Sunday, February 14, 2016

Mmiliki wa Arsenal anunua shamba la £500m......................

Mmiliki wa Arsenal anunua shamba la £500m

  • 11 Februari 2016
Image captionStan Kroenke
Mashabiki wa Arsenal kwa mda mrefu wamelalamika kuhusu kushindwa kwa kilabu hiyo kununua wachezaji wazuri kila dirisha la uhamisho linapokuwa wazi.
Lakini mwana hisa mkuu katika kilabu hiyo Stan Kroenke amenunua shamba kubwa la ng'ombe lililogharimu pauni milioni 500.
Shamba hilo limepitia kaunti sita na Kroenke ambaye ana thamani ya pauni bilioni 5,sasa anamiliki zaidi ya ekari 865,000 za ardhi nchini Marekani,ikiwa ni eneo lililo mara tatu zaidi ya ukubwa wa mji wa Los Angeles,na mara nne na nusu ya ukubwa wa mji wa New York.
Image captionShamba alilonunua Kroenke mjini Texas
Ni watu wanane pekee wanaomiliki ardhi kubwa zaidi ya Kroenke nchini Marekani.
Image captionStan Kroenke
  • Je,umewahi kuwa na ndoto ya kujenga nyumba yako?
Image copyrightmukesh
Image captionMukesh
Mtu tajiri zaidi nchini India Mukesh Ambani amefanya hivyo na amefanya hivyo kwa mtindo.
Mukesh mwenye umri wa miaka 58 ambaye ndio mwanzilishi wa Cricket Franchise Mumbai Indians ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 alijenga jumba refu lenye ghrofa 27,na futi 400,000 mraba mjini Mumbai.
Likiwa na thamani ya dola bilioni ,jumba hilo kwa jina Antilla limedaiwa kuwa jumba ghali duniani.
Ni nani asiyetaka ghorofa sita za chini ya ardhi za kuegesha magari,maeneo matatu ya kuegesha ndege na wafanyikazi 600?.
  • Kwa nini uwe na jahazi moja la kifahari iwapo unaweza kumiliki majahazi matano kama hayo?
Image captionJahazi la kifahari
Mmiliki wa kilabu ya Chelsea Roman Abrahamovic amejenga majahazi mengi kutokana na uwezo wake wa thamani ya pauni bilioni 5.2 na sasa ndiye anayemiliki jahazi kubwa la kifahari duniani kwa jina the Eclipse.
Jahazi hilo lililogharimu pauni bilioni 1.5 linajivunia kidimbwi cha kuogelea chenye mita 16, nafasi ya kuegesha ndege 3 aina ya helikopta na sakafu ya kucheza densi.
Na iwapo Abrahamovich anahitaji mbinu ya haraka ya usafiri ,basi anamiliki ndege ya Boeing 767 ya kibinafsi.

No comments:

Post a Comment