Tuesday, July 19, 2016

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AFDB YAIPIGA JEKI TANZANIA DOLA MILIONI 200

by RORYA MAENDELEO

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kulia), akiwa katika picha ya pamoja  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB, Tania Kandiero, alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, kwa mazungumzo maalumu, akiwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto), akimsikiliza kwa makini  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn. Aliyeketi kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Kushoto) akibadilishana “Business Card”  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), (Katikati), akiwa katika mazungumzo maalumu na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi yake Jijini Dar es slaam, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
 Kaimu Kamisha Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta Mtagwaba akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani), ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akibadilishana “Business Card”  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa katika mazungumzo maalumu na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto) akizungumza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
 …………………………………………………………………………………………………………………….
Na Benny Mwaipaja-WFM 
BENKI ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, imeahidi kuchangia Dola Milioni 200, sawa na Shilingi 433.6b, kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2016/2017. 
Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu, Dkt. Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es salaam 
Makamu huyo wa Rais wa AfDB aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Tania Kandiero, amesema kuwa mchango huo umeongezeka kwa dola Milioni 50 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo ilichangia Dola Milioni 150. “Misaada na mikopo inayotolewa na Benki yetu kwa serikali ya Tanzania imefikia Dola za Marekani 1.9b hivi sasa” Alieleza Dkt. Kacou 
Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake mahili ya maendeleo inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo. “Tuna malengo matano ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula, kuiendeleza kiviwanda, kuiunganisha na kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla” aliongeza Dkt. Kacou 
Amepongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimamia vizuri nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kwamba uamuzi huo utaharakisha maendeleo ya nchi. Akizungumza na ujumbe huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameshukuru uamuzi wa Benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika Bajeti Kuu ya serikali kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS). 
Amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), pamoja na kununua ngege tatu za abiria ili kuboresha usafiri wa anga. 
“Vilevile tumeamua katika Bajeti ya mwaka huu kununua meli mpya itakayo tumika kutoa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa majini” Aliongeza Dkt. Mpango 
Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, serikali imejipanga kukuza sekta ya viwanda ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. “Mpango huo utakwenda sambamba na kuboresha sekta ya kilimo ili malighafi itakayozalishwa na wakulima, licha ya kuinua uchumi wa wakulima wetu, lakini pia viwanda vitapata malighafi ya kutosha” alisisitiza Dkt. Mpango 
Amerejea msimamo wa serikali kuwa haitakubali kupokea misaada inayoambatana na masharti magumu na isiyo na tija kwa nchi na kwamba jitihada zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo nchini zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili ziweze kutumika kuleta maendeleo. 
“Hatutakubali misaada isiyozingatia vipaumbele vyetu na ile inayohatarisha uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe” alieleza Dkt. Mpango.Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali wa kukusanya mapato yake ya ndani kwa kuwahimiza watu kulipa kodi na kubana matumizi yasiyo ya lazima umeanza kuleta matunda na kuongeza pia nidhamu ya matumizi ya pesa katika jamii. 


Ameiahidi Benki hiyo ya maendeleo ya Afrika-AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. 

