Friday, July 10, 2015

Tano bora wa ccm hawa hapa.

a ndio matokeo yaliyowekwa kwenye mitandao kuhusu Wagombea watano Uraiswa CCM DodomaByNewsroom TZAonJuly 11, 2015481sharesShareTweetShareSharecommentsJuly 10 2015 inaripotiwa taarifa nyingine kutoka Dodoma Tanzania… Watu wengi wamekaa tayari kujua nini ambacho kitaamriwa Dodoma kuhusu Mgombea Urais ambae anateuliwa na CCM kugombea Urais wa Tanzania 2015.Majina yalikuwa mengi zaidi ya 38, hii ndio list ambayo imetangazwa kuingia Top Five kupitia ukurasa wa Twitter wa CCM @ccm_tanzaniaKikao cha KAMATI KUU (CC) kimekamilika na kufanikiwa kuwateua wagombea wake 5 ambao ni…pic.twitter.com/tfx47nUWR1— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania)July 10, 2015Saa chache zilizopita Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauyealiongea na waandishi wa habari kwamba majina matano yamewasilishwa Kamati Kuu na majibu itakuwa ni kesho, Team yamillardayo.comiko Dodoma tayari kama kuna taarifa yoyote tofauti utaipata hapahapa mtu wangu.Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Kituo cha polisi Bunju chachomwa Moto.

NEWZZ ALERT:KITUO CHA POLISI
BUNJU CHACHOMWA MOTO.
Image
Habari Zinazoendana
Baadhi ya Polisi wakiwatawanya watu (hawapo pichani) kwa
mabomu ya machozi mara baada ya tukio la kuchomwa
moto kituo cha polisi Bunju, tukio hilo limetokea.Kituo cha
polisi Bunju kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar kimechomwa
moto na baadhi ya Wananchi kufuatia tukio la kudaiwa kwa
Mwanafunzi mmoja kugongwa na gari na kufa papo ha

Kikao cha ccm Top 5 yaendelea

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO
CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI
DODOMA LEO, TANO BORA YA
WAGOMBEA KUPATIKANA BAADA
YA KIKAO HIKI
Habari Zinazoendana
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM,
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC)
kinachoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa
White House, Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma. Kikao
hiki kinapitia majina yote 38 ya Watangaza nia ya kugombea
Urais kwa tiketi ya CCM, ambapo majina matano
yatapatikana baada ya kikao hiki.Kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM - Zanzibar, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu
Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (kulia)
pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman
Kinana.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa
kwenye Kikao cha kupitia Wagombea wanaowania nafasi ya
Urais wa Tanzania kupitia CCM, ambapo majina matano
yatapatikana katika kikao hiki na kupelekwa kwenye Mkutano
wa Halmashauri kuu ya CCM ili kupata majina matatu
yatakayokwenda kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu.
Baadhi ya Wapigapicha za Habari wakichukua taswira ya
Wazee wa Kamati ya Ushauri wa Chama.Wazee wa Kamati
ya Ushauri ya CCM ikiongozwa na Rais Mstaafu awamu ya
Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya tatu,
Mh. Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM,
Mzee Pius Msekwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mh. Aman
Abeid Karume, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Cleopa Msuya
pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Sali

Diamod na Dewji kusherehesha singida.

MOHAMMED DEWJI AWAAGA RASMI
WAKAZI WA SINGIDA MJINI
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia
wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya
kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati
wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa
Singida.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ).
Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu
nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa
jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na
kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na
afya.
Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi
waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB) wakati
wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu
wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.
Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za
sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya
na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma
maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano
mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo
elimu na Afya
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni
kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa
pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya
miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha
wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa
kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania
nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu
yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji
wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa
majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana
kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo
yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha
kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo."
alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida
walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria
kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama
wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza
vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini"
alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na
ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari
bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa
huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya
wananchi 1,000.
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu
ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za
Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya
kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema
Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia
baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na
majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na
Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba
walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya
kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika
shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida
mjini.
Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi
na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya
manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi
wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza
bungeni.
Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima
viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya
baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.
Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10,
unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati
akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama
ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia
asilimia 81.
Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga
barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na
kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi
chote!
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache
ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza
kutogombea tena.
Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba:
"kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-
barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa
nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu
Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake,
ikiwemo mimi mwenyewe."
Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi
yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa
dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo
kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.
"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na
ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika
njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu,
lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki
pale pale.
"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na
kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge
katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani
dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo,
haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi
yangu, kwa Singida na watu wake! "
Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake huku machozi
yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea
tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.
Watoto hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada
ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la
ubunge wa Singida mjini.
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana
na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni
mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu
la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge
wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi
kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya
People's Club.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia
jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa
Singida mjini.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz
akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano
mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa
jimbo hilo.
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake
wakishambulia jukwaa.
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya
Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake
wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika
viwanja vya People's Club, Singida mjini.
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali
kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika
katika viwanja vya People's Club kusikiliza taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh.
Mohammed Dewji.
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do
ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa
wananchi wa Singida mjini.
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati
akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini
waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh.
Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia)
akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses
Iyobo .
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky
akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a
Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.

