Monday, June 19, 2017

Victor makotieno atema cheche IPTL

Uamuzi wa ICSID kuhusu IPTL mshindi Ni Tanzania

Septemba 12, 2016 Mahakama ya Usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji iliwasilisha rasmi maamuzi yake Kwa pande zilizokuwa kwenye mgogoro kuhusu mradi wa kufua umeme Nchini, IPTL. Mahakama hiyo iliamuru kwamba Benki ya Standard Chartered ya Hongo Kong ( SCB-HK ) ilipwe dola za Kimarekani 148 milioni sawa na Fedha za Kitanzania shilingi 320 bilioni. Mahakama hiyo Pia imeamuru kuwa kuchotwa Kwa Fedha kutoka akaunti maalumu ya TEGETA Escrow hakukuondoa Haki ya ya Benki ya SCB-HK kwenye kampuni ya IPTL na hivyo kisheria kwamba Benki hiyo Kwa sasa ndio mwenye uhalali wa shughuli zote za IPTL.

Ilinichukua Siku takribani 2 kusoma na kusoma tena tuzo hii (Award ) ili kuweza kuielewa haswa maana yake Kwa Nchi yetu. Ikumbukwe kwamba niliongoza Kamati ya Bunge iliyoagiza uchunguzi wa sakata la TEGETA Escrow Account na kuandaa Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC iliyosomwa na kukubaliwa rasmi na Bunge na kupitisha maazimio 8 yaliyopaswa kutekelezwa na Serikali. Baada ya kuisoma Kwa kina Tuzo hiyo ya ICSID nilichoona Ni kwamba masuala Yale Yale ambayo PAC iliyafafanua Bungeni Mwezi Novemba mwaka 2014 ndio hayo hayo yaliyopelekea tuzo hiyo. Kwa maana hiyo Ni kwamba iwapo Serikali ingetekeleza Maazimio ya Bunge yote Leo hii tungekuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kulimaliza suala Hilo kabisa na kuachana kabisa na mgogoro huu ambao unanyonya Fedha za Watanzania.

Kuna masuala makuu 2 ambayo yakieleweka suala la kashfa ya IPTL litakuwa limeeleweka na maamuzi yanaweza kufanyika kumalizana nalo.

1. baada ya mbia ya kampuni ya Mechmar kufilisika nchini Malaysia, Ni Nani mwenye Haki na Mali za IPTL?
2. Tozo ya malipo ya umeme uliozalishwa na IPTL ilizidishwa? 
Kwenye Taarifa ya Kamati ya PAC tulionyesha Kwa vielelezo na ushahidi kwamba kampuni ya PAP haikuwa ina umiliki wa kihalali wa asilimia 70 ya Hisa za IPTL. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alionyesha dhahiri kuwa vyeti vya Hisa ( shares certificates ) za kampuni ya Mechmar kwenye IPTL walikuwa nazo Benki ya SCB-HK Kama dhamana ya mkopo waliowapa IPTL. CAG aliziona hati hizo Kwa macho yake kwenye uchunguzi wake ambao ndio uliotumika na PAC kufikia maazimio 8 ya Bunge.

Vile vile Kamati ya PAC ilionyesha Kwa ushahidi kuwa PAP hawakufuata sheria za Tanzania katika kumiliki IPTL ikiwemo kwamba walikwepa kodi kupitia kampuni iliyoitwa PiperLink ya British Virgin Island. TRA walikiri mbele ya Kamati kuwa wakati Mahakama Kuu inatamka kuwa PAP wapewe ' masuala ( affairs ) ya IPTL ) hawakuwa na uhalali wa kufanya Biashara Tanzania kwani hawakuwa wamepewa kibali na Kamishna Mkuu wa Kodi cha kuthibitisha utwaaji wao wa kampuni ya IPTL. Hivyo Kamati ililiambia Bunge kuwa PAP ni matapeli wa Kimataifa waliopiga ganzi Mfumo wa Serikali ya Tanzania Kwa kutumia rushwa na hivyo kuhalalishiwa umiliki wa IPTL ili kuchota Fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya TEGETA Escrow Benki Kuu ya Tanzania.

