\
KATIBA YA ACT SASA NJEEEEEEE
KERO NA SHIDA ZA WANAINCHI ZITAWEZA KUTATULIWA HENDAPO WATAYATEKELEZA HAYA .
(ALLIANCE
FOR CHANGE AND TRANSPARENCY)
(ACT-Wazalendo)
Chama
cha Wazalendo
KATIBA
TOLEO LA 2015
Kama ilivyoidhinishwa
naMkutano Mkuu wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Jumamosi Tarehe 28 Machi 2015
Ukumbi wa Kadinali
Rugambwa, Dar es Salaam.
YALIYOMO
KWA KUWA tumeamua kupambana dhidi
ya rushwa, ufisadi, uzembe na uvivu;
NA KWA KUWA tumeamua kuhakikisha
kuwa maliasili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima
itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na kuleta maendeleo sawia na endelevu
ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa;
NA KWA KUWA tumeamua kujenga Chama
cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na
unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato
na kwa kuzingatia misingi ya haki kwa watu wake wote;
NA KWA KUWA tumeamua kushiriki
katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Mwafrika
na kujenga bara lenye sauti yenye nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa
ulimwenguni;
NA KWA KUWA tumeamua kupigania
demokrasia, umoja, utu, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa;
NA KWA KUWAkwa nia moja tumeamua
kujenga Chama chenye kufuata misingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic Socialism), na misingi asili
iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) ikiwemo Azimio la Arusha[1];
na
NA KWA wajibu tulio nao wa kujenga,
kukuza na kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania;
HIVYO BASI; Sisi Wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wazalendo (ACT) uliofanyika Dar es salaam leo tarehe
28 Machi 2015, tumepitisha
KATIBA MPYAya Chama chetu itakayojulikana kama
KATIBA MPYAya Chama chetu itakayojulikana kama
KATIBA YA ACT YA MWAKA
2015.
SURA YA KWANZA
JINA, MAKAO MAKUU, ALAMA, ITIKADI, LUGHA, MISINGI NA MALENGO
YA CHAMA
SEHEMU YA I
JINA, MAKAO MAKUU, ALAMA, ITIKADI NA LUGHA
Jina la Chama
litakuwaniALLIANCE FOR CHANGE AND
TRANSPARENCY
2. Makao Makuu ya Chama
(1)Makao Makuu ya
Chama yatakuwa ni Dar es Salaam
(2)Kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibarna Mwanza.
(2)Kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibarna Mwanza.
(1) Alama za Chama zitakuwani:
i.
Rangi za Chama ambazo ni Zambarau na Nyeupe;
ii.
Bendera ya Chama ambayo itakuwa ni ya rangi ya
Zambarau ama Nyeupe ikiwa na nembo ya chama katikati ya bendera;
iii.
Nembo ya Chama
iv.
Wimbo rasmi wa Chama
v.
Vazi rasmi la Chama.
(2) Halmashauri Kuu ya
Chama itatengeneza na kufafanuamuundo na yaliyomo
ndani ya Nembo ya Chama, Wimbo rasmi wa Chama na Vazi rasmi la Chama
kupitia Kanuni za uendeshaji Chama zitakazotungwa na Halmashauri Kuu ya
chama. Halmashauri Kuu itakuwa na uwezo wa kubadili alama za chama kutokana na mahitaji ya wakati.
ndani ya Nembo ya Chama, Wimbo rasmi wa Chama na Vazi rasmi la Chama
kupitia Kanuni za uendeshaji Chama zitakazotungwa na Halmashauri Kuu ya
chama. Halmashauri Kuu itakuwa na uwezo wa kubadili alama za chama kutokana na mahitaji ya wakati.
4. Itikadi na Falsafa ya ACT:
(1)
ACT inaamini katika msingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic Socialism).
Misingi mikuu ya
ujamaa wa Kidemokrasia ni:
i.
Undugu;
ii.
Usawa;
iii.
Uhuru;
iv.
Heshima kwa kila mtu; na
v.
Demokrasia
(2)
Falsafa ya ACT ni UNYERERE, ikiwa ni dhamira ya
kurudisha, kuhuisha na kupigania misingi mama iliyoasisi Taifa la Tanzania,
kama ilivyoainishwa katika Azimio la Arusha na kwa mazingira ya Tanzania ya
sasa.
(3)
Shabaha
kuu ya ACTni kupigania na kusimamia uwajibikaji na uwazi nchini Tanzania
na Afrika kwa ujumla na kwamba mabadiliko ni ajenda ya kudumu.
(4) Chama kinazingatia elimu, uadilifu, uwajibikaji,
kujitegemea na bidii katika kazi kama njia kuu za kujikomboa dhidi ya umaskini,
ujinga, maradhi na rushwa, ambavyo ndio maadui wakuu wa Taifa la Tanzania na
Afrika kwa ujumla.
(1) Lugha rasmi ya
chama itakuwa niKiswahili.
(2) Bila kuathiri ibara ndogo ya (1) ya
ibara hii hapo juu, lugha ya Kiingereza
inaweza kutumika sambamba na lugha ya Kiswahili inapobidi.
inaweza kutumika sambamba na lugha ya Kiswahili inapobidi.
(3) Nyaraka
zote muhimu, ikiwemo Katiba hii, zitaandikwa katika lugha ya Kiswahili na
kutafsiriwa katika lugha ya Kiingereza.
(4) Chama
kitaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano mbadala zikiwemo
lugha za alama kwa kadri ya mahitaji.
i)
Uzalendo
ii)
Usawa
iii)
Kupinga
na Kupiga Vita ubaguzi
iv)
Uadilifu
v)
Uwazi
vi)
Uwajibikaji
vii)
Demokrasia
viii)
Uhuru
wa Mawazo na Matendo
ix)
Utu
x)
Umoja
5) Misingi
hi itafafanuliwa katika nyaraka mbalimbali zitakazotolewa na Chama kwa mujibu
wa Katiba hii na Kanuni za uendeshaji wa Chama.
7. Malengo
ACT itapambana kuhakikisha kwamba inashinda uchaguzi
na kuunda serikali ili kutekeleza malengo yafuatayo:
i)
Kuhakikisha
kwamba serikali inatumia raslimali yote ya nchi kwa ajili ya kuondosha
umaskini, ujinga, maradhi, rushwa, na kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla;
(ii)
Kupigania
na kulinda uongozi bora na Utawala wa Sheria;
(iii) Kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia raslimali
na serikali inayowajibika kwa umma wa Watanzania;
(iv)
Kuhakikisha usawa mbele ya Sheria kwa
raia wote wanaume kwa wanawake bila kujali kabila, rangi, imani za kidini,
itikadi, utamaduni ama hadhi ya mtu kiuchumi na kijamii;
(v)
Kuendeleza na kudumisha Demokrasia na
utamaduni wa mfumo wa vyama vingi vya siasa;
(vi)
Kuchochea, kuimarisha na kulinda
uzalendo, uadilifu, uwajibikaji na uwazi kama misingi mikuu katika uongozi wa
nchi;
(vii) Kuchochea
na kuendeleza mapambano katika kulinda haki za watoto, wanawake na watu wenye
ulemavu;
(viii)Kupigania
haki na heshima ya wafanyakazi, wakulima, wafugaji na wajiasiliamali katika
ngazi zote;
(ix)
Kudhibiti soko huria ili kuhakikisha
kuwa haliathiri haki za utu za wafanyakazi na walaji wenye kipato cha chini;
(x)
Kulinda na kuendeleza mazingira bora kwa
vizazi vya leo na vijavyo;
(xi)
Kuhakikisha kuwa idhini, mikataba na
ushirikiano wa kikanda barani Afrika ambavyo Tanzania ni mwanachama kama vile
Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) vinaendana na misingi mikuu ya kidemokrasia
na kuendeleza kuheshimu utawala wa sheria Afrika;
(xii) Kuhimiza
ushirikiano na mahusiano na vyama vingine vinavyoamini katika demokrasia jamii
Afrika na duniani kote;na
(xiii) Kuunga
mkono na kusukuma mbele juhudi za kuundwa kwa Shirikisho la Kisiasa la Afrika
Mashariki na kupigania umoja wa Afrika.
SURA YA PILI
UANACHAMA NA UONGOZI
SEHEMU YA I
UANACHAMA
8.Uanachama wa ACT utakuwa wazi kwa raia wote
(1) Uanachama wa ACT
utakuwa wazi kwa raia wote wenye umri wa kupiga kura bila kubagua jinsia,
kabila, dini, au hali yoyote.
a) Kila
raia atakayekuwa ameandikishwa kuwa mwanachama wa ACT atapewa kadi ya uanachama
itakayoonyesha pamoja na habari nyingine, jina lake, anuani, saini yake na
saini ya afisa wa Chama aliyemwandikisha.
b) Kikundi
cha watu kinaweza kujiunga na ACT kama kikundi kwa umoja wao, na kwamba kikundi
hicho kinakubali itikadi na misingi ya kuanzishwa kwa ACT.
(2) Sifa mahsusi za mtu anayetaka kujiunga
uanachama wa ACT:
i.
Awe raia wa Tanzania;
ii.
Awe ana umri wa kupiga kura kwa mujibu wa Sheria
za Tanzania;
iii.
Awe anakubaliana na itikadi, falsafa na misingi
ya ACT;
iv.
Awe na akili timamu;
v.
Awe na moyo na utayari wa kukitumikia Chama na
kueneza itikadi, falsafa na misingi yake.
vi.
Aonyeshe uzalendo na upendo wa kuitumikia nchi
yake; na
vii.
Asiwe Mwanachama wa chama kingine cha siasa
baada ya kujiunga na ACT.
(3) ACT itakuwa na aina zifuatazo za wanachama:
i.
Wanachamawa Kawaida
Ni wanachama
wote waliojiandikisha na kulipa ada ya ACT na kuzingatia masharti ya Katiba
hii.
ii.
Wanachama Vikundi
Ni
wanachama wanaotokana na jumuiya, taasisi, mashirika au vikundi mbalimbali
ambavyo vimeamua kujiunga na Chama kupitia umoja wao.
iii.
Wanachama
wanafunzi
Hawa
ni wanachama ambao hawajatimiza umri wa kupiga kura na ambao wanajiandaa
kujiunga na Chama siku za usoni
9.Ada ya Uanachama
(1) Kila
mwanachama atawajibika kulipa ada za uanachama kama itakavyoainishwa kwenye
Kanuni za Uendeshaji Chama zitakazotungwa na Halmashauri Kuu ya Chama.
(2) Bila
kuathiri Sheria zinazohusu vyama vya siasa nchini, pamoja na misingi na masharti
ya Katiba hii, kila mtu au kundi la watu wanaokubaliana na misingi, malengo,
sera na mipango ya Chama wanaweza kutoa ada ya kundi la uanachama.
(3) Kutakuwa
na kiingilio kwa kila mwanachama na kundi lolote litakalotaka kujiunga na Chama
itakavyoainishwa kwenye Kanuni za Uendeshaji Chama zitakazotungwa na
Halmashauri Kuu ya Chama
(4) Utaratibu
wa ulipaji wa kiingilio na ada vitafafanuliwa katika kanuni za Uendeshaji
Chama.
10. Haki za mwanachama wa ACT
(1) Kila mwanachama wa ACT atakuwa na
haki ya:
i.
Kushiriki shughuli zote za Chama kwa mujibu wa
kanuni na taratibu zilizowekwa;
ii.
Kusikilizwa na kuuliza maswali kuhusu maendeleo
na mwenendo wa Chama;
iii.
Kuchagua
na kuchagliwa kuwa kiongozi ndani ya Chama;
iv.
Kuwasilisha pendekezo au maelezo kwenye kikao
chochote cha Chama, hadi katika ngazi ya Halmashauri Kuu;
v.
Kukosoa kiongozi yeyote ndani ya vikao vya
Chama;
vi.
Wajumbe wanaweza kuitisha kikao chochote endapo
tu asilimia sabini na tano ya wajumbe wa kikao hicho watatia saini kuhitaji
kikao hicho kiitishwe;\
vii.
Bila kuathiri yaliyomo katika kipengele (f) hapo
juu, wajumbe wanaohitaji kikao hicho lazima waonyeshe kuwa viongozi katika
ngazi husika wameshindwa kuitisha vikao hivyo zaidi ya mara tatu kwa mujibu wa
katiba na utaratibu wa kuitisha vikao vya namna hiyo utafafanuliwa kwenye
kanuni za Chama.
(2) Kila
mwanachama wa ACT atakuwa na wajibu wa:
a) Kujifunza
na kupanua uelewa kuhusu itikadi, falsafa na misingi ya ACT;
b) Kushiriki
kikamilifu katika kuhakikisha kwamba ACT inashinda katika chaguzi mbalimbali
zitakazoitishwa nchini kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi;
c) Kuzingatia
nidhamu ya ACT;
d) Kushiriki
kikamilifu katika shughuli za Chama na kutekeleza kwa vitendo sera na maamuzi
ya Chama;
e) Kushiriki
kikamilifu katika kukomesha vitendo vyovyote ndani na nje ya Chama vinavyoweza
kuhatarisha uhai na maslahi ya Chama;
f) Kueneza
itikadi, falsafa na misingi ya ACT kwa umma, na kujifunza mahitaji ya umma kwa
wakati na kuhakikisha kwamba yanazingatiwa katika sera za Chama;
g) Kuwa
mfano na sura ya ACT kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na umakini; na
h) Kulipa
ada na kuchangia mchango wowote kwa mipango maalumu na shughuli za ACT kama
itakavyokuwa imeamuliwa na vikao vya Chama.
11. Kukoma Uanachama
i.
Mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa:
ii.
Atajiuzulu mwenyewe kwa hiari yake kwa kuandika
barua kwa Katibu wa ngazi yake au Katibu Mkuu kwa kueleza kusudio la kuacha
kuwa mwanachama na kurudisha kadi ya uanachama;
iii.
Kujiunga na chama kingine cha siasa;
iv.
Kufukuzwa uanachama kwa mujibu wa kanuni
zilizowekwa katika Katiba hii; au
v.
Atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa
katika Katiba hii.
(2)
Mwanachama
anaweza kusimamishwa uanachama ili kupisha uchunguzi kuhusu mwenendo wake
utakaofanywa na Kamati ya Uadilifu katika ngazi husika.
(3)
Mwanachama
anaweza kufukuzwa kwenye Chama kwa sababu zinazotokana na mwenendo usiofaa kwa
mujibu wa masharti na Kanuni za Katiba hii, namara baada ya kufukuzwa,
uanachama wake utakoma.
(4)
Pamoja na sababu nyingine kama zilivyoelezwa
katika katiba hii na kanunizitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote
ambayeatasaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama
kingine
au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote
kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT.
au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote
kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT.
(5)
Hakuna mwanachama atakayesimamoshwa au kufukuzwa
uanachama hadipale ambapo mashart yaliyoainishwa katika Katiba hii na Kanuni za
Uendeshaji Chama yatakapokuwa yamefuatwa.
(6)
Uamuzi wa
kumsimamisha uanachama ama kumfukuza mwanachamayeyote hautakuwa na nguvu hadi
pale uamuzi huo utakapokuwa umewasilishwa kwa mwanachama husika kwa maandishi.
(7)
Bila kuathiri ibara ndogo ya (6) ya ibara hii,
mwanachama ambaye atakataakupokea taarifa ya maandishi juu ya uamuzi wa
kusimamishwa au kufukuzwa uanachama uliochukuliwa dhidi yake, atahesabika
kwambaameshawasilishiwa taarifa hiyo kwa mujibu wa ibara ndogo ya (6) na
uamuziwa kumsimamisha au kumfukuza uanachama utakuwa na nguvu.
