Uvaaji wa Chupi - Afya ya Uzazi
by rorya maendeleo..
Na Mdau Joyce MasikaLeo naomba nikukumbushe somo la Afya ya uzazi. Somo hili litafafanua faida na hasara au madhara yatokanayo na uvaaji wa nguo za ndani hasa Chupi.Uvaaji wa chupi kihistoria ulianza karne ya 19 baada ya uvumbuzi wa viwanda na mapinduzi yake yaliyoambatana na mapinduzi ya teknolojia.Enzi za mama zetu na babu zetu uvaaji wa chupi haukuwepo hapa Tanzania. Uvaaji wa chupi uliletwa na wamisionari na wakoloni wakati wanaleta dini Africa. Kabla ya hapo waafrica hatukuwa na utamaduni wa KUVAA chupi.Mtoto akizaliwa hakuvalishwa chupi kamwe kama ilivyo Leo.Mwanamke pia enzi hizo alikuwa havai chupi. Mwanaume naye pia alikuwa havai chupi? Watu wote walikuwa hawavai chupi. Mwanamke alikuwa hachuchumai chini pindi akijisaidia kutokana na kwamba hawakuwa wanavaa chupi hivyo wakitaka kujisaidia haja ndogo walikuwa wanasimama tu na kupanua miguu na kuanza kukojoa.Nyakati za leo ambapo uvaaji chupi kwa wanaume na wanawake uko juu sana kuanzia watu tunapokuwa watoto wadogo hali ya Afya ya viungo vya uzazi imeendelea kuwa mbaya sana. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya kuvaa chupi :1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako.Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jinzi, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana.Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu. Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida. Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana.Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako.
3. Chupi husababisha ugumba kwa wanaume.Sababu nyingi za ugumba tunaweza ukizipata kutoka kwa madaktari wetu wa hospitali zetu. Lakini kwangu mimi sababu nyingine ya ugumba wa wanaume kuwa ni kuvaa chupi zinazobana sana.Mwanaume wengi siku hizi hawavai chupi. Anavaa kaptura au boxa badala ya chupi. Tena havai kaptura inayobana sana. Anavaa isiyobana viungo muhimu kwa uzalishaji wa watoto. Mbegu za kiume huzalishwa kwa wingi wakati wa baridi. Kuvaa chupi inayobana kwa muda mrefu husababisha korodani kuchemka sana na kushindwa kuzalisha mbegu nyingi. Mwanaume mwenye mbegu chache hushindwa kutungisha mimba kwani mbegu zake zinakwenda ukeni huku zikiwa dhaifu na kushindwa kuogelea ukeni.
4. Chupi husababisha miwasho sana kwenye mapaja ya mwanaume na mwanamke.Epuka kuvaa chupi zinazobana ili kuepukana na miwasho.
No comments:
Post a Comment