Sunday, November 6, 2016

Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?

Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?


Bi Hillary Clinton (kushoto) na mumewe Bw Bill Clinton mjini Las Vegas, Nevada.Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionBaadhi wamependekeza aitwe BROTUS, First Dude, First Gentleman na wengine First Laddie
Swali ambalo limekuwa likiulizwa tangu kubainika kwa uwezekano kwamba Bi Hillary Clinton anaweza akawa rais wa Marekani ni jina ambalo mumewe atapewa.
Kwa sasa Bi Clinton, anayewania urais kupitia chama cha Democratic, amekuwa akiongoza katika kura za maoni kitaifa na katika majimbo mengi yanayoshindaniwa.
Wengi wamekuwa wakichakura kwenye Google.
Katika ngazi ya kimataifa, nafasi kama atakayoichukua Bw Bill Clinton si jambo geni. Mumewe Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Joachim Sauer, ambaye ni mprofesa wa kemia, huitwa jina lake tu.
Mfadhili Philip John May, mumewe waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, sawa na Ujerumani, hana jina rasmi.
Lakini nchini Marekani, kumekuwa na utamaduni wa kumrejelea Rais na Mke wa Rais ambaye huitwa First Lady na ambaye kwa Kiswahili huitwa Mama wa Taifa.
Kwa kuwa hali kama ya sasa haijawahi kutokea, si swali rahisi kujibu.
Nafasi inayokaribia zaidi ni ya mke wa gavana wa jimbo Marekani ambaye kwa Kiingereza huitwa First Gentleman.
Kwa sasa Marekani ina wanaume sita kama hao.
Jina hilo lilivuma mtandaoni Bi Clitnon alipoidhinishwa na kamati kuu ya Democratic kuwania urais Julai. Google wanasema swali kuhusu jina atakalopewa mume wa rais liliulizwa sana wakati huo.
Lakini FGOTUS (First Gentleman of the United States) huenda lisivutie kama FLOTUS, ufupisho wa mke wa rais (First Lady of the United States).
Baadhi wamependekeza aitwe First Dude au First Laddie, kwa sababu ya asili ya Clinton ya Celtic.
Hillary Clinton akiwa Cincinnati, Ohio.Image copyrightAP
Image captionMfuasi akiwa na bango linalosoma: "First Laddie"
Akihojiwa na Jimmy Kimmel Novemba mwaka jana, Bi Clinton mwenyewe alisema hana uhakika ni jina gani litafaa.
"Sasa kuna tatizo zaidi kwa sababu marais wote wa zamani wa Marekani pia huitwa Bwana Rais."
"First dude, first mate, first gentleman, sina uhakika," Bi Clinton alisema.
Bw Clinton majuzi aliingilia mjadala huo kwenye kampeni: "Sijali wataniita nini bora tu (Bi Clinton) ashinde."
"Nitakuwa First Volunteer (Mtu wa Kwanza Kujitolea). Natumai kuwa mtu atakayekuwa tayari zaidi kumfanyia kazi bila malipo."

No comments:

Post a Comment