Wednesday, May 18, 2016

Mwana Chuo Mzumbe ajifungua mtoto na kumuua kwenye ndoo

Mwanafunzi wa chuo cha mzumbe ajifungua salama mtoto kamuua na kumuweka kwenye ndoo kisha akapoteza maisha muda mfupi baada ya kutokwa na damu nyingi na kukosa msaada. Jamani tijitahidi sana sana kuongea na watoto wetu na kuwafundisha pia tuwaombee kila siku. Mungu awalinde watoto wote hapa duniani awaepushe na mabaya yote Amen

CUF NA CCM WAANZA KUBAGUANA KWENYE HUDUMA ZA KIJAMII VISIWANI ZANZIBAR, CCM WABAGULIWA KATIKA MADUKA NA MABASI

CUF NA CCM WAANZA KUBAGUANA KWENYE HUDUMA ZA
KIJAMII VISIWANI ZANZIBAR, CCM WABAGULIWA KATIKA
MADUKA NA MABASI
Pemba. Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid amefunga maduka matatu ya
rejareja na kusimamisha magari ya abiria kati ya Wete na Mtambwe kwa madai ya kutoa
huduma kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa.
Wafanyabiashara waliofungiwa ni Said Juma Seif, Titi Juma Othman wa Mtambwe na
Hamad Haji wa Mchangamdogo.
Alisema wafanyabiashara hao wamelalamikiwa na wafuasi wa CCM, wakiwatuhumu
kukataa kuwahudumia kutokana na itikadi zao za vyama.
Rashid alisema baada ya kufanya uchunguzi, walibaini kuwa wafanyabiashara hao
wanawabagua wanaCCM.
“Tumelazimika kuyafungia maduka hayo matatu baada ya Serikali ya Wilaya kujiridhisha
kwamba yanawabagua wanachama wa CCM,” alisema.
Akizungumzia hatua hiyo, Haji aliitaka Serikali kufanya uchunguzi kwanza kabla ya
kuchukua hatua akisema hahusiki na masuala ya kisiasa. Alisema hizo ni chokochoko za
wabaya wake.
Usafiri wasitishwa
Mkuu huyo wa wilaya, aliagiza kuzuiwa kwa magari yote ya kubeba abiria kwenye
Barabara ya Wete – Mtambwe kwa madai hayohayo ya kuwabagua wanaCCM.
Alisema mbali ya hatua hiyo, atawasiliana na wizara husika ili kuchukua hatua kwa
wahusika kwa kukiuka leseni.
Hata hivyo, haikufahamika mara moja kama zuio hilo alilosema ni la muda usiojulikana
litayahusu magari ya Ruti B ambayo leo ndiyo yaliyotarajiwa kutoa huduma kwani
yaliyozuiwa jana kwenda Mtambwe, nyumbani kwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ni
ya Ruti A.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wete, Mmanga Juma Ali alisema katika
utekelezaji wa agizo hilo hakutakuwa na huruma: “…Hatutaishia hapo wanaofanya
ubaguzi huo watafikishwa mahakamani.”
Hata hivyo, baadhi wa wahuduma wa vyombo vya usafiri walisema si wao
wanaowashusha, bali ni wananchi na kwamba dereva na konda hawawezi kufanya hivyo
kwa kuwa lengo lao ni kutafuta faida.
Maalim Seif atema cheche
Wakati uongozi wa Wete ukichukua hatua hiyo, Maalim Seif ameendelea na ziara yake
visiwani hapa aliwataka Wazanzibari kuonyesha kuwa wanaikataa Serikali ya Dk Ali
Mohamed Shein.