Ofisi mpya ya CCM kufunguliwa Leo na JK Dodoma

JK AZINDUA UKUMBI WA KISASA WA
MIKUTANO WA CCM MJINI DODOMA
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Dodoma
mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa
jengo jipya la mikutano la CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongoza
sherehe fupi za uzinduzi wa jengo jipya la mikutano la CCM
mjini Dodoma
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya CRJE Ndugu Hu Bo
akihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa Jengo la kisasa
la mikutano la CCM mjini Dodoma.
Viongozi wakifurahia hotuba ya Mkurugenzi wa CRJE
Balozi wa China Nchi Mhe. LU Youqing akizungumza wakazi
wa uzinduzi wa Jengo jipya la Ukumbi wa mikutano la CCM
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa jengo la
ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini Dodoma.
Bendera za CCM zikipepea nje ya ukumbi wa jengo jipya la
kisasa la mikutano Dodoma Convention Center.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa
salaam za kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Taifa
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuja kutoa hotuba ya ufunguzi
wa Ukumbi mpya wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini
Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Kikwete akihutubia
wakati wa sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa kisasa wa
mikutano wa CCM mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akibonyeza tufe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa jengo jipya
la ukumbi wa kisasa wa mikutano la CCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampunzi ya
ujenzi ya CRJE kutoka China Ndugu Hu Bo kama ishara ya
kukabidhiwa jengo la ukumbi wa kisasa la mkutano la
Dodoma Convention Center.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya
wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre,
Katibu Mkuu wa CCM , Abrahman Kinana, baada ya kuzindua
rasmi ukumbi huo leo, mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete akiwa
kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu,Balozi
wa China Nchini Mhe. LU Youqing na Viongozi wa CCM
mkoa wa Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na viongozi
wengine wa ngazi ya juu CCM wakiwa wamekaa kwenye
meza kuu ndani ya ukumbi mpya wa kisasa wa mikutano
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akisalimiana na Waziri Mkuu
Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye kwenye ukumbi mpya wa
mikutano wa CCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete(wa nne toka
kushoto),Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) Dk.Ali
Mohamed Shein (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa kwenye
picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa jengo.na Balozi Seif
Idd (kushoto) Makamu wa Rais Dk.Mohamed Bilal,Katibu wa
NEC Oganaizesheni Dk.Mohamed Seif Khatib,Balozi wa
China Nchini Mhe. LU Youqing,Mama Salma Kikwete, Mhe.
Anna Abdala na Mzee Pius Msekwa.
(Picha zote na Adam Mzee)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Ratiba ya kikao Leo cha ccm

Urais ccm. Vikao vyafanyika Leo mkutano mkuu kesho.

URAIS CCM: VIKAO VYAFANYIKA LEO,
MKUTANO MKUU KESHO
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari nje ya
ukumbi wa NEC,Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa vikao vyote vitafanyika
leo kikiwemo cha Kamati ya Usalama na Maadili
pamoja na vikao vya mchujo wa wagombea
kuanzia watano(5) mpaka kupata watatu
(3) ,mgombea wa Urais Zanzibar kisha kesho
tarehe 11 Julai utafanyika mkutano mkuu wa CCM
ambao atapatikana mgombea mmoja wa CCM kwa
nafasi ya Urais.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa za vikao
vitakavyofanyika leo mjini Dodoma kutoka kwa
msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye nje ya ukumbi wa
NEC mjini Dodoma.