Gari linaloweza kuundwa kwa saa nne pekee
Gari la kielektroniki linaloweza kujiendesha na ambalo huenda likawa katika barabara za Uingereza limezinduliwa nchini humo.
Gari hilo lenye mtindo wa kipekee na ambalo limetumia vifaa vyepesi kuundwa linaweza kutengezwa na mtu mmoja kwa saa nne kulingana na kampuni inayotengeza magari hayo.
Gari hilo litakuwa tayari kuingia barabarani wakati sheria za magari ya kujiendesha itakapoidhinishwa .
Serikali inatarajia kwamba magari hayo yataanza kuendeshwa ifikiapo 2020.
''Malori ya siku hizo hayakubaliki,yana kelele,yanaharibu mazingira na sio rahisi kutumia'', alisema Denis Sverdlov, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kitekenolojia ya Automotive Technology.
Tunatengeza malori vile yanavyopaswa kutengezwa,bei rahisi,maridadi,hayana kelele,masafi na yalio na usalama wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment