Fedha zilizolipwa FIFA zazua balaa.
Barua inayosemekana iliandikwa na rais wa shirikisho la soka nchini Afrika kusini, Danny Jordaan, inaonekana kuongeza uzito kwenye shutuma kwamba serikali ya nchi hiyo ilificha malipo ya pesa kiasi cha dola milioni kumi kwa FIFA .
Barua hiyo iliyoandikwa miaka kumi iliyopita iliyotumwa kwa katibu mkuu wa shirikisho hilo la soka duniani, Jerome Valcke imechapishwa kwenye vyombo vya habari bila idhini.
Inasema kuwa kufuatia mazungumzo na waziri wa mambo ya nje Bwana Jordaan aliomba pesa hizo zilipwe kwa njia zisizo za moja kwa moja.
Maafisa wa Afrika Kusini wamesisitiza kuwa pesa hizo hazikuwa za rushwa kwa ajili ya kupokea mashindano ya fainali ya kombe la dunia la mwaka 2010.
Wanasema yalikua ni malipo halali kuunga mkono maendeleo ya soka katika nchi za Caribbean.
No comments:
Post a Comment