Tuesday, July 19, 2016

BAVICHA WATOA TAMKO TENA JUU YA KIKAO CHA CCM DODOMA.

Taarifa kwa umma na waandishi wa habari

Ndugu waandishi wa habari kwanza tunawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa kuwaeleza Watanzania adhima yetu ya kwenda Dodoma, katika kuhakikisha BAVICHA tunaisimamia kauli Jeshi la Polisi na ya Mhe. Raisi, na kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote hadi mwaka 2020 tukianza na mkutano haramu wa CCM hapo tarehe 23 July 2016.

Tunaendelea na msimamo wetu kuamini mkutano huo sio halali,kwakuwa ni Mkusanyiko wa Kisiasa ambao Mhe. Raisi na Jeshi la Polisi waliikataa vinginevyo watoke hadharani kukanusha Agizo na msimamo wao ulioathiri tayari vyama vya upinzani vikiwemo CHADEMA na ACT kwa kuzuiwa kukutana.

Sisi BAVICHA tunaheshimi kauli ya Kiongozi wetu mkuu wa chama,aliyotuomba tusiende Dodoma, kauli hii imeipa nafuu kubwa CCM kwakuwa hawakuwa na ubavu wa kutuzuia tusizuie mkutano wao.

Tulijipanga kila kona ya nchi hii,na hata jeshi la Polisi lisingeweza kutuzuia katika kutekeleza azima yetu,ya kutaka haki na usawa wa Kidemokrasia katika nchi hii ya Kidemokrasia.

Sasa basi,baada ya M/kiti kutuomba vijana wake tusiende Dodoma, sasa tunaamua kuja na plan B,ambapo hatutaenda Dodoma lakini hatutaruhusu mkutano wa CCM ufanyike mpaka pale Serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za Kidemokrasia kwa kila chama,kufanya siasa maana hivi tunavyoongea CCM wao wanafanya mikutano ya hadahara na wengine wanazuiwa.

Tunayo taarifa ya Baadhi ya mawaziri na wabunge wa CCM wao wanafanya mikutano ya hadhara katika majimbo mbali mbali,na picha za matukio hayo tunazo kwa ushahidi hivyo tukashitaki wapi?

Tunazo taarifa za Wakuu wa wilaya wakifanya mikutano ya hadhara na wanachi,hivi kati ya mkuu wa wilaya na vyama vya siasa nani mwenye mamlaka ya kufanya siasa!??

Tunaomba Watanzania waone na wapaze sauiti jinsi nchi yao inavyoongozwa Kidikteta,na kukosa usawa.Leo Dodoma kumepelekwa Polisi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Singida,Dar es salaam na Iringa wakiwa na kila aina ya Vifaa vya kivita.

Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Polisi wengi wasio na Idadi wakiwa na silaha nzito za kivita wanaenda kulinda mkutano wa Kisiasa,hii haijawahi kutokea.

Mtakumbuka Polisi wamewahi kuzuia mikutano mingi sana ya CHADEMA kwa kigezo kutokea machafuko na hali ya usalama ni ndogo,lakini hii imekuwa tofauti sana kwa upande wa Ccm wao usalama ni mdogo sana kupita maelezo katika mkutano wao wa tarehe 23 July,lakini vimepelekwa mpaka vifaru vya jeshi kuimarisha usalama.

Hii ni double standard ya hali ya juu,inayooneshwa na jeshi la Polisi kwa vyama vya siasa na huwa mara nyingine tunasema Polisi wanatumika na Ccm na huu ni ushahidi wa kwanza mkubwa kabisa.

Polisi wa nchi hii wako radhi wao wafe lakini Ccm isiguswe na wapo radhi hata kuua wapinzani ili Ccm iendelee kuwa madarakani,uko wapi usawa wa Kidemokrasia??? Uko wapi weledi wa kiutendaji wa jeshi letu la Polisi?.

UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINADAMU.

Tokea BAVICHA tumatangaza kwenda Dodoma, majeshi yaliyopelekwa Dodoma kuisaidia Ccm yamekuwa yakifanya unyanyasaji mkubwa kwa raia,wamekuwa wakikamata wananchi hivyo na kuwaweka ndani bila kuwafungulia kesi,na jina la mtu aliyekamatwa tokea siku ya jumatano mpaka Leo hajafunguliwa kesi,wala kufikishwa Mahakamani na hata mawakili wanapoenda kujua hatima yake wanafukuzwa na Polisi.

Polisi wanaingia katika Nyumba vya kulala wageni usiku,kufanya ukaguzi,kinadada wanadhalilika kwakuwa wengine wanakutwa uchi wa mnyama na Polisi wa kiume,huu ni unyanyasaji mkubwa unaofanywa na jeshi la polisi Dodoma.


Sasa tunawaomba vijana wetu wote nchi nzima watulie na wasubirie maamuzi ya kikao kikubwa cha kamati ya Utendaji,kitakachokaa siku ya jumatano ya tarehe 20.07.2016 Kukutana na M/kiti wetu tukiwa tayari na Plan B ya kuipigania Demokrasia ya Taifa letu.

TAARIFA MPYA KUHUSU MKUTANO MKUU MAALAUM WA CCM UTAKAOFANYIKA JULAI 23, 2016 MJINI DODOMA


Friday, July 15, 2016

WANAWAKE WAFUGA NYUKI KUOKOA MISITU YA PUGU NA KAZIMZUMBWI


Maofisa wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake wa Afrika (WAF) Anna Salado na Alicia (kushoto) wakipata maelezo ya fugaji nyuki katika msitu wa hifadhi wa Pugu.

BALOZI WILSON MASILINGI ZIARANI SEATTLE JIMBO LA WASHINGTON

Balozi wa Tanzania nchi ni Marekani muheshimiwa Wilson Masilingi yupo ziarani katika jimbo la Washington alipata fursa ya kuzungumza na jumuiya ya watanzania waishio hapo ambapo alieleza mikakati ya ziara hiyo ni kupanua Milango ya kibiashara Kati ya Tanzania na Marekani kutokana na kuwa jimbo la Washington ni moja ya majimbo ambayo ni makao makuu ya makampuni makubwa duniani 


Katika Ziara hiyo alitembelea kiwanda cha ndege cha Boeing na kupanga mikakati ambayo serikali ya awamu ya tano inatarajia kununua ndege mbili za kisasa ili kufufua shirika la air Tanzania ,pia alipata nafasi ya kutembelea Microsoft na kampuni ya Starbucks ambayo inaendesha migahawa mikubwa ya kahawa duniani. Balozi Huyo alimaliza mazungumzo yake kwa kukutana na Chama cha wafanyabiashara cha Seattle .

Ziara hizo ni moja mikakati ya serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika kupunguza matumizi ya serikali kusafirisha viongozi kutoka Tanzania kuja kufanya mazungumzo badala ya kutumia Mabalozi na wawakilishi waliopo kwenye nchi hizo
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa kwenye mkutano na Watanzania Seattle jimbo la Washington nchini Marekani siku ya Jumamosi July 16, 2016. Habari na Picha na Katunda Catunda Mwakilishi wa Vijimambo Seattle, WA
katibu wa jumuiya ya watanzania Seattle (Tanzaseattle) Hajji Rajab Hajji akimkaribisha balozi
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiongea kwenye mkutano na Watanzania Seattle jimbo la Washington nchini Marekani siku ya Jumamosi July 16, 2016.
Wakati wa chakula.
 Watanzania Seattle wakifuatilia mkutano na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi  siku ya Jumamosi July 16, 2016.
 Mkutano ukiendelea.
Watanzania Seattle wakimsikiliza katibu wa Jumuiya ya Watanzania Hajji Rajab Hajji alipokua akimkaribisha Mhe. Balozi.
 Mkutano ukiendelea

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKUBALI OMBI LA RAIS FILIPE NYUSI WA MSUMBIJI KUSHIRIKI MAZUNGUMZO YA AMANI NCHINI MSUMBIJI


Monday, July 18, 2016
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji.

Ujumbe huo uliwasilishwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe Maalum wa Rais Nyusi Meja Jenerali Mstaafu Mariano de Araujo Matsinhe ambaye aliongozana na Mshauri wa Diplomasia wa Rais Nyusi, Kanali Manuel Mazuze, Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Monica Patricip Clemente Mussa na Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini Rachide Usualle.

Katika Ujumbe huo, Rais Nyusi amemuomba Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kushiriki mazungumzo ya amani nchini Msumbiji, ambapo Dk. Kikwete amekubali.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na ujumbe wa Rais Filpe Nyusi uliofika kuwaslisha ujumbe maalum jijini Dar es Salaam jana

RAIS JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMRI MKUU DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JULAI 18,2016


1..Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi DCP na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam.
2Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kedmon Andrew Mnubi akila kiapo cha Ahadi ya uadilifu pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
3

3.Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mwamini Marco Rwantale akila kiapo cha Ahadi ya uadilifu pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
4Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisaini hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
5Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Frasser Rweyemamu Kashai akisaini hati hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam
6Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo vya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na Naibu Kamishna wa Polisi DCP mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula kiapo cha Maadili ya Watumishi wa umma Ikulu jijini Dar es Salaam.
9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagawia vitafunwa wageni mbalimbali waliofika Ikulu kwa ajili ya kushuhudia Maafisa wa Polisi walipondishwa vyeo wakati wakila kiapo.
10Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagawia vitafunwa baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
11 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Polisi waliokula kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam.
13Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda akizungumza kabla ya kiapo hicho cha Ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA MAAFISA WA JESHI LA POLISI ALIOWAPANDISHA VYEO VYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DCP NA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI (SACP) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JULAI 18,2016