(8)
Kila mtu ambaye amekoma kuwa mwanachama
atalazimika kurudisha mali za Chama zilizo chini yake. Hata hivyo, ada,
michango na mali zingine ambazo atakuwa amechangia alipokuwa mwanachama hazitarudishwa
(9)
Pale mwanachama atakapokuwa amepoteza uanachama
wake kwa njia yoyote ile anaweza kuomba tena uanachama wa ACT na anaweza
kukubaliwa kuwa mwanachama tena kwa mujibu wa Katiba hii, labda tu pale ambapo
Halmashauri Kuu ya ACT itakuwa imeamua vinginevyo.
(1) Kutakuwa na
rejesta ya orodha ya wanachama wote katika kila Tawi,
Kata na katika kila Jimbo la
Uchaguzi, na rejesta hii itahuishwa kila baada ya miezi sita. Makatibu wa Chama
katika ngazi husika watatuma orodha ya wanachama kwa ngazi inayofuata kwa ajili
ya kumbukumbu za Chama katika kila ngazi.
(2)
Katibu wa Chama Mkoa atatunza orodha ya
wanachama wote kwenye mkoa wake na atapokea orodha ya wanachama wote
walioandikishwa kila jimbo katika mkoa wake.
(3)
Sekretariati ya Chama Makao Makuu itatunza
rejesta ya wanachama wote nchi nzima.
Kila
mwanachama wa ACT atatoa ahadi tano zifuatazo:
i)
Nitapambana
dhidi ya dhuluma, fitina, unafiki uongo, rushwa na ufisadi kwa uwezo wangu
wote;
ii)
Nitapambana
dhidi ya umasikini na nitasimamia utajiri wa nchi yangu kwa faida ya wote;
iii)
Nitashiriki
kujenga Taifa lenye kujitegemea, lisilo na unyonyaji, ubaguzi na lenye misingi
ya Haki;
iv)
Nitashiriki
kujenga Umoja wa Afrika; na
v)
Nitapigania
kuwepo kwa demokrasia ndani na nje ya Chama changu.
vi)
Nitajielimisha
kila mara na nitatumia elimu yangu kwa manufaa ya jamii na Tanzania kwa ujumla
SEHEMU YA II
UONGOZI
14. Sifa za Kiongozi
Sifa, mwenendo na maadili
ya Kiongozi wa ACT
1) Sifa,
mwenendo na maadili ya viongozi wa ACT vimeainishwa kwa kina kwenye Kanuni za
Mwenendo na Maadili ya Viongozi wa ACT.
2) Kanuni
za Mwenendo na Maadili ya Viongozi zimeambatanishwa kama Nyongeza ya kwanza na
ni sehemu ya Katiba hii.
15. Aina za Viongozi
i.
Viongozi wa kuchaguliwa na mikutano
mikuu ya kila ngazi;
ii.
Viongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa na
vikao vya uongozi katika ngazi mbalimbali za Chama;
iii.
Viongozi watakaoteuliwa na Kiongozi Mkuu
wa chama kwa mujibu wa Katiba hii
iv.
Watendaji/waajiriwa/watumishi katika
Chama;
v.
Viongozi wa Ngome za Chama
watakaochaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa katiba hii na kanuni za ngome zao;
na
vi.
Viongozi wanaotokana na nafasi zao kama
zilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile Diwani,
Mbunge, Waziri, Waziri Mkuu, Rais, n.k.
(2) Kila kiongozi aliyechaguliwa au
kuteuliwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa
Chama atashika wadhifa wake kwa kipindi
cha miaka tano.
(3) Halmashauri Kuu inaweza kuitisha
uchaguzi wakati wowote kabla ya muda wa miaka mitano kwisha kama itaona inafaa
na ni kwa manufaa ya Chama na/au Taifa na viongozi ambao muda wao wa uongozi
utafupishwa kwa mujibu wa ibara ndogo hii watahesabika kwamba wamekaa
madarakani kwa kipindi cha miaka mitano
(4)
Kiongozi
aliyechaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, atashika wadhifa wake hadi
kipindi cha Uchaguzi Mkuu alichochaguliwa/teuliwa kwisha na anaweza kugombea au
kuteuliwa kwa kipindi kingine cha miaka mitano ambacho kitakuwa ndio ukomo wake
wa kugombea au kuteuliwa kushika nafasi hiyo.
(5)
Kiongozi
aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena, mradi awe
ametimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi. Isipokuwa mwanachama yeyote waACT atakuwa kiongozi kwa vipindi visivyozidi viwili
katika nafasi moja ya uongozi katika ngazi husika.
(6)
Ibara hii itahusu
pia viongozi wa NGOME za ACT-Vijana, Wazee na Wanawake.
(7)
Kwa muktadha wa
ibara ndogo ya (5) ya ibara hii, Kiongozi aliyechaguliwa/kuteuliwa kushika
wadhifa kwa kuziba nafasi iliyoachwa wazi atahesabiwa kwamba amekaa kwenye
wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano ikiwa amedumu kwenye nafasi hiyo kwa
kipindi cha miaka miwili au zaidi
16. Haki za Kiongozi
Pamoja na haki
za mwanachama zilizoanishwa katika Katiba hii, Kiongozi wa
ACT pia ana haki zifuatazo:
i) Haki
ya kukiwakilisha Chama katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali;
ii) Kuandaa
na kupendekeza programu mbalimbali za Chama ili kuleta ustawi katika Chama;
iii) Haki
ya kujitetea au kutoa taarifa juu ya jambo au mashtaka yoyote juu yake na ana
haki ya kukata rufaa kwenye vikao vya juu iwapo hajaridhika na uamuzi
uliotolewa na kikao cha chini; na
iv) Haki
ya kupata habari au taarifa zote zilizojadiliwa na kutolewa uamuzi na wanachama
au uongozi wa juu katika kumbukumbu za vikao vinavyomhusu.
17. Ukomo wa Uongozi
(1) Mwanachama wa
ACT-Tanzania atakoma kuwa Kiongozi wa Chama:
i)
Kwa kujiuzulu kwa
hiari yake;
ii)
Kwa kuachishwa
uongozi au kufukuzwa uanachama;
iii)
Kwa kushindwa kutimiza
wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya Katiba;Kanuni au maadili ya Chama;
iv)
Kwa kufariki
dunia;
v)
Kupatwa na
matatizo ya akili;
vi)
Muda wa uongozi
kumalizika;
vii) Kupatikana
na hatia mahakamani kwa kosa la jinai linalokidhalilisha chama.
(2)
Kamati ya Uongozi
ya kila ngazi au Halmashauri Kuu kwa ngazi ya Taifa itaziba kwa muda nafasi
yoyote ya kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu wa ngazi husika.
(3)
Nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa
na vikao husika kwa kufanya uteuzi mpya katika muda usiozidi miezi sita tangu
nafasi kuwa wazi.
(4)
Muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu ibara
ndogo ya (2) hapo juu hautazidi miezi kumi na miwili (12) na ndani ya kipindi
hicho uchaguzi mpya ufanyike kuziba nafasi iliyoachwa wazi.
(5)
Bila kuathiri masharti
ya ibara ndogo ya (4) hapo juu, hakutafanyika uchaguzi rasmi wa kuziba nafasi
kama kumebakia miezi sita tu au chini ya hapo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa kawaida
wa Chama unaofuata kufanyika.
18. Kukasimu Madaraka
(i.)
Kamati ya Uongozi ya kila ngazi au Kamati Kuu
Taifa zinaweza kukasimu baadhi ya madaraka kwa Sekretarieti yake kwa azimio la
wingi wa kura za wajumbe wa kikao
(ii.)
Halmashauri Kuu inaweza kukasimu baadhi ya
madaraka yake kwa Kamati Kuu kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe
(iii.)
Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Halmashauri Kuu
baadhi ya madaraka yake, lakini kwa azimio maalumu kwa ajili hiyo.
SURA YA TATU
NIDHAMU NA UTATUZI WA MIGOGORO
KATIKA CHAMA
19. Kuteuliwa kwa Kamati ya Uadilifu
(1)
Kila Kata itakuwa na Kamati ya Uadilifu
ya Kata itakayoteuliwa na Mkutano Mkuu wa Kata. Kamati ya Uadilifu ya Kata itaundwa
na wajumbe wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5), kwa kuzingatia kuwa
kutakuwa na angalau mjumbe mmoja (1) mwanamke kama Kamati itakuwa na wajumbe
watatu (3), au angalau wajumbe wawili (2) wa kike kama Kamati itakuwa na
wajumbe watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa Chama katika ngazi ya Kata
atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Kata.
(2)
Kila jimbo litakuwa na Kamati ya
Uadilifu ya Jimbo itakayoteuliwa na Mkutano Mkuu wa Jimbo. Kamati ya Uadilifu
ya Jimbo itaundwa na wajumbe wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5),
kwa kuzingatia kuwa kutakuwa na angalau mjumbe mmoja (1) mwanamke kama Kamati
itakuwa na wajumbe watatu (3), au angalau wajumbe wawili (2) wa kike kama
Kamati itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa Chama katika
ngazi ya Jimbo atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Jimbo.
(3)
Kila mkoa utakuwa na Kamati ya Uadilifu
ya Mkoa itakayoteuliwa na Mkutano Mkuu wa Mkoa. Kamati ya Uadilifu ya Mkoa
itaundwa na wajumbe wasiopungua watatu (3) na wasiozidi watano (5), kwa
kuzingatia kuwa kutakuwa na angalau mjumbe mmoja (1) mwanamke kama Kamati
itakuwa na wajumbe watatu (3) au angalau wajumbe wawili (2) wa kike kama Kamati
itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa Chama katika ngazi
ya Mkoa atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Mkoa.
(4)
Kutakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Taifa,
ambayo itakuwa ni moja kati ya Kamati za Kudumu za Chama, na itaundwa na
wajumbe watakaochaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya ACT kwa mapendekezo ya
Kamati Kuu.
i)
Kamati ya Uadilifu ya Taifa itakuwa na
wajumbe wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa (9).
ii)
Mwanachama yeyote mwaminifu na mwenye
uelewa wa Chama na siasa za nchi na dunia anaweza kuomba ujumbe wa Kamati ya
Uadilifu.
iii)
Halmashauri Kuu ya Taifa itateua wajumbe
wa Kamati ya Uadilifu wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa (9), kwa
kuzingatia kuwa kutakuwa na angalau
wajumbe wawili (2) wanawake kama Kamati itakuwa na wajumbe watano (5), au
angalau wajumbe watatu (3) wanawake kama Kamati itakuwa na wajumbe wanaozidi
watano (5). Hakuna afisa au kiongozi wa Chama katika ngazi ya Taifa
atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Taifa.
iv)
Halmashauri Kuu itachagua Mwenyekiti wa
Kamati ya Uadilifu ya Taifa kwa mapendekezo ya Kamati Kuu kwa kuzingatia kuwa
Mwenyekiti atakuwa mtu mwenye angalau Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu
kinachotambulika na mamlaka husika nchini.
(5)
Hakuna chombo kitakachokuwa na mamlaka
ya kuivunja Kamati ya Uadilifu ya Taifa, isipokuwa HalmashauriKuu ya Taifa kwa
idadi ya zaidi ya nusu ya kura zote za wajumbe waliohudhuria na kupiga kura.
(6)
Muda wa wajumbe wa Kamati ya Uadilifu
utakuwa miaka minne, lakini wanaweza kuteuliwa tena baada ya muda wao kwisha na
kuwepo kwake kutazingatia masharti mengine ya Katiba hii.
20. Mamlaka ya Kamati za Uadilifu
(1)
Kamati ya Uadilifu ya Kata itakuwa na
mamlaka juu ya masuala yote ya kinidhamu na kimaadilikwa wanachama na viongozi katika
ngazi ya Kata na ngazi za chini yake isipokuwa wale waliotajwa katika ibara
ndogo za (2) na (3).
(2)
Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itakuwa na
mamlaka kuhusu masuala yote ya kinidhamu kwa viongozi katika ngazi ya Jimbo na wawakilishi
wa chama (wenyeviti na wajumbe) kwenye serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji
na halmashauri za miji midogo. Kamati hii haitakuwa na mamlaka kwa viongozi
waliotajwa katika ibara ya (3) na (4). Kamati ya uadilifu ya Jimbo kitakuwa
ndicho chombo cha rufaa na mapitio kwa masuala ya kinidhamu katika ngazi ya
Kata na uamuzi wake utakuwa ni wa mwisho.
(3)
Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itakuwa na
mamlaka ya masuala yote ya kinidhamu yanayohusu viongozi wa ngazi ya Mkoa
isipokuwa waliotajwa kwenye ibara ndogo ya (4), pamoja na wawakilishi wa chama
(madiwani) kwenye Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya. Pia kitakuwa
chombo cha rufaa na mapitio kwa masuala ya kinidhamu katika ngazi ya Jimbo na
uamuzi wake utakuwa wa Mwisho.
(4)
Kamati ya Uadilifu ya Taifa itakuwa na
mamlaka ya kinidhamu kuhusu maafisa na viongozi katika ngazi ya Taifa, pamoja
na viongozi na wanachama wengine waandamizi wakiwemo wabunge, wajumbe wa Kamati
za Kudumu na wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, pamoja na masuala yote
ya kinidhamu yatakayoelekezwa kwake na vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.
(5)
Kamati ya Uadilifu Taifa ndicho
kitakachokuwa chombo cha Rufaa kwa masuala ya kinidhamu kutoka ngazi ya Mkoa.
(6)
Halmashauri Kuu itakuwa ndiyo ngazi ya
rufaa ya kitaifa na uamuzi wake utakuwa wa mwisho.
21. Kazi ya Kamati za Uadilifu
(1) Kamati za Uadilifu zitakuwa na kazi zifuatazo:
i)
Kufanya uchunguzi
kamili, kwa imani na weledi na bila upendeleo, kuhusu tuhuma zilizowasilishwa
dhidi ya mwanachama, mjumbe, afisa, mwakilishi au kiongozi wa Chama katika
ngazi husika;
ii) Kutoa
taarifa kwa maandishi kuhusu matokeo ya uchunguzi na sababu na mazingira
yaliyosababisha kufikia hitimisho;
iii) Kutoa adhabu yeyote kwa mujibu wa Katiba hii
isipokuwa kusimamisha au kufukuza uanachama au uongozi;
iv) Kutoa
mapendekezo kwa Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa au Kamati ya Uongozi kwa ngazi ya
Mkoa na Jimbo kwa adhabu ambazo haina mamlaka nazo;
v) Kamati
Kuu kwa ngazi ya Taifa au Kamati ya Uongozi kwa ngazi ya Mkoa na Jimbo
itayapitia mapendekezo ya Kamati ya Uadilifu na kutoa mapendekezo yake kwa
Halmashauri Kuu kwa ngazi ya Taifa au Halmashauri ya Mkoa au Jimbo kwa ngazi
hizo kwa maamuzi ya mwisho;
vi) Kikao
katika ngazi husika kitapokea na kutoa maamuzi ndani ya siku kumi na nne (14)
kuhusu mapendekezo ya Kamati ya Uadilifu kwa kukubali mapendekezo yote,
kurekebisha au kukataa na itatoa maamuzi yake na sababu za maamuzi hayo kwa
wote walioathirika; na
vii) Kikao
katika ngazi husika kitatoa maelekezo na maamuzi yanayolenga kuimarisha nidhamu
ndani ya Chama, ikiwemo kusimamisha au kufukuza uanachama.
viii)
Uamuzi wa kikao husika
utaanza kutekelezwa mara moja kama hapatakuwa na rufaa ndani ya siku 14 tangu
maamuzi yatolewe.
(2) Namna na
mchakato wa Kushughulikia Mashauri ya Nidhamu na uadilifu
itaelezwa kwenye Kanuni za Uendeshaji
Chama zitakazotungwa na
Halmashauri Kuu ya Chama.
