KESHA LA ASUBUH
ALHAMIS FEB.11/2016.....
🌲🌲🌲🌲🌲🌲
KRISTO ALIITUKUZA SHERIA NA KUIFANYA IHESHIMIKE..........
📖📖📖📖📖📖
Bwana akapendezwa kwa ajil ya hak yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Isaya 42:21
🌲🌲🌲🌲🌲🌴
➡Sheria ya serikal ya Mungu ilikuwa itukuzwe kwa kifo cha mwana pekee wa Mungu. Kristo alibeba hatia ya dhambi za ulimwengu. Utoshelevu wetu unapatikana tu kwa mwana wa Mungu kufanyika mwanadam na kufa. Aliteseka kwa sababu alitegemezwa na MUNGU. Alistahimil kwa sababu hakuwa na doa lolote la kutotii au dhambi. Kristo alishinda kwa niaba ya mwanadam kwa namna hiyo akichukua uhalali wa adhabu.Alithibitishia watu uzima wa milele hal.akiitukuza sheria na kuifanya iheshimike.......
➡Kila mtu anawajibika kufuata nyayo za kristo aliye kielelezo kikuu kwa jamii ya wanadamu. Alisema "NIMEZISHIKA AMRI ZA BABA YANGU " Mafarisayo walifikiri kuwa alikuwa anajaribu kuhafifisha madai ya sheria ya MUNGU lakini sauti yake ilisikika masikioni mwao ikisema "MSIDHANI YA KUWA NALIKUJA KUITANGUA TORATI AU MANABII "LA" SIKUJA KUTANGUA BALI KUITIMILIZA.
➡Kwa maana amin nawaambia mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie..
➡Kristo alikuja kuitukuza sheria na kuifanya iheshimike alikuja kuitukuza amri ya kale ambayolikuwa nayo tangu mwanzo. Kisha tunahitaji torati na manabii. Tunahitaj agano la kale kutuletea hatuabkwa hatua hadi agano jipya ambalo halichukui nafasi ya agano la kale lakin linafafanua kwa uwaz zaid mpango wa wokovu likifanya mfumo wa dhabihu na sadaka kuonekana katika umuhim wake na pia umuhim wa lile neno tulilokuwa nalo tangu mwanzo .
➡Utiifu uliokamil unaunganishwa na kila nafs na utiifu kwa mapenz ya MUNGU yanayobainishwa utakufanya kuwa mmoja na kristo... Imeandikwa juu yake hiv "TAZAMA NIMEKUJA KATIKA GOMBO LA CHUO NIMEANDIKWA KUYAFANYA MAPENZI YAKE EE MUNGU WANGU NDIYO FURAHA YANGU :, NAAM SHERIA YAKO IMO MOYONI MWANGU...
🌷🌷🌷🌷🌷🌷
➡MWISHO⬅
🌴🌴🌴🌴🌴🌴
Wednesday, February 10, 2016
KESHA LA ASUBUI LEO 11/02/2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment