Marekani na kura ya Uingereza
Mkuu wa kitengo cha shirikisho la uhifadhi nchini Marekani ,Janet Yellen, ametupilia mbali hoja ya Marekani kuingia kwenye kipindi cha mpito na kuyumba kwa uchumi wake endapo Uingereza itajiondoa katika umoja wa ulaya.
Wakati akijibu maswali kutoka katika kamati ya Senate Yellen amesema kipindi cha mpito na kuyumba kwa uchumi wa nchi yake hakutokani ama haitakuwa chanzo cha kura hiyo, hakuna ajuaye nini kitatokea.
Ameeleza imani yake kwa wawekezaji kwamba watafanya maamuzi sahihi na kuamua kwa busara katika masoko ya fedha, ambako italeta taswira bei shirikishi na viwango vya juu vya riba kwa wakopaji walio wengi.
No comments:
Post a Comment