Friday, June 17, 2016

DRFA, KIFA WAITWA TFF


indexShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Kinondoni (KIFA) uliofanyika Juni 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.
Kutokana na malalamiko hayo, TFF imewaita wagombea wote wa ngazi ya juu wa KIFA wakiwamo viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho kitakachofanyika kesho Jumamosi Juni 18, 2016 saa 3.00 asubuhi.
Pia, imewaita viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sambamba na Kamati za Uchaguzi za DRFA kadhalika ile ya KIFA ambazo zilisimamia uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa mara ya pili mwishoni mwa wiki baada ya ule wa kwanza kuahirishwa mwezi uliopita.

SERIKALI KUONGEZA MUDA WA KUFUNGA MADUKA MAKUBWA (SHOP MALLS) DAR ES SALAAM


p.txtNa: Frank Shija, MAELEZO
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inakusudia kuruhusu baadhi ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda wa kawaida wa maduka kufungwa ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  alipomwakilisha Makamu wa Rais kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo linatokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo kwa wafanyakazi  kwani uchelewa kutoka maofisini jambo lilalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya mambo muhimu matatu katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuongeza muda wa kufunga maduka hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa pikipiki wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu matatu ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza muda wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na desturi ya kuwajali wateja wao hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na wateja wao walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo wakustahilifunga hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia pale panapohitajika msaada wao kama ambavyo wamekuwa wakitoa misaada katika kuchangia huduma za kijamii kama vile madawati.

KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA


Naibu Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto),akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ting, Father Fernandez, wakati akipokea msaada wa mageti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Juni 17, 2016. Kampuni hiyoimetoa mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44.
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID KAMPUNI
———————————————————————-
YA kusambaza ving’amuzi vya televisheni ya Ting ya jijini Darves Salaam, imekabidhi mageti ya chuma  27 kwa
uongozi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ili kuwadhibiti “wakora” wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki za maji.
Akipokea msaada huo leo Juni 17, 2016 kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanjanin hapo,
Naibu Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura, ameishukuru
kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utakomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa miundo mbinu ya uwanja huo wa soka wa kisasa kabisa hapa nchini “Mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, nilifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
uwanja huu na kujionea uharibifu mkubwa kwenye vyoo ambapo koki za maji zimeibiwa na hivyo kusababisha baadhi ya vyoo kufungwa na kupelekea usumbufu mkubwa kwa mashambiki was ok.” Alisema Naibu waziri. Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ting, Mchungungaji Dkt. Veron Fernandosalisema kampuni yake ambayo inajishughulisha na uagizaji na usambazaji wa ving’amuzi, imeona inao wajibu mkubwa wa kusaidia sekta ya michezo kwenye eneo hilo la kutunza
miundombinu ya uwanja wa Taifa.
Alisema, Ting imetoa jumla ya mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44 ambayo
yatasaidia kudhibiti wezi wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki na kuharibu miundombinu mingine.
K-VIS
MEDIA imeshuhudia koki za maji kwenye baadhi ya vyoo zikiwa zimeng’olewa.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt. Vernon Fernados, akimuonyesha moja ya mageti hayo Naibu Waziri Anastazia James Wambura
 Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye vyoo vya juu vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeathirika sana na wizi huo, Mageti hayo yatafungwa kwenye vyoo hivyo vya juu uwanja mzima
Continue reading →

WAFANYAKAZI WA HOTELI YA SOUTHERN SUN WAFANYA USAFI KWENYE FUKWE ZA BAHARI YA HINDI


WAFANYAKAZI  wa Hoteli ya Southern Sun ya jijini Dar es Salaam leo wameadhimisha Siku ya Usafi wa Fukwe za Bahari Duniani kwa kufanya usafi wa kwenye fukwe za maeneo ya Salender Bridge jijini Dar es Salaam.
 
Wafanyakazi hao wamesema wamechukua hatua hiyo ili kuthamini siku hiyo inayoadhimishwa duniani kote na kuionesha dunia kwamba Tanzania ni moja ya nchi zinazojali hatua hiyo ya kuziweka fukwe za bahari katika hali ya usafi kwa ajili ya kuviokoa viumbe mbalimbali vinavyoishi baharini.
Aidha akizungumza na Blog ya Bayana Mratibu wa shughuli hiyo, Halima Nneka, alisema kuwa hiyo wao imekuwa ni tabia yao ya kufanya usafi kwenye sehemu mbalimbali za fukwe za bahari kwa kuwa wanathamini sana mazingira hayo kuwa katika hali ya usafi kwani inasaidia hata vijana na watu wanaotembelea maeneo hayo kujali na kuiga mfano wao huo.
“Kwakweli huwezi ukaenda pahala ambako ni safi, halafu wewe uitumie sehemu hiyo na kisha  uiwache ikiwa katika hali ya uchafu. Kwa mtu mstaarabu lazima naye atafanya usafi katika sehemu hiyo, aliyoikuta ikiwa safi kabla ya kuitumia,”alisema Mneka.
Aidha amezitaka Taasisi mbalimbali jijini Dar es Salaam, zilizoko kwenye maeneo ya Bahari kutenga walau hata siku moja katika mwezi kwa ajili ya kufanya usafi wa mazingira kwenye sehemu za fukwe za bahari, kwani ni sehemu ambazo jamii na wageni mbalimbali wanaoingia nchini hupenda kutembelea kwa ajili ya kupumzika na kupata hewa safi.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Southern Sun ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kufanya usafi kwenye fukwe za maeneo ya Salender Bridge jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha Siku ya Usafi wa Fukwe za Bahari Duniani leo. 

NAIBU SPIKA AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA CHINA


 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang wakati alipofanya mazungumzo na Kamati hiyo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akizungumza na Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje
kutoka Bunge la China
  kushoto  ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang ambaye pia ni Kiongozi wa
Msafara huo.
 Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang (katikati) akisanini Kitabu cha Wageni alipomtembelea Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
 Kiongozi wa Msafara Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang  akimkabidhi Naibu Spika Dkt Tulia Ackson zawadi mara baada ya kuzungumza nae ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akiangalia zawadi aliyopewa na  na Kiongozi wa Msafara Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang
mara baada ya kuzungumza nao ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Bunge)