisema TRA inakabiliwa na changamoto kubwa ya kupambana na bidhaa za magendo ambazo huingia kupitia bandari 11 bubu zilizomo wilayani humo.

Bandari hizo ni Kilutu, Kiheli, Sueli, Shuka, Mayungiyungi, Milamba, Mapimbi, Limayao, Kisongo, Kimwera na Nchinga.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho alisema kuwa amemfahamu mfanyabiashara huyo na shughuli hizo tangu mwaka 2008 na amekuwa akishusha mizigo hiyo wakati wowote, huku vijana wakijipatia ajira za muda.

“Huyu jamaa alikuwa hachagui muda wa kuleta mizigo, alikuwa akileta muda wowote, usiku na mchana kwa sababu hapakuwa na mtu wa kumghasi,” alisema mkazi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Alisema mfanyabiashara hiyo amekuwa anawauzia bidhaa hizo wenye maduka na hata wanakijiji wamekuwa wakinunua sukari hiyo.

Mkazi mwingine alisema licha ya kumuona mfanyabaishara huyo akishusha mizigo yake mara kwa mara, alikuwa hajui kama bidhaa hizo ni za magendo.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, anawatangazia vijana wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2016.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, anawatangazia vijana wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2016.

Barua zilizoainisha sifa za kijana kujiunga na mafunzo ya JKT zimetumwa kwa Waheshimiwa Wakuu wa mikoa. Mchakato wa zoezi la kuwapata vijana wenye sifa unaanza Aprili 2016 hadi tarehe 20 Mei 2016.

Sifa za mwombaji ni kama zifuatazo:-

1. Awe raia halisi wa Tanzania.

2. Umri. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la saba hadi kidato cha sita ni miaka 18 hadi 23.Vijana wenye elimu ya Stashahada umri ni miaka 18 hadi 26 na Vijana wenye elimu ya Shahada na kuendelea umri ni miaka 18 hadi 30.

3. Awe na afya njema, akili timamu.

4. Asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).

5. Mwenye tabia nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

6. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2010, 2011, 2012, 2013 na 2014 wenye ufaulu ufuatao:-

      (a) Waliomaliza 2010 hadi 2012 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 32.

      (b) Waliomaliza 2013 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 38.

      (c) Waliomaliza 2014 wawe wamefaulu na wawe na GPA isiyopungua 0.6.

7. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.

8. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).

9. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate)

10. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate/Transcript).

11. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.

12. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.

13. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo..

Waombaji wenye sifa wapeleke maombi yao kwa Waheshimiwa wakuu wa mikoa. Makao Makuu ya JKT hayatapokea na hayapokei maombi yoyote, kwa vijana watakaoomba nafasi hizo wazingatie maelekezo yatakayotolewa kuepuka usumbufu.

Friday, April 8, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AREJEA NYUMBANI APRIL 7,2016 KUTOKA NCHINI RWANDA IKIWA NI SAFARI YAKE YA KWANZA NJE YA NCHI TANGU ACHAGULIWE KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AREJEA NYUMBANI APRIL 7,2016 KUTOKA NCHINI RWANDA IKIWA NI SAFARI YAKE YA KWANZA NJE YA NCHI TANGU ACHAGULIWE KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Leave a reply

1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili April 7, 2016.

3 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016.

4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange huku Inspekta jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu akisubiri zamu yake  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili April 7, 2016

5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Msajili wa vyama vya Siasa Mhe Jaji Francis Mutungi mara baada ya kutua  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili  April 7, 2016.

6 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili April 7, 2016.

7

8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili  April 7, 2016

TANZANIA: UDHIBITI WA SILAHA ZA MAANGAMIZI UNAHITAJI UTASHI WA KISIASA

TANZANIA: UDHIBITI WA SILAHA ZA MAANGAMIZI UNAHITAJI UTASHI WA KISIASA
Na Mwandishi  Maalum
Wakati Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kuhusu upokonyaji wa  silaha za maangamizi  zikiwamo za  nyukilia kushindwa kwa miaka  kumi na tano kuwasilisha taaria ya mapendekezo ya kina kuhusu utekelezaji wa jukumu hilo, Tanzania kwa upande wake imeungana na  mataifa mengine   katika kutoa wito wa  kuhakikisha kwamba silaha  za maagamizi haziangukii  mikononi mwa magaidi na makundi mengine hatari.

Jana Jumatatu, Kamisheni kuhusu ukoponyaji wa  silaha,   imeanza mkutano wake wa wiki mbili ambapo   washiriki wanajadiliana na  kubadilishana mawazo kuhusu dhima ya upokonyaji wa silaha za maangamizi na masuala mengine yahusianayo na silaha.

Akichangia majadiliano  katika siku ya kwanza ya mkutano , Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, amesema, utashi wa kisiasa unahitajika  hasa kutoka kwa nchi ambazo  zinamiliki  silaha za  nyukilia  na  silaha ninyingine za maangamiii ili  kuifanya dunia   iendele kuwa mahali salama.

Akabainisha kwamba kutonyesha nia ya kweli ya kudhibiti malimbikizo ya silaha hizo na, kwa Kamisheni kutowasilisha mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa   ripoti yake  kwa kipindi cha miaka  kumi na tano sasa ni wazi kwamba  kunatoa mwanya  wa silaha hizo kuangukia mikononi mwa makundi ya kigaidi na mengineyo.

Ni katika kuliongopa hilo  Tanzania kupitia kwa mwakilishi wake, Balozi  Manongi imeeleza kwamba   hoja ya kwamba kwa nchi kumiliki silaha za maangamizi zikiwamo za nyukilia kunazifanya   nchi hizo kuwa na  nguvu  lakini pia kujenga mazingira ya  Amani kuwa haina tija  wala matinki yoyote.

“ Suala la upunguzaji  wa silaha za nyukilia  na  silaha nyingine za maangamizi ni  jambo linaloitia wasi wasi mkubwa nchi yangu, ni wazi kwamba hatari zitokanazo na nyukilia ziwe kwa  bahati mbaya,  za kimkakati au  kukosewa kwa mahesabu siyo tu kunaitishia dunia  lakini pia na wanadamu”. akasema Balozi na kuongeza kwamba “ Tanzania  inaendelea kuikata ile dhana kwamba kwa namna moja silaha ya nyukilia zinatoa dhamana ya uwepo wa  Amani. Kwa upande wetu hatujawahi kujihisi tukiwa na Amani kwa misingi ya  kwamba  silaha hizo amana zinamilikiwa na  rafiki  zetu au washirika  wao.

Balozi Manongi ametahadharisha kuwa ,  katika  mazingira ya sasa ambapo  pamekuwapo na ongezeko  kubwa la  makundi yasiyo ya kiserikali yanayotaka kuzipindua serikali halali, hakuna uhakika kwamba makundi hayo  hayawezi kugeukia mbinu zozote zile ambazo zinaweza kuingia mikononi mwao.

Kuhusu  Kamisheni ya   Umoja wa Mataifa kutowasilisha  ripoti yoyote mbele ya  Baraza Kuu    kwa miaka  kumi na  tano,  Balozi Manongi asema. Kamisheni hiyo haiwezi kukwepa majukumu yake   na hasa kama inataka  kuendelea kujijenga uhalali.

“Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa,  limetoa wito wa kuitaka  Kamisheni ifanye tathmini  na kutoa  mapendekezo kuhusu matatizo mbalimbali katika eneo  hili la upokonyaji wa silaha, na  kutoa  maamuzi ya utekelezaji. Mapendekezo ya  Kamisheni kwa Baraza Uuu  yanatakiwa kutekelezwa na huu ni wajibu wa msingi wa Kamisheni”. akasisitiza Balozi Manongi.

Pamoja  na  mapungufu kwa upande wa Kamisheni,  Tanzania imesema bado na  Imani   na Kemisheni hiyo na inaitambua  kama chombo pekee  halali na  chenye maamuzi  katika Umoja wa Mataifa kuhusu  upunguzaji wa silaha za  maangamizi.

