Saturday, July 15, 2017

Ufahamu Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo kiundani

Rorya maendeleo Blog. 13 hours ago

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. 

Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'. 

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'. 

Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO  
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu. 

Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers' Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo. 

Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo. 

Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo. 

Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda. 

Chembe za urithi 'Genetics':  Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia. 
Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. 

Matumizi ya pombe/vilevi:  Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe. 

Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa. 

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO  
Hata hivyo ni mara chache sana mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili. 
Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi:- 

Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. 
Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain' 
Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. 

Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo. 

Kushindwa kumeza vizuri chakula. Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni. Kujisikia vibaya baada ya kula. Kupungua uzito. Kukosa hamu ya kula. Kutapika damu. Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito. Kichefuchefu & kutapika. 

JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:- 
Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteka wake ni vidonda vya tumbo. 

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-  

Kupima damu 'Blood test'  
Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative' 

Kupima pumzi 'Breath test' 
Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi. 

Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'  
Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi.  Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria. 

X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'  
Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray. 

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'. 

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO  
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa. 

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole. 

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni. 

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol. 

Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine,    hutumika kama mbadala kama dawa aina ya 'PPIs' hazitokuwepo. 

H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo 'Histamine' ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni. 

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka. 

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

Watu wanaokunywa kahawa wanaishi miaka mingi: Utafiti

Rorya blog 5 hours ago

Ukikunywa vikombe vitatu vya kahawa kwa siku unaweza kuishi miaka mingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa karibu watu nusu milioni kutoka nchi 10 za Ulaya. 

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida na Annals of Internal Medicine, unasema kuwa unywaji wa kahawa unaweza kuongeza maisha ya mtu. 

Lakini wataalamau wanasema kuwa ni vigumu kusema kuwa ikiwa ni unywaji kahawa unachangia watu kuishi miaka mingi au ni maisha ya kiafya wanayoishi wanywaji kahawa. 

Watafiti kutoka shirika la Agency for Research on Cancer and Imperial College London, wanasema wamegundua kuwa unywaji wa kahawa nyingi unahusiana na hatari kidogo ya kufariki hasa kutokana na magonjwa ya moyo. 

Waliafikia uamuzi baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 35 kutoka nchi 10 za Ulaya. 

Waliawauliza watu wakati wakianza utafiti kuhusu kiasi cha kahawa walikuwa wakinywa kisha wakaangali vifo vilivyotokea katika kipindi cha miaka 16. 

Lakini cha kuvunja moyo kwa wanywaji wa kahawa, ni kuwa ugunduzi huu haueleweki vyema. 

Kwa mfano haukuonyesha ni kipato cha kiwango gani wanywaji pombe hupata ikilinganishwa na wale wasiokunywa kahawa. 

Huenda ikawa labda watu walio na uwezo wa kununu vikombe vitatu vya kahawa kila siku wana pesa zaidi, na kwa njia moja au nyingine huwasaidia kulinda afya zao.  miaka mingi: Utafiti

Muungwana Blog · 5 hours ago

Ukikunywa vikombe vitatu vya kahawa kwa siku unaweza kuishi miaka mingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa karibu watu nusu milioni kutoka nchi 10 za Ulaya. 

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida na Annals of Internal Medicine, unasema kuwa unywaji wa kahawa unaweza kuongeza maisha ya mtu. 

Lakini wataalamau wanasema kuwa ni vigumu kusema kuwa ikiwa ni unywaji kahawa unachangia watu kuishi miaka mingi au ni maisha ya kiafya wanayoishi wanywaji kahawa. 

Watafiti kutoka shirika la Agency for Research on Cancer and Imperial College London, wanasema wamegundua kuwa unywaji wa kahawa nyingi unahusiana na hatari kidogo ya kufariki hasa kutokana na magonjwa ya moyo. 

Waliafikia uamuzi baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 35 kutoka nchi 10 za Ulaya. 

Waliawauliza watu wakati wakianza utafiti kuhusu kiasi cha kahawa walikuwa wakinywa kisha wakaangali vifo vilivyotokea katika kipindi cha miaka 16. 


Lakini cha kuvunja moyo kwa wanywaji wa kahawa, ni kuwa ugunduzi huu haueleweki vyema. 

