Sunday, July 16, 2017

TANZIA: Waziri Mwakyembe afiwa na mkewe

Rorya maendeleo 1 hour ago

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe amepatwa na msiba wa kufiwa na mke wake Bi. Linah George Mwakyembe usiku wa kuamkia leo. 

Bi. Linah alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Agha Khan alipokuwa akipatiwa matibabu hadi umauti  ulipomkuta. 


Saturday, July 15, 2017

MAGAZETI YA LEO JULAI 16,2017


Rr

Mitandao ya kijamii inaweza kusababisha magonjwa ya akili - Utafiti

Rorya · 2 days ago

Je, unapenda kufungua mitandao mbalimbali ya jamii kama Facebook, Tweeter, Instagram, Google Plus, Snapchat, LinkedIn, Youtube na mingineyo kila siku? 

Kama jibu ni ndiyo, basi uko hatarini kupata tatizo la msongo wa mawazo na wasiwasi. 

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi. 

Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi kubuniwa na kuboreshwa.

Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa

Rorya maendeleo 5 hours ago

Kipimo sahihi cha maendeleo na mafanikio ya biashara ni ukuaji wa biashara. Tunategemea biashara iwe inakua kadiri siku zinavyokwenda. Ukuaji wa biashara tunaouzungumzia ni kuongezeka kwa idadi ya watu inaowafikia, kuongezeka kwa mauzo, kupata faida kubwa na kuweza kufungua matawi zaidi ya biashara hiyo. 

Kukua kwa biashara ni ndoto ya kila mtu anayeingia kwenye biashara lakini ni wachache sana ambao wanaweza kukuza biashara zao. Wengi wamekuwa wanaendesha biashara zilizodumaa na wakati mwingine zinakufa kabisa. Hakuna bahati nzuri kwa wale ambao wanakuza biashara zao na wala hakuna bahati mbaya kwa wale wanaoshindwa kuzikuza. 

Tofauti pekee inaanzia kwenye maarifa waliyonayo watu kwenye ukuzaji wa biashara. 
Wale ambao wanakuza biashara zao wanajua vitu ambavyo wengine hawavijui. Kwa kuwa vitu hivi siyo siri bali ni maarifa ambayo kila mtu anaweza kuyapata na kuyatekeleza, leo tutakwenda kuangalia njia tano za uhakika za wewe kuweza kukuza biashara yako na kufikia ndoto zako za kibiashara. Jifunze njia hizi na zitumie kwenye biashara yako ili uweze kufika mbali. 

1. Tengeneza timu sahihi ya kibiashara.  
Kwanza kabisa ni vyema ukajua biashara haiwezi kukuzwa na mtu mmoja, wewe mwenyewe huwezi kufanya kila kitu ambacho biashara yako inataka kifanywe. Unahitaji kuwa na watu ambao watakusaidia kwenye biashara yako na watu hawa ni vyema ukawa umewaajiri. Hapa kwenye kuajiri kuna changamoto kubwa sana kwenye biashara nyingi. Wengi wamekuwa wakiajiri mtu ambaye yupo tayari kupokea mshahara kidogo bila ya kujali ataleta mchango gani kwenye biashara. 

Biashara ni kama timu ya mpira wa miguu, kadiri wachezaji wanavyoelewana vizuri na kusaidiana ndivyo timu inavyopata ushindi. Unahitaji kuwa na timu sahihi kwenye biashara yako. unahitaji kuajiri watu ambao wana uwezo na vipaji tofauti. Angalia ni maeneo gani muhimu ya biashara yako na ajiri watu ambao wanaweza kuyafanyia kazi maeneo hayo na kuleta majibu mazuri. Ajiri watu ambao wana vitu ambavyo wewe huna, hii itakunufaisha wewe kwa kukupa muda wa kufanyia kazi yale ambayo ni muhimu zaidi kwa biashara yako. 

2. Wekeza sehemu ya faida kwenye biashara yako.  
Watu wengi wanaoingia kwenye biashara wamekuwa wakifikiri kwamba biashara ikishaanza basi wao ni kuchuma faida na kuendesha maisha yao. Kwa njia hii wamekuwa wanatumia kila faida wanayoipata na hivyo kupelekea biashara kubaki pale ilipo au hata kurudi nyuma, yaani kupata hasara. Biashara haiwezi kukua kama hakuna uwekezaji endelevu kwenye biashara hiyo. 

Tuchukulie biashara kama mfano wa ng’ombe, ng’ombe anapozaa ndama, unaweza kukamua maziwa na kuyatumia au kuyauza. Lakini pia ndama naye anataka maziwa ili aweze kukua, sasa kama utamsahau ndama na kufurahia maziwa, utashindwa kuendeleza ufugaji wako. Unatakiwa kuhakikisha ndama amepata sehemu yake ya maziwa na wewe ndiyo utumie maziwa yanayobaki. 

Wafanyabiashara wengi wamekuwa hawana mpango wa uwekezaji kwenye biashara zao, wanachofanya ni kununua vitu pale vinapoisha. Kwa njia hii biashara haiwezi kukua, biashara inakua pale sehemu ya faida inaporudi kwenye biashara kama uwekezaji. Na unafanya hivyo ukiwa unajua kabisa kwamba nimeongeza kiasi fulani kwenye mtaji na nimefanya hivyo kwa kununua kitu fulani ambacho hakikuwepo awali, au nimeongeza mzigo ambao nimekuwa nanunua. 