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI..... PRF MBARAWA

by RORYA MAENDELEOraw1Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe alipotembelea kukagua ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.raw2Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akisalimiana na Wakazi wa kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.raw3Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimbeba mtoto aliyehudhuria kikao cha Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe mara baada ya kutoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.raw4Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akicheza na wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe waliokuwa na furaha mara baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.raw5Muonekano wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.raw6Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Iringa Bi. Elikael Manase akitoa maelezo kwa  Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari ya mmomonyoko wa ardhi unavyoathiri sehemu ambayo Mkongo wa Taifa umepita eneo la Lukumburu Mkoani Njombe.raw7Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mbele) akitoka kukagua eneo lililoathirika na mmomonyoko wa ardhi eneo la Lukumburu Mkoani Njombe.raw8Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati alipotembelea kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe.raw9Wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakimsikiliza Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea kuangalia utendaji kazi, Mkoani Njombe.raw10Wakazi wa Kijiji cha Usalule, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotoa taarifa ujenzi wa barabara ya Njombe–Makete yenye urefu wa KM 109.4 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
……………………………………………………………………………………………
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 109.4 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Njombe ili kurahisisha huduma ya usafiri wa barabara kwa wakazi wa mikoa hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo mkoani Njombe wakati akiongea na wakazi wa kijiji cha Usalule, kata ya Ulembwe, wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukagua barabara hiyo.
Profesa Mbarawa amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo imetenga kiasi cha sh.bilioni 19 katika bajeti ya mwaka  wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
“Tumejipanga na tuna nia dhabiti kuhakikisha barabara hii tutaijenga  kwa kiwango cha lami na katika kuharakisha kazi hii tutatafuta makandarasi wawili  ili ujenzi huu ukamilike kwa haraka”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewataka wananchi kushirikiana na Makandarasi watakapoanza ujenzi huo ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kulete tija kwa wananchi wa Mikoa ya kanda ya kati.
Amesema kuwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Njombe upo katika hatua za kutangaza zabuni ili kupata Makandarasi wenye uwezo wa kujenga barabara hiyo kwa kuzingatia viwango kulingana na mkataba.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Eng. Yusuph Mazana amesema kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Njombe-Makaete yenye urefu wa KM 109.4 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umekamilika na Mhandisi mshauri M/s Crown Teach Consult Ltd ameshawasilisha taarifa ya usanifu wa kina.
“Tumepokea taarifa ya usanifu wa kina kutoka kwa Mhandisi Mshauri hivyo tunahaidi  kusimamia utekelezaji wa mradi huu kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani”,amesisitiza Eng. Mazana.
Waziri Prof. Mbarawa ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara hiyo Mkoani Njombe.

MH. LUHAGA MPINA ATEMBELEA KIWANDA CHA PEPSI


lug1Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina (Kulia) akifurahia Jambo na Meneja Mahusiano wa kiwanda cha Pepsi bw,Alexander Nyirenda alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kiwalani Temeke Jijini Dar es salaaam mapema hii leo.        
lug2Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa ameambatana na Maafisa wa Mazingira kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira Nchini( NEMC)akikagua mfereji unaotiririsha maji machafu kutoka katika kiwanda hicho na kusababisha madhara kwa wanainchi wanaozunguka eneo hilo.       
lug3Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha Pepsi kilichopo Kiwalani,Temeke jijini dar es salaam           

CHADEMA NA MAKONDA VITANI DAR AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NI *BATILI* NA HALIWEZI KUTEKELEZEKA.


YAH: KUTAARIFU WANANCHI WA DAR ES SALAAM YA KWAMBA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NI *BATILI* NA HALIWEZI KUTEKELEZEKA.




Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki Meya Isaya Mwita Charles anapenda kutoa ufafanuzi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam Juu ya agizo ka Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliyeagiza kuwe na msako wa nyumba kwa nyumba kutambua wasio na kazi maalum.

Yafuatayo ni muhimu sana kutambuliwa na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kama *haki* yao ya msingi kabla ya utekelezwaji wa Amri hii ya Mkuu wa Mkoa.

Kwanza zoezi hili ni BATILI na haliwezi kutekelezeka kwenye Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam kwa sababu za msingi zifuatazo:

*i)* Sheria ya makosa ya Jinai Inaelezea utaratibu wa kukaguliwa nyumbani kama search warrant ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na ambayo Inaelezea wanatafuta nini.

*ii)* Sheria hiyo pia inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikishia ushahidi wa uongo.

*iii)* Kamwe popote duniani Kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.

*iv)* Kwa maagizo hayo inasemekana wananchi watawekwa ndani Kwa kukataa kutii agizo hilo, hakuna sheria Tanzania inayoruhusu Mwananchi kuwekwa ndani kwasababu za hovyo Kama hizo.

Naomba nimalizie Kwa kusema wananchi wote wa Jiji la Dar wawe na Amani kabisa na wajue haki zao na wajue kuzitetea, sisi viongozi wao tupo imara kusimamia haki zao na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.