Sunday, June 26, 2016

WATUMISHI EGA WAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI SERIKALI.

by rorya

k1Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k2Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari  akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairukik3Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki.
k4k6 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k7Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
——————————————————-
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya Serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
“Nataka mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.
Waziri Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.
Hatua hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.
Aidha, watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.
Akizungumzia utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Dkt Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.
Katika kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126 mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.
Wakala hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29 zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Baraza la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.

MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI


Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi  wa Operesheni  za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji itakayotumika  kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.m2Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.m3Mhandisi wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical, akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera.m4Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu  wa Mradi wa Uwekaji  Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni.m5Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni.
(Picha na Mpiga Picha Wetu)

KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI YA COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO


Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili  katika Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketijuzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo,kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo,Abdallah Zuberi,kulia ni Hussein Chuse na anayefuatia ni
Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri,
 Mjumbe wa Kamati ya Mashindano namUsajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akiuliza swali wakati wa kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo
Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union,Salim Bawaziri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kumalizika kikao hicho 
Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mashindano na usajili.
Picha kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano cha timu ya Coastal Union.

BENKIYA CBA TANZANIA YAFUTURISHA WATEJA WAKE....................


by roryab4b6b1Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,DK.Gift Shoko akiongea na wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) waliohudhuria futari maalumu iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.b2Imam Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa akitoa  mawaidha wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya CBA  katika Hoteli ya Serana jijini Dar es Salaam, jana kwa ajili ya wateja wakati wa kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani.b3Baadhi ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam .b7Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA,Dk.Gift Shoko  (wa nne kushoto )  na Imam Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa (wa tano) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

Quaresma late winner books last eight slot for Portugal at Euro '16


Portugal's forward Cristiano Ronaldo celebrates. — AFP
Portugal's forward Cristiano Ronaldo celebrates. — AFP
LENS: Cristiano Ronaldo's Portugal snatched a place in the quarter-finals of Euro 2016 on Saturday as the Real Madrid superstar's parried shot was headed into a gaping net by Ricardo Quaresma to defeat Croatia late in extra-time.
The 1-0 win in a game which only burst into life in the final minutes in Lens earned Ronaldo's side a quarter-final meeting with Poland in Marseille on Thursday.
After scraping through their group without a single victory, Portugal's star power finally shone through just as the match seemed to be heading for penalties.
“The best team doesn't always win and that happened tonight,” Croatia coach Ante Cacic said.
Poland progressed to the quarter-finals of a Euros for the first time by beating Switzerland in a penalty shootout in Saint-Etienne, delighting celebrity fan Russell Crowe.
Arsenal-bound Granit Xhaka's wild and wide spot kick cost the Swiss dear as the Poles were a perfect five from five from the spot.
“POL!!! Final 8!!!” tweeted “Gladiator” star Crowe, who has taken this rugged Polish team and swashbuckling winger Jakob Blaszczykowski to his heart.

Post-Brexit clash

Ronaldo's Real Madrid teammate Gareth Bale failed to score for Wales in a post-Brexit all-British clash against Northern Ireland, but his cross was deflected into his own net by Gareth McAuley for the decisive goal.
The 1-0 win at a raucous Parc des Princes in Paris was probably the dullest game of the tournament so far, but Bale said Wales could not care less as they reached the last eight of a major tournament for the first time since the 1958 World cup.
“It's an ugly win but who cares,” said Bale.
“You can't ask for any more. It's incredible.” Wales will face Belgium or Hungary in Lille on Friday for a place in the semi-finals.
In Lens, a Croatia team that has played some of the most attractive football of the finals failed to find a way past the Portuguese defence.
Ronaldo was muzzled for the vast majority of a dull encounter that became the first match in Euros history in which neither team managed a shot on target during the regulation 90 minutes.
Domagoj Vida had a golden chance to settle the game for Croatia but headed wide after Portuguese goalkeeper Rui Patricio failed to collect a corner.
However, Patricio saved his country seconds later when he turned Ivan Perisic's header onto the post.
Portugal then snatched their first victory of the tournament at the death as Quaresma was perfectly positioned to head in after Subasic saved Ronaldo's low shot.
A jubilant Quaresma sprinted to the corner flag where he disappeared under a heap of celebrating teammates.

Goal of the tournament

At Saint-Etienne's Stade Geoffrey Guichard, Blaszczykowski opened the scoring for Poland but Switzerland drew level in spectacular style with Xherdan Shaqiri's bicycle kick, a potential goal of the tournament.
When the teams could not be separated in extra-time, it was Xhaka who cracked first in the penalty shootout, blasting well wide with Switzerland's second spot kick.
The Poles scored all five penalties, rounded off by Grzegorz Krychowiak's emphatic finish which put his nation into the quarter-finals of a major tournament for the first time since the 1982 World Cup.
“I'm delighted, it was a historic moment for us, because we are in the top eight in Europe,” Blaszczykowski said.
After Crowe added his congratulations, European Union president Donald Tusk, who is Polish, shared his nation's joy, tweeting: “I have waited for this for so many years! My God I am happy!” France's clash with the Republic of Ireland on Sunday, which evokes memories of Thierry Henry's infamous handball in a 2009 World Cup playoff, was given further edge with a row over tickets.
Ireland coach Martin O'Neill is angry because Irish fans received just 4,500 tickets for the match in the 59,000-capacity Stade de Lyon.
“It's totally disproportionate for a stadium of this size,” O'Neill complained.
“For us, or any team that was going to be playing in the round of 16 here, to be allocated less that 5,000 tickets is, I think, pretty unfair, honestly.”