Hata Gavana wa Benki Kuu alipowaomba PAP uhalali wa wao kumiliki IPTL walichotoa ni kitu kinachoitwa Deed of Assignment badala ya shares certificates. Watanzania watakumbuka kuwa Deed of Assignments ndizo zilizotumika kuiba Benki Kuu kwenye wizi wa EPA mwaka 2004-2005. Jambo la kushangaza Ni kwamba karatasi hiyo ya kugushi ilikubaliwa na hivyo Bwana Harbinder Singh Seth wa PAP akaruhusiwa kuchota mabilioni ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Kwa mujibu wa Mwanasheria wa TANESCO Bwana Richard Rweyongeza TANESCO waliilipa PAP $245m Sawa na shilingi 530 bilioni. Itakumbukwa kuwa wakati PAC inasoma Taarifa yake Fedha hizo zilikuwa tshs 306 bilioni tu.

Katika tuzo yake ICSID imethibitisha kuwa PAP hakuwa mmiliki wa IPTL na hivyo alilipwa Fedha za TEGETA Escrow kimakosa. Hoja hii imethibitisha Hoja ya PAC na Bunge la Tanzania ambayo ilipingwa vikali na Serikali ya wakati huo ambayo iligeuka mtetezi wa PAP. Uamuzi wa ICSID kwamba TANESCO wailipe SCB-HK unathibitisha kuwa PAP alipewa Fedha za TEGETA escrow kitapeli.

Baada ya kumaliza hoja hiyo twende Hoja ya pili; je Hata Kama PAP wangekuwa Ni Wamiliki halali wa IPTL walilipwa ziada?

Itakumbukwa kwamba PAC ililiambia Bunge kuwa mgawo wa Fedha ulipaswa kusubiri kukokotoa kanuni za mgawo ambazo ziliamriwa na Mahakama hiyo ya ICSID. Hoja kubwa ya PAC ilikuwa ' Ni Kwanini tulifanya haraka kutoa Fedha kabla ya Uamuzi wa kiwango gani kilipwe? '. Hoja hii ndio iliyochagiza kuwa mule ndani ya TEGETA escrow kulikuwa na Fedha za umma. Uamuzi wa kukokotoa ukatolewa Mwezi Februari mwaka 2014 lakini katika mjadala mzima wa sakata la TEGETA escrow Serikali ilikataa kata kata kutekeleza Uamuzi huu. Hata kwenye Hoja za TANESCO mahakamani huko hawakuwa kabisa na Hoja kulinda Uamuzi ule. Hata hivyo ICSID imeamua kuwa tulikuwa tunaliwa Kwa kulipa tozo kubwa zaidi ya kiwango tulichopaswa kulipwa. Hii maana yake Ni kwamba Hata kwenye hizo za wizi tuliilipa PAP zaidi ya tulichopaswa kuwalipa.
Katika magazeti ya Leo wakili aliyeiwakilisha TANESCO anasema " tulibishania Hoja ya kulipa Kwa viwango vya zamani ikaamuriwa hesabu zifanyike upya Mahakama iliamuru hesabu zifanyike upya Kwa kutumia mkopo wa wana Hisa ". Hii ndio Hoja ambayo PAC iliijenga Kwa muda mrefu na kubezwa na Serikali ndani ya Bunge Kwa mbwembwe zote. Wakili wa TANESCO anaendelea " kutokana na hesabu hizo gharama ilikuwa chini. IPTL ililipwa zaidi hivyo inatakiwa kurejesha Dola za Marekani zaidi ya milioni 100 Kwa TANESCO ".

Hii ndio ilikuwa Hoja ya PAC ambayo ilitokana na maagizo ya CAG kwamba TANESCO wakae chini na SCB-HK kupiga hesabu upya. Hoja hii ilikataliwa na Serikali na TANESCO wenyewe ilipotolewa na PAC lakini Leo mwanasheria wa TANESCO aliyeiwakilisha TANESCO katika Mahakama ya Usuluhishi ya ICSID anakiri tuliwalipa zaidi IPTL.