Awali akizungumza  mwanzoni mwa mkutano wa Kamisheni, Mwakilishi  Maalum  wa Masuala ya  upokonyaji wa silaha,  Bw. KIM  won-soo, pamoja na  mambo mengine alikiri kwamba   Kamisheni ilikuwa inaingia katika kipindi  kingine ambapo  kuna mgawanyiko  mkubwa  miongoni wa  jumuiya ya kimataifa kuhusu upokonyaji wa silaha za nyukilia na silaha nyingine za maangamizi.

Akasema kila mjumbe anafahamu kuhusu mgawanyiko huo. Ambao  umejidhihirisha wazi kuanzia mkutano wa majereo kuhusu Mkataba wa upunguzaji  na usambazaji wa silaha za nyukilia ( NPT) uliofanyika mwaka jana,  kushindwa kuanza kwa utekelezaji wa mkataba  unaozuia majaribio ya silaha za nyukilia, na kutokuwapo kwa mwendelezo wa majadiliano katika  mkutano kuhusu upunguzaji wa silaha.

Hata hivyo na kama ilivyokuwa kwa wajumbe wengine, Bw. KIM  won –soo alionyesha matumaini yake kwa Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kuhusu  upunguzaji wa silaha za nyukilia  za  maangamizi  na kwamba wajumbe wake wakifanya kazi  kwa pamoja na  ushirikiano  na bila kutiliana mashaka hapata kuwa na sababu ya  kuwenda kutafuta njia mbadala nje ya Umoja wa Mataifa.

Magufuli Ndani ya Rwanda.

ay, April 7, 2016
RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI SHUGHULI ZA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI (KWIBUKA) KIGALI NCHINI RWANDA

Na Mwandishi Maalumu, RWANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameungana na wananchi wa Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takribani milioni 1.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika eneo la Gisozi Mjini Kigali, yalipo makumbusho ya mauaji ya Kimbari ambapo Rais Magufuli na Mkewe wakiwa na mwenyeji wao Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mkewe Mama Janeth Kagame wameweka shada la mauaji katika eneo walipouawa idadi kubwa ya wananchi wa Rwanda na pia wakawasha mwenge wa matumaini kwa walionusurika katika mauaji hayo na kwa Taifa zima la Rwanda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na Mkewe Janeth Kagame na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasha mwenge wa matumaini kuashiria kutotokea tena kwa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame wakisikiliza historia ya jinsi mauaji ya kimbari yalivyotokea katika eneo la kumbukumbu ya mauji hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame wakiwa wamesimama kutoa heshima kwa watu waliofariki katika mauaji hayo ya kimbari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiangalia kwa uchungu mafuvu ya watu waliopoteza maisha katika mauaji hayo ya kimbari.
............................................................
Pamoja na kupata historia ya mauaji hayo ya kimbari, Rais Magufuli akiongozwa na mwenyeji wake Rais Kagame ametembelea jumba maalum lililohifadhi kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha, ambapo amepata maelezo kutoka kwa wahifadhi wa makumbusho hiyo, na pia kujioonea picha na mabaki ya mifupa na mafuvu ya binadamu waliouawa.

Akizungumza mara baada ya kutembelea jumba hilo la makumbusho Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kusema tukio hilo halipaswi kurudia.

"Haitatokea tena, hatuwezi kubadilisha yaliyopita lakini tunaweza kubadilisha mambo ya sasa na yajayo, mauaji haya hayapaswi kutokea tena" Amesema Rais Magufuli.

Wageni mbalimbali waliofika kwenye kumbukumbu hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha za watoto waliouwawa kinyama katika eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari  Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu katika Jengo la makumbusho ya mauaji ya Kimbari Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu chenye maelezo mbalimbali kuhusu mauaji hayo ya kimbari.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimpokea Rais Magufuli katika viwanja vya Gishozi kabla ya kwenda kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya watu waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Rais Magufuli pamoja na Mama Janeth Magufuli, Janeth Kagame wakielekea kwenye makaburi ya halaiki katika makumbusho ya mauaji ya Kimbari, Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Rais Magufuli ambaye aliingia nchini Rwanda jana tarehe 06 April, 2016 ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie Madarakani Tarehe 05 Novemba, 2015 ameondoka Mjini Kigali jioni hii na kurejea Jijini Dar es salaam.