Wednesday, February 24, 2016

PROF. MABARAWA AITAKA KADCO KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI

kad1
Muonekano wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa KIA mkoani Kilimanjaro unaojengwa njia za kutua na kuruka ndege na kukarabatiwa jengo la abiria. Ujenzi huo unafanywa na kampuni ya NACO kutoka Uholanzi.
kad2
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege katika  Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa KIA mkoani Kilimanjaro.
kad3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akielekea kukagua ujenzi wa njia za kuruka na kutua ndege mara baada ya kukagua hanga la uwanja huo. Katikati ni Mkurugenzi wa Via Avaiation Bi. Susan Mashibe ambaye ni Muwekezaji wa Hanga hilo.
kad4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Via Avaiation Bi. Susan Mashibe ambaye ni Muwekezaji wa Hanga katika Uwanja wa Ndege wa KIA.
kad5
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Arusha, Eng. John Kalupale (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) kuhusu ujenzi wa barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa Km 26 unavyoendelea.
kad6
Muonekano wa moja ya makalvati makubwa yaliyojengwa katika barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa Km 26.
kad7
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Kia-Mererani Km 26.
kad8
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akikagua karakana ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA mkoani Manyara.
………………………………………………………………………………………………………..
Serikali imeitaka kampuni ya KADCO inayoendesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kuongeza mapato na kuimarisha ulinzi ili kulinda hadhi ya uwanja huo, kuchangia pato la serikali na kudhibiti hujuma dhidi ya watu wasio waaminifu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo wakati akikagua utendaji wa uwanja huo na mradi wa ujenzi wa njia za kurukia ndege na jengo la abiria unaondelea katika uwanja huo.
Prof. Mbarawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa KADCO Bw. Bakari Mururusi, kuhakikisha kuwa uwanja huo kuanzia mwaka huu wa fedha unazalisha mapato yanayowiana na hadhi yake na kuchangia kikamilifu mapato ya Serikali na kuachana na utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea.
“Siridhiki na kiasi cha bilioni 18 mnazozalisha kwa mwaka, nawataka kuanzia sasa mkusanye mapato ya kutosha na kudhibiti vitendo vya hujuma ili kuupa hadhi inayostahili uwanja huu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Amemtaka Muwekezaji wa Hanga (garage) la Uwanja huo kujiandaa kuondoka kutokana na kutowekeza kikamilifu katika kipindi cha miaka 10 alichokodishiwa na kusisitiza kuwa nia ya Serikali ni kukabidhi hanga hilo kwa Shirika la Ndege nchini (ATCL), ifikapo Julai mwaka huu ili lifanye kazi kwa faida na madhumuni yaliyokusudiwa.
“Nia ya Rais ni kufufua ATCL liwe na hadhi inayoshatahili hivyo hanga hili tutawapa ATCL na kuwasimamia ili wafanye kazi kikamilifu na kuleta mapato kwa Serikali”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amemweleza Mkurugenzi wa Kampuni ya Via Aviation inayomiliki hanga hilo kwa miaka 10 kuwa Serikali hairidhishwi na mapato yanayotokana na hanga hilo hivyo imejipanga kuitumia kuleta faida zaidi kwa Serikali katika mkakati wake wa kukuza uchumi.
Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa Km 26 inayojengwa na Kampuni ya Chicco kwa gharama ya shilingi bilioni 32.2 na kumtaka mkandarasi huyo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Manyara, Eng. Yohani Kasaini amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa licha ya barabara hiyo kupita katika ukanda wa tambarare jumla ya makalavati makubwa 6 na madogo 85 yanajengwa ili kukabiliana na changamoto ya mafuriko na hivyo kuiwezesha barabara hiyo kupitika wakati wote wa mwaka.
Barabara ya Kia-Mererani ina umuhimu wa kipekee kiuchumi kwani inapita katika ukanda wenye rasilimali zenye madini ya Tanzanite, eneo zuri la kilimo, ufugaji, utalii na misitu hivyo kukamilika kwake kutapunguza gharama za usafiri na kuvutia watalii wengi kuja nchini.
Serikali iko katika mkakati wa kuimarisha uwanja wa ndege wa KIA kwa kukarabati jengo la abiria na njia za kutulia na kurukia ndege ambapo kampuni ya NACO kutoka Uholanzi inajenga uwanja huo ili kuuwezesha kufanya kazi kisasa, kuruhusu ndege nyingi kutua na kuongeza mapato ya uwanja huo na Serikali kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo mkoani Manyara kufanyakaz kwa umoja, uwazi, uadilifu ili kuiwezesha lengo la wizara hiyo la kujenga miundombinu itakayoliwezesha taifa kufikia uchumi wa kati 2025 kutimia kwa wakati.

MBUNGE WA ISMANI WILIAM LUKUVI ATOA MSAADA WA PESA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IDODI

MBUNGE WA ISMANI WILIAM LUKUVI ATOA MSAADA WA PESA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IDODI

DSC_0580
Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa  kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha  kiasi cha Tsh milioni 2 za  kulipa fidia  ya ardhi kwa  wananchi  watakaohamishiwa makazi mapya  kutoka  kitongoji  cha Kitanewa Idodi ambao  nyumba   zao zilisombwa na mafuriko
Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi fedha hizo, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
……………………………………………………………………………………………………..
 Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE  wa jimbo  la  Isimani  Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole
waathirika  wa mafuriko wa kata  ya Mapogolo tarafa ya  Idodi wilaya ya 
Iringa mkoani Iringa kwa kuwakabidhi msaada  wa pesa  zaidi ya Tsh 
milioni 9  kwa ajili ya kusaidia mahitaji  mbali mbali ikiwa ni pamoja 
na  kurejesha  miundo mbinu  ya maji  safi  iliyoharibiwa na mafuriko.
Bw Lukuvi  ambae  pia ni  waziri  wa Ardhi  ,nyumba na maendeleo ya makazi
 alikabidhi msaada  huo  jana  baada ya  kutembelea  waathirika  hao 
waliopo kambi  ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara  ya
kutoka Iringa  kuelekea hifadhi ya  Taifa ya Ruaha ambayo kwa   sasa
imekarabatiwa baada ya  awali barabara   hiyo kukatika kutokana na
mafuriko hayo , alisema   kuwa  lengo lake  kama mbunge  wa  jimbo  
hilo la Isimani na  serikali ni kuona  wananchi  waliokumbwa na
mafuriko   wanaendelea  kusaidiwa .
Alisema  kuwa  awali aliomba msaada  wa mahindi   tani 100  kutoka   serikali kwa
ajili ya waathirika  hao  wa mafuriko Idodi na  Pawaga  ikiwa ni  
pamoja na  kuwasaidia  msaada  wa  fedha   kiasi cha  zaidi ya Tsh
milioni 3 kwa ajili ya  kuwawezesha  waathirika  hao  wa mafuriko  
kupata mahitaji mengine kama mboga na  pesa ya  kusagia mahindi hayo .
Bw  Lukuvi alisema  kuwa kwa ajili ya kurejesha  huduma ya maji kijijini
hapo  amewasaidia kiasi cha Tsh  miliobni 4 ambazo  wameomba  kwa ajili
ya  kuboresha miundo mbinu  hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa  ajili
ya kukiwezesha   kijiji kulipa fidia ya ardhi  kwa  wananchi waliotoa
ardhi  yao kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha  Kitanewa ambao
wanapaswa  kuhamishwa eneo  hilo la mafuriko la  kupewa makazi mapya .
” Waambieni   watu  wenye mashamba ambayo yatachukuliwa kwa ajili ya
viwanja mwaka   huu  wavune mazao yao na  baada ya  hapo kila  mmoja 
muweze  kumlipa  fidia ya  Tsh 200,000 na  baada ya  hapo waitini 
wataalamu  wa ardhi  ili  waweze  kupima  viwanja na  mpanfgilio  mzuri 
zaidi kwa  ajili ya makazi mapya …….pia nataka hata mashamba ya 
kawaida  ya wananchi kupimwa  ili kupata hati za ardhi
zitakazowawezesha  kutumia kupata mikopo ….ila  nitawaletea mashine
za  kufyatulia tofari ambazo  unaweza  kuzijengea  bila  kuchoma “
Alisema kuwa  kwa  ajili ya  kuhamasisha ujenzi  wa  nyumba   bora mwananchi
atakayekuwa  wa kwanza  kupandisha  jengo atamchangia bati japo kwa 
sasa amekwisha  toa bati  zaidi ya 300 kwa  mkuu  wa wilaya ya  Iringa
kwa ajili ya  waathirika   hao.
Bw  Lukuvi  pia  amewapongeza wadau  mbali mbali zikiwemo taasisi za dini ,watu  binafsi
,taasisi ya  kifedha pamoja na mifuko  ya  hifadhi  za  jamii  kwa 
kujitolea  misaada  mbali mbali kwa ajili ya waathirika  wa mafuriko na 
wagonjwa  wa Kipindupindu  Pawaga  .
Pamoja na  kuwashukuru wadau hao  Lukuvi  alimpongeza   waziri  Mkuu Kassim Majaliwa kwa    kuwatembelea waathirika  hao wa Mafuriko na  wale  wa Kipindupindu Pawaga .
Hata  hivyo  Lukuvi  alimpongeza  mkuu  wa wilaya ya  Iringa Bw Richard
Kasesela na  viongozi wote  akiwemo mkuu  wa mkoa Amina Masenza kwa  
kusimamia shughuli  mbali mbali  ikiwemo ya urejeshaji wa miundo mbinu
ya barabara   iliyokuwa  imekatika katika barabara ya Iringa – Ruaha .
Katika  hatua  nyingine  Bw  Lukuvi aliagiza  serikali ya  kijiji cha Mapogolo
kutowabagua  wananchi  katika  kugawa chakula   hicho  cha msaada na 
kutaka  hata  ambao  si waathirika  wa mafuriko ambao  wana njaa wapewe 
chakula   hicho  cha msaada kwa  waathirika wa mafuriko .
  
Wakati huo  huo Waziri Lukuvi  alisema  kuwa serikali inakusudia  kuijenga 
barabara ya Iringa- kuelekea   hifadhi ya  Ruaha  kwa  kiwango cha  lami
kama  mbavyo Rais Dr John Magufuli alivyoahidi wakati  wa kampeni
kupitia ilani ya  uchaguzi ya CCM
Pia  kwa ajili ya  kuwafanya  wananchi  kunufaika watalii wanaotembelea
hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa alisema  tayari  jitihada za  kujenga
viwanja  vidogo  vya ndege  nje ya  hifadhi ya  Ruaha  zimeanza na 
kuwa  lengo la  serikali ni  kuwahamisha wafanyakazi  wanaoishi  ndani
ya  hifadhi  hiyo na  kujumuika na  wananchi  nje ya  hifadhi ili 
waweze  kupata mahitaji kama  wananchi  wengine.

VIJANA TOKA JKT KUPATA AJIRA DAR.

6 (1)
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imejipanga kuajiri vijana waliopita Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kama mgambo ikiwa ni jitihada za Halmashauri hiyo kupambana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya kazi hiyo kwa baadhi ya mgambo kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Bi.Tabu Shahibu wakati akitoa ufafanuzi kwa njia ya simu kuhusu malalamiko ya wananchi yanayohusu mgambo wa Halmashauri hiyo kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakitimiza majukumu yao.
 “Tumeona tuanze kuajiri vijana waliopata mafunzo kupitia  JKT ili kuondokana na malalamiko ya rushwa kutoka kwa baadhi ya mgambo wanaofanya kazi hiyo katika Halmashauri ya yetu,tunaamini vijana hao wamefundishwa maadili ya utumishi na uzalendo,
“Nasisitiza askari mgambo yoyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa tutamchukulia hatua kwa kukatisha mkataba wake wa kazi na atachukuliwa hatua za kisheria Alisema Tabu.
Bi. Tabu aliwataka wananchi watoe taarifa za askari mgambo yeyote anayejihusisha na vitendo vya rushwa ili kufanikisha wamewaondoa na kurudisha imani ya wananchi kwa Jeshi la mgambo nchini.
Aidha, Bi. Tabu amewaonya mgambo waliomaliza mkataba ama kufukuzwa kazi kutotumia vitambulisho feki kufanya kazi za mgambo na kujihusisha na vitendo vya rushwa katika manispaa yake la sivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria na atakayekamatwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia kitambulisho ambacho siyo halali kinyume cha sheria.
Mgambo wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa katika Manispaa mbalimbali nchini hali inayosababisha usubufu kero kwa wananchi na Serikali kupoteza mapato yake kwani fedha nyingi huishia mikononi mwa watu ambao sio waaminifu.