Kwa mfano haukuonyesha ni kipato cha kiwango gani wanywaji pombe hupata ikilinganishwa na wale wasiokunywa kahawa. 

Huenda ikawa labda watu walio na uwezo wa kununu vikombe vitatu vya kahawa kila siku wana pesa zaidi, na kwa njia moja au nyingine huwasaidia kulinda afya zao. 

Jaffo awatahadhalisha ma-Ded, na Ma-DC Kuhusu Utapeli

Rorya maendeleo Blog 1 hour ago


VIONGOZI wa kada mbalimbali nchini, wametahadharishwa kuwa makini na watu wanaofanya vitendo vya utapeli kwa kutumia majina na picha za viongozi wa juu, wakiwamo mawaziri ili kujipatia fedha.. 

Tahadhari hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Tamisemi), Selemani Jafo, alipokuwa akifunga mafunzo ya viongozi hao kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo ni ya awamu ya pili kutolewa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na ofisi ya Rais Tamisemi na yamejumuisha viongozi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa. 

Jafo alisema kumeibuka wimbi la utapeli wa kutumia majina ya viongozi kuwalaghai viongozi mbalimbali kwenye wilaya kutuma fedha. 

“Kumekuwapo na watu wanatumia picha na majina ya viongozi kutuma ujumbe mfupi wa kuwataka wakuu wa wilaya au mikoa na wakurugenzi kutuma fedha wakidai kuwa kiongozi fulani amepatwa na jambo fulani la dharura. Naomba mjiepushe na watu hawa kwa kuwa ni matapeli,” alisema Jafo. 

Alisema matapeli hao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi wa ngazi za juu serikalini kwa madai kwa wanauguliwa au wamepata shida mbalimbali wawapo safarini jambo ambalo si kweli. 

“Nataka kuwapa angalizo kuweni makini. Kama mtu atakuwa na shida kama ni waziri atampigia katibu wake au atatumia nafasi yake kutoa taarifa ili kupatiwa huduma lakini si kwa kupigiwa simu au kutuma ujumbe mfupi,” alisema Jafo. 

Aidha, aliwataka kusimamia mipango ya maendeleo iliyopo kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha na kuhimiza wafanye kazi kwa manufaa ya Taifa na siyo kwa manufaa yao. 

Jafo aliwataka wakatumie mafunzo hayo kama chachu ya kuwafanya kuwa na weledi mkubwa zaidi tofauti na ilivyo kuwa hapo awali. 

Nabu Waziri Jafo aliwataka wakurugenzi kutozalisha madeni ya watumishi katika halmashauri zao. 

“Hakuna sababu yoyote ya halmashauri kuwa na madeni ambayo hayana msingi na msiwahamishe watumishi bila kuwa na maandalizi ya malipo,” alisema. 

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Denis Rweyemamu, alisema mafunzo yanalenga kuwajengea uwezo ili kufanya kazi kwa malengo ya maendeleo. 

Alibainisha kuwa licha ya viongozi hao kufanya kazi vizuri, bado walitakiwa kupata mafunzo ili kuongeza weledi katika utendaji kazi.

Serikali yagoma kupokea Misaada yenye Masharti haya

Rorya maendeleo Blog. 1 hour ago



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Taifa halipo tayari hata kidogo kupokea misaada yenye masharti ambayo haiendani na mila na desturi za Kitanzania. 

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Craca Machel pamoja na ujumbe walioambatana nao Ikulu- Jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kuna baadhi ya wafadhili wanaisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na bajeti vizuri sana na bila masharti mabaya lakini kuna baadhi ya wafadhili wanaonyesha wazi kuwa wanataka Serikali ikubali masharti yao ambayo yanaenda kinyume na maadili ya taifa kitu ambacho hakiwezekani. 

Amesema kutokana na changamoto hiyo Serikali itaendelea kusimamia maadili ya Taifa ipasavyo na imeweka mipango na mikakati mizuri kwa ajili ya kuongeza mapato yake ya ndani ili kuondokana na utegemezi kutoka kwa baadhi ya wafadhili ambao baadhi yao wanaahidi kuchangia bajeti kuu ya Serikali lakini mwisho hawafanyi hivyo. 

Kuhusu Sekta ya afya, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imeongeza maradufu bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa viwango vinavyotakiwa nchini. 

