- Saa 2 zilizopita
Monday, April 18, 2016
MAJALIWA AMPA POLE MBOWE KWA KUFIWA NA KAKA YAKE
MAJALIWA AMPA POLE MBOWE KWA KUFIWA NA KAKA YAKE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha kaka yake Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe (kulia kwake) wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana akisalimiana na wanafamilia wakati alipokwenda kumpa pole Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwanasiasa mkongwe,Kingunge Ngombale- Mwiru wakati alipokwenda kumpa pole Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Ratiba ya Mkutano wa Bunge la Bajeti 2016/17 Linaloanza Kesho Tarehe 19 Hadi Mwezi wa 7 Tarehe 1
Ratiba ya Mkutano wa Bunge la Bajeti 2016/17 Linaloanza Kesho Tarehe 19 Hadi Mwezi wa 7 Tarehe 1
Mkutano wa Tatu (3) wa Bunge la Kumi na Moja (11) unatarajia kuanza mjini Dodoma kesho tarehe 19 Aprili 2016. Mkutano huu ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali.
Wabunge wote wametakiwa kuwasili mjini Dodoma siku ya Jumapili tarehe 17 Aprili 2016
Hali tete kwa rais wa Brazil
Hali tete kwa rais wa Brazil
Maandamano makubwa yanapangwa kufanywa sehemu mbalimbali Brazil, ambako wabunge wanatarajiwa kupiga kura leo, ikiwa wanataka Rais Dilma Rousseff ashtakiwe au la, kwa sababu ya kubadilisha bajeti. Wanaompinga lazima wapate theluthi mbili ya kura zote , kuweza kumshtaki rasmi kiongozi huyo katika baraza la Seneti.
Waandishi wa habari wanasema, kizuizi cha urefu wa mita mbili, kilichowekwa baina ya waandamanaji hao, mahasimu ni ishara ya mgawanyiko mkubwa nchini, baina ya wafuasi na wapinzani wa Rais Rousseff.
Anawashutumu wanasiasa wanaotaka kuitoa madarakani serikali yake iliyochaguliwa na wananchi wa nchi hiyo.
Sunday, April 17, 2016
Saturday, April 16, 2016
VYETI ,VYETI, VYETI ....
VYETI ,VYETI, VYETI .....Vyeti vimeokotwa , vyeti vya FADHILI MASAWE MICHAEL kidato cha nne amemalizia shule ya secondary GG .SHULUA .iliyoko box 60138.Dar es salam,
Kidato cha sita amesomea shule ya MWENGE sec, School baada ya hapo kajiunga na masfunzoo ya JKT kwa muujibu, kikosi cha BULOMBOLA .tafahari unaombwa kama unamfaham au unaweza mfikishia taarifa kuwa vyeti yake vimekotwa viko mahali salama tuwasiliane kwa no;0755-233755 AU. 0784900291 sambaza ujumbe huu kila group yawezekana taarifa hizi zikamfikia ahsanteni sana.👏