WAZIRI MUHONGO AITAKA TPDC NA WABIA KUONGEZA KASI KATIKA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA GESI KIMIMINIKA.

HON2
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo ametaka kasi iongezwe katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na usindikaji wa gesi kimiminika unaotarajiwa kuanza mkoani Lindi mara baada ya taratibu za maandalizi kukamilika.
Profesa Muhongo alisema hayo katika kikao kwa ajili ya kujadili hatua iliyofikiwa  ya maandalizi  ya ujenzi  wa kiwanda hicho kilichoshirikisha watekelezaji wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo  ya Petroli Nchini (TPDC) na makampuni yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi  nchini.
Makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo ni pamoja na Shell, Statoil, Ophir Energy, Pavilion na Exxon Mobil. Pia kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
Mara baada ya kupokea  taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika  gesi kimiminika Profesa Muhongo alilitaka shirika la TPDC kushirikiana kwa karibu na makampuni ya  utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo na kwa kasi  ya haraka ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.
Profesa Muhongo alisema  Tanzania ina utajiri mkubwa wa gesi hivyo ni vyema watekelezaji  wakachangamkia  fursa hiyo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika ambayo  mahitaji yake ni makubwa  duniani hususan katika  bara la Asia.
“Ifikapo mwaka 2025 inategemewa kuwa mahitaji  ya  gesi  duniani  yatakuwa ni kiasi cha tani milioni 440 kwa mwaka hususan katika nchi za Asia ambazo ni karibu na Afrika, hii ni fursa ambayo tunatakiwa kuichangamkia ili kuendana na  soko  itakapofika kipindi hicho,”
alisema Profesa Muhongo.
Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa  gesi  ya kimiminika imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoendelea huku akitolea mfano wa Algeria ambayo ni nchi ya kwanza duniani kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata na kusindika  gesi  kimimika ambayo kwa  sasa imepiga hatua kubwa  kimaendeleo.
Katika maandalizi ya awali ya mradi huo, Profesa Muhongo aliagiza uundwaji wa timu kwa ajili ya maandalizi ya mradi huo  ikishirikisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya  Fedha, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), taasisi mbalimbali pamoja na wawakilishi kutoka katika makampuni  yanatofanya utafiti wa gesi na mafuta nchini ambayo ni mtekelezaji wa mradi huo.
Alisisitiza kuwa ni vyema timu hiyo ikawa na wataalam wenye uzoefu mkubwa watakaofanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Aliagiza kuwa timu hiyo kukamilisha taratibu zote za maandalizi kabla ya mwezi Novemba, mwaka huu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio alisema kuwa shirika  lake limekuwa likishirikiana na wabia wa ujenzi wa kiwanda hicho  katika hatua zote za maandalizi  ya awali na kuahidi kuongeza kasi  ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI, KATIBU MKUU WALA VIAPO KUIONGOZA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI, KATIBU MKUU WALA VIAPO KUIONGOZA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA

mas1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas2
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas3
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni  mara baada ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas5
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni kabla ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mas6
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, mara baada ya Jaji huyo kuwaapisha kuwa viongozi wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo. Injinia Masauni katika Tume hiyo amekuwa Makamu Mwenyekiti, na Meja Jenerali Rwegasira amekuwa Katibu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.