(3)Mwanachama,
mjumbe, mwakilishi au kiongozi yeyote ambaye hakuridhishwa
na maamuzi ya kikao kilichotoa maamuzi ya kinidhamu atakata rufaa kwa
mamlaka ya rufaa ndani ya siku kumi na
nne (14) tangu maamuzi yatolewe.
(4) Maamuzi ya Mamlaka ya Rufaa yatakuwa ya mwisho.
22. Makosa Yanayoweza Kusababisha Hatua za Kinidhamu
(1)
Makosa yafuatayo yanaweza kusababisha
hatua za kinidhamu kwa mwanachama, afisa, mjumbe, mwakilishi au kiongozi wa
Chama:
i)
Kukiuka miiko na maadili ya uongozi kama
yalivyoainishwa katika Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Viongozi ambazo zimeambatanishwa
kama Nyongeza ya Kwanza na ni sehemu ya Katiba hii;
ii) Kukataa
kutekeleza wajibu na/au majukumu ya kikatiba;
iii) Kufanya
fujo au kutoa vitisho dhidi ya mwanachama au kiongozi mwingine;
iv) Kughushi
au kutoa taarifa za uwongo kuhusu mahesabu au madai ya uwongo kwa lengo la
kujipatia fedha kwa njia isiyo halali;
v) Kuharibu
mali ya Chama kwa makusudi;
vi) Kupinga
Itikadi, falsafa, misingi, katiba au sera za Chama katika majukwaa ya kisiasa;
vii) Kusababisha
mgawanyiko ndani ya Chama;
viii)
Kufanya kitendo chochote ambacho
kinagharimu na/au kuharibu taswira ya Chama au taifa katika umma;
(2)
Kuthibitika kutenda kosa lolote hapo juu
au linalofanana na hayo kutahesabiwa kuwa ni utovu wa nidhamu na kutasababisha
kutolewa adhabu stahiki zikiwemo:
i.
Karipio;
ii.
Karipio kali;
iii.
Onyo;
iv.
Onyo kali;
v.
Faini;
vi.
Kusimamishwa kugombea nafasi ya uongozi
kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja;
vii.
Kusimamishwa uanachama; au
MUUNDO WA CHAMA NA VIKAO
23. ACT-Tanzania ni Chama cha kitaifa
(1) ACT-Tanzania
ni Chama cha kitaifa, na kitakuwa na uwakilishi katika kila
ngazi katika muundo wa uchaguzi wa nchi kama ifuatavyo:
a)
ACT Tawi
b)
ACT Kata
c)
ACT Jimbo
d)
ACT Mkoa
e)
ACT Taifa
(2) Uundaji wa ngazi moja ya Chama utafanyika baada
ya kuwa na muundo na uongozikatika ngazi
za chini kwa angalau asilimia 40 . Mfano, ili kuunda ngazi ya Kata ni lazima
kuwe na angalau asilimia 40 ya matawi yenye uongozi katika kata husika.
(3)
Kwa kuzingatia Ibara ndogo ya (1) hapo
juu, ngazi ya juu ya Chama itateua Kamati ya muda itakayokuwa na wajibu wa
kuratibu shughuli za Chama na kuwaunganisha wanachama katika eneo lisilo na
uongozi wa kikatiba mpaka wanapofikia uwezo wa
kuwa na uongozi wa kikatiba.
24. Ngazi ya ACT Tawi
(1) Ngazi ya ACT
Tawi itaundwa katika eneo la kijiji, Mtaa au Sheia kwa
Tanzania Zanzibar
(2) Idadi
ya chini ya Wanachama wa ACT Tawi itakuwa ni watu ishirini (20)
(3) Viongozi wa ACT Tawi watakuwa ni:
(3) Viongozi wa ACT Tawi watakuwa ni:
(i.) Mwenyekiti wa ACT Tawi;
(ii.) Katibu wa ACT Tawi;
(iii.) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT Tawi;
(iv.) Mwekahazina wa ACT Tawi
(v.) Katibu wa Mipango na Chaguzi
(vi.) Wenyeviti wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee
katika Tawi;
(vii.) Makatibu wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee
katika Tawi; na
(viii.) Wajumbe wanne wa Kamati ya Uongozi watakaochaguliwa na
Mkutano mkuu wa Tawi, wanaume wawili na wanawake wawili.
(4) Vikao
vya ACT Tawi vitakuwa ni:
i.
Mkutano Mkuu wa
Tawi - Ndicho Kikao Kikuu kupita vyote kwenye ngazi ya tawi na wajumbe
wake ni viongozi wote wa ACT Tawi na wanachama wote kwenye tawi;
ii.
Kamati ya Uongozi–Ni
chombo cha utendaji cha Mkutano Mkuu wa Tawi na wajumbe wake ni viongozi wote
waliotajwa kwenye ibara ndogo ya (3) ya ibara hii pamoja na Mwenyekiti wa
Kijiji/Mtaa anayetokana na ACT na mwakilishi wa wenyeviti wa vitongoji na
mwakilishi wa wajumbe wa serikali ya kijiji/Kamati ya Mtaa.
iii.
Sektretarieti ya
Tawi – Ni kikao cha utendaji wa kazi za siku kwa siku kwenye ofisi ya tawi
mwenyekiti wake akiwa ni Katibu wa tawi, katibu wa kikao ni Katibu mwenezi wa
tawi na wajumbe ni Mwekahazina wa tawi, Katibu wa Mipango na chaguzi tawi na
makatibu wa ngome za vijana, wanawake na wazee kwenye tawi.
(5)
Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT Tawi
i)
Kuchagua viongozi
wa ACT-Tawi kama walivyotajwa katika ibara ndogo ya (3) hapo juu, isipokuwa
kwamba viongozi wa ngome kwenye tawi watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya
ngome zao;
ii)
Kupiga kura ya
maoni na kupendekeza wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na
Vitongoji;
iii)
Kujadili taarifa
ya Kamati ya Uongozi ya ACT Tawi na kutoa maamuzi au maelekezo ya utekelezaji;
iv)
Kupokea maamuzi
na maagizo ya vikao vya juu vya Chama na kutoa maelekezo kwa Kamati ya Uongozi
ya ACT Tawi kwa utekelezaji;
v)
Kujadili utekelezaji
wa itikadi, falsafa, sera na mipango ya Chama inayohusu masuala ya jamii katika
eneo la kijiji, mtaa ama Sheia;
vi)
Kutoa mwongozo na
maelekezo kwa wawakilishi wa Chama walio kwenye Serikali ya Kijiji au Kamati ya
Mtaa;
vii) Kujadili na kuzingatia taarifa za utendaji wa NGOME za
ACT Vijana, Wanawake na Wazee katika Tawi na kutoa maelekezo; na
viii)
Kuidhinisha
programu za Chama katika eneo lao.
(6)
Kazi za Kamati ya
Uongozi ya ACT Tawi
i)
Kuendesha
shughuli za kila siku za Chama katika eneo lake;
ii)
Kuandaa Mkutano Mkuu
wa ACT Tawi na ajenda zake;
iii)
Kuhamasisha
wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa, sera na madhumuni ya
Chama;
iv)
Kufanya uteuzi wa
mwisho wa wagombea kwenye serikali za mitaa, vijiji na vitongoji;
v)
Kuendesha na
kusimamia Kampeni za Uchaguzi wa wagombea wa Chama katika Uchaguzi wa
Kiserikali;
vi)
Kusimamia na
kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya ngazi husika;
vii)
Kusimamia
utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama;na
viii)
Kuhakikisha Chama
kinashika hatamu kwenye uchaguzi wa Tawi na kinapata kura nyingi za mwenyekiti
wa kijiji/mtaa, Ubunge na Urais katika ngazi ya Tawi.
(7)
Kazi za Sekretarieti ya ACT Tawi:
i.
Kuandaa Kikao cha
Kamati ya Uongozi ya Tawi na agenda zake;
ii.
Kusimamia
uendeshaji wa shughuli za kila siku za Chama katika Tawi;
iii.
Kuandaa mikakati
na kuishauri Kamati ya Uongozi ya Tawi juu ya kampeni za wagombea wa Chama
katika chaguzi za kiserikali;
iv.
Kuhamasisha
wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa, sera na madhumuni ya
Chama;
v.
Kutekeleza
maamuzi ya vikao vya Tawi na ngazi za juu vya Chama;
vi.
Kuweka kumbukumbu
sahihi za wanachama na wafuasi wa Chama katika madaftari ya wanachama na
wafuasi vijana wa Chama kwa mujibu wa Kanuni za Chama;
vii.
Kuandaa taarifa
mbalimbali za Chama katika Tawi na kuziwasilisha kwenye ngazi za juu kwa mujibu
wa Kanuni za Chama.
(8)
Kazi za Mwenyekiti wa ACT Tawi
i)
Atakuwa Mwenyekiti wa mikutano na vikao
vyote vya ACT Tawi;
ii) Atakuwa
msemaji mkuu wa Chama katika ACT Tawi;
iii) Atakuwa
ndiye mwenezi na mhamasishaji mkuu wa siasa ya Chama katika eneo lake;
iv) Katika
mikutano anayoongoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida, atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura za
wajumbe wanaoafiki na wasiofiki zitalingana; na
v) Atahakikisha
kuwa Chama kinashinda ngazi ya Tawi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
(9)
Kazi za Katibu wa ACT Tawi
i)
Atakuwa Katibu wa mikutano na vikao
vyote vya ACT Tawi;
ii) Atawajibika
kuandaa na kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za Chama
katika Tawi;
iii) Atakuwa
Mtendaji Mkuu wa ACT Tawi;
iv) Atakuwa
Mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika Tawi;
v) Atatunza
daftari la wanachama wote waliopo katika eneo lake;
vi) Ataitisha
vikao vya tawi vya Kamati ya Uongozi na Mkutano Mkuu kwa maelekezo ya
Sekretariat na Kamati ya Uongozi;
vii) Atakuwa
ndiye mwajibikaji mkuu wa masuala yote yahusuyo fedha na mali za Chama katika
eneo lake; na
viii) Kuhakikisha
kuwa Chama kinashinda ngazi ya Tawi katika uchaguzi wa kiserikali.
(1) Ngazi ya ACT Kata/Wadi
itaundwa katika eneo la kiutawala la Kata/Wadi
katika Serikali za Mitaa.
katika Serikali za Mitaa.
(2) Vikao vya Chama
vya ACT Kata/Wadi vitakuwa ni:
i)
Mkutano Mkuu wa
ACT Kata/Wadi;
ii)
Kamati ya Uongozi
ya ACT Kata/Wadi; na
iii)
Sekretariat ya
Kata/Wadi.
(3) Viongozi
wa Chama ngazi ya ACT- Kata/Wadi
i)
Mwenyekiti wa Chama Kata/Wadi;
ii) Katibu
wa Chama Kata/Wadi;
iii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama wa Kata/Wadi;
iv) Mwekahazina wa Chama Kata/Wadi;
v) Katibu wa Mipango na Chaguzi wa Kata/Wadi;
vi) Wenyekiti NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee Kata/Wadi;
vii) Makatibu NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee
Kata/Wadi; na
viii)
Wajumbe wanne wakuchaguliwa
wa Kamati ya Uongozi ya ACT Kata / Wadi watakaochaguliwa na mkutano mkuu wa
Kata/Wadi, wanaume wawili na wanawake wawili.
(4)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
ACT-Kata/Wadi:
i)
Wajumbe wote wa
kamati ya uongozi ya ACT Kata/Wadi;
ii)
Wenyeviti wote wa ACT Tawi kwenye Kata/Wadi;
iii)
Makatibu wote wa
ACT Tawi kwenye Kata/Wadi;
iv)
Katibu
Mawasiliano na Uenezi, Katibu wa Uchaguzi na Mwekahazina wa kila tawi ndani ya
Kata/Wadi;
v)
Wenyeviti wote wa
Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee wa matawi kwenye kata/wadi;
vi)
Makatibu wote wa
Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee wa matawi kwenye kata/wadi;
vii)
Diwani, Diwani wa
Viti Maalum, Mbunge/Mwakilishi anayeishi katika Kata;
viii)
Wenyeviti wa
Serikali za Vijiji na Wenyeviti wa Kamati za Mitaa wanaotokana na ACT kwenye
kata;
ix)
Wawakilishi
wawili wa kila ACT-Kijiji/mtaa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu.
(5)
Kazi za Mkutano Mkuu wa Kata/Wadi
i)
Kuchagua viongozi
wa ACT Kata kama walivyoorodheshwa kwenye ibara ndogo ya (3) ya ibara hii,
isipokuwa viongozi wa ngome watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya ngome zao;
ii)
Kupiga kura ya
maoni katika kuchagua mgombea udiwani katika kata husika kwa mujibu wa taratibu
zilizowekwa na Kanuni za ACT;
iii)
Kujadili taarifa
za Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi na kutoa maamuzi au maelekezo kwa
utekelezaji;
iv)
Kupokea maamuzi
na maagizo ya vikao vya juu na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Kamati ya Uongozi;
v)
Kuzingatia,
kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa Itikadi, Falsafa, Misingi na Sera
za Chama katika Kata/Wadi;
vi)
Kujadili na kutoa
mapendekezo kwa ngazi za juu, kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii
yanayojitokeza katika Kata/Wadi, ambayo yanahitaji hatua za kichama ngazi
za juu;
vii)
Kuidhinisha
Programu ya Chama katika Kata/Wadi;
viii)
Kuchagua wajumbe
wa Kamati ya Uadilifu ya Kata;na
ix)
Kujadili taarifa
za utendaji wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee katika Kata/Wadi.
(6)
Mkutano Mkuu wa ACT Kata utakutana mara mbili
(2) kwa mwaka. Mikutano maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na
Kamati ya Utendaji kadri itakavyolazimu.
(7)
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya
Kata/Wadi:
i)
Mwenyekiti wa
ACT-Kata/Wadi;
ii)
Katibu wa
ACT-Kata/Wadi;
iii)
Katibu Mwenezi wa
ACT-Kata/Wadi;
iv)
Katibu wa Mipango
na Chaguzi Kata/Wadi;
v)
Mweka hazina wa
Kata/Wadi
vi)
Wenyeviti wa
NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee ngazi ya Kata/Wadi;
vii)
Wajumbe wawili wa
kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi;
viii)
Diwani wa
kuchaguliwa na wa viti maalum wanaotokana na ACT kwenye kata/wadi husika;
ix)
Wawakilishi
watatu (angalau mmoja awe mwanamke kama yupo) wa wenyeviti wa Mitaa, vijiji na
vitongoji na wajumbe wa serikali na kamati za vijiji/mitaa.
(8)
Kazi za Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi.
i)
Kufanya uteuzi wa
awali wa wagombea nafasi za uenyekiti, ujumbe na ujumbe viti maalum wa serikali
za mitaa, vijiji na vitongoji;
ii)
Kupokea na
kujadili majina ya wagombea wa Chama katika uchaguzi wa Madiwani na kupeleka
kwa Mkutano Mkuu wa ACT Kata/Wadikwa kupigiwa kura ya maoni;
iii)
Kuandaa Mkutano
Mkuu wa Kata/Wadina agenda zake;
iv)
Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji
washughuli za Chama katika Kata;
v)
Kusimamia
uchaguzi wa viongozi wa Chama katika matawi;
vi)
Kuandaa mikakati
na kusimamia kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali ndani ya
kati/wadi;
vii)
Kuhamasisha
wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa, sera na madhumuni ya
Chama;
viii)
Kutekeleza
maamuzi ya vikao vya juu vya Chama;
ix)
Kuweka kumbukumbu
sahihi za uanachama na ufuasi wa Chama katika madaftari ya wanachama na wafuasi
vijana wa Chama kwa mujibu wa kanuni za Chama;
x)
Kuandaa taarifa
mbali mbali za Chama Kata/Wadi na kuziwasilisha kwenye ngazi ya Jimbo kwa
mujibu wa Kanuni za Chama;
xi)
Kuweka katika
majalada maalum kumbukumbu za vikao na nyaraka nyingine za mawasiliano katika
Chama;
xii)
Kufuatilia
utendaji kazi wa viongozi wa kiserikali katika Kata/Wadi waliotokana na Chama
na kutoa ushauri au maelekezo kwa kadri inavyowezekana;
xiii)
Kusimamia na
kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya Kata husika;
xiv)
Kufuatilia
utendaji na utekelezaji wa maelekezo ya Chama kwa viongozi wawakilishi wa Chama katika mabaraza ya Serikali
za Mitaa;
xv)
Kutoa msaada kila
inapobidi kwa viongozi wawakilishi wa Chama katika mabaraza ya Serikali za
Mitaa;
xvi)
Kutayarisha na
kusimamia programu za Chama katika ngazi husika;
xvii)
Kusimamia
utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama; na
xviii)
Kusimamia utendaji
wa NGOME za ACT Vijana, Wanawake na Wazee katika Kata.