Jambo la kushangaza Ni kwamba, licha ya ushindi huu mkubwa Kwa Tanzania na TANESCO wanasheria wanataka tukate rufaa. Magazeti ya Serikali ya Dailynews na habari leo ndio yameongoza na habari hiyo. Ikumbukwe kuwa magazeti hayo ndio Siku zote yamekuwa yakiitetea pap na Bwana Seth. Ni dhahiri kuwa ama wanasheria wanataka waendelee kulipwa Fedha kwenye kesi au kuna shinikizo kubwa kutoka Kwa wanaofadika na mchezo huu wa kutapeli ili waendelee kufisadi Nchi. Uamuzi huu wa ICSID unatuweka kwenye nafasi nzuri sana ya kulimaliza kabisa suala la IPTL kwani umetuonyesha kuwa;
1)Kwa miaka yote ya uwepo wa IPTL tumekuwa tunapigwa Kwa kulipa capacity charges Mara mbili ya kiwango tulichopaswa kulipa
2)Tulitapeliwa na Bwana Seth kupitia kampuni ya PAP ambayo Wamiliki wake wengine 50% mpaka sasa hawajulikani Ni kina Nani licha ya kuwajua Kwa jina la Simba Trusts ya Australia.  

Wakati wanasheria na baadhi ya maofisa wa Serikali waliofadika na mgawo wa TEGETA escrow wanataka kukata rufaa wanajua kuwa maamuzi ya ICSID hayana rufaa Kwa mujibu wa Ibara ya 53 ya mkataba wa ICSID ( no appeal except those provided for in the ICSID Convention ). Hadhi  yake Ni Sawa na maamuzi ya Mahakama ya juu kabisa ya Tanzania Kwa mujibu wa Ibara ya 54 ya mkataba wa ICSID ( convention ). Hata hivyo maamuzi hayo yanaweza kuombewa kufutwa Kwa kutumia Ibara ya 52(2) Kwa sababu maalumu ambazo Ni

a). Baraza la Usuluhishi halikuundwa kisheria ( properly constituted ). Ijulikane kuwa Baraza hili huteuliwa na washiriki wa kesi. SCB-HK waliteua msuluhishi wao, TANESCO waliteua wao na Kwa pamoja wakateua Rais wa Baraza. Hivyo TANESCO hawana Hoja maana Hata msuluhishi waliteua wao kakubaliana na maamuzi haya ya tuzo hii.
b). Kwamba Baraza lilienda nje ya mamlaka yake. TANESCO walishiriki mwanzo mwisho na hawakuwa na malalamiko kuhusu Hilo wanawezaje kuwa na malalamiko sasa. Hata msuluhishi wao kakubali maamuzi haya.
c). Kwamba kulikuwa na rushwa kwenye kufikia maamuzi haya. TANESCO wanaweza kutoa ushahidi Kama Hata msuluhishi waliyemteua wao alihongwa!
d) kwamba tuzo haina sababu za kufikia maamuzi haya. Kwa walioisoma tuzo hii wanajua kuwa sababu zipo kinagaubaga kabisa.

Kwa maoni yangu kutaka kesi iendelee Ni kutaka kulinda maslahi ya wanaofadika na suala zima la IPTL. Suala hili sasa liishe. Nchi imeshaliwa sana. Itoshe.

Ushauri wangu Kwa Serikali Ni Kama ifuatavyo

1. Kutekeleza tuzo hii ya ICSID bila kusita
2. Kuiamrisha kampuni ya PAP kurejesha Fedha zote za ziada ilizolipwa kutoka akaunti ya TEGETA escrow. Kwa mujibu wa tuzo hii Ni jumla ya tshs 202 bilioni
3. Kuitaka kampuni ya PAP kuilipa Benki ya SCB-HK kutokana na hati iliyowasilisha Benki Kuu kwamba madai yeyote yakitokea katika IPTL PAP ndio watalipa ( indemnity ).
4. Kuchunguza na kuishtaki PAP na Bwana Harbinder Singh Seth Kwa utapeli na utakatishaji wa Fedha Kwa mujibu wa sheria za Tanzania
5. Kuchunguza na kuwashitaki maofisa wote wa Serikali walioshirikiana na Seth kuchota Fedha Benki Kuu
6. Kuilipisha faini Benki ya StanBic Tanzania Kwa kushiriki kwenye vitendo vya kutakatisha Fedha kufuatia miamala ya TEGETA escrow
7. Kufunga kabisa suala la IPTL Kwa kuvunja mkataba na kuitwaa mitambo Kwa mujibu wa sheria za Tanzania

Natumai kuwa watu wenye nafasi za Uongozi wa umma ambao maamuzi Yao yamefikisha Nchi hapa watachutama na kuondoka katika Uongozi wa umma. Tumefikishwa hapa na wizi na tamaa za watu madalali wa matapeli. Ninaamini kuwa Rais John Pombe Magufuli hatakubali Nchi hii kuendelea kupigwa na matapeli.

Victor makotieno
Rorya
19/06/ 2017

Thursday, June 8, 2017

Ushahidi wa Boss FBI wamtesa Trump

Ushahidi wa Boss FBI wamtesa Trump

Baraka...
Kamati ya Bunge la Seneti la masuala ya usalama nchini Marekani imechapisha ushahidi utakaotolewa na mkurugenzi aliyetimuliwa kazi FBI ambaye amesema Rais Trump alimtaka mkurugenzi huyo kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama. 

James Comey alitoa uchambuzi wa ushaidi wa mazungumzo kati yake na rais Trump aliyofanya naye mara tano wakati Trump alipokuwa akirudia kutaka amsikilize na kumheshimu wakati ambapo Comey anasema alikuwa akifanya kazi zake bila kuegemea upande wowote. 

Wakili wa Trump amesema rais Trump anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi. 

Maafisa wawili wanaohusika na usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria

Monday, June 5, 2017

Picha mbalimbali toka Siasa nikilimo 2017... Uvccm

Mkuu wa wilaya Bw. kasesela.katika picha ya pamoja ma Bw. zenda kiongozi wa Uvccm taifa katikati ni Bw. Victor Y. Otieno

Makamu wa Rais wa chuo Kikuu cha Iringa katika tabasamu.










































Dc. Kasesela katika Ubora wa hapa kazi tu


Mkuu wa Mkuo Iringa mwishoni mama kipenzi cha wengi katika picha ya pamoja na Naibu katibu Mkuu CCM Taifa.

Friday, June 2, 2017

Msukuma: Nina majina ya Wabunge Waliohongwa kutetea Mchanga wa Madini

Baraka. 
Kwa kipindi kifupi kilichopita bunge letu lilianza kurudi kwenye misingi ya kizalendo, ila tokea hii budget ya madini ianzwe kusomwa vijembe,majigambo,maneno ya kuudhi,kejeli zimerejea mahali pake.

Leo kwa mara nyingine mbunge wa Geita, mh Msukuma aliomba dakika za nyongeza kutoka kwa Hawa Ghasia na kuwashambulia wabunge wa upinzani badala ya kuzungumza hoja. 

Mh. Msukuma alisema wapinzani wamehongwa na anawajua ingawa hakuwataja, pia akasema Msigwa anamiliki nyanya,kuku na mbwa hawezi jua mambo ya madini kama vile haitoshi akamrudia Mnyika kwamba anamiliki mchanga wa matofali

Saturday, March 4, 2017

Tafuta Mke/ Mme wa maisha hapa.

Blog yangu Leo hii nimeanza kutoa ufumbuzi wa kuweza kukutanisha kina Dada na vijana wakiume ambao Wenda mazingira yamesababisha mpaka Leo bado wameshindwa kupata wenzi wa maisha.
Tuandikie taarifa zako kwenye email yetu ya (roryamaendeleo@gmail.com )kisha tutatoa taarifa hizo kwenye blog hii ili kukuwezesha kukutana na Mme /  mke wa ndoto zako.

Wednesday, February 8, 2017

Freeman Mbowe, gwajima na wengine 63 watajwa kwenye list ya wauza madawa ya kulevya.

MAJINA YA WATU 65 NDIYO ANAYATAJA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AKIWATAKA WAFIKE KITUO CHA KATI DAR ES SALAAMU KWA MAHOJIANO

Mmiliki wa Slipway, Mmiliki wa Yatch Club, Mwinyi Machapta, Salehe wa MMI, Rose yupo China, Kiboko wa Mbezi, Hafidh wa Mbezi .....Idd Azzan atakiwa kufika Central Polisi Ijumaa saa Tano Asubuhi!! ...

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye atakiwa kufika Central Polisi Siku Ijumaa Saa Tano Asubuhi

Makonda pia amtaja Askofu wa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtaka naye afike kwa ajili ya mahojiano. Source  mwananchi .....leo

Tuesday, February 7, 2017

ibada za mashetani zashamiri mashuleni


Na Mchambuzi wetu toka roryamaendeleo

WAKATI wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Loleza iliyoko mkoani Mbeya hivi majuzi waliamua kumtimua shetani shuleni kwao kwa kumcharaza viboko nchi ya jirani ya Kenya mambo ni tofauti ambapo shetani amefanikiwa kuwaingia wanafunzi mioyoni na kuishi ndani yao.

kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Raisi Daniel Arap Moi Toroitich iliyo kuwa ikizunguka mikoa yote ya Kenya kuchunguza ibada za shetani, kama ufa hautazibwa sasa kudhibiti kasi ya wanafunzi wa Kenya kujihusisha na shughuli za Kishetani basi ukuta utajengwa.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa wakala kadhaa wa shetani hivi sasa wanazunguka katika mashule na vyuo vya elimu ya juu nchini Kenya wakidai kuwa wao ni maafisa wa Jumuiya ya Kikristo ya Wanafunzi "Kenya Students Christian Fellowship" lakini kinyume na hayo wakiwasajili wanafunzi kuwa watenda kazi wa shetani.

Ripoti hiyo imewashutumu walimu wa Kenya kwa kutokuwa waangalifu kiasi cha kuruhusu wageni kuingia hovyo kwenye mipaka ya shule ambapo imebainika kuwa baadhi ya wageni hao huwaletea wanafunzi madawa ya kulevya na zawadi ghali za kuwashauri wajiunge na ibada na kazi za shetani.

Ripoti ya Tume ya Rais Moi imetoa wito na tahadhari ikijulikana wazi kuwa vijana ndio tegemeo la Taifa kwa kusukuma gurudumu la maendeleo na kwamba upo umuhimu wa serikali kuchukua tahadhari kupambana na shetani kabla hajaipokonya vijana wake wanaopotoka kwa kasi.

Akielezea jinsi alivyoponea chupuchupu kuopolewa na shetani mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili nchini Kenya ambaye sasa ameacha shule ameeleza kuwa aliingizwa kwenye ibada za shetani kwa mara ya kwanza katika maisha yake baada ya mama wa kambo, kumpa fedha nyingi sana kiasi cha kumpelekea ajihoji ni nini maana yake.

Mwanafunzi huyo ameieleza Tume ya Rais Moi ya kuchunguza ibada za shetani kuwa mama yake huyo pia alimpa saa ya mkononi ya thamani ambayo kila alipokuwa akiivaa ilikuwa ikimnyonya sana damu yake.

Katika tukio la kushangaza mwanafunzi huyo ameeleza kuwa siku moja akitoka shuleni alikutana na mwanamke mmoja mrembo sana akiwa na mwanaume ndani ya gari jeusi aina ya "mercedes Benz." Walipomkaribia walifunga breki na kumuita, watu hao wawili mwanamke na mwanaume walijitambulisha kwake ndipo walipomwomba aongozane nao mpaka kwenya hoteli moja ya kifahari ya jijini Nairobi.

Walipofika hotelini kwa mujibu wa ripoti ya tume hiyo watu hao waliagiza vyakula na vinywaji kisha wote watatu wakuendelea kisha wakamshawishi kwa lugha laini wakimbembeleza ajiunge na ibada za shetani.

Watu hao hawakuishia hapo tu bali walimwambia mwanafunzi huyo baba yake mzazi aliyefariki kwenye ajali ya gari mnamo mwaka 1992 alitolewa kafara kwa shetani na mamaye wa kambo yule aliyemuingiza kwenye ibada za shetani.

Baada ya watu wale kumshawishi kwa bidii alikubali kujiunga nao ambapo ana elezea kuwa wakimpa nguvu za kishetani za kuweza kubadili umbo lake la kibinadamu kuwa nyoka aina ya Cobra ,

Pia kwa nguvu za roho chafu za shetani aliweza kusafiri kimiujiza mpaka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Ulaya pia walimpa nguvu za kuweza kupelekea ajali barabarani.

Mwanafunzi huyo anaelezea kuwa aliamua kubwaga manyanga na kuacha dini ya shetani siku alipopokea barua iliyoandikwa kwa kutumia damu tupu ikimtaka awatoe kafara kaka yake na dada yake ambao ni mapacha .

Anasema haikuwa lelemama kuhama kutoka kwa shetani kurejea maisha ya kawaida. Ilibidi Chama cha Wanafunzi Wakristo shuleni kwake wamfanyie maombi ya pekee ambapo baadaye walimu "alikata shauri kumuachisha masomo akapumzike nyumbani mpaka atakapoachana na shetani kabisa.

Naye mwanafunzi mmoja wa kike toka kidato cha kwanza katika shule moja ya sekondari mkoani Rift Valley huko Kenya ameelezea kuwa yeye aliingizwa kwenye ibada za shetani kwa kupewa zawadi kidogo kidogo na wasichana wenzake wa kidato cha nne waliokuwa ni wakala awa shetani shuleni hapo.

Amesema kuwa vitu alivyokuwa akipewa na wasichana hao ni pamoja na juisi za matunda na vinywaji vinginevyo, mkate, nyanya za kupona vyakula vingine vilivyosindikwa Wasichana hao pia kila mara walikuwa na mazoea ya kumpa fedha za matumizi kiasi cha shilingi 5000/- za Kenya

Lakini msichana huyo alishikwa na butwaa siku wasichana hao walipomfuata na kumtaka ajiunge na dhehebu lao la shetani kama hatua ya kulipia vitu ambavyo wamekuwa wakimpatia lijaribu kila awezavyo kuwaeleza kuwa kanisa lake linapinga ibada za shetani, hivyo alikuwa tayari kuwalipa zawadi zao lakini asijiunge nao.

Wasichana wale walikataa kata kata kurejeshewa zawadi zao. Ndipo msichana yule anaelezea kuwa kimiujiza alikuta tayari yeye ni mmoja wa waabudu shetani wazuri.

Toka Tume ya Rais Moi ilipotoa ripoti yake baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kwamba yale yaliyosimuliwa na viongozi wa tume hiyo siyo ya kweli.

Akithibithisha kiasi gani mambo hayo yana ukweli Mwenyekiti wa tume hiyo Rev, Bernard Muindi aliiambia gazeti la "Daily Nation kuwa

"people questining the report on devil worship have no basisi to do so , the report is reality , we have live evidence in our report, such as in "shimo la Tewa and Maragua,where we witnessed young men strip naked before getting down to worship" yaani Mombasa.

"Watu wanahoji kuhusu ukweli wa ripoti ya tume ya kuchunguza ibada za shetani, wanapaswa kuacha kufanya hivyo. Ripoti hii ni kweli na mengine hatujaelezwa bali tumeshuhudia kwa macho yetu huko "Shimo la Tewa Mombasa na Margua vijana wakijipanga kwenye mstari wakiwa uchi kama walivyozaliwa na kumuabudu shetani". Akielezea kuhusu matukio hayo Rev Muindi amesema kuwa huko Maragua walimbamba mwanafunzi mmoja mnamo majira ya saa 9 mchana akiabudu uchi wakati ambapo katika shule ya sekondari ya shimo la Tewa huko Mombasa walishuhudiwa na wanafunzi wakiwachinja kuku na kunywa damu zao.

Naye kiongozi wa chama cha kisiasa cha NDP Bw Raila Odinga ameitaka serikali ya Kenya kutopuuza taarifa za ripoti ya Tume ya Rais Moi sababu watakaoathirika na ibada za kishetani ni wananchi.

Mwenyeketi wa Baraza la Maimamu wa Kiislamu nchini Kenya Bw Juma Ngao amesema kuwa serikali ya nchi hiyo ni lazima ihakikishe inafanyia kazi, maoni yote yaliyotolewa na wananchi kwenye ripoti hiyo.

Naye kiongozi mmoja wa kanisa la Wasabato nchini Kenya Bw. Alex Ayub amesema kwa muda mrefu waabudu shetani wamekuwa wakiiba vitu kanisani mwao na kuvitumia kutengenezea alama zao.

Alama hizo za waabudu shetani zimetajwa kuwa ni pamoja na misalaba yenye nyoka , nyota yenye pembe saluti yeye pembe na namba 666

Maajenti (mawakala) wa shetani waliotajwa kuwa wamekuwa wakishawishi wanafunzi kujiunga na madhehebu ya shetani ni pamoja na wanafunzi wanaosoma vidato vya juu kuanzia kidato cha tatu mpaka cha nne hasa wanafunzi toka familia zenye uwezo mkubwa kifedha.

Wengine ni wasichana warembo sana vijana wa kiume wenye sura za kuvutia wafanyakazi wa "Matatu"hususani toka Nairobi ambao hutumia pesa na muziki uliofunguliwa kwa sauti kuvutia wanafunzi.

Matajiri kadhaa wanaoabudu shetani wamekuwa wakigawa zawadi kwa wanafunzi wanao kubali kujiunga na ibada zao na wengine ni wahubiri wa kujitegemea wanaoendesha mikutano ya Injili iliyojaa miujiza