Wednesday, July 22, 2015

Haya ndio maamuzi ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi kwa vile Obama hatowatembelea?


Haya ndio maamuzi ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi kwa vile Obama hatowatembelea?


DCF 1.0
Babu Owino ni Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi, aliwasilisha barua yake kwa Balozi wa Marekani ambaye yuko Kenya, ndani ya barua kulikuwa na Ujumbe wa Wanafunzi wa Chuo hicho kwamba wanahitaji Rais Obama akitua Kenya apitie na Chuoni hapo kwa ajili ya kuongea nao !!
sonu
Babu Owino.
Ratiba ikaonesha kwamba Rais Obama hatofika hapo… hawakupenda kwa sababu mwaka 2006 Rais Obama akiwa Senator wa Illinois alitembelea Chuoni kwao na akapanda mti wa kumbukumbu.
Obama-iyo-Wangari-Maathai-oo-geed-ku-beeray-Nairobi-University-2006-kii
Hii ilikuwa mwaka 2006, Rais Obama akipanda mti Chuo Kikuu Nairobi pamoja na Marehemu Mama Wangari Maathai.
Kwenye barua ya wanafunzi hao ilionesha  kwamba wapo ambao wako tayari kujiua, wengine watajipanga kuukojolea mti aliopanda mwaka 2006… Babu Owino alikutana na Rais Kenyatta na wakaongea kidogo tu kwamba hiyo haikuwa kitu kizuri kufanya kwenye ugeni mkubwa kama huu.
Capture-3
Picha iliyonaswa Rais Kenyatta akiongea na Babu Owino siku chache zilizopita.
Mengine ni haya na yameshateka mitandao ya Kenya tayari, wanafunzi wa Chuo Kikuu Nairobi wameuchoma moto mti huo uliopandwa na Rais Obama, kuna mengine yatafuatia? Niko karibu na updates za Nairobi kila wakati likinifikia jipya utalipata hapahapa mtu wa nguvu.

No comments:

Post a Comment