Akizungumza na watendaji na viongozi wa CUF wa Wilaya ya Micheweni, Kaskazini
Pemba, Maalim Seif aliwataka kutomtegemea yeye pekee kufanya hivyo.
“Tukikazana, Serikali hii itaondoka, ikiwa mnangoja Maalim Seif au Marekani kuiondoa,
kwa sheria ya kimataifa haitawezekana kwani Marekani haiwezi kuingilia mambo ya ndani
ya Zanzibar,” alisema
Makamu huyo za zamani wa Rais wa Zanzibar, alijitoa kwenye uchaguzi wa marudio
uliofanyika Machi 20 ambao Dk Shein aliibuka kidedea.
Uchaguzi huo ulikuwa wa marudio baada ya ule wa Oktoba 25 kufutwa na Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha siku ambayo alikuwa atangaze
matokeo yote.
Katika mkutano huo, Maalim Seif alisema Serikali ya CCM imeanza kutikisika kutokana na
vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na wahisani pamoja na hatua ya chama chake CUF
kutowatambua viongozi wake pamoja na Serikali. “CCM wajue wamekalia kuti kavu, siku
yoyote wataanguka... tufanye kazi mpaka haki yetu tuhakikishe imerudi na wenzetu
hawana safari ya kudumu,” alisema.
Aliwataka wanachama wake kuonyesha kwa vitendo kutoitambua Serikali ikiwamo
kukataa kulipishwa kodi za ovyovyo pamoja na kujitenga na viongozi wa Serikali katika
utekelezaji wa majukumu yao.
“Mfano tunaweza kuamua siku fulani kuanzia saa sita, tunasimamisha vyombo vyote vya
usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonyesha hatuitaki
Serikali ya CCM,” alisema huku akishangiliwa na umati uliofurika katika ofisi za chama
hicho.
CUF yajipanga kwenda ICC
Alisema kuna mwanasheria mzalendo ambaye ameanza kukusanya vielelezo mbalimbali
kabla ya kufungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC dhidi ya viongozi wenye
dhamana ya kusimamia vyombo vya ulinzi na usalama wa raia.
Alisema tayari Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano, wamepewa notisi ya kuarifiwa kufunguliwa
mashtaka ICC kutokana na vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu uliofanyika
Zanzibar.
CCM yamjibu
Akizungumzia kauli za Maalim Seif, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
alisema chama chake hakina muda wa kujibizana na CUF baada ya kumalizika kwa
uchaguzi na kwamba watakutana tena majukwaani na chama hicho kwenye uchaguzi wa
2020.
Baraza la wawakilishi kesho
Wakati hayo yakiendelea Baraza la Wawakilishi linatarajiwa kuanza kesho Chukwani, nje
kidogo ya mji wa Unguja.
Macho na masikio ya wananchi yataelekezwa katika Muswada wa Sheria ya Mafuta na
Gesi ambao unaweza kutegua kitendawili cha rasilimali hiyo kubaki ndani au nje ya
Muungano.
Katibu mpya wa Baraza hilo, Raya Issa Msellem alisema muswada huo utasomwa kwa
mara ya kwanza na wajumbe watapata nafasi ya kuuchangia.MWANANCHI

MAMA MZAZI ATUMIWA PICHA YA VIDEO YA NGONO YA BINTI YAKE AKIBAKWA NA MWANAUME NYUMBA YA KULALA WAGENI

MAMA MZAZI ATUMIWA PICHA YA VIDEO YA NGONO YA
BINTI YAKE AKIBAKWA NA MWANAUME NYUMBA YA
KULALA WAGENI
Dar es Salaam. Mama mzazi wa binti mmoja mkazi wa Dakawa wilaya ya Mvomero
mkoani Morogoro hivi karibuni alipokea ujumbe wa picha ya video katika simu yake ya
mkononi na haraka aliifungua akiwa na shauku ya kuitazama.
Lahaula! Shauku yake ya kuitazama video hiyo aliyodhani ni sawa na nyingine za matukio
ambazo amekuwa akiziona zikisambazwa mitandaoni, iligeuka huzuni na fedheha kubwa
alipoona ikimwonyesha bintiye akidhalilishwa na wanaume huku akilalamika asirekodiwe
bila mafanikio.
Mama huyo alijizoazoa haraka na simu yake akatimua mbio hadi Polisi kuripoti tukio hilo
lililolenga kumdhalilisha binti yake na kuifedhehesha familia nzima. Hicho ndiyo kiini cha
vijana 11 wa Dakawa kukamatwa ili waisaidie Polisi kuhusu walioshiriki tukio hilo na
walioisambaza video hiyo kwa mama huyo na kwenye mitandao ya kijamii hasa
WhatsApp.
Katika video hiyo, wakati mwanamme mmoja akimdhalilisha huyo binti, mwingine
alikuwa akirekodi na baada ya kukamilisha tendo hilo lisilo na utu tena bila huruma
waliwatumia watu wengine katika eneo la Dakawa.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa aliliambia gazeti hili jana kuwa miongoni
mwa watu wa kwanza kuona video ile alikuwa mama wa msichana. “Alikimbia polisi
kwenda kutoa taarifa,”alisema Betty.
Baada ya kufika Polisi, Betty alisema polisi walimwambia mama huyo hawawezi
kuandika maelezo hadi mhusika ambaye ni binti yake afike kituoni. Walisema hivyo kwa
sababu ni mtu mzima hivyo anatakiwa kutoa maelezo mwenyewe. Saa chache baada ya
kuandikisha maelezo yake, polisi waliwakamata vijana wawili kwa tuhuma za kuhusika na
unyama huo. Betty alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na leo watafikishwa
mahakamani.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na kwamba hadi jana watuhumiwa
11 walikamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Kamanda Matei alisema tisa kati yao wanaoshikiliwa ni kwa kosa la kusambaza picha za
utupu huku vijana wawili ambao ni Zuberi Thabiti (30) na Iddy Adamu (32) ni kwa kosa
la kufanya mapenzi na msichana huyo kwa nguvu huku wakirekodi.
Ilivyokuwa
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walifanya kitendo
hicho Aprili 28 mwaka huu majira ya saa 1.00 usiku katika nyumba ya kulala wageni
yenye jina la ‘Titii’ iliyopo Dakawa.
Kamanda Matei alisema kuwa binti huyo aliitwa kwenye nyumba hiyo ya wageni na
Thabiti ambaye ni mkazi wa Mbarali wilaya ya Mbeya ambaye alikuwa na uhusiano naye
kimapenzi. Baada ya kuingia chumbani alimkuta pia Adamu mkazi wa Makambako,
Njombe ambao walimlazimisha kufanya mapenzi huku mmoja akimrekodi picha za video
na baadaye kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Wanaoshikiliwa kwa kosa la kusambaza picha za utupu ni Rajabu Salehe (26), Said
Athman (26), Musi Ngai (36), Said Muhammed (24), John Peter (24), Hassan
Ramadhan (27), Ramadhan Ally (26), Lulu Peter (38) na Magreth Njonjone (30).
Wote ni wakazi wa Dakawa, Morogoro na wamevunja Sheria ya Makosa ya Mitandao,
kifungu namba 14, kifungu kidogo (1) (a)
Kamanda Matei alisema wakati wa tukio hilo watuhumiwa hao walimtisha binti huyo kwa
kisu ili asipige kelele wakati akidhalilishwa na walimtaka asitoe siri hiyo vinginevyo
watamuua.
Kamanda alisema wawili hao ni marafiki wa msichana huyo na kwamba Thabiti ambaye
ni mpenzi wa sasa wa msichana huyo alipanga na Adamu ambaye ni mpenzi wake wa
zamani kumkomesha.
Alisema Thabiti alimwambia mpenzi wake wakutane hotelini. Msichana alipofika
aliwakuta chumbani huku Adamu akiwa ameshika kisu na kamera. “Wakamlazimisha
afanye vile na kumtishia kumuua kama angekataa,”alisema Matei.
Hata hivyo, Betty alisimulia kisa hicho na kusema watuhumiwa hao walifanya unyama
huo kwa sababu ya usaliti wa mapenzi. Alisema msichana alidaiwa kujihusisha kimapenzi
na dereva wa mpenzi wake.
Kwa mujibu wa Betty, baada ya mpenzi wake kugundua alipanga njama ili kuwakomoa
wote wawili. Alisema mpenzi wake alimwambia wakutane hotelini na alipofika alimkuta
Zuberi pamoja na dereva wa mchumba wake hotelini.
“Akawambia wafanye kile kitendo huku akirekodi video,”alisema Betty. “Nia yake ilikuwa
kuwakomoa…kwa nini atembee na dereva wake,”alisema Betty na kwamba baada ya
hapo picha hizo zilianza kusambaa.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),
Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hali hiyo inaonyesha jinsi maadili yanavyozidi
kuporomoka katika jamii.
“Hilo siyo kosa la kisheria peke yake ni udhalilishaji mkubwa,”alisema.
Dk Hellen alisema licha ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu kukemea suala hilo ni vyema jamii ikazingatia suala la maadili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Edda
Sanga alisema vyama vya kutetea haki za wanawake vinafanya mkutano wa pamoja
kujadili suala hilo.
“Leo (jana) tumekutana ili tujadili na kuja na tamko la pamoja,”alisema Sanga na
kuongeza kwamba jambo hilo halivumiliki kwa sababu vitendo kama hivyo vinaendelea
kujitokeza mara kwa mara.MWANANCHI

BAVICHA wamvaa Rais Magufuli, Jaji Mkuu

BAVICHA wamvaa Rais Magufuli, Jaji Mkuu
BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) limemtaka Rais John Magufuli kuacha
kuingilia bunge na kuamuru nini kijadiliwe, anaandika Pendo Omary.
Limefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa
Bunge kuagiza kuondolewa baadhi ya vipengele katika Hotuba ya Godbless Lema
ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Mambo ya
Ndani.
Vipengele hivyo vilihusu; mauaji ya viongozi wa kisiasa, mkataba tata wa Lugumi,
uuzwaji wa nyumba za serikali, Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, sakata la vitambulisho vya
taifa (Nida), mwenendo wa rais, kashfa ya ununuzi wa rada na bunge kulinda
walarushwa.
Katika mkutano na waandishi wa habari leo kwenye Makao Makuu ya chama jijini Dar es
Salaam, Julius Mwita, Katibu Mkuu BAVICHA amesema, “vipengele katika hotuba ya
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – Wizara ya Mambo ya Ndani vililazimika kuondolewa
bungeni kwa sababu ya Rais John Magufuli.
“Tunashuhudia Rais Magufuli ndio anaongoza bunge kutoka Ikulu. Baadhi ya wabunge
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapigiwa simu na kutishwa akiwemo Livingstone
Lusinde, Mbunge wa Mtera.
“Hata spika na naibu spika wanapata maelekezo ya kuendesha bunge kutoka kwa rais.
Hotuba hii tutaendelea kuisambaza hadi kila mtu aisome,” amesema Mwita.
Mwita amesema, kutajwa kwa Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani kudaiwa
kuwa mbia wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited, iliyoingia mkataba tata na Jeshi
la Polisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. 35 Bilioni, ni sababu tosha ya
waziri huyo kuwajibika au Rais Magufuli kutengua uteuzi wake ili kuipa uhuru Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuchunguza mkataba huo.
“Tunajua wazi bunge lingekubali mkataba wa Lugumi ujadiliwe kungemuingiza Kitwanga
kwenye mgogoro. Rais Magufuli ni swahiba wa Kitwanga. Jipu la Lugumi limeonekana
kuwa mwiba. Tunamtaka Rais Magufuli achukue hatua,” amesema Mwita.
Aidha, Mwita amemtaka Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu kufuta kauli ya kusifia
Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 aliyoitoa hivi karibuni nchini Uingereza
alipokuwa akizungumza na Watanzania waishio huko kuhusu faida na hasara za sheria
hiyo.
“Kazi ya jaji yoyote sio kusifu sheria. Anapaswa kutafsiri sheria kwa msingi wa Katiba.
Tunamtaka Jaji Mkuu aondoe tamko hilo haraka. Litasababisha majaji wengine kushidwa
kutafsiri sheria hiyo la sivyo tutaitisha “petition” nchi nzima kupinga suala hili. Sisi vijana
ndio tunaoumia na sheria hii kuliko makundi mengine,” amesema Mwita.
Katika mkutano huo Mwita aliongozana na Emmanuel Masonga, Mwenyekiti BAVICHA
Mkoa wa Njombe na Edward Simbeye, Mwenezi BAVICHA.

Liverpool, Sevilla zatinga fainali ya UEFA Europe League

Liverpool, Sevilla zatinga fainali ya UEFA Europe
League
Michezo miwili ya marudiano ya Ligi ya Vilabu Barani Ulaya (UEFA
Europe League) imechezwa usiku wa Alhamisi ambapo vilabu vya
Liverpool ya Uingereza na Sevilla ya Hispania wamefuzu kucheza
mchezo wa fainali.
Liverpool ilikuwa mwenyeji wa Villarreal ambapo iliibuka na ushindi wa
goli 3-0, magoli ya Liverpool yakifungwa na Bruno Soriano ambaye
alijifunga dk. 7, Daniel Strurridge dk. 63 na Adam Lallana dk. 81 hivyo
kufuzu kwa ushindi wa goli 3-1.
Mchezo mwingine ilikuwa ni Sevilla ambayo ilikuwa mwenyeji wa
Shakhtar Donetsk na Sevilla kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ya
Sevilla yalifungwa na Kevin Gameiro dk. 9, 47 na Mariano dk. 59 na
goli la kufutia machozi la Shakhtar Donetsk likifungwa na Eduardo na
hivyo kufuzu kwa ushindi wa goli 5-3.
Baada ya matokeo hayo, Liverpool na Sevilla zitapambana katika
mchezo wa fainali.

Tuesday, May 17, 2016

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA, RAJABU LUHWAVI ATEMBELEA SHINA LA CCM USAGARA, TANGA LEO, APELEKA FASTA KERO ZA WANACHAMA WA SHINA HILO KWA MKUU WA MKOA

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA, RAJABU LUHWAVI ATEMBELEA SHINA LA CCM USAGARA, TANGA LEO, APELEKA FASTA KERO ZA WANACHAMA WA SHINA HILO KWA MKUU WA MKOA

RORYA
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajabu Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kata ya Usagara Mashariki, Ramadhani Makange, alipowasili kwenye Shina namba kumi, Tawi la Usagara Mashariki mkoani Tanga, kusikiliza kero za wananchi na wachama wa CCM katika shina hilo leo
 Wanachama wa CCM Shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wakimshangilia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipowasili kwenye shina hilo wilaya ya Tanga mjini, leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiwa na Mwenyekiti wa Shina namba kumi, tawi la CCM la Usagara Mashariki wilaya ya Tanga mjini, Abubakar Manyoka (kulia) na  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Usagara Mashariki Ramadhani Makange (kushot), alipowasili kwenye shina hilo leo kusikiliza kero za wanachama akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama wilaya ya Tanga mjini.
 Baadhi ya wanachama wa shina namba kumi tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga mjini, wakiwa tayari kumsikiliza naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi 
Mwenyekiti wa Shina namba kumi, tawi la CCM, Usagara Mashariki, Abubakari Manyoka akifungua kikao cha tawi hilo, kabla ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi kuzungumza na wanachama wa tawi hilo, lililopo wilaya ya Tanga Mjini leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Usagara Mashariki Ramadhani Makange
 Mwenyekiti wa shina namba kumi, tawi la CCM, Usagara Mashariki, Abubakar Manyoka, akimkabidhi taarifa iliyosheheni kero zinazowahusu wanachama wa shina hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza na wanachama wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga Mjini leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Usagara Mashariki Ramadhani Makange na kulia ni Mwenyekiti wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga Mjini Abubakar Manyoka
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza na wanachama wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga Mjini leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Usagara Mashariki Ramadhani Makange na kulia ni Mwenyekiti wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga Mjini Abubakar Manyoka
 Wanachama wa shina namba kumi, Tawi la CCM Usagara Mashariki, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, rajab Luhwavi alipozungumza nao kusikiliza akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama katika wilaya ya Tanga Mjini, leo. 
 Mmoja wa wanachama wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga mjini, akitoa dukuduku na kero zinazowakabili wanachama wa CCM wa shina hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Rajab Luhwavi alipozungumza na wanachama wa tawi hilo leo
 Mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mafunzo ya Chama katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Frank Uhahula akieleza namna ya kupata ufumbuzi wa baadhi ya changamoto ambazo wanachama wa shina namba kumi tawi la CCM Usagara Mashariki, walimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi alipozungumza nao leo akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama katika wilaya ya Tanga Mjini.
 Mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mafunzo ya Chama katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Frank Uhahula akieleza namna ya kupata ufumbuzi wa baadhi ya changamoto ambazo wanachama wa shina namba kumi tawi la CCM Usagara Mashariki, walimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi alipozungumza nao leo akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama katika wilaya ya Tanga Mjini.
 Diwani wa Kata ya Usagara Mashariki Carlos Hiza, akimwambia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajabu Luhwavi kero zinazowakabili wananchi, alipozungumzana wanachama wa CCM Shina namba kumi, tawi la CCM la Usagara Mashariki katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama katika wilaya ya Tanga mjini leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Baa, Rajab Luhwavi akiongozana na baadhi ya wanachama wa CCM shina namba kumi tawi la CCM Usagara Mashariki, kwenda kushiriki msiba wa Mama wa  mmoja wa wanachama wa CCM anayeishi katika eneo la shina hilo, Mwalimu Tajiri, baada ya kuzungumza na wanachama wa CCM wa shina hilo leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa Mama wa mmoja wa wanachama wa CCM shina namba kumu tawi la Usagara Mashariki wilaya ya Tanga mjini, Mwalimu Tajiri, wakati wa kwenda mazikoni leo.
 Mmoja wa wanachama wa CCM kutoka shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki wilaya ya Tanga mjini Mwalimu Tajiri akifarijiwa wakati wa msafara wa kwenda mazikoni kuzikwa mama yake mzazi leo

LUHWAVI ATINGA KWA MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA KUWASILISHA KERO ZA WANACHAMA WA SHINA NAMBA KUMI, TAWI LA CCM USAGARA
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akikabirishwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella, baada ya kuwasili kwenye Ofisi wa mkuu wa mkoa huyo, kuwasilisha kero za Wananchi, baada ya kuzungumza na wanachama wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama wilaya ya Tanga mjini leo.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella akimpeleka Ofisini kwake, Luhwavi. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiwasili ndani ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha Wagemi katika Ofsi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga baada ya kuwasili na ujumbe wake katika ofisi hiyo leo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela
 Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela akifurahi baada ya kukabidhiwa risara yeneye kero za wananchi na wanachamawa CCM Shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki, na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi
 LUhwavi akiwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela kabla ya kuondoka.
 Luhwavi akiagana na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela kabla ya kuondoka
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela kabla ya kuondoka Tanga, kwenda mkoani Kilimanjaroleo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimuaga Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela kabla ya kuondoka Tanga, kwenda mkoani Kilimanjaroleo.  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO. Picha nyingine za Luhwavi kutembelea shina namba tisa Kitongoji cha Reli Chini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro leo:>BOFYA HAPA

Kipindi cha Jukwaa Langu May 16 2016. Ziara ya Waziri mkuu UK. Uraia pacha by John Bukuku on May 17, 2016 in JAMII with No comments Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London

Kipindi cha Jukwaa Langu May 16 2016. Ziara ya Waziri mkuu UK. Uraia pacha

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London

Serikali yakanusha kuhusu Mashine za kukoboa mpunga na mahindi Halmashauri ya Kahama kufanya kazi saa 24.

Serikali yakanusha kuhusu Mashine za kukoboa mpunga na mahindi Halmashauri ya Kahama kufanya kazi saa 24.

DSCN3456Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
SERIKALI imekanusha madai kuhusu mashine za kukoboa mpunga na mahindi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama kufanya kazi wakati wa usiku au saa 24.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salome Makamba ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali kuviruhusu Viwanda Wilayani Kahama kufanya kazi masaa 24 ili kufidia uzalishaji uliokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokatika wakati wa mchana.
Akijibu swali Mhe. Jafo amesema kuwa, Serikali haijatoa zuio lolote kwa Halmashauri hiyo kwa mashine za kukoboa nafaka kufanya kazi nyakati za usiku ambapo amefafanua kuwa changamoto iliyopo ni kwamba viwanda hivyo vinatumia umeme wa jenereta ambao umekuwa hautoshelezi kuendesha mashine wakati wote hali iliyopelekea kuwepo kwa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
“Halamshauri imewasiliana na Meneja wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) Kahama na yatari tatizo hilo limeanza kushughulikiwa ili kupata umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa ambapo tayari kituo cha usamabazaji kimeanza kujengwa Kahama”, alisema Mhe. Jafo.
Ameongeza kuwa, Halmashauri wilayani hapo inahamasisha Wawekezaji wa viwanda vidogo vikiwemo vya kukoboa mpunga, mahindi pamoja na mazao mengine ili kupanua wigo wa mapato kupitia ushuru wa huduma (Service Levy) na ajira kwa vijana.
“Hakuna sababu yoyote kwa Serikali kuzuia wawekezaji katika viwanda vidogo na vikubwa, azma ya serikali ni kupanua uwekezaji wa viwanda kadri iwezekanavyo kwa kuzingatia fursa zilizopo, tunachofanya ni kuboresha mazingira yatakayosaidia uwekezaji huo kufanyika kwa faida ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unakuwepo.

TFF yatakiwa kusimamia ligi kwa ustadi

TFF yatakiwa kusimamia ligi kwa ustadi

wamburaNa Beatrice Lyimo – MAELEZO
Dar es Salaam
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Issaya Mwita ameiomba shirikisho la Michezo wa mpira wa miguu nchini (TFF) kuendelea kusimamia ligi kwa ustadi kulingana na ratibu na taratibu za mpira wa miguu kama zililivyoanishwa na Shirikisho la Soka Duniani( FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF).
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa Mstahiki Meya huyo inasema kuwa TFF inatakiwa kusimamia ligi hiyo ili kuainisha, kubainisha, kutajirisha na hatimae kutatua changamoto husika na kuwa na kiwango stahiki katika msimu unaofuata ukilinganisha na changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita.
Aidha, ameipongeza klabu ya Yanga Africans Football Club kwa kunyakua ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya ishirini na sita(26) tangu kuanzisha kwa mashindano ya ligi kuu Tanzania yajulikanayo kama Vodacom Premier League.
Alifafanua kuwa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam inaiomba klabu hiyo kuthamini ubingwa wao kwa kuonyesha viwango vya kimataifa ili kufanya jiji kuwa chuo cha mafunzo ya michezo wa mpira miguu, bila kuridhika na kiwango walichonacho.
Mbali na hayo alitoa wito kwa wadau wa mchezo wa  mpira wa miguu kushirikiana ipasavyo ili kufanya ligi ya Tanzania iwe miongoni mwa ligi bora Barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Serikali za Vijiji zakumbushwa kusimamia Sheria ya Ardhi.

Serikali za Vijiji zakumbushwa kusimamia Sheria ya Ardhi.

indexNa Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
…………………………………….
SERIKALI za Vijiji nchini zimekumbushwa kusimamia vizuri Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999 ambayo imeweka utaratibu wa kufuata kwa mtu anayehitaji kupata ardhi kwa matumizi mbalimbali.
Agizo hilo limetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Chemba, Mhe. Juma Nkamia ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali wa kufuta uamuzi uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara wa kuwazuia wakulima ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa, tamko lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara liliwahusu wakulima waliokuwa wavamizi katika eneo la hifadhi ya Wanyamapori ya Makame kutoka katika Wilaya za Kiteto, Babati, Chemba, Kondoa na Mkoa wa Iringa waliokuwa wanaendesha shughuli za kilimoi katioka hifadhi hiyo kinyume cha Sheria.
Amefafanua kuwa, uamuzi huo ulitolewa kufuatia azimio la kikao cha pamoja cha Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya za Kiteto cha Chemba kilichokaa tarehe 12 Novemba, 2015.
“Kikao hicho kilishirikisha viongozi wa Vijiji vitano vinavyounda Mamlaka ya Hifadhi (WMA) ambavyo ni Ngobolo, Katikati, Ndedo, Irkiushbor na Makame pamoja na wawakilishi wa wakulima 10 kutoka kila Wilaya”, alisema Mhe. Jafo.
Aidha, kwa mujibu wa Sheria, hairuhusu shughuli yoyote ya kibinadamu ikiwemo kilimo, ufugaji au makazi kuendeshwa katika hifadhi.
“Naomba kutoa wito kwa wananchi kuzingatia Sheria za nchi ili kuepuka migogoro katika jamii, Serikali za vijiji zinakumbushwa kusimamia vizuri Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999 ambayo imeweka utaratibu wa kufuata kwa mtu anayehitaji kupata ardhi kwa matumizi mbalimbali, lengo ni kuzuia migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima ambayo kwa sehemu kubwa inatokana na kutozingatiwa kwa Sheria za ardhi”, alisema Mhe. Jafo.

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU ISUJA WA DODOMA

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU ISUJA WA DODOMA

rorya 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo la Dodoma , Beatus Kinyaiya katika mazishi ya Askofu Mstaafu wa Dodoma Mathias Isuja yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa   Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Aprili 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja  katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa  Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba,  Aprili  20, 2016.

BUNGENI DODOM

BUNGENI DODOM

rorya 

Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  kuongoza kikao cha kwanza cha  mkutano wa tatu wa Bunge   Aprili 19, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Waziri Kiongozi  wa Zanzibar  Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2016.

ZIARA YA MAJALIWA KWENYE JIMBO LAKE LA UCHAGUZI LA RUANGWA

ZIARA YA MAJALIWA KWENYE JIMBO LAKE LA UCHAGUZI LA RUANGWA 

rorya.

Waziri Mkuu,KassimMajaliwa akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa kuhutubia mkutano wa hadhara Aprili 10, 2016.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa (jina halikupatikana) akimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara  kijijini hapo, Aprili 10, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mwendesha pikipiki maarufu na hodari, Zaina Amour wa kijiji cha Nandagara wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi  wakizungumza   na mwendesha pikipiki maarufu na hodari, Zaina Amour wa kijiji cha Nandagara wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016.Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KATIKA VIWANJA VYA KOLOLO JIJINI KAMPALA MEI 12,206

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KATIKA VIWANJA VYA KOLOLO JIJINI KAMPALA MEI 12,206

1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
6Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala
9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala
10 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
11Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa wa Sudani Kusini Salva Kir mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
13 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya tukio la uapisho.