(9) Kamati
ya Uongozi ya ACT-Kata itakutana mara nne kwa mwaka yaani kila baada ya miezi
mitatu. Vikao maalum/dharula vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu.
(10)
Wajumbe wa
Sekretariet ya Kata/Wadi watakuwa ni:
i)
Katibu wa Kata
/Wadi – Mwenyekiti;
ii)
Katibu wa
Mawasiliano na Uenezi Kata/Wadi – Katibu;
iii)
Mweka hazina wa
kata/wadi;
iv)
Katibu mipango na
chaguzi; na
v)
Makatibu wa ngome
za vijana, wanawake na wazee kwenye kata/wadi.
(11)
Kazi za Sekretarieti ya ACT Kata/Wadi:
(i)
Kuandaa Kikao cha
Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi na agenda zake;
(ii)
Kusimamia
uendeshaji wa shughuli za kila siku za Chama katika kata/wadi;
(iii)
Kuandaa mikakati
na kuishauri Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi juu ya kampeni za wagombea wa Chama
katika chaguzi za kiserikali;
(iv)
Kuhamasisha
wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa, sera na madhumuni ya
Chama;
(v)
Kutekeleza
maamuzi ya vikao vya Kata/Wadi na ngazi za juu vya Chama;
(vi)
Kuweka kumbukumbu
sahihi za wanachama na wafuasi wa Chama katika madaftari ya wanachama na
wafuasi vijana wa Chama kwa mujibu wa Kanuni za Chama;
(vii) Kuandaa taarifa mbalimbali za Chama katika Tawi na
kuziwasilisha kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa Kanuni za Chama.
(12)
Kazi za Mwenyekiti wa Kata/Wadi:
i)
Atakuwa na madaraka ya kuangalia mambo
yote ya Chama katika Kata/Wadi yake;
ii)
Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa
Chama wa Kata au Wadi na Kamati ya Uongozi ya Kata au Wadi;
iii)
Katika Mikutano anayoiongoza, zaidi ya
kuwa na kura yake ya kawaida, Mwenyekiti wa Chama wa Kata/Wadi pia atakuwa na
kura ya uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana;
iv)
Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa
Chama katika Kata/Wadi; na
v)
Atahakikisha Chama kinashinda uchaguzi
wa udiwani na kupata kura nyingi za Urais na Ubunge katika eneo lake.
(13)
Kazi za Katibu wa Kata/Wadi:
i)
Atakuwa Katibu wa vikao vyote vya
kikatiba vya Chama katika Kata/Wadi;
ii)
Atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama
katika Kata/Wadi;
iii)
Atakuwa ndiye Mkuu wa mipango ya Chama
katika Kata /Wadi;
iv)
Atatunza orodha ya ACT Matawi, idadi ya
ACT Matawi na wanachama waliopo kwa kila ACT Tawi lililoko katika Kata/Wadi
yake;
v)
Atatunza kumbukumbu za mali za Chama
zisizoondosheka na zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama
ya Kata/Wadi hiyo;
vi)
Atawajibika na kutoa taarifa za kila
mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za Chama katika Kata/Wadi kwa ngazi ya Jimbo;
vii)
Atakuwa ndiye mdhibiti Mkuu wa mali za
Chama katika Kata/Wadi;
viii)
Atawajibika kuandaa na kuitisha mikutano
yote ya vikao halali vya Chama vya Kata/Wadi kwa maelekezo ya secretariat na
Kamati ya Uongozi na kwa kushauriana na Mwenyekiti wake wa Kata/Wadi;
ix)
Atafuatilia na kuratibu masuala ya
ulinzi na usalama wa Chama katika Kata/Wadi yake;
x)
Atafanya kazi yoyote itakayokuwa
imetajwa penginepokatika Katiba hii;na
26. ACT Jimbo
ACT Jimbo itaundwa kwenye eneo la Jimbo la Uchaguzi
wa Ubunge/Uwakilishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwa kwa
mujibu wa Katiba
na Kanuni za Chama.
(1) Vikao vya Chama vya ACT Jimbo vitakuwa ni:
i)
Mkutano Mkuu wa
ACT Jimbo;
ii) Kamati ya Uongozi ya
ACTJimbo; na
iii) Sekretarieti ya ACT Jimbo.
(2) Viongozi
wa ACT-Jimbo
i)
Mwenyekiti wa Jimbo;
ii)
Katibu wa Jimbo;
iii)
Katibu wa
Mawasiliano na Uenezi wa Jimbo;
iv)
Mweka Hazina wa Jimbo;
v)
Katibu Mipango na
Chaguzi Jimbo;
vi)
Wenyeviti wa
NGOME katika Jimbo;
vii)
Makatibu wa NGOME
katika Jimbo; na
viii)
Wajumbe wanne wa
kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi Jimbo watakaochaguliwa na mkutano mkuu wa
Jimbo, wanaume wawili na wanawake wawili.
(3) Kwa wilaya
zenye majimbo zaidi ya moja, Viongozi wa jimbo ambalo ndio Makao Makuu
ya wilaya watakuwa ndio wawakilishi wa Chama wilaya kwamambo yote ya kiserikali
yanayohusu chama katika wilaya husika. Ikiwa
kiongozi yeyote wa jimbo la makao ya wilaya hayupo, atawakilishwa kwenye shughuli za serikali ya wilaya na kiongozi mwenye cheo hicho hicho kutoka kwenye jimbo lisilo makao makuu ya wilaya.
kiongozi yeyote wa jimbo la makao ya wilaya hayupo, atawakilishwa kwenye shughuli za serikali ya wilaya na kiongozi mwenye cheo hicho hicho kutoka kwenye jimbo lisilo makao makuu ya wilaya.
(4) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT Jimbo
i)
Wajumbe wote wa
Kamati ya Uongozi ya ACT Jimbo;
ii)
Wenyeviti wote wa
Kata/Wadi katika jimbo;
iii)
Makatibu wote wa
Kata/Wadi katika jimbo;
iv)
Makatibu wa
Uenezi, Makatibu wa Mipango na Wekahazina wote wa Kata/Wadi katika Jimbo;
v)
Wenyeviti wa
Ngome zote za Kata/Wadi katika Jimbo;
vi)
Makatibu wa Ngome
zote za Kata/Wadi katika Jimbo;
vii)
Madiwani na
Madiwani wa Viti maalum wanaotokana na ACT katika Jimbo.
(5) Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT-Jimbo
i)
Kuchagua Viongozi wa ACT Jimbo waliotajwa katika
ibara ndogo ya (2) hapo juu, isipokuwa katibu wa Jimbo atachaguliwa kwa
kupendekezwa kwa Kamati Kuu ambayo ndiyo itafanya uteuzi wa mwisho;
ii)
Bila kuathiri kipengele cha (i) hapo juu,
viongozi wa ngome zote watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo ya ngome husika;
iii)
Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya
utendaji na mapato na matumizi ya Jimbo;
iv)
Kupokea na kuzingatia mikakati ya ushindi wa ACT
katika chaguzi za kiserikali ndani ya Jimbo;
v)
Kuzingatia na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa
Kamati ya Uongozi ya Jimbo juu ya maamuzi na maagizo ya vikao vya juu;
vi)
Kujadili taarifa za Kamati ya Uongozi ya Jimbo na
kutoa maamuzi au maelekezo kwa
utekelezaji;
vii)
Kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa Itikadi,
Falsafa, Misingi na Sera za Chama katika
Jimbo;
viii)
Kutoa mwongozo na maelekezo kwa wawakilishi wa
Chama katika vyombo vya maamuzi vya kiserikali;
ix)
Kuzingatia na kutoa mapendekezo kwa ngazi za
juu, juu ya masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojitokeza katika Jimbo
na yanayohitaji hatua za kichama ngazi za juu;
x)
Kuidhinisha Programu ya Chama katika Jimbo;
xi)
Kupiga kura ya maoni ya wagombea wa Ubunge/uwakilishi
katika Jimbo husika; na
xii)
Kuchagua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Jimbo.
(6) Mkutano Mkuu wa Jimbo utafanyika mara mbili kwa mwaka. Mikutano
maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya Jimbo
kadri itakavyolazimu.
(6) Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya ACT
Jimbo:
(ii)
Mwenyekiti wa
Jimbo;
(iii)
Katibu wa Jimbo;
(iv)
Katibu wa
Mawasiliano na Uenezi wa Jimbo;
(v)
Mweka Hazina wa
Jimbo;
(vi)
Katibu Mipango na
Chaguzi Jimbo;
(vii) Wenyeviti wa NGOME katika Jimbo;
(viii)Makatibu
wa NGOME katika Jimbo;
(ix)
Wajumbe wanne wa
kuchaguliwa wa Kamati ya Uongozi Jimbo;
(x)
Mbunge na/au
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi katika jimbo husika;
(xi)
Meya na/au Naibu
Meya anayetokana na ACT ikiwa anaishi ndani jimbo husika;
(xii) Mwakilishi wa Madiwani wote wanaotokana na ACT katika
jimbo
(xiii)Wenyeviti
na Makatibu wa Kamati mbalimbali zilizoundwa katika ngazi ya jimbo;
(xiv)Wajumbe
wote wa Kamati Kuu wanaoishi katika Jimbo watakaoingia kama waalikwa lakini
watakuwa hawana haki ya kupiga kura.
(7)
Kazi za Kamati ya Uongozi ya ACT Jimbo
i.
Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Jimbo;
ii.
Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji
wa shughuli za kila siku za Chama katika Jimbo;
iii.
Kusimamia misingi mikuu ya ACT katika
jimbo husika;
iv.
Kusimamia uchaguzi wa ndani ya chama
katika kata/wadi;
v.
Kupanga mipango ya kampeni za uchaguzi
katika jimbo;
vi.
Kuhakikisha chama kinaenea kwenye jimbo
lote;
vii.
Kupanga na kuandaa mkutano mkuu wa Chama
jimbo;
viii.
Kufanya uteuzi wa awali wa wagombea
udiwani kwenye kata/wadi zilizo katika jimbo;
ix.
Kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa
nafasi mbalimbali katika ngazi ya Mitaa, vijiji na vitongoji;
x.
Kuunda Kamati ndogo kadri itakavyoona
inafaa; na
xi.
Kujaza kwa muda nafasi za uongozi
zilizowazi katika jimbo.
(8)
Vikao vya Kamati ya Uongozi ya jimbo
vitakutana angalau mara nne (4) kwa mwaka na vinaweza kuitishwa kwa dharula
pale panapokuwa na uhitaji kufanya hivyo.
(9)
Wajumbe wa Sekretariati ya ACT Jimbo
i.
Katibu wa ACT Jimbo (Mwenyekiti);
ii.
Katibu wa Mawasiliano na Uenezi Jimbo
(Katibu)
iii.
Mweka Hazina wa ACT Jimbo;
iv.
Katibu wa Mipango na Chaguzi Jimbo
v.
Makatibu wa NGOME katika Jimbo; na
vi.
Makatibu wa Kamati mbalimbali katika
Jimbo;
vii.
Makatibu wa NGOME katika Jimbo;
(10) Kazi
za Sekretarieti ya Jimbo
i. Kupokea taarifa ya majina ya wagombea udiwani katika
Kata zilizo ndani ya Jimbo na kura walizopigiwa za maoni;
ii. Kuandaa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Jimbo na agenda
zake;
iii. Kuandaa mikakati na kuendesha shughuli za kila siku za
Chama katika Jimbo;
iv. Kuandaa mikakati itakayopitishwa na Kamati ya Uongozi
ya Jimbo kwa ajili ya kusimamia kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za
kiserikali;
v. Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza
itikadi, falsafa, sera na madhumuni ya Chama;
vi. Kutekeleza maamuzi ya vikao vya Kamati ya Uongozi na
Mkutano mkuu Jimbo;
vii. Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na wafuasi wa
Chama katika madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa mujibu wa
Kanuni za Chama;
viii.
Kuandaa taarifa
mbalimbali za Chama katika Jimbo na kuziwasilisha kwenye ngazi za juu kwa
mujibu wa Kanuni za Chama;
ix. Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu za vikao na
nyaraka nyingine za mawasiliano katika Chama;
x. Kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya
Jimbo; na
xi. Kazi nyingine zozote watakazoagizwa na Kamati ya
Uongozi ya Jimbo.
(11)
Sekretariati ya
Jimbo itakutana mara moja kila mwezi na inaweza
kukutana kwa dharula au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au
kwa maagizo ya vikao vya juu.
kukutana kwa dharula au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au
kwa maagizo ya vikao vya juu.
(12)
Kazi za Mwenyekiti wa ACT-Jimbo
i)
Atakuwa na wajibu wa kusimamia mambo
yote ya Chama katika Jimbo;
ii)
Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mikakati
ya ushindi wa Chama katika chaguzi za serikali ndani ya Jimbo, na utendaji wake
utapimwa kutokana na, pamoja na mambo mengine, ufanisi wa Chama katika chaguzi
za kiserikali ndani ya Jimbo;
iii)
Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu na Kamati
ya Uongozi ya Jimbo;
iv)
Katika mikutano anayoiongoza, zaidi ya
kuwa na kura yake ya kawaida, Mwenyekiti wa Chama wa Jimbo atakuwa na kura ya
uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana;
v)
Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa
shughuli za kila siku za Chama katika Jimbo; na
vi)
Atahakikisha chama kinashinda uchaguzi
wa Ubunge na kupata kura nyingi za Urais.
(13)
Kazi za Katibu wa Jimbo
i) Atakuwa
Katibu wa mikutano na vikao vya Kamati ya Uongozi na Mkutano Mkuu wa Jimbo;
ii) Atakuwa
mwenyekiti wa vikao vya Sekretarieti ya Jimbo;
iii) Atakuwa
ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama katika Jimbo na atafanya kazi chini ya Kamati ya
uongozi ya Jimbo;
iv) Atakuwa
ndiye Mkuu wa mipango ya Chama katika Jimbo;
v) Ataitisha
na kuongoza vikao vya viongozi watendaji wakuu wa Chama katika Jimbo kwa
madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda ya vikao vya Jimbo na kuchukua hatua
za utekelezaji wa maamuzi ya Chama;
vi)
Ataitisha vikao vya Kamati ya Utendaji
na Mkutano Mkuu wa Jimbo kwa maelekezo ya Sekretariat na Kamati ya Uongozi na
kwa kushauriana na Mwenyekiti wa Jimbo;
vii)
Atatunza orodha ya Kata/Wadi, Matawi na
wanachama wa Jimbo lake;
viii)
Atatunza kumbukumbu za mali za chama
zisizoondosheka na zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama
ya Jimbo lake;
ix)
Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama
za Jimbo;
x)
Atawajibika kutoa taarifa za utendaji wa
shughuli za Chama katika Jimbo kila mwezi kwa ngazi ya Mkoa;
xi)
Atafuatilia na kuratibu masuala ya
ulinzi na usalama wa Chama katika Jimbo lake; na
xii)
Kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa
penginepo katika Katiba hii.
