Friday, April 15, 2016

UFUNGUZI WA HUDUMA YA AFYA KWA JAMII KWA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA NA MIKOA JIRANI

Haya ni baadhi ya matukio katika picha ya sherehe kubwa ya ufunguzi  na uzinduzi wa kampeni ya afya kwa wakazi wa jiji la Mwanza na hata mikoa jirani hasa kanda ya ziwa. Huduma hii ni ya siku mbili na kufuatiwa na mahubiri yatakayoanza Jumapili ya tarehe 31 mwezi huu wa 8.
Kikosi cha vijana cha watafuta njia wakipita kwa mwendo wa haraka huku wakitoa hesima mbele ya mgeni rasmi
Kikosi cha vijana cha watafuta njia wakipita kwa mwendo wa haraka huku wakitoa hesima mbele ya mgeni rasmi
Eneo la shughuli katika uwanja wa michezo wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Sehemu ya wahudhuriaji wa tukio hilo
Dkt. Bhangi, mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza akiongea na mkutano kwa niaba ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mwanza
Sehemu za huduma za Afya zikiendelea
Mtaalamu wa afya Dkt. Obeid Kabinza akiendