Sunday, February 14, 2016

Mahakama ya ICC kutoa uamuzi dhidi ya RUTO

Mahakama ya ICC kutoa uamuzi dhidi ya RUTO
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai -ICC ya Mjini THE HAGUE nchini UHOLANZI inatarajiwa kutoa uamuzi ambao huenda utakuwa na athari kwa kesi inayomkabili Naibu Rais wa KENYA WILLIAM RUTO
WILLIAM RUTO
RUTO na mushtakiwa mwenzake, mwandishi wa habari JOSHUA ARAP SANG wameshitakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na ghasia zilizotokea nchini KENYA baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Awali mashtaka kama hayo yaliyomkabili Rais wa KENYA, UHURU KENYATTA yalifutiliwa mbali na Mwendesha Mashataka Mkuu wa ICC, FATOU BENSOUDA kwa ukosefu wa ushahidi.

Wasanii wagawanyika kuhusu wagombea Uganda..........

Wasanii wagawanyika kuhusu wagombea Uganda1002kbps | HDS (akamai_hds) | unmediated | 640x360


13 Februari 2016 Imebadilishwa mwisho saa 12:45 GMT
Watu mashuhuri na siasa si jambo geni. Lakini wana ushawishi kiasi gani kwa mashabiki wao hilo bado lina utata.
Uchaguzi wa Uganda unatarajiwa kufanyika wiki ijayo, na wasanii nchini humo wamegawanyika kwa maana ya mgombea gani wamwuunge mkono.
Lakini jambo moja la wazi wana mashabiki wengi miongoni mwa idadi kubwa ya vijana nchini humo. Kama anavyoripoti Zuhura Yunus.

Ligi kuu Tanzania kuendelea tena...........

Ligi kuu Tanzania kuendelea tena


Image captionKikosi cha watoto wa mtaa wa Msimbazi maarufu kama Simba
Mshikemshike wa ligi kuu Tanzania bara utaendelea tena wikiendi hii ambapo jumamosi kutapigwa jumla ya michezo mitano.
Stand United watakua wenyeji wa Wekundu wa msimbazi Simba Sport klabu, huku Mgambo Jkt wakipimana ubavu na African Sport.
Mbeya City wao watakua katika dimba lao la sokoine mjini Mbeya, kuwaalika wanakishamapanda timu ya Toto Afrikans toka Mkoani Mwanza.
Majimaji watakuwa wageni wa Ndanda Fc mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Nangwanda sijaona huko mkoani mtwara, Jkt Ruvu watakipiga na Kagera Sugar.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya jumapili kwa michezo miwili kuchezwa Mwadui Fc watapima ubavu na Tanzania Prisons, huku Coastal Union wakiwaalika Azam Fc.

Mmiliki wa Arsenal anunua shamba la £500m......................

Mmiliki wa Arsenal anunua shamba la £500m

  • 11 Februari 2016
Image captionStan Kroenke
Mashabiki wa Arsenal kwa mda mrefu wamelalamika kuhusu kushindwa kwa kilabu hiyo kununua wachezaji wazuri kila dirisha la uhamisho linapokuwa wazi.
Lakini mwana hisa mkuu katika kilabu hiyo Stan Kroenke amenunua shamba kubwa la ng'ombe lililogharimu pauni milioni 500.
Shamba hilo limepitia kaunti sita na Kroenke ambaye ana thamani ya pauni bilioni 5,sasa anamiliki zaidi ya ekari 865,000 za ardhi nchini Marekani,ikiwa ni eneo lililo mara tatu zaidi ya ukubwa wa mji wa Los Angeles,na mara nne na nusu ya ukubwa wa mji wa New York.
Image captionShamba alilonunua Kroenke mjini Texas
Ni watu wanane pekee wanaomiliki ardhi kubwa zaidi ya Kroenke nchini Marekani.
Image captionStan Kroenke
  • Je,umewahi kuwa na ndoto ya kujenga nyumba yako?
Image copyrightmukesh
Image captionMukesh
Mtu tajiri zaidi nchini India Mukesh Ambani amefanya hivyo na amefanya hivyo kwa mtindo.
Mukesh mwenye umri wa miaka 58 ambaye ndio mwanzilishi wa Cricket Franchise Mumbai Indians ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 alijenga jumba refu lenye ghrofa 27,na futi 400,000 mraba mjini Mumbai.
Likiwa na thamani ya dola bilioni ,jumba hilo kwa jina Antilla limedaiwa kuwa jumba ghali duniani.
Ni nani asiyetaka ghorofa sita za chini ya ardhi za kuegesha magari,maeneo matatu ya kuegesha ndege na wafanyikazi 600?.
  • Kwa nini uwe na jahazi moja la kifahari iwapo unaweza kumiliki majahazi matano kama hayo?
Image captionJahazi la kifahari
Mmiliki wa kilabu ya Chelsea Roman Abrahamovic amejenga majahazi mengi kutokana na uwezo wake wa thamani ya pauni bilioni 5.2 na sasa ndiye anayemiliki jahazi kubwa la kifahari duniani kwa jina the Eclipse.
Jahazi hilo lililogharimu pauni bilioni 1.5 linajivunia kidimbwi cha kuogelea chenye mita 16, nafasi ya kuegesha ndege 3 aina ya helikopta na sakafu ya kucheza densi.
Na iwapo Abrahamovich anahitaji mbinu ya haraka ya usafiri ,basi anamiliki ndege ya Boeing 767 ya kibinafsi.

Rais wa Brazil asema Zika haitaathiri Olimpiki

Rais wa Brazil asema Zika haitaathiri Olimpiki


Image copyrightReuters
Image captionRais Dilma Rousseff wa Brazil
Rais wa Brazil Dilma Rouseff amesisitiza kuwa ongezeko la visa vya virusi vya Zika halitaathiri michezo ya Olimpiki mjini Rio De Jeneiro mnamo mwezi Agosti.
Bi Rousseff amesema kuwa kukabiliana na ugonjwa huo na utafutaji wa chanjo ni swala la dharura.
Rais huyo amesema kuwa ana imani atapata ufanisi katika kuwaangamiza mbu wanaosambaza virusi hivyo.
Alijiunga na wanajeshi 2000 katika kampeni ya kitaifa ya kutoa hamasa kuhusu njia za kumaliza kuenea kwa ugonjwa huo.
Ugonjwa huo unahusishwa na kuzaliwa kwa watoto walio na kasoro.

Al-Shabab wasema ndio walioshambulia ndege.................

Al-Shabab wasema ndio walioshambulia ndege

  • Saa 3 zilizopita
NdegeImage copyrightHarun Maruf
Image captionNdege hiyo ilitoboka shimo ikiwa angani
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab kutoka Somalia limesema ndilo lililoshambulia ndege iliyotoboka shimo ikiwa angani mapema mwezi huu.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa barua pepe al-Shabab wamesema shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi operesheni za kijasusi zinazoendeshwa na mataifa ya Magharibi nchini Somalia.
Shimo hilo kwenye ndege hiyo lilitoboka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Mogadishu, ikiwa futi 10,000 (3,048m) juu angani.
Ndege hiyo ilifanikiwa kutua kwa dharura.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo, iliyokuwa ikielekea Djibouti, ilikuwa imebeba watu karibu 60.
Maafisa nchini Somalia baadaye walitoa video inayoonesha watu wawiliwakimkabidhi abiria mmoja anayeshukiwa kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga kitu kinachoonekana kama Laptop kabla ya mlipuaji kuabiri ndege hiyo.
Msemaji wa serikali anasema kuwa watu hao ndio washukiwa wakuu katika ulipuaji huo.
Inasadikika kuwa mmoja kati ya watu walioleta kipakatilishi hicho alikuwa ni mfanyikazi wa shirika linalohudumu katika uwanja huo wa ndege wa Mogadishu.
Watu 20 wamekamatwa wakiwemo wale wawili walionaswa kwenye video hiyo.

Van Gaal:''Mkutano na Mourinho utanikata tamaa''

Van Gaal:''Mkutano na Mourinho utanikata tamaa''

  • 13 Februari 2016
Image copyrightPA
Image captionMourinho na Van Gaal katika mkutano wa hapo awali.
Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa atakata tamaa iwapo Manchester United ilifanya mazungumzo na Jose Mourinho.
United haikutoa tamko lolote baada ya ripoti hizo za juma lililopita kwamba maafisa wa kilabu hiyo walifanya mazungumzo na wawakilishi wa aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho.
Alipoulizwa iwapo anafikiri kulikuwa na mazungumzo,Van Gaal alisema: katika soka hilo linawezekana,lakini sidhani kama kulikuwa na mazungumzo.
Amesema kuwa alikuwa na uhusiano mzuri na mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward na mmiliki Glazers na kwamba wangemwambia.
Manchester United kwa sasa hawako katika michuano ya kilabu bingwa Ulaya,na wako nafasi ya tano katika jedwali la ligi ikiwa pointi sita nyuma ya manchester City ambao wako katika nafasi ya nne.
Image copyrightReuters
Image captionVan Gaal
Van gaala amebaye alichukua ukufunzi wa kilabu hiyo 2014 na kuiongoza United katika nafasi ya nne mwaka uliopita alikubaliana na pendeko kwamba nafasi nyengine ya nne itaonekana kama mafanikio.
United itachuana na Sunderland katika uwanja wa Stadium of light siku ya jumamosi.