Ngazi
ya ACT Mkoa itaundwa katika kila eneo la Nchi la kiutawala la Mkoa.
(1) Vikao vya ACT-Mkoa
i)
Mkutano Mkuu wa
Mkoa;
ii)
Kamati ya Uongozi
ya Mkoa; na
iii)
Sekretariet ya
Mkoa.
(2) Viongozi wa ACT-mkoa
i.
Mwenyekiti wa ACT Mkoa;
ii.
Katibu wa ACT Mkoa;
iii.
Mweka hazina wa ACT Mkoa;
iv.
Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT
Mkoa;
v.
Katibu wa Mipango na Uchaguzi wa Mkoa;
vi.
Wenyeviti wa Ngome za Vijana, Wanawake
na Wazee Mkoa;
vii.
Wajumbe wanne wa kuchaguliwa wa Kamati
ya Uongozi Mkoa watakaochaguliwa na Mkutano mkuu wa Mkoa, wanaume wawili na
wanawake wawili.
(3)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT Mkoa:
i.
Wajumbe wote wa Kamati
ya Uongozi ya Mkoa;
ii.
Wenyeviti na Makatibu
wa majimbo yote yaliyomo kwenye mkoa;
iii.
Makatibu wa uenezi,
mipango na wekahazina wa majimbo yote yaliyomo kwenye mkoa;
iv.
Wajumbe wanne wa kamati
za uongozi za majimbo wa kuchaguliwa, wanaume wawili na wanawake wawili;
v.
Wabunge na wabunge wa
viti maalum wanaotokana na ACT kwenye mkoa;na
vi.
Wajumbewa Kamati Kuu, Halmashauri
Kuu na Mkutano Mkuu wanaoishi katika Mkoa.
(iv.)
Mkutano Mkuu wa ACT
Mkoa utafanyika mara mojakwa mwaka. Mkutano Mkuu Maalumu au wa dharula unaweza
kuitishwa wakati wowote kwa mahitaji maalumu na/au ya dharula.
(v.)
Kazi za Mkutano Mkuu wa
ACT Mkoa
i.
Kuchagua Viongozi wa
ACT Mkoa waliotajwa katika ibara ndogo ya (2) hapo juu, isipokuwa katibu wa
Mkoa atachaguliwa kwa kupendekezwa kwa Kamati Kuu ambayo ndiyo itafanya uteuzi
wa mwisho;
ii.
Bila kuathiri kipengele
cha (i) hapo juu, viongozi wa ngome zote watachaguliwa kwa mujibu wa miongozo
ya ngome husika;
iii.
Kupokea, kujadili na
kupitisha taarifa ya utendaji na mapato na matumizi ya Mkoa;
iv.
Kupokea na kuzingatia
mikakati ya ushindi wa ACT katika chaguzi za kiserikali ndani ya Mkoa;
v.
Kuzingatia na kutoa
maelekezo ya utekelezaji kwa Kamati ya Uongozi ya Mkoa juu ya maamuzi na
maagizo ya vikao vya juu;
vi.
Kujadili taarifa za
Kamati ya Uongozi ya Mkoa na kutoa maamuzi au maelekezo kwa utekelezaji;
vii.
Kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa
Itikadi, Falsafa, Misingi na Sera za Chama
katika Mkoa;
viii.
Kutoa mwongozo na
maelekezo kwa wawakilishi wa Chama katika vyombo vya maamuzi vya kiserikali kwa
mambo yanayohitaji msimamo wa chama kimkoa;
ix.
Kuzingatia na kutoa
mapendekezo kwa ngazi za juu, juu ya masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii
yanayojitokeza katika Jimbo na yanayohitaji hatua za kichama ngazi za juu;
x.
Kuidhinisha Programu ya Chama katika Mkoa;
xi.
Kuchagua wajumbe wa
Kamati ya Uadilifu ya Mkoa.
(6) Mkutano Mkuu wa Mkoa utafanyika
mara moja kwa mwaka. Mikutano
maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya
Mkoa kadri itakavyolazimu.
maalum/dharula inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya
Mkoa kadri itakavyolazimu.
(7) Wajumbe wa
Kamati ya Uongozi ya ACT Mkoa:
i.
Mwenyekiti wa
Mkoa;
ii.
Katibu wa Mkoa;
iii.
Katibu wa
Mawasiliano na Uenezi wa Mkoa;
iv.
Mweka Hazina wa
Mkoa;
v.
Katibu Mipango na
Chaguzi Mkoa;
vi.
Wenyeviti wa
NGOME katika Mkoa;
vii.
Makatibu wa NGOME
katika Mkoa;
viii.
Wajumbe wanne wa kuchaguliwa
wa Kamati ya Uongozi Mkoa;
ix.
Wawakilishi
wawili wa wabunge na/au wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkoa husika;
x.
Mwakilishi wa
mameya/wenyeviti na mwakilishi wa manaibu Meya/makamu wenyeviti wa halmashauri
wanaotokana na ACT katika mkoa; na
xi.
Wenyeviti na
Makatibu wa Kamati mbalimbali zilizoundwa katika ngazi ya Mkoa.
(8) Kazi za Kamati ya Utendaji ya Mkoa
i)
Kuratibu shughuli
za chama katika Mkoa;
ii)
Kufanya uteuzi wa
awali wa wagombea ubunge/uwakilishi katika mkoa;
iii)
Kufanya uteuzi wa
mwisho wa wagombea udiwani kwenye mkoa;
iv)
Kutoa ushauri na
misaada ya kiutendaji kwa uongozi wa ACT-Jimbo katika Mkoa;
v)
Kuratibu shughuli
za kampeni za wagombea Urais na Ubunge katika mikoa na mgawanyo wa majukumu
kijimbo;
vi)
Kuratibu na
kuunganisha shughuli za NGOME za Chama katika Mkoa;
vii)
Kuwa kiunganishi
cha Chama na shughuli za kiserikali katika Mkoa;
viii)
Kuratibu na kutoa
taarifa kwa Chama ngazi ya Taifa juu ya hali ya kisiasa, kijamii na kiutawala
ndani ya Mkoa;
ix)
Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji wa
shughuli za kila siku za Chama katika Mkoa;
x)
Kusimamia misingi mikuu ya ACT katika Mkoa
husika;
xi)
Kusimamia uchaguzi wa ndani ya chama katika Majimbo;
xii)
Kupanga mipango ya kampeni za uchaguzi katika
Mkoa;
xiii)
Kuhakikisha chama kinaenea kwenye Mkoa wote;
xiv)
Kupanga na kuandaa mkutano mkuu wa Chama Mkoa na
agenda zake;
xv)
Kuunda Kamati ndogo kadri itakavyoona inafaa; na
xvi)
Kujaza kwa muda nafasi za uongozi zilizowazi
katika Mkoa.
(9) Kikao cha kawaida cha Kamati ya Uongozi ya Mkoa
kitafanyika mara nne kwa mwaka. Vikao maalum / dharula vinaweza kuitishwa na
Sekretariet wakati wowote kadri itakavyohitajika.
(10) Wajumbe
wa Sekretariati ya Mkoa
i)
Katibu wa Mkoa (Mwenyekiti);
ii)
Katibu wa Mawasiliano na Uenezi Mkoa;
iii)
Mweka Hazina wa ACT Mkoa;
iv)
Katibu wa mipango na uchaguzi;
v)
Makatibu wa NGOME za ACT Mkoa; na
vi)
Makatibu wa Kamati mbalimbali
zilizoundwa katika mkoa.
(11)
Kazi za Sekretariati ya Mkoa
i.
Kupokea taarifa ya majina ya wagombea
ubunge katika majimbo yaliyo ndani ya Mkoa na kura walizopigiwa za maoni;
ii.
Kuandaa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Mkoa
na agenda zake;
iii.
Kuandaa mikakati na kuendesha shughuli
za kila siku za Chama katika Mkoa;
iv.
Kuandaa mikakati itakayopitishwa na
Kamati ya Uongozi ya Mkoa kwa ajili ya kusimamia kampeni za wagombea wa Chama
katika chaguzi za kiserikali;
v.
Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama
kwa kueneza itikadi, falsafa, sera na madhumuni ya Chama;
vi.
Kutekeleza maamuzi ya vikao vya Kamati ya
Uongozi na Mkutano mkuu Mkoa;
vii.
Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na
wafuasi wa Chama katika madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa
mujibu wa Kanuni za Chama;
viii.
Kuandaa taarifa mbalimbali za Chama
katika Mkoa na kuziwasilisha kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa Kanuni za Chama;
ix.
Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu
za vikao na nyaraka nyingine za mawasiliano katika Chama;
x.
Kuweka kumbukumbu za mali, mapato na
matumizi ya Mkoa; na
xi.
Kazi nyingine zozote watakazoagizwa na
Kamati ya Uongozi ya Mkoa.
(12)
Sekretariati ya
Mkoa itakutana mara moja kila mwezi na inaweza
kukutana kwa dharula au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au
kwa maagizo ya vikao vya juu.
kukutana kwa dharula au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au
kwa maagizo ya vikao vya juu.
(13)
Kazi za Mwenyekiti wa Chama Mkoa.
i)
Atashughulikia au atakuwa na madaraka ya
kuangalia mambo yote ya Chama katika Mkoa;
ii)
Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa
Chama wa Mkoa, na Kamati ya Uongozi ya Mkoa;
iii)
Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya
kuwa na kura yake ya kawaida, Mwenyekiti wa Chama wa mkoa atakuwa pia na kura
ya uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana; na
iv)
Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa
Chama wa Mkoa.
(14) Kazi
za Katibu wa Chama wa Mkoa:
ii)
Atakuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote
za Chama katika mkoa na atafanya kazi chini ya uongozi wa Kamati ya Uongozi ya
Chama mkoa;
iii)
Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mipango
ya Chama katika Mkoa;
iv)
Ataitisha na kuongoza vikao vya viongozi
watendaji wakuu wa Chama katika mkoa kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa
agenda za Kamati ya Uongozi ya Mkoa na kuchukua hatua za utekelezaji wa maamuzi
ya Chama;
v)
Kutunza orodha ya Majimbo, Kata/Wadi, Matawi,
na wanachama wa mkoa wake;
vi)
Kutunza kumbukumbu za mali za Chama
zisizohamishika na zinazohamishika zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama
ya mkoa huo;
vii)
Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama
wa mkoa;
viii)
Atawajibika kutoa taarifa za kila mwezi
kuhusu utendaji wa shughuli za Chama katika mkoa kwa ngazi ya Kamati Kuu Taifa;
ix)
Atakuwa na wajibu wa kuandaana kuitisha
mikutano yote ya vikao vya Chama mkoa kwa maelekezo ya sekretarieti na Kamati
ya Uongozi Mkoa kwa kushirikiana na Mwenyekiti wake;
(a) Atafuatilia
na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wa Chama katika mkoa wake; na
(b) Atafanya
kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.
28.ACT Zanzibar
(1) Kutakuwa na Kamati Maalum ya Kamati Kuu kwa upande wa Zanzibar.
(2) Wajumbe wa Kamati
Maalum ya Chama Zanzibar watakuwa ni:
i)
Makamu Mwenyekiti
Zanzibar (Mwenyekiti wa Kamati);
ii)
Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar (Katibu wa Kamati);
iii)
Wajumbe wa Kamati
Kuu watokao Zanzibar;
iv)
Manaibu Katibu
Taifa wa Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee;
v)
Wenyeviti wa
Mikoa Zanzibar ; na
vi)
Maofisa katika idara mbalimbali za Ofisi ndogo
ya Makao Makuu Zanzibar watakuwa wajumbe
wasiona kura.
(3) Kazi za Kamati Maalumu Zanzibar:
i) Kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu juu ya masuala
mbalimbali yahusuyo Zanzibar;
ii) Kusimamia utendaji wa Sekretarieti ya ofisi ya Makao
Makuu Zanzibar;
iii) Kupendekeza mambo ya kisera yahusuyo Zanzibar;
iv) Kuleta mapendekezo kwa Kamati Kuu juu ya uteuzi wa
wagombea ubunge na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar kabla ya Kamati Kuu
kufanya uteuzi wa mwisho;
v) Kuteua maafisa wa idara mbalimbali za Ofisi ndogo ya
Makao Makuu Zanzibar;
vi) Kuratibu shughuli za chama Tanzania visiwani;
vii) Kutoa ushauri na misaada ya kiutendaji kwa uongozi wa
ACT katika Mikoa ya Zanzibar;
viii) Kuratibu shughuli za kampeni za wagombea Urais na
Urais wa Zanzibar katika eneo lote la visiwani;
ix) Kuratibu na kuunganisha shughuli za NGOME za Chama
Visiwani;
x) Kuwa kiunganishi cha Chama na shughuli za kiserikali
katika Zanzibar;
xi) Kuratibu na kutoa taarifa kwa Chama ngazi za juu
kuhusu hali ya kisiasa, kijamii na kiutawala Zanzibar;
xii) Kuandaa
mikakati na kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za Chama visiwani;
xiii) Kusimamia
misingi mikuu ya ACT visiwani;
xiv) Kuhakikisha
chama kinaenea Zanzibar yote;
xv) Kupendekeza majina ya wagombea urais na makamu wa Rais
Zanzibar; na
xvi) Kufanya uteuzi wa awali wa mgombea uspika na naibu
spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
(4) Kwa shughuli za kiutendaji Zanzibar,
patakuwa na Sekretarieti ya Ofisi ndogo
ya Makao Makuu Zanzibar yenye wajumbe wafuatao:
ya Makao Makuu Zanzibar yenye wajumbe wafuatao:
i)
Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar (Mwenyekiti);
ii)
Manaibu Makatibu
wa Taifa wa Ngome za Vijana, Wanawake na
wazee;
wazee;
iii)
Maofisa wa idara mbalimbali
zilizopo Ofisi ndogo ya Makao Makuu
Zanzibar; na
Zanzibar; na
(5) Kazi
za Sekretarieti ndogo Zanzibar:
i)
Utekelezaji wa
kazi za kila siku za chama Zanzibar;
ii) Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu
yanayohusuZanzibar; na
iii) Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya
Kamati Maalum Zanzibar.
29. ACT-Taifa
(1)
ACT-Taifa ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwakwa
kuzingatia masharti ya Kanuni za Chama zilizotungwa na HalmashauriKuu yaTaifa.
i)
Kiongozi wa ACT Taifa;
ii)
Mwenyekiti wa ACT Taifa;
iii)
Makamu Mwenyekiti wa ACT Taifa upande wa
Zanzibar;
iv)
Makamu mwenyekiti ACT Taifa upande wa Bara;
v)
Katibu Mkuu wa ACT Taifa;
vi)
Naibu Katibu Mkuu ACT Taifa upande wa Zanzibar;
na
vii)
Naibu Katibu Mkuu ACT Taifa upande waBara.
(3) Vikao vya Chama Taifa:
i)
Mkutano Mkuu Taifa – ndicho kikao cha
juu kabisa katika ACT na
ndicho chenye maamuzi ya mwisho kuhusu jambo lolote ndani ya
chama;
ndicho chenye maamuzi ya mwisho kuhusu jambo lolote ndani ya
chama;
ii)
Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia Taifa;
iii)
Halmashauri Kuu ya Taifa;
iv)
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa; na
v)
Sekretarieti ya Kamati Kuu.
(4) Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT watakuwa wafuatao:
i.
Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya
Taifa;
ii.
Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo;
iii.
Wawakilishi 15 wa ngome za chama taifa
kwa wawakilishi watano kila ngome;
iv.
Wawakilishi 12 wa wanafunzi wa vyuo
vikuu waliochaguliwa na umoja wao kwa mujibu wa Kanuni zitakazowekwa na Ngome
ya Vijana, kwa masharti kwamba angalau theluthi moja ya wajumbe hawa watakuwa
wanawake;
v.
