Monday, September 27, 2021
Monday, September 13, 2021
Saturday, September 11, 2021
Monday, September 6, 2021
Monday, May 10, 2021
VIDONDA VYA TUMBO -AINA, CHANZO, DALILI & TIBA.
Tuesday, September 12, 2017
RAIS DK. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI MKUU FROF. IBRAHIM HAMIS JUMA,
Rais Dk John Magufuli akimuapishaJaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Profesa Ibrahim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande na kuwa jaji wa nane kushika wadhifa huo tangu nchi ipate uhuru huku akiwa Mtanzania wa sita. Wapili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini hati ya kiapo cha Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma baada ya kumuapisha
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma leo
Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Juma akizungumza baada ya kuapishwa leo
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Juma kuapishwa
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akiteta jambo na Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande (kulia) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya majaji waliohudhuria hafla ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi akifuatilia kwa makini hafla hiyo
Jaji Kiongozi Ferdinand Wambaliakiteta jambo na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande (kulia) wakati wa hafla hiyo
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla hiyo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Jum. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumz na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wakati wa hafla hiyo
Rais Dk. John Magufuli akiwa na Jaji Mkuu na Spika wa Bunge wakati wa hafla hiyo
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na Majaji mbalimbali, mwisho mwa hafla hiyo,leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Sunday, July 16, 2017
UMOJA WA VIJANA WA CCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA MWANZA WAKAKABIDHIWA VYETI NA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA
Sunday, July 16, 2017Mgeni Rasmi Katika Mahafali ya wahitumu wa Vyuo vikuu Mkoa wa Mwanza Ndugu Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Rodrick Mpogolo , Akiongozana na Daniel Zenda K.katibu Idara Vyuo na Vyuo Vikuu , Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndgugu Anthony Dialo, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg Raymond Mwalimu, Waheshimiwa Wabunge wa Ilemela na Nyamagana pamoja na viongozi wa secretariat ya Mkoa, Katibu wa CCM Nyamagana na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi, Makundi ya Kijamii, Machinga, wapiga debe, Mama Ntilie na wajasiliamali. Mahafali yaliyofanyika Ukumbi Rock City Mall.
Ndugu Mgeni Rasmi amewasihi sana wahitimu kuwa Wabunifu wa miradi za kuweza kujitegemea haswa katika Kilimo na Ufugaji, Mgeni Rasmi aliwakumbusha wahitimu kuenenda sawa na Imani ya Ccm kama ilivyoainishwa katika katiba ya CCM Ibara ya nne (4) na aliwataka wahitimu Wajiajiri(Blue colour Job) na kutumia Maarifa waliyonayo katika Jamii na kuondokana na dhana ya kuajiriwa.
Aliendelea kusisitiza Umuhimu wa Database yani taarifa za wahitimu wote zinaumuhimu sana kwa kutumikia chama cha Mapinduzi na Taifa kwa Ujumla.
Mahafali ya kwanza kubwa Mkoani wanafunzi/Makada walio hitimu 256 na washiriki walio hudhuria 612 wanachama.
Mahafali hiyo ilifana kwa kuanza Shughuli ya kijamii kutembelea kituo cha Watoto waliofanyiwa Ukatili(Foundation Karibu Tanzania) kaimu katibu Idara Vyuo na Vyuo Vikuu ndg Daniel Moses Zenda aliongoza Shughuli hiyo na kujionea namna Ukatili waliofanyiwa watoto hao. Pamoja na kushiriki na kutoka Mchango Ulioandaliwa na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
Imetolewa na
Idara Vyuo na Vyuo Vikuu.



















