Saturday, June 25, 2016

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YATOA ELIMU YA UBIA KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KWA WABUNGE


by rorya1Mgeni Rasmi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua Semina  iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta  ya Umma ilifofanyika leo Mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Mswekwa ikiwa na Lengo la kuwajengea uwezo wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikisha Sekta Binafsi katika miradi ya maendeleo.2Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Vijana Kazi Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama(wa kwanza kushoto) akifuatilia Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ikilenga kuwajengea uwezo wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikiana kati ya Sekta Binafsi na ile ya Umma (PPP) Katika miradi ya maendeleo. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo.3Mbunge wa Ileje Mhe. Janet Mbene akitoa maoni yake  wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu  umuhimu wa kushirikisha Sekta Binafsi katika miradi ya maendeleo.4Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo  jinsi miradi itakayotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi inavyoweza kuchangia kukuza maendeleo.5Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi  wa semina ya kuwajengea uwezo Wabunge kuhusu umuhimu wa Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP) akifurahia jambo mapema leo Bungeni Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bajeti Mhe. Josephat Kandege.
Continue reading →
by JOHN BUKUKU on JUNE 25, 2016 in JAMII with NO COMMENTS
P11Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye uzinduzi wa kituo cha Mawasiliano cha Polisi Call Centre Biafra Kinondoni.
…………………………………………………………………………………………………
Jonas Kamaleki, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kuwadhibiti majambazi ipasavyo kwa kuwanyanganya silaha kwenye matukio ya kiuharifu ili kukomesha vitendo viovu katika Taifa.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii.
“Inashangaza jambazi anavamia kituo cha polisi anaua na anaondoka wakati polisi wapo na wana silaha na risasi wanazo lakini wanashindwa kumnyang’anya silaha,”alishangaa Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa ujambazi na vitendo vya uharifu nchini inabidi vikomeshwe mara moja ili watanzania waishi kwa amani na kufanya maendeleo kwani wananchi wanataka maendeleo.
Akiongelea kuhusu maslahi na vitendea kazi kwa jeshi la polisi, Rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kuliwezesha jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa ubora zaidi.
Rais Magufuli ameonyesha kuwa na imani na jeshi la polisi licha ya kuwa na kasoro ndogo ndogo kwa baadhi ya polisi ambao wanalichafua jeshi hilo.
Aidha ametoa agizo kwa TCRA kushirikiana na jeshi la polisi nchini ili kuweza kurekodi simu na kutoaprint out mara moja tofauti na ilivyo sasa.
Kuhusu kundi la wafanyakazi wanaofanyakazi kwenye Dawati la Taarifa la polisi, Mhe. Rais amemtaka Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu kuwafikiria na kuwapatia posho ya kazi kwani kazi wanayoifanya ni ngumu mno na inahitaji umakini zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemwomba Mhe. Rais kuliongezea fedha jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa ustadi zaidi na kukomesha vitendo vya uharifu nchini.
Makonda amelipongeza jeshi la polisi kwa kudhibiti matukio ya ujambazi hapa nchini hususan kwenye mabenki.
Mpango huu wa Usalama wa Jamii umezinduliwa leo na utadumu hadi 2019 na unatarajiwa kutoa matokeo makubwa ya kudhibiti uharifu nchini.

MAGUFULI AWATAKA POLISI KUDHIBITI MAJAMBAZI NCHINI

No comments:

Post a Comment