Wawakilishi watatu wa ACT Nje
watakaochaguliwa na wanachama walio nje ya nchi kwa sharti kwamba angalau mmoja
awe mwanamke;
vi.
Wawakilishi watano wa Wabunge na
wawakilishi wanaotokana na ACT;
vii.
Wawakilishi watano wa Madiwani
wanaotokana na ACT; na
viii.
Mjumbe mmoja atakayewakilisha kila
mwanachama kikundi.
(5) Kazi za Mkutano Mkuu wa Chama Taifa:
i)
Kuchagua Kiongozi
wa ACT Taifa;
ii)
Kuchagua
Mwenyekiti wa ACT Taifa;
iii)
Kuchagua Makamu
Mwenyekiti wa ACT Taifa (Tanzania Bara);
iv)
Kuchagua Makamu
Mwenyekiti wa ACT Taifa (Zanzibar);
v)
Kujadili taarifa
za Halmashauri Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji;
vi)
Kuteua mgombea wa Urais na mgombea mwenza wake
kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
vii)
Kujadili na kuridhia Itikadi, Falsafa, Misingi
na Sera za Chama kisha kuweka mikakati na miongozo ya utekelezaji;
viii)
Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa
kuzingatia mapendekezo ya Halmashauri Kuu;
ix)
Kupokea na
kujadili taarifa ya Bodi ya wadhamini wa Chama juu ya mali na raslimali za
Chama;
x)
Kuidhinisha Ilani
(Manifesto) ya Chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu;
xi)
Kujadili na
kuthibitisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Chama; na
xii)
Kujadili na kufanyia
maamuzi agenda nyingine yoyote iliyoletwa kwake na Halmashauri Kuu au Kiongozi
Mkuu wa chama.
(6)
Mkutano Mkuu Taifautakutana mara moja katika
kipindi cha miaka mitano.Mkutano Mkuu maalum/dharula unaweza kuitishwa wakati
wowote ukiwepo ulazima kwa utaratibu utakaowekwa na Kanuni
(7) Kutakuwa naMkutano
Mkuu wa Taifa wa Kidemokrasia (National Democratic
Congress) ambao ni mkutano wa Wanachama wa ACT. Mkutano huu:
i.
Wajumbe wa mkutano huu
ni wanachama wote wa ACT-Tanzania, wadau, wafadhili na wananchi wote kwa ujumla
watakaopenda kuhudhuria;
ii.
Utafanyika mara moja
kwa mwaka kwa mikoa kupokezana na unaweza kuitishwa mara nyingi zaidi kama kuna
hitaji la kufanya hivyo;
iii.
Mkutano Mkuu wa
Wanachama utakuwa ndio jukwaa la Kiongozi wa Chama kutoa mwelekeo wa kisera wa
Chama na jukwaa la wanachama wote kuhoji utendaji wake.
iv.
Mkutano Mkuu wa
wanachama utajadili hali ya siasa na uchumi ya Nchi, Afrika na dunia kwa kila
mwaka.
v.
Mkutano Mkuu wa
Wanachama litakuwa jukwaa la majadiliano lakini hautakuwa na maamuzi yoyote.
vi.
Mambo yote
yaliyojitokeza na kupendekezwa katika majadiliano ya Mkutano Mkuu wa Wanachama yanayohitaji
maamuzi ya vikao mbalimbali yatawasilishwa katika vikao husika vya chama kwa
maamuzi na yanayohitaji utekelezaji tu, yatawasilishwa kwa vyombo vya
utekelezaji kwa ajili hiyo.
(8) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya ACT
Taifa:
i.
Wajumbe wote wa Kamati
Kuu;
ii.
Wenyeviti wote wa
Mikoa;
iii.
Makatibu wote wa Mikoa;
iv.
Makatibu wa Ngome taifa
v.
Wawakilishi tisa wa
Ngome za Vijana, Wanawake na Wazee kwa kila ngome kuwakilishwa na wajumbe
watatu;
vi.
Wawakilishi watano wa wabunge na wawakilishi wanaotokana na ACT;
vii.
Wawakilishi watatu wa
wanafunzi wa elimu ya juu watakaochaguliwa kwa utaratibu utakaoelezwa kwenye
mwongozo wa Ngome ya Vijana;
viii.
Wawakilishi watatu wa
madiwani wanaotokana na ACT; na
ix.
Wajumbe kumi na tano
(15), ambapo angalau wajumbe watano (5) watakuwa wanawake, waliochaguliwa na
Mkutano Mkuu wa Taifa.
(9) Kazi za Halmashauri Kuu ya Chama ya Taifa:
i.
Kupendekeza wagombea wa
Urais na Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana kuwasilisha
mapendekezo yake katika Mkutano Mkuu wa Taifa;
ii.
Kuteua mgombea Urais wa
Zanzibar;
iii.
Kuchagua Katibu Mkuu wa
Chama;
iv.
Kuchagua wajumbe wanane
kuingia kwenye Kamati Kuu;
v.
Kusikiliza na kutoa
maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kwa mujibu wa Katiba hii;
vi.
Kujadili mikakati ya
uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya Mkutano Mkuu na kuifanyia
maamuzi panapostahili;
vii.
Kuthibitisha mikakati
na raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za
Serikali hususani Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa;
viii.
Kuandaa ratiba na Kanuni
za Uchaguzi wa ndani ya chama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama;
ix.
Kutunga na kuzifanyia
marekebisho Kanuni za kuendesha shughuli za Chama;
x.
Kujadili taarifa za
Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji;
xi.
Kusimamia utendaji kazi
wa Kamati Kuu;
xii.
Kupendekeza kwa Mkutano
Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na mabadiliko yake;
xiii.
Kujadili rasimu ya
Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu kwa maamuzi;
xiv.
Kuteua Wadhamini wa
Chama;
xv.
Kuthibitisha miongozo
ya NGOME za Vijana, Wanawake na Wazee;
xvi.
Kujadili na kuidhinisha
majina ya wagombea wa nafasi za Kiongozi Mkuu, Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti.
(10)
Halmashauri Kuu ya
Taifa itakutana angalau mara mbili kila mwaka. Vikao maalum/dharula vinaweza
kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.
(11)
Kiongozi wa Chama
ataendesha vikao vya Kamati ya Uongozi wa Kitaifa ambayo itakutana kadri
inavyoona inafaa. Inapotokea Kiongozi wa Chama hayupo, Mwenyekiti ataendesha
vikao vya Kamati ya Uongozi wa Kitaifa.
(12)
Wajumbe wa Kamati Kuu
ya Chama Taifawatakuwa:
i.
Kiongozi wa ACT;
ii.
Naibu Kiongozi wa ACT,
kama yupo;
iii.
Mwenyekiti wa ACT
Taifa;
iv.
Makamu wenyeviti Taifa;
v.
Katibu Mkuu Taifa;
vi.
Manaibu Katibu wakuu
Taifa;
vii.
Wenyeviti wa Ngome za Vijana,
Wanawake na Wazee Taifa;
viii.
Wenyeviti wa Kamati za
Kudumu za Chama Taifa;
ix.
Makatibu wa Kamati za
Kudumu za Chama Taifa;
x. Wajumbe
wanane waliochaguliwa na Halmashauri Kuu kuingia Kamati Kuu kwa kuzingatia kuwa
wajumbe sita watatoka bara na ambao angalau wawili (2) watakuwa wanawake, na
wajumbe wawili (2) watatoka Tanzania Zanzibar na ambao angalau mjumbe mmoja (1)
atakuwa mwanamke;
xi.
Wajumbe watano
walioteuliwa na Kiongozi wa Chama kwa mujibu wa Katiba hii
xii. Rais
wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar
au Makamu wa Rais wa Zanzibar
aliyetokana na ACT;
xiii. Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Spika wa Baraza la wawakilishi waliotokana
na ACT;
xiv.
Waziri Mkuu au Kiongozi
wa Kambi ya Upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na Kiongozi wa Kambi
ya upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar;
xv.
Washauri wa chama
Taifa, na
xvi.
Mwenyekiti na Katibu wa
Bodi ya Wadhamini.
(13)
Kazi za Kamati Kuu ya
Chama Taifa:
i.
Kuunda Kamati za kudumu
Makao Makuu ya chama;
ii.
Kuteua washauri wa
chama wasiozidi 3 kwa mapendekezo ya Kiongozi baada ya kushauriana na
Mwenyekiti;
iii.
Kuteua Wajumbe na Makatibu wa Kamati za kudumu za
Chama Makao Makuu;
iv.
Kuidhinisha wasemaji wa
kisekta (wenyeviti wa kamati za kudumu za chama) kama walivyopendekezwa na
Kiongozi wa Chama;
v.
Kutoa mapendekezo kwa
Halmashauri Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu;
vi.
Kuandaa na kutoa
Mapendekezo kwa Halmshauri Kuu, Mikakati ya kuendesha shughuli za Chama kwa
kila mwaka na kwa kipindi cha miaka mitano;
vii.
Kuandaa na kutoa
mapendekezo kwa Halmashauri Kuu, Mikakati ya kupata mahitaji ya raslimali za
kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali;
viii.
Kuandaa na kutoa
mapendekezo kwa Halmashauri Kuu juu ya ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa ndani
ya chama;
ix.
Kupitia na kutoa kwa
Halmashauri Kuu mapendekezo ya haja ya kuzifanyia marekebisho au maboresho
Kanuni za Chama ama Katiba ya Chama;
x.
Kujadili taarifa za
Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji;
xi.
Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati
Kuu;
xii.
Kufanya mapitio ya Sera
za Chama na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu kwa kuzingatia matokeo ya
Utafiti uliofanywa na Sekretarieti ya Kamati Kuu;
xiii.
Kusimamia utekelezaji
wa maamuzi na maelekezo ya Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu;
xiv.
Kuwa kiungo na
kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama vingine vya siasa nchini,
Afrika Mashariki na nchi nyingine;
xv.
Kuteua kamati au tume
za kushughulikia masuala maalum ya kichama kwa muda maalum;
xvi.
Kuteua wakaguzi wa
mahesabu ya Chama kwa kila mwaka;
xvii.
Kuthibitisha uteuzi wa
wagombea Uspika, Ubunge na Uwakilishi;
xviii.
Kuandaa agenda za
Halmashauri Kuu na Mapendekezo ya agenda za Mkutano Mkuu;
xix.
Kuandaa hoja za
kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama;
xx.
Kuratibu utendaji wa
ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar;
xxi.
Kusimamia utendaji kazi
wa NGOME za Vijana, Wanawake na Wazee; na
xxii.
Kuthibitisha Uteuzi wa
Manaibu Katibu wakuu wa Tanzania bara na visiwani kutokana na mapendekezo ya
Kiongozi wa Chama atakayependekeza majina ya manaibu katibu wakuu kwa
kushauriana na Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu Taifa.
(14) Kamati Kuu itakutana mara nne (4) kwa
mwaka. Vikao maalum/dharula vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu
wa kanuni za Chama.
(15)
Kutakuwa na kamati za kudumu za Utendaji Makao Makuu ya Chama
zitakazoundwa na Kamati Kuu, ie.
zitakazoundwa na Kamati Kuu, ie.
i.
Kamati ya Fedha na Raslimali;
ii.
Kamati ya Mawasiliano na Uenezi;
iii.
Kamati ya Mipango na Mikakati;
iv.
Kamati ya Chaguzi na Kampeni;
v.
Kamati ya Katiba na Sheria;
vi.
Kamati ya Utafiti na Sera;
vii.
Kamati ya Uadilifu ya Taifa;
viii.
Kamati ya ACT - Amani
ix.
Kamati ya Mambo ya Nje.
(16) Kamati Kuu
inaweza kuunda Kamati zingine kama itakavyoona inafaa kwa
ufanisi wa Chama.
ufanisi wa Chama.
(17) Kutakuwa na Kikosi cha Amani cha Chama kitakachoitwa ACT-Amani
kuanziangazi
ya Tawi hadi Taifa ambapo katika ngazi hii ya Taifa kitakuwa chini ya Kamati ya
ACT- Amani. Kazi ya kikosi itakuwa ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa
wanachama, viongozi na mali za Chama.
(18) Muundo na
kazi za Kamati zitaainishwa katika Kanuni za uendeshaji
zitazotungwa na Halmashauri Kuu.
zitazotungwa na Halmashauri Kuu.
(19)
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama Taifa:
i.
Katibu Mkuu –
Mwenyekiti wa Sekretarieti;
ii.
Naibu Katibu Mkuu
Bara;
iii.
Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar;
iv.
Makatibu wa
Kamati zote Makao Makuu; na
v.
Makatibu wa NGOME zote za Chama Taifa.
(20) Katibu wa
Mawasiliano na Uenezi atakuwa ndiye msemaji wa Chama na ndiye
Katibu wa secretariet ya Kamati Kuu.
Katibu wa secretariet ya Kamati Kuu.
(21) Kazi za Sekretariati ya Kamati Kuu
ya Chama Taifa
i) Utekelezaji wa kazi za kila siku za uendeshaji
shughuli za Chama;
ii) Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu;
iii) Kuajiri watumishi wa makao makuu; na
iv) Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya
Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.
(22) Kutakuwa na Kamati ya Uongozi ya Kitaifa
itakayoundwa na:
a) Kiongozi wa Chama
b) Mwenyekiti
wa Chama
c) Naibu
Kiongozi wa Chama (kama yupo)
d) Makamu
Wenyeviti wa Chama
e) Katibu
Mkuu
f) Wajumbe
wasiozidi wawili watakaoteuliwa na Kiongozi wa Chama
(23)Kazi ya Kamati ya Uongozi
wa Kitaifa itakuwa ni kushauriana kuhusu mambo
mbalimbali ya chama lakini sio kikao cha maamuzi
(24)Bila
kuathiri masharti ya Katiba hii, Kamati ya Uongozi wa Kitaifa inaweza kufanya
maamuzi kwa jambo lolote ambalo ni la dharura na ambalo kusubiri kwake vikao
vya kawaida vya chama kunaweza kuathiri taswira, uhai na/au ustawi wa chama.
(25) Kazi na sifa za Kiongozi wa Chama
i)
Atakuwa kiongozi mkuu wa Chama na
Mwenyekiti wa kikao cha Mkutano Mkuu wa kidemokrasia
ii)
Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na
mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT pamoja na vikao vya chama;
iii)
Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu
baada ya kushauriana na kukubaliana na Mwenyekiti wa Chama Taifa na uteuzi kuthibitishwa
na Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii;
iv)
Kuteua wasemaji wa kisekta ambao pia
watakuwa ni wenyeviti wa Kamati za Makao Makuu;
v)
Kuteua Naibu Kiongozi wa Chama kwa
kushauriana na Kamati ya Uongozi atakapoona haja hiyo;
vi)
Kiongozi wa Chama anaweza kuteua
mwanachama mwingine mwenye mchango maalumu kuingia katika vikao vya chama kwa
kushauriana na Mwenyekiti na Katibu Mkuu kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo
kwa maslahi ya chama;
vii)
Kupendekeza majina ya washauri wa chama
baada ya kushauriana na Mwenyikiti;
viii)
Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu
masuala ya sera na mtazamo wa Chama katika mambo ya kitaifa na kimataifa;
ix)
Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye
Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na
masuala mengine ya kitaifa na kimataifa;
x)
Ataendesha vikao vya Kamati za Kisekta
ili kutengeneza misimamo ya kisera ya chama na kuwasilisha mapendekezo ya
kisera katika vikao vya chama kwa maamuzi
xi)
Iwapo Kiongozi wa Chama hayupo kwa
sababu yoyote ile na pale ambapo hakuna Naibu Kiongozi wa Chama, basi Mwenyekiti
wa Chama atamteua moja ya wasemaji wa kisekta kuwa Kaimu Kiongozi wa Chama;
xii)
Iwapo kiti cha Kiongozi wa Chama
kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi
au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, Naibu
Kiongozi wa Chama au kama na yeye hayupo basi aliyechaguliwa kutoka miongoni
mwa wasemaji wa kisekta, atashikilia nafasi yake kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu
Maalum wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi kumi na miwili tangu kuwa
wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi wa Chama, mwingine.
xiii)
Mtu atakayechaguliwa kuwa Kiongozi wa
Chama lazima awe na sifa za kuwa mbunge
xiv)
Endapo Kiongozi wa Chama atashindwa
katika uchaguzi wowote wa kiserikali, Halmashauri Kuu ya Taifa itabidi ikutane katika
kipindi kisichozidi miezi sita tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ili kujadili
mazingira ya kushindwa kwake na kupiga kura ya siri ya kuamua kama Kiongozi wa
Chama anastahili kuendelea na nafasi yake au la. Kiongozi wa Chama ataendelea
na nafasi yake endapo zaidi ya nusu ya wajumbe watapiga kura ya kuwa na imani
naye.
(26) Halmashauri Kuu ya Taifa inaweza
kumsimamisha Kiongozi wa Chama kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa
zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa. Hata hivyo, kura ya imani haitapigwa
hadi kuwe na hoja maalumu kwa ajili hiyo na ambayo imeungwa mkono na zaidi ya
theluthi moja ya wajumbe wote wa Halmashauri Kuu.
(27) Kiongozi wa Chama ataweza kuondolewa
kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la
Mkutano Mkuu wa Taifa litakaloungwa mkono na zaidi ya nusu ya kura za wajumbe
halali
waliohudhuria na kupiga kura.
waliohudhuria na kupiga kura.
(28) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Taifa :
i)
Atakuwa mlinzi mkuu wa sera
zilizopendekezwa na kupitishwa au jambo lolote litakaloamuliwa na kupitishwa na
vikao vya chama;
ii)
Atahakikisha kuwa ngazi zote za chama
zinatekeleza maamuzi yaliyotolewa navikao;
iii)
Atahakikisha kuwa ngazi zote zinafanya
kazi ndani ya mipaka ya katiba, kanuni, sera na maamuzi yoyote yaliyoagizwa na
vikao vikuu vya chama;
iv)
Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi
na usalama katika Chama Taifa;
v)
Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya
chama ya kitaifa isipokuwa vikao vya utendaji na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia
wa Wanachama;
vi)
Atafanya shughuli nyingine za Chama kama
atakavyoelekezwa na vikaovya Chama
vii)
Atapendekeza kwa Kamati Kuu majina ya
watu wanaofaa kuteuliwa kuwa Manaibu Katibu wakuu kwa kushauriana na Kamati ya
Uongozi ya Kitaifa
viii)
Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya
kuwa na kura yake ya kawaida atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura ya
wajumbe wanaoafiki na wasioafika zitalingana
(29) Iwapo
Mwenyekiti wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile basi Makamu
Mwenyekiti kutoka Bara atakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama kama
Mwenyekiti anatoka Zanzibar, au Makamu Mwenyekiti kutoka Zanzibar kama
Mwenyekiti anatoka Bara. Na kama huyo Makamu Mwenyekiti aliyetajwa
kwanza naye hayupo, basi makamu mwenyekiti aliyebakia atakaimu nafasi ya
uenyekiti.
Mwenyekiti kutoka Bara atakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama kama
Mwenyekiti anatoka Zanzibar, au Makamu Mwenyekiti kutoka Zanzibar kama
Mwenyekiti anatoka Bara. Na kama huyo Makamu Mwenyekiti aliyetajwa
kwanza naye hayupo, basi makamu mwenyekiti aliyebakia atakaimu nafasi ya
uenyekiti.
(30)
Iwapo kiti cha mwenyekiti wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu,kuondoka
katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa
kufanya kazi au kifo, Mkutano Mkuu maalumu wa Taifautaitishwa katika muda
usiozidi miezi kumi na mbili tangu kuwa wazi kwa kiti
hicho ili kuchagua Mwenyekiti mwingine. Katika muda huo, Halmashauri Kuu ya chama itateua Mwenyekiti wa muda kuziba nafasi hiyo kwa muda.
hicho ili kuchagua Mwenyekiti mwingine. Katika muda huo, Halmashauri Kuu ya chama itateua Mwenyekiti wa muda kuziba nafasi hiyo kwa muda.
(31) Halmashauri Kuu ya Taifa inaweza
kumsimamisha Mwenyekiti wa Chama kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa
zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa. Hata hivyo, kura ya imani haitapigwa
hadi kuwe na hoja maalumu kwa ajili hiyo na ambayo imeungwa mkono na zaidi ya
theluthi moja ya wajumbe wote wa Halmashauri Kuu.
(32) Mwenyekiti wa Chama ataweza kuondolewa
kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la
Mkutano Mkuu wa Taifa litakaloungwa mkono na zaidi ya nusu ya kura za wajumbe
halali
waliohudhuria na kupiga kura.
waliohudhuria na kupiga kura.
(33) Kazi za Makamu Wenyeviti wa Chama Taifa
a. Watakuwa
wasaidizi wakuu wa Mwenyekiti wa Chama na watafanya kazi zozote za Chama watakazopewa
na Mwenyekiti wa Chama Taifa;
b. Watakuwa
washauri wakuu wa Ngome za chama katika maeneo yao (Bara na Zanzibar)
c. Watakuwa
wajumbe maalumu katika vikao vyote vya Ngome za chama kitaifa;
d. Makamu
Mwenyekiti Zanzibar ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Zanzibar;
e. Watamshauri
Mwenyekiti katika majukumu yake ya kila siku kwa maeneo yao;
f. Watakuwa
wahamasishaji wa chama katika maeneo yao; na
g. Watakaimu
nafasi ya mwenyekiti kama hayupo kwa mujibu wa Katiba hii
h. Halmashauri
Kuu inaweza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani
naye na ambayo itaungwa mkono na zaidi ya nusu ya wajumbe wote waliohudhuria
kikao cha Halmashauri Kuu wakati hoja hiyo inatolewa.
(34) Kazi za Katibu Mkuu wa Chama Taifa
i)
Atakuwa Katibu wa mikutano ya chama
katika ngazi ya Taifa;
ii)
Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa shughuli
zote za utendaji za Chama;
iii)
Ataitisha na kuongoza vikao vya sekretariet
ya Kamati Kuu ya Chama kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda za Kamati
Kuu na kuchukua hatua za utendaji wa maamuzi ya Chama;
iv)
Atakuwa na uwezo wa kuajiri, kuachisha
kazi na kusimamia nidhamu ya watumishi wote wa kwa kushauriana na sekretarieti
yaChama kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, taratibu za Chama na sheria za nchi;
v)
Atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha
mikutano yote ya vikao vya Chama katika ngazi ya Taifa kwa kushauriana na
Kiongozi wa Chama na Mwenyekiti wa Chama, na kuchukua hatua za utekelezaji wa
maamuzi ya Chama;
vi)
Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama
zinazohamishika na zisizohamishika; na
vii)
Atafanya kazi yoyote itakayokuwa
imetajwa penginepo katika Katiba hii na/au kwa maelekezo ya vikao vya Chama.
viii)
Halmashauri Kuu itakuwa na uwezo wa
kumuondoa Katibu Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na kama kura hiyo
itaungwa na zaidi ya nusu ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa Halmashauri Kuu
ambapo hoja hiyo imetolewa.
(35) Kazi za Manaibu Katibu Wakuu wa Chama
Taifa
i)
Kutakuwa na Naibu Katibu Mkuu
atakayeishi na kufanya kazi zake Zanzibar na mwingine ataishi na kukaa Tanzania
Bara. Isipokuwa kwa kuishi kwao hivyo hakutapunguza upeo wa madaraka yao ya
kushughulikia kazi za Chama kwa Tanzania nzima;
ii)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama atakayefanya
kazi Zanzibar ndiye atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano ya Kamati
maalumu ya Halmashauri Kuu ya Chama Taifa Zanzibar;
iii)
Mmoja wao atamsaidia Katibu Mkuu kukaimu
kiti chake wakati Katibu Mkuu hayupo;
iv)
Manaibu Katibu Mkuu wa Chama watakuwa
ndio wasaidizi wakuu wa Katibu Mkuu wa Chama na watafanya kazi zozote za Chama
watakazopewa na Katibu Mkuu wa Chama;
v)
Watakuwa Makatibu wasaidizi wa vikao
vyote vya Chama wakimsaidia Katibu Mkuu;
vi)
Watamsaidia Katibu Mkuu kusimamia
shughuli, taratibu na Kanuni zote za Kiutawala za Chama za kila siku;
vii)
Watakuwa wajumbe wa vikao vyote ambavyo
Katibu Mkuu wa Chama Taifa anashiriki kwa wadhifa wake;
viii)
Naibu Katibu Mkuu Bara ndiye atakuwa
mkuu wa utawala na itifaki wa Chama;
ix)
Watafanya kazi nyingine zozote za Chama
zitakazokuwa zimetajwa penginepo katika Katiba hii na/au kwa maelekezo ya Vikao
vya Chama.
- Akidi katika vikao vyote itakuwa ni asilimia 50
ya wajumbe wote wanaopaswa kuhudhuria kikao husika.
- Bila kuathiri ibara ndogo ya (1) ibara hii, kamati
kuu yaweza kupunguza idadi ya wajumbe watakaopaswa kuhudhuria vikao
mbalimbali kwa wakati fulani kwa asilimia zisizozidi hamsini kwa azimio litakaloungwa mkono na asilimia
75 ya wajumbe wa Kamati Kuu.
- Ikiwa wajumbe walioalikwa wamealikwa kwa
kupunguza idadi kwa mujibu wa ibara
ndogo ya (2) ya ibara hii, basi akidi kwenye vikao hivyo itakuwa asilimia 75
ya wajumbe wanaopaswa kuhudhuria.
SURA YA TANO
NGOME ZA CHAMA NA JUMUIA YA WABUNGE WA ACT
31. NGOME ni vitengo au jumuiya za Chama
1) NGOME
ni vitengo au jumuiya za Chama ambazo zitaundwa na vijana, wanawake na wazee
ambao ni wanachama wa ACT.
2) Kutakuwa
na Ngome za Vijana, Wanawake na Walezi.
3) NGOME
za chama zitakuwa na jukumu kuu la kueneza itikadi, falsafa, misingi na sera za
chama kwa makundi yao husika (Vijana, Wanawake na Walezi).
4) Kanuni
za uendeshaji wa Ngome zitatungwa na Ngome husika na
kuidhinishwa na Halmashauri Kuu kabla ya kuanza kutumika.
kuidhinishwa na Halmashauri Kuu kabla ya kuanza kutumika.
5) Kanuni
na miongozo ya Ngome lazima zizingatie misingi ya Katiba hii. Pale
ambapo kuna mgongano wa kitafsiri kati ya Katiba hii na Kanuni za Ngome, Tafsiri ya Katiba ndiyo itakayotamalaki.
ambapo kuna mgongano wa kitafsiri kati ya Katiba hii na Kanuni za Ngome, Tafsiri ya Katiba ndiyo itakayotamalaki.
32. Kutakuwa na jumuiya ya wabunge wa ACT
Kutakuwa na jumuiya ya wabunge wa
ACT itakayoundwa na wabunge wote wa ACTkwa mujibu wa Katiba hii na Kanuni za Chama.
Jumuiya itaunda utaratibu wake wakuijiendesha bila kuathiri masharti ya Katiba
hii na kanuni za uendeshaji kazi za chama.
SURA YA SITA
MAPATO NA MALI
ZA CHAMA:
(1) Mapato ya Chama ni:
i)
Ada na viingilio
vya wanachama.
ii)
Michango ya hiari
ya wanachama na wafuasi wa Chama.
iii)
Michango ya hiari
ya watu wa ndani na nje wanaounga mkono Chama.
iv)
Misaada kutoka
kwa vyama rafiki vya kisiasa vya ndani na nje ya nchi.
v)
Misaada na ruzuku
kutoka ndani na nje ya nchi.
vi)
Mapato
yanayotokana na hisa na miradi halali ya Chama.
(2) Mali za Chama ni:
i)
Mali zozote zinazohamishika na zisizohamishika.
ii) Hisa
za Chama katika miradi ya kiuchumi.
iii) Mali
za NGOME Taasisi zingine katika Chama.
34. Kutakuwa na bodi ya wadhamini wa Chama
1)
Kutakuwa na bodi ya wadhamini wa Chama yenye wajumbe wasiopungua
saba (7) na wasiozidi tisa (9) itakayoteuliwa na Halmashauri Kuu.
2)
Mali zote za kudumu, vitega uchumi na dhamana zote zitawekwa chini ya
jina lililosajiliwa la Bodi ya
Wadhamini.
3)
Bodi ya wadhamini itateuliwa kila baada ya miaka mitano ya Uchaguzi Mkuu
wa viongozi wa Chama.
4)
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini watateuliwa na Kamati Kuu na kuidhinishwa naHalmashauri Kuu.
5)
Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini watachaguliwa na wajumbe
wenyewe kutoka miongoni mwao.
6)
Wajumbe wa Kamati Kuu hawatateuliwa katika Bodi ya Wadhamini, isipokuwa
Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini watakaoingia kwenye kamati kuukwa
nafasi zao.
7)
Kanuni za Chama zitaainisha taratibu za mikutano ya Bodi ya wadhamini.
35. Ukaguzi wa Hesabu
za Chama
(1) Kutakuwa na Kanuni za Fedha za Chama
zitakazoidhinishwa na Halmashauri
Kuu. Kanuni hizi zitaainisha utaratibu wa fedha ndani ya Chama.
Kuu. Kanuni hizi zitaainisha utaratibu wa fedha ndani ya Chama.
(2) Kutakuwa na Idara ya Ukaguzi wa ndani wa Hesabu za
Chama.
(3) Hesabu za Chama zitakaguliwa kila mwaka na Kampuni
ya Wakaguzi wa Nje
itakayoteuliwa na Kamati Kuu.
itakayoteuliwa na Kamati Kuu.
(4) Hesabu za Chama zitatawasilishwa
katika vikao vya Chama na kwa Msajili wa
Vyama ili azifikishe kwa vyombo vingine kwa mujibu wa Sheria ikiwamo ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali.
Vyama ili azifikishe kwa vyombo vingine kwa mujibu wa Sheria ikiwamo ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali.
(5) Mweka Hazina atatoa
taarifa kwa umma kuhusu taarifa ya fedha ya Chama kila baada ya muda maalum
kama itakavyoamriwa na Halmashauri Kuu.
SURA YA SABA
MAMBO YA JUMLA KUHUSU KATIBA
1) Mapendekezo
ya mabadiliko yoyote ya Katiba yatafanywa na Hamashauri Kuu ya Taifa kabla ya
kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.
2) Mapendekezo
yoyote ya mabadiliko ya Katiba yatajadiliwa katika ngazi za chini za Chama
kabla ya Halmashauri Kuu kuandaa Rasimu ya mapendekezo kwa Mkutano Mkuu.
3) Mkutano
Mkuu ndio pekee wenye mamlaka ya kubadili Katiba.
4) Mapendekezo
ya marekebisho ya Katiba yatafikishwa katika ngazi ya Jimbo si chini ya siku 60
kabla ya tarehe ya Mkutano Mkuu unaohusika kujadilimabadiliko.
5) Kamati
za Jimbo zitatakiwa kurejesha maoni yakena ya wanachamaangalau marekebisho ya katiba.
(1) Halmashauri
Kuu itatunga Kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Chama kwa kuzingatia masharti
ya Katiba hii.
(2) Kukitokea
mgongano kati ya kipengele cha Katiba na kile cha Kanuni, kipengele cha Katiba
kitatamalaki.
(3) Halmashauri
Kuu itakuwa na mamlaka ya kuzifanyia marekebisho Kanuni za Chama ili kwenda na
mahitaji na wakati.
(4) Kamati
Kuu itatunga mwongozo wa uendeshaji wa vikao vya Chama.
38. Kuvunjwa kwa Chama
(1) Chama
kitavunjwa rasmi endapo robo tatu (3/4)
ya wajumbe wote watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama wa Taifa ulioitishwa kwa
madhumuni ya kuvunjwa kwa Chama watapitisha hoja hiyo. Mkutano huo utatangaza
rasmi kuvunjwa kwa Chama na kusimamishwa kwa shughuli zote za Chama.
(2) Katika
tukio la kuvunjwa kwa Chama, Bodi ya Wadhamini wa Chama itahodhi mali zote za
chama na kipaumbele kitakuwa ni kulipia madeni yote ya Chama. Endapo kutakuwa
na salio lolote la mali ya Chama baada ya kulipa madeni yote, salio hilo
litawasilishwa au kukabidhiwa kwa Taasisi yoyote ambayo shughuli zake zinaakisa
misingi iliyoanzisha chama hiki kama itakavyoamuliwa na Bodi ya Wadhamini.
(3) Katika
tukio la kuvunjwa kwa Chama kwa nia ya kuungana na Chama kingine cha Siasa,
Bodi ya Wadhamini wa Chama itahodhi mali yote ya Chama na kuitumia mali hiyo
kulipia madeni yote ya Chama. Endapo kutakuwa na salio lolote la mali ya Chama
baada ya kulipa madeni ya Chama salio hilo litatumika kufuatana na azimio la
kuvunja Chama ili kuungana na Chama kingine.
Kuanza
Kutumika kwa Katiba Hii:
Katiba hii itaanza kutumia Tarehe 28 Machi 2015,
baada ya kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama Taifa.
NYONGEZA YA KWANZA
KANUNI ZA MWENENDO NA MAADILI YA
VIONGOZI WA ACT
SEHEMU YA I:
MASHARTI YA JUMLA
Ibaya ya 1:
Dhumuni la Maadili ya Uongozi
Dhumuni
la Kanuni hizi za mwenendo na maadili ya viongozi ni kuweka viwango vya tabia
na mienendo ya viongozi wa chama ili kuwafanya wawe na uwezo wa kimaadili
kuiongoza jamii katika namna ya utii wa sheria na misingi ya ACT.
Ibara ya 2:
Wanaohusika na Kanuni hizi za Mwenendo
na Maadili
Kanuni
hizi zitawahusu viongozi wote wa chama ndani ya ACT katika ngazi zote, wagombea
katika uchaguzi wowote ule wanaogombea kwa tiketi ya ACT na mwanachama yeyote
wa ACT-Tanzania anayeshikilia nafasi ya uongozi katika taasisi ya umma.
Kanuni
hizi pia zitakuwa ni rejea na nyongeza ya Katiba ya ACT.
SEHEMU YA II:
SIFA ZA KIONGOZI
Ibara ya 3: Kiongozi wa
ACT:
1)
Awe
Mzalendo;
2)
Asiidhalilishe
nchi yake Tanzania na Watanzania;
3)
Awe
na mtazamo wa kimaendeleo na mbunifu;
4)
Awe
mwadilifu;
5)
Awe
na maadili ya kiutamaduni, mwenendo na awe ni mtu wa kuchangamana na watu;
6)
Awe
na mapenzi ya dhati kwa chama na mweledi;
7)
Asiwe
amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai linalohusiana na kukosa uaminifu;
8)
Asiwe
amewahi kunyang’anywa haki ya kiraia na/au ya kisiasa, isipokuwa kama
alirudishiwa haki hiyo baada ya
kuthibitika kutokuwa na kosa;
9)
Awe
na umri wa miaka 18 au zaidi;
10)
Ajue
kusoma na kuandika; na
11)
Asiwe
amewahi kufungwa jela kwa kipindi kinachozidi miezi sita bila parole kwa kosa
linalohusiana na kukosa uaminifu.
SEHEMU YA III:
MAADILI YA VIONGOZI
Ibara ya 4: Sheria na
Kanuni ambazo kiongozi wa ACT anapaswa kuzitii
Kiongozi
wa ACT atatii Katiba ya Nchi, Sheria za Nchi, Katiba ya ACT na kanuni zake
pamoja na Nyongeza hii ya Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Viongozi.
Ibara ya 5:
Mwenendo bora wa Kiongozi
Kiongozi
wa ACT atapaswa kuwa na viwango vifuatavyo vya kiuongozi:
1)
Uzalendo
na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi;
2)
Kuzijua
na kuziheshimu haki za binadamu na kuwahimiza wanachama na viongozi wengine
kufanya hivyo;
3)
Kujielimisha
wakati wote
4)
Kufanya
kazi zake kwa kuzingatia misingi ya Demokrasia, Uwazi na Mashauriano;
5)
Kuwa
tayari kupokea na kuwasikiliza wote wanaomuijia;
6)
Kukuza
utamaduni wa mashirikiano na kuwawezesha wanachama kutekeleza wajibu wao;
7)
Kuwataka
wanachama kuheshimu maelekezo halali na kusimamia utekelezaji wa shughuli
zilizoainishwa;
8)
Kuheshimu
ratiba ya kazi, muda na kuwasilisha ripoti panapohitajika;
9)
Kuchapa
kazi kwa bidii, umakini na weledi
10)
Kuwafanya
wanachama watambue mipango na programu za chama na kwa nafasi yake, kiongozi
awe mfano wa kuigwa katika kutekeleza mipango na programu hizo;
11)
Awe
mtetezi wa Umoja wa Taifa na Afrika;
12)
Kupinga
na kupigana dhidi ya ubaguzi wa aina zote;
13)
Kutangaza
mali zake kwa mujibu wa sheria hii ya miiko na maadili ya Viongozi;
14)
Kujitahidi
kuwa mkweli katika kutimiza wajibu wake na katika jambo lingine lolote
linalohusu mwenendo kwa hiari ama kwa kuombwa;
15)
Asiwe
mtu wa kujali maslahi yake binafsi dhidi ya maslahi ya umma;
Ibara ya 6:
Matendo ya Ubaguzi na Utengano
Katika
kutekeleza majukumu yake, kiongozi hataruhusiwa kumpendelea mtu yeyote kwa
misingi ya udugu/urafiki, ukabila, familia, ukoo, udini, jinsia, mkoa ama
kufanya tendo lolote litakalopelekea ubaguzi na kuwatenga watu katika madaraja.
Ibara ya 7:
Makatazo mengineyo
Kiongozi
pia hataruhusiwa kufanya yafuatayo:
1.
Kushindwa
kulipa deni linalotokana na dai ama mkataba halali; kutoa ama kupokea rushwa,
kutaka kuabudiwa na kupewa upendeleo, utapeli, utakatishaji fedha na makosa
mengine yanayohusiana na rushwa;
2.
Kuweka
maslahi ya mataifa ya nje mbele badala ya maslahi ya Tanzania;
3.
Kutenda
ama kuunga mkono tendo lolote linalolenga kukidhalilisha chama na/au nchi yetu;
4.
Kutumia
vibaya mali za chama na za taifa yeye mwenyewe ama kwa makusudi kuwaacha
wanachama kufanya hivyo; kujibinafsisha mali au mchango uliotolewa kwa ajili ya
chama na/au taifa, mradi ama tawi analosimamia;
5.
Matumizi
ya maneno na matendo yanayolenga kushusha hadhi, kudhalilisha utu, kumsimamisha
ama kumfukuza mwanachama ama kiongozi mwingine kinyume na katiba ya chama na
kanuni za uendeshaji chama;
6.
Kutumia
udikteta na ukandamizaji;
7.
Kutumia
madaraka vibaya kwa kuwanyanyasa watu na kuvunja sheria;
8.
Kujimilikisha
ngazi/idara/kitengo cha chama anachoongoza;
9.
Na
mwenendo wowote ambao unaweza kushusha uadilifu, kazi ama nafasi aliyonayo kama
itakavyotafsiriwa na Halmashauri Kuu kwa mujibu wa Katiba ya ACT, Katiba ya
Tanzania na sheria za nchi.
SEHEMU YA V:
MASUALA KINZANI YANAYOHUSIANA NA KAZI
Ibara ya 8:
Masuala Kinzani
Inapotokea
kiongozi ana wajibu wa kufanya maamuzi kwenye jambo lolote ambalo ana maslahi
binafsi nalo, atatakiwa kuwataarifu viongozi wa juu yake ama mkuu wa taasisi
iliyomwajiri ama kumteua na kuwataka radhi kwamba hatafanya uamuzi huo. Maslahi
binafsi yaweza kutokana na nafasi yake au sababu nyingine yoyote iwe ni mchango
wake mwenyewe ama kitu alichochangia na wengine ama ni mshauri tu.
Ibara ya 9: Viongozi
kutofanya biashara
Kiongozi
wa kuchaguliwa au kuteuliwa kwenye vyombo vya serikali kuanzia ngazi ya jimbo
na kuendelea, hataruhusiwa kumiliki, kufanya ama kuendesha biashara ya binafsi.
Ikitokea kiongozi wa namna hiyo ana biashara ya binafsi, mbali ya kuitangaza
hadharani, atatakiwa kuiweka biashara yake chini ya menejimenti binafsi na
kutangaza hilo hadharani.
SEHEMU YA VI:
KUTANGAZA MALI BINAFSI ZA KIONGOZI
Ibara ya10:
Tangazo la mali binafsi za kiongozi
Kila
kiongozi wa ACT wa kuchaguliwa ama kuteuliwa kwenye ngazi ya Jimbo au zaidi
atawasilisha tangazo la mali zake binafsi, zilizo ndani ama nje ya nchi, kwenye
Ofisi ya Katibu Mkuu.
Fomu
ya tangazo la mali ikionyesha mali halisi za kiongozi itawasilishwa ofisini kwa
Katibu Mkuu si zaidi ya tarehe 30 Juni ya kila mwaka, kwa viongozi ambao bado
wako madarakani na katika kipindi kisichozidi siku 15 tangu wamalize muda wao
kwa viongozi waliomaliza muda wao wa uongozi. Viongozi wapya waliochaguliwa
watatakiwa kuwasilisha tangazo la mali ofisini kwa Katibu Mkuu wa chama katika
kipindi cha mwezi mmoja tangu walipoingia madarakani.
Kiongozi
yeyote ambaye fomu yake ya tangazo la mali haikukubaliwa, atatakiwa kuwasilisha
nyingine ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Na kama fomu ya tangazo la mali
haikukubaliwa kwa mara ya pili na kwa sababu ambazo amefahamishwa yeye
mwenyewe, Ofisi ya Katibu Mkuu itaandaa taarifa na kuiwasilisha kwa chombo/mamlaka
iliyomchagua/kumteua huyo kiongozi kwa ajili ya hatua stahiki dhidi ya kiongozi
mhusika. Taarifa ya Mali na Madeni ya Viongozi itawekwa wazi kwenye tovuti ya
chama na daftari la mali na madeni litakuwa wazi kwenye ofisi ya Katibu Mkuu.
Ibara ya 11. Viongozi
kutangaza mali kabla hawajamaliza muda wao
Kila
kiongozi aliyeko madarakani kwa kuchaguliwa ama kuteuliwa kwenye ngazi ya Jimbo
au zaidi na ambaye ametangaza mali zake kwa mujibu wa ibara ya 10 ya nyongeza
hii, atalazimika kutangaza mali zake miezi sita kabla ya kipindi chake cha
uongozi kumalizika. Baada ya hapo ofisi ya Katibu Mkuu itafanya uchunguzi juu
ya tangazo hilo na kuweka hadharani ripoti.
Ikiwa
uchunguzi utaonyesha kwamba kuna uvunjifu wa maadili, mali ilinunuliwa kwa njia
haramu, rushwa ama wizi, kiongozi ataondolewa kwenye nafasi yake na kupelekwa
kwenye vyombo vya nidhamu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
SEHEMU YA VII:
ADHABU NA MAREJEO MENGINE
Ibara ya 12:
Adhabu kwa kiongozi mwenye hatia
Bila
kuathiri sheria nyingine za nchi, kiongozi yeyote atakayevunja masharti ya
nyongeza hii ya kanuni za mwenendo na maadili, atakabiliwa na mojawapo ya
adhabu zifuatazo:
1.
Onyo
kwa maandishi;
2.
Karipio
kwa maandishi;
3.
Kuachishwa
uongozi; na
4.
Kuachishwa
uongozi kutakakofuatiwa na uchapishaji wa sababu za kuachishwa kwenye magazeti
ikiwa ni kwa maslahi ya umma.
Kiongozi
atakayeng’ang’ania kukaa kwenye nafasi ambayo ameondolewa ama kusimamishwa,
ataondolewa uanachama.
Ibara ya 13:
Haki ya Kujitetea
Kiongozi
yeyote aliyepatikana na hatia kwa mujibu wa Maadili na Miiko iliyoainishwa
katika nyongeza hii atakuwa na haki ya kusikilizwa.
Ibara
ya 14: Rufaa
Kiongozi
yeyote atakayeadhibiwa adhabu yoyote iliyomo kwenye nyongeza hii ya mwenendo na
maadili ya viongozi, anaweza kukata rufaa kwa ngazi ya juu inayofuata kwa
maandishi akielezea utetezi wake ama maelezo mengine kwenye kosa ambalo kwalo
uamuzi ulichukuliwa. Utetezi huo uifikie ngazi ya rufaa ndani ya siku 14 baada
ya kutaarifiwa.
Mchakato
wa rufaa hautasimamisha utekelezaji wa uamuzi uliokwishachukuliwa isipokuwa
kama mrufani ameomba hivyo na baada ya mamlaka ya rufaa kujiridhisha kwamba
mamlaka ya chini ilikosea katika uamuzi wake ama kwamba ilipotoshwa wakati
ikichunguza na kuchukua uamuzi huo.
SEHEMU YA VIII:
MASHARTI MENGINEYO NA MASHARTI YA
MPITO
Ibara ya 14:
Chombo
chenye wajibu wa utekelezaji wa kanuni hizi za mwenendo na maadili
Kamati
ya Uadilifu ya kila ngazi ndiyo itakuwa na wajibu wa kutekeleza kanuni hizi za
mwenendo na maadili ya viongozi isipokuwa pale itakapokuwa imeelezwa
vinginevyo. Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama itahakikisha kunakuwepo utengamano
katika utekelezaji wa kanuni hizi za mwenendo na maadili na Katiba ya Chama.
Kila
ripoti ya mwaka ya Katibu Mkuu itaonyesha nini kimeonekana katika utekelezaji
wa kanuni hizi za mwenendo na maadili ya viongozi.
Masharti
yote yaliyotangulia yanayokinzana na kanuni hizi za asili yanabatilishwa rasmi.
Ibara ya 15:
Kuanza kutumika kwa Kanuni hizi
Kanuni
hizi za mwenendo na maadili ya viongozi zimepitishwa rasmi kuwa nyongeza ya
katiba ya chama na Mkutano Mkuu wa Taifa wa ACT jijini Dar es salaam na kuanza
kutumika leo tarehe 28 Machi 2015.
[1]Tamko
la Azimio la Arusha lililotolewa na Chama cha TANU mnamo mwezi Februari mwaka
1967 . Tutazingatia misingi ya Azimio hili na hususani Miiko ya Uongozi kama
itakavyofanyiwa marejeo mara kwa mara,
pamoja na Maazimio mengine yatakayotangazwa na chama kwa mujibu wa
Katiba hii yatakuwa ni marejeo halali ili kufikia maamuzi yeyote ya kisera ya
Chama cha ACT – Tanzania.
katiba ni zuri na yaitaji utekelezaji tu. ACT chapeni kazi watanzania wakomboleweeeeee.
No comments:
Post a Comment