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Graca Machel, Craca Machel waipongeza Serikali kwa jitihada inazozifanya katika uimarishaji wa sekta ya afya nchini na wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa ipasavyo.

Rooney asepa na Wachezaji wanne wa Bongo

Rorya maendeleo

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema wanatarajia kuandaa mpango maalumu wa kuwasaidia wachezaji wa hapa nchini angalau wanne kila mwaka kwenda England kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. 

“Tunataka soka la Tanzania ilipige hatua ili siku moja na sisi tuwe na wachezaji wanaocheza  katika Ligi Kuu England. 

 “Tunajipanga ili tuweze kuleta maskauti hapa nchini kwa ajili ya kuangalia wachezaji na ikiwezekana angalau kila mwaka Watanzania wanne waweze kwenda England kwa ajili kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa ili siku moja tuweze kuwaona wakipambana na akina Rooney katika ligi kuu ya nchi hiyo,” alisema Tarimba.

Friday, July 14, 2017

Kesi ya Mbowe na DC yaanza kusikilizwa

Rorya maendeleo· 2 hours ago

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Moshi, jana ilianza kusikiliza kesi inayomkabili Mkuu wa Wilaya (DC) ya Hai, Gelasius Byakanwa. 

Kiongozi huyo amefunguliwa kesi na Kampuni ya Kilimanjaro Veggies Ltd, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. 

Katika shauri hilo, kampuni hiyo inamlalamikia mkuu huyo wa wilaya kwa kushiriki kuharibu shamba la mboga mboga linalomilikiwa na Mbowe katika Kijiji cha Nshara wilayani Hai, Mkoa wa Kilimajnaro. 

Wakili wa upande wa utetezi anayemwakilisha mkuu huyo wa wilaya, Modestus Njau, aliiomba mahakama hiyo kukubali ombi la 

kumjumuisha katika shauri hilo Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutokana na umuhimu wake. 

Pamoja na hayo, wakati kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Aishael Sumari ikiendelea, upande huo wa utetezi uliiomba 

mahakama hiyo iahirishe shauri hilo ili kupata muda mzuri wa kupitia madai ya mlalamikaji. 

Akizungumza mahakamani hapo, wakili huyo alidai kuna umuhimu wa kumjumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi 

hiyo kwa kuwa mshtakiwa ni mkuu wa wilaya na anashtakiwa kutokana na majukumu ya Serikali aliyokuwa akiyatekeleza. 

Kwa mujibu wa Wakili Njau, sheria ya Tamisemi ya mwaka 1997, sehemu ya 14, kifungu kidogo cha kwanza na cha pili, kinataja kazi za mkuu wa wilaya na majukumu yake na kwamba majukumu hayo ndiyo yaliyosababisha afikishwe mahakamani. 

Kutokana na maombi hayo, Wakili wa Kampuni ya Uwakili ya D’Souza & co ya jijini Arusha inayoiwakilisha Kampuni ya Mbowe, Meirad Souza, alikubaliana na maombi hayo, lakini akataka yawasilishwe kwa maandishi. 

Akitoa uamuzi wake, Jaji Sumari alimtaka mdaiwa kuleta majibu pinzani ya kiapo, Julai 27 mwaka huu na mlalamikaji arudishe majibu Agosti 3, 

mwaka huu. 

Pamoja na hayo, Jaji Sumari aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa. 

Juni 30 mwaka huu, Kampuni ya Uwakili ya D’ Souza & Co ya jijini Arusha, kwa niaba ya Kampuni ya Kilimanjaro Veggies Ltd, 

inayomilikiwa na Mbowe, ilimfungulia kesi mkuu huyo wa Wilaya ya Hai na kumtaka alipe fidia ya zaidi ya Sh milioni 549.3. 

Katika kesi hiyo namba 20/2017 yenye maombi madogo namba 51/2017, mdai anaomba zuio la muda liweze kutolewa dhidi ya mkuu huyo wa wilaya ili asifanye chochote katika shamba lililoharibiwa mazao lenye ukubwa wa ekari 2.7.

ACACIA kulipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini

ACACIA kulipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini

.Kampuni inayomiliki Makampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA imesema italipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini. 

Sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katka sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali, ambapo asilimia 1 ni kwaajili ya usafirishaji kwenda nje.