Tuesday, July 5, 2016

Rais Magufuli atengua leo hii na kufanya uteuzi mwingine.......

Rais Magufuli atengua na kufanya uteuzi mwingine leo July 05 2016

Taarifa niliyoipokea kutokea ikulu inasema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.


Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB.


Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu⦁ Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri⦁ Dkt. Razack B. Lokina⦁ Bi. Rose Aiko⦁ Prof. Joseph Bwechweshaija⦁ Bw. Said Seif Mzee⦁ Dkt. Arnold M. Kihaule⦁ Bw. Maduka Paul Kessy⦁ Bw. Charles SingiliUteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo July 5 2016.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA MITATU NA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA ZOTE 139 JUNE 26,2016


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza majina ya Wakuu wapya wa Wilaya zote nchini 139 pamoja na mabadiliko ya wakuu wa Mikoa watatu uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam June 26, 2016
            TAARIFA KAMILI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
  1. Arusha           -           Mrisho Mashaka Gambo
  2. Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti
  3. Ngorongoro  -           Rashid Mfaume Taka
  4. Longido         -           Daniel Geofrey Chongolo
  5. Monduli         -           Idd Hassan Kimanta
  6. Karatu                        -           Therezia Jonathan Mahongo


DAR ES SALAAM
  1. Kinondoni     –           Ally Hapi
  2. Ilala                –           Sophia Mjema
  3. Temeke         -           Felix Jackson Lyaviva
  4. Kigamboni     -           Hashim Shaibu Mgandilwa
  5. Ubungo          -           Hamphrey Polepole

DODOMA
  1. Chamwino     –           Vumilia Justine Nyamoga
  2. Dodoma        -           Christina Solomon Mndeme
  3. Chemba         -           Simon Ezekiel Odunga
  4. Kondoa          –           Sezeria Veneranda Makutta
  5. Bahi                -           Elizabeth Simon
  6. Mpwapwa      -           Jabir Mussa Shekimweli
  7. Kongwa          -           John Ernest Palingo

GEITA
  1. Bukombe      -           Josephat Maganga
  2. Mbogwe         -           Matha John Mkupasi
  3. Nyang’wale     -           Hamim Buzohera Gwiyama
  4. Geita               -           Herman C. Kipufi
  5. Chato             -           Shaaban Athuman Ntarambe

IRINGA
  1. Mufindi          -           Jamhuri David William
  2. Kilolo             -           Asia Juma Abdallah
  3. Iringa              -           Richard Kasesela

KAGERA
  1. Biharamulo   -           Saada Abraham Mallunde
  2. Karagwe         -           Geofrey Muheluka Ayoub
  3. Muleba          -           Richard Henry Ruyango
  4. Kyerwa           -           Col. Shaban Ilangu Lissu
  5. Bukoba          -           Deodatus Lucas Kinawilo
  6. Ngara             -           Lt. Col. Michael M. Mtenjele
  7. Missenyi         -           Lt. Col Denis F. Mwila

KATAVI
  1. Mlele              -           Rachiel Stephano Kasanda
  2. Mpanda         -           Lilian Charles Matinga
  3. Tanganyika    -           Saleh Mbwana Mhando

KIGOMA
  1. Kigoma           -           Samsoni Renard Anga
  2. Kasulu                        -           Col. Martin Elia Mkisi
  3. Kakonko       -           Col. Hosea Malonda Ndagala
  4. Uvinza                        -           Mwanamvua Hoza Mlindoko
  5. Buhigwe         -           Col. Elisha Marco Gagisti
  6. Kibondo        -           Luis Peter Bura

KILIMANJARO
  1. Siha                -           Onesmo Buswelu
  2. Moshi             -           Kippi Warioba
  3. Mwanga         -           Aaron Yeseya Mmbago
  4. Rombo           -           Fatma Hassan Toufiq
  5. Hai                 -           Gelasius Byakanwa
  6. Same              -           Rosemary Senyamule Sitaki

LINDI
  1. Nachingwea   –           Rukia Akhibu Muwango
  2. Ruangwa        -           Joseph Joseph Mkirikiti
  3. Liwale             -           Sarah Vicent Chiwamba
  4. Lindi               -           Shaibu Issa Ndemanga
  5. Kilwa              -           Christopher Emil Ngubiagai


MANYARA
  1. Babati             -           Raymond H. Mushi
  2. Mbulu                        -           Chelestion Simba M. Mofungu
  3. Hanang’         -           Sara Msafiri Ally
  4. Kiteto              -           Tumaini Benson Magessa
  5. Simanjiro       -           Zephania Adriano Chaula

MARA
  1. Rorya              -           Simon K. Chacha
  2. Serengeti        –          Nurdin Hassan Babu
  3. Bunda             –          Lydia Simeon Bupilipili
  4. Butiama         -           Anarose Nyamubi
  5. Tarime           -           Glodious Benard Luoga
  6. Musoma        -           Dkt. Vicent Anney Naano

MBEYA
  1. Chunya          -           Rehema Manase Madusa
  2. Kyela              -           Claudia Undalusyege Kitta
  3. Mbeya                        –           William Ntinika Paul
  4. Rungwe          -           Chalya Julius Nyangidu
  5. Mbarali          -           Reuben Ndiza Mfune

MOROGORO
  1. Gairo              -           Siriel Shaid Mchembe
  2. Kilombero     -           James Mugendi Ihunyo
  3. Mvomero       -           Mohamed Mussa Utali
  4. Morogoro      -           Regina Reginald Chonjo
  5. Ulanga                        -           Kassema Jacob Joseph
  6. Kilosa             -           Adam Idd Mgoyi
  7. Malinyi           -           Majula Mateko Kasika

MTWARA
  1. Newala           -           Aziza Ally Mangosongo
  2. Nanyumbu    -           Joakim Wangabo
  3. Mtwara           -           Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
  4. Masasi                        -           Seleman Mzee Seleman
  5. Tandahimba-           Sebastian M. Walyuba

MWANZA
  1. Ilemela           -           Dkt. Leonald Moses Massale
  2. Kwimba          -           Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
  3. Sengerema     -           Emmanuel Enock Kipole
  4. Nyamagana    -           Mary Tesha Onesmo
  5. Magu              -           Hadija Rashid Nyembo
  6. Ukerewe        -           Estomihn Fransis Chang’ah
  7. Misungwi       -           Juma Sweda

NJOMBE
  1. Njombe          -           Ruth Blasio Msafiri
  2. Ludewa                      -           Andrea Axwesso Tsere
  3. Wanging’ombe          -           Ally Mohamed Kassige
  4. Makete                       -           Veronica Kessy

PWANI
  1. Bagamoyo      -           Alhaji Majid Hemed Mwanga
  2. Mkuranga      -           Filberto H. Sanga
  3. Rufiji               -           Juma Abdallah Njwayo
  4. Mafia              -           Shaibu Ahamed Nunduma
  5. Kibaha           -           Asumpter Nsunju Mshama
  6. Kisarawe        -           Happyness Seneda William
  7. Kibiti               -           Gulamu Hussein Shaban Kifu

RUKWA
  1. Sumbawanga-           Dkt. Khalfan Boniface Haule
  2. Nkasi              -           Said Mohamed Mtanda
  3. Kalambo        -           Julieth Nkembanyi Binyura

RUVUMA
  1. Namtumbo    -           Luckness Adrian Amlima
  2. Mbinga           -           Cosmas Nyano Nshenye
  3. Nyasa             -           Isabera Octava Chilumba
  4. Tunduru        -           Juma Homela
  5. Songea           -           Polet Kamando Mgema

SHINYANGA
  1. Kishapu         -           Nyambonga Daudi Taraba
  2. Kahama         -           Fadhili Nkulu
  3. Shinyanga      -           Josephine Rabby Matiro


SIMIYU
  1. Busega           -           Tano Seif Mwera
  2. Maswa                        -           Sefu Abdallah Shekalaghe
  3. Bariadi           -           Festo Sheimu Kiswaga
  4. Meatu             -           Joseph Elieza Chilongani
  5. Itilima             -           Benson Salehe Kilangi


SINGIDA
  1. Mkalama       -           Jackson Jonas Masako
  2. Manyoni        -           Mwembe Idephonce Geofrey
  3. Singida           -           Elias Choro John Tarimo
  4. Ikungi             –           Miraji Mtaturu
  5. Iramba           -           Emmanuel Jumanne Luhahula

SONGWE
  1. Songwe           -           Samwel Jeremiah
  2. Ileje                -           Joseph Modest Mkude
  3. Mbozi             -           Ally Masoud Maswanya
  4. Momba          -           Juma Said Irando


TABORA
  1. Nzega             -           Geofrey William Ngudula
  2. Kaliua             -           Busalama Abel Yeji
  3. Igunga                        -           Mwaipopo John Gabriel
  4. Sikonge          -           Peres Boniphace Magiri
  5. Tabora           -           Queen Mwashinga Mlozi
  6. Urambo         -           Angelina John Kwingwa
  7. Uyui                -           Gabriel Simon Mnyele

TANGA
  1. Tanga             -           Thobias Mwilapwa
  2. Muheza          -           Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
  3. Mkinga           -           Yona Lucas Maki
  4. Pangani          -           Zainab Abdallah Issa
  5. Handeni        -           Godwin Crydon Gondwe
  6. Korogwe        -           Robert Gabriel
  7. Kilindi                        -           Sauda Salum Mtondoo
  8. Lushoto         -           Januari Sigareti Lugangika

Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA GATES FOUNDATION MELINDA GATES PAMOJA NA KUWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 29,2016 Leave a reply1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe

Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo.2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam3  4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Zainab Telack kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es Salaam5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Mlingwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wapya wa Wilaya mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya watatu wa Mkoa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu kutoka kushoto, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakwanza kushoto.DSC_9479Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam11Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wateule wakila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam 

HOTUBA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MARA BAADA YA KUWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA MITATU JUNE 29, 2016 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA RWANDA MHE PAUL KAGAMEA JULAY 01,2016


1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
3cc2f933-1527-49f0-b66b-1403be649696 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
4c8ac4c6-2dff-49bd-8ffc-431ea6239279Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.
5c8d0e50-d0a2-4916-9f19-f42484ad0a49Rais wa Rwanda Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere
8a80f98b-082c-4107-9acb-eff7191e3fc2

f4c2ff8c-d96d-4867-b3dd-49676bdb9c5cRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.
83f285fe-9960-4171-a83b-e0fada18b417Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
62c36e90-7d99-4f89-bf57-1bf38c399472Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam
3b669abe-5ec5-43e5-8184-051218980984Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
906d1b60-3fc4-47ea-8341-8980265c4ae5Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME NA MWENYEJI WAKE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFURI JULY 1,2016


1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam.
2 Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wageni mbalimbali katika dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
b3ff6130-dc8c-46bb-ac8a-be2c9e4a779b Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
bafab001-c53e-4dda-a103-10a8edf2ea52

bf16a6e9-319e-42e0-a9bb-2219d3daa1c9


8d8a9af6-a6e4-4ec4-b42d-e3d6fe0df90bRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame, Kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
8d354df4-2d8c-4a1a-9b5a-231c17e224a1 Kijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha mama Janeth Magufuli katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
18925452-2561-4758-b650-3b20a37f0dcfKijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha Rais Dkt. john pombe magufuli  mara baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuondoka kwenye viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam.

HOTUBA YA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ALIYOITOA WAKATI ZIARA YA RAIS WA RWANDA MHE PAUL KAGAME ALIYOIFANYA TANZANIA JULY 01,2016