3. Kuwa tayari kubadilika.  
Tunaishi kwenye kipindi ambacho mabadiliko yanatokea kwa kasi sana, kila siku kuna vitu vipya vinakuja na vitu vya zamani vinakosa thamani. Kuna biashara ambazo zilikuwa maarufu miaka kumi iliyopita ila kwa sasa hazipo kabisa, na kwa kipindi hiko cha miaka kumi pia zimekuja biashara ambazo watu hawakuwahi kuzidhania. 

Mabadiliko yanatokea na yataendelea kutokea kila siku kwenye maisha na biashara zetu. Wale ambao wao tayari kwenda na mabadiliko wananufaika, wale ambao hawapo tayari wanaachwa nyuma na mabadiliko haya. 

Kila siku jifunze kuhusu biashara yako na biashara kwa ujumla, jua kinachoendelea kwenye ulimwengu wa biashara, jua mbinu mpya za ufanyaji wa biashara na angalia jinsi teknolojia mpya zinaathiri biashara yako. pale unapoona mabadiliko yanaathiri biashara yako usisite na wewe kubadilika. Kung’ang’ania kile ambacho umezoea kufanya kwenye biashara kutakuchelewesha kufika mbali kwenye biashara yako. 

KITABU; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.  

4. Toa huduma bora kabisa kwa wateja wako.  
Wateja ulionao ndiyo sababu biashara yako ipo, kama hakuna wateja hakuna biashara, haijalishi una bidhaa au huduma bora kiasi gani. Hivyo katika mipango yoyote ya kuikuza biashara yako, wateja lazima wawe kipaumbele cha kwanza. 

Wateja wako wanaweza kuwa mabalozi wazuri au wabaya wa biashara yako. Wateja wanaoridhika na huduma wanazozipata wanakuwa mabalozi wazuri na watakuletea wateja wengi zaidi. Lakini wale ambao hawaridhishwi watakuwa mabalozi wabaya kwa kutoa taarifa ambazo siyo sahihi kuhusu biashara yako. 

Ili kutoa huduma bora kwa wateja wako, wape ahadi kubwa halafu toa zaidi ya kile ambacho umeahidi. Na pia inapotokea mteja amepata changamoto kwenye biashara yako msaidie kuitatua. Kwa njia hii utatengeneza uhusiano mzuri na wateja wako kitu ambacho kitaiwezesha biashara yako kukua zaidi. 

5. Epuka hatari zisizo za lazima. 
Kwenye ulimwengu wa biashara, hatari ni kitu cha kawaida, kuna maamuzi mengi ya hatari ambayo unahitaji kufanya ambayo yanaweza kuleta faida kubwa kama yakifanikiwa. Lakini pia yakishindwa yanaleta hasara kubwa. Pamoja na kwamba biashara zipo kwenye mazingira ya hatari, bado siyo sahihi kuchukua kila hatari. Epuka zile hatari ambazo siyo za lazima kwenye biashara yako. 

Hapa unahitaji kufikiri vyema kabla ya kuchukua maamuzi. Na pia unahitaji kuilinda biashara yako dhidi ya hatari ambazo huwezi kuzizuia kwa kuikatia biashara hiyo bima. Kwa kuwa na bima una uhakika wa kuendelea na biashara hata kama kuna ajali iliyopelekea wewe kupoteza sehemu kubwa ya biashara yako.

Maradhi Ya Gesi Tumboni (Colic) Msokoto Wa Tumbo


Rorya maendeleo  8 hours ago

MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo 

Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya 

kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. 

Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo. 

TIBA:  
Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. 

Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. 

Njia Bora Za Asili Za Kukuza Nywele Zako Mambo Unayotakiwa Kuyafanya


Rorya maendeleo 

 hours ago

Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair,tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo.Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu. 

Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi.Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani?Zina tabia gani?Zinataka nini? 

1.Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda. 
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi.Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako.Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri.Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua. 

2.Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe. 
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri. 

3.Linda unyevu wa nywele zako 
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri. 

4.Zifahamu nywele zako 
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu.Unajuaje? 
Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi. 

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi. 
Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka. 

Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita. 
Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana. 
Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka. 

5.Mafuta ya Kupaka kichwani. 
Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele  aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia.Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana.Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree. 

6.Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana. 
Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako.Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana.sio kitana.Chanuo kubwa(wide toothed comb). 

7.Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue. 
Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu.Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka.Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda. 

8.Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo. Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi.Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24. 

Nafasi za kazi leo Julai 15


Rorya maendeleo Blog 1 hour ago


Bonyeza Links zifuatazo kusoma zaidi na kuapply: 

6 Job Opportunities at KP Recruiters, Sales Executives 

Job Opportunity at Heifer International, Communications Officer 

Job Opportunity at Melia Serengeti, Assistant Financial Controller 

Job Opportunity at Kilombero Sugar Company, Deadline is 21 July 2017 

Job Opportunity at GIZ, Advisor 

Job Opportunity at ALISTAR, Group Procurement Manager 

Job Opportunity at PCI, HR & Administration Manager 

Geographic Service Team (GST), Finance Administrator 

Job Opportunity at ABT Associate, Administrative Assistant 

Job Opportunity at NMB, Special Asset Management 

Job Opportunity at TIGO Tanzanian, Relations & Monitoring Officer