Monday, July 11, 2016

Uingereza na Kenya zachunguza matumizi ya dawa



Image copyrightGETTY
Image captionUingereza na Kenya zachunguza matumizi ya dawa
Maafisa wa kupambana na matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku katika riadha kutoka Uingereza watazuru Kenya baada ya ufichuzi wa shirika la habari la Ujerumani uliothibitisha kuwa matumizi ya madawa hayo haramu bado yapo katika kambi moja ya riadha nchini Kenya.
Ufichuzi wa shirika la habari la ARD/WRD uliopeperushwa hapo jana ulionesha nyuso za madaktari wakenya wanaowapa wanariadha husika madawa hayo kinyume cha sheria.
Hii ni hata baada ya Kenya kupitisha sheria kali ya kupambana na kuenea kwa matumizi ya madawa hayo haramu.
Aidha ufichuzi ulibaini kuwa madaktari hao huwapa madawa hayo haramu wanariadha kutoka Uingereza ambao wanafanyia mazoezi yao nchini Kenya.
Kwa mujibu wa ARD, kambi ya masafa ya juu iliyoko mjini Iten Kenya ilikuwa na ushahidi wa kukiukwa kwa sheria za shirika la kupambana na madawa hayo duniani WADA.
''Katika video hiyo iliyopeperushwa na runinga ya taifa, ya dakika nane, mwandishi mpekuzi aliyejifanya kuwa kocha wa riadha na wakala waliokuwa wamevaa kamera za siri walifaulu kununua dawa hizo za kuongeza nguvu mwilini.
Image copyrightAP
Image captionTakriban wanariadha 40 kutoka Kenya wamegunduliwa kuwa walitumia madawa hayo yaliyopigwa marufuku
Hii ikiwa ni miezi michache tu baada ya ufichuzi mwengine kama huo kusababisha Kenya kutishiwa kuondolewa kwenye mashindano ya dunia kwenye mizani sawa na Urusi.
Hata hivyo hivyo Kenya ilijifurukuta na kupitisha kuwa sheria kali mswada huo wa kupambana na matumizi hayo ya dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Kufuatia ufichuzi huo sasa shirika la kupambana na mihadarati nchini Uingereza UKAD limetuma wachunguzi Kenya ilikupeleleza madai hayo na kupendekeza hatua itakayochukuliwa dhidi ya wanariadha husika.
Mkurugenzi wa UKAD Nicole Sapstead ameiambia BBC kuwa ''bila shaka hatuwezi kufichua haswa nini tunachokichunguza ila, tunaendeleza upelelezi wetu chini kwa chini ilitufichue haswa kiini cha tatizo hilo kwetu kama Riadha ya Uingereza na hata Kenya ambako ndiko tuhuma hizi zilikoanzia.''
Serikali ya Kenya kwa upande wake imesema kuwa inafanya uchunguzi wa kina kabla ya kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.

No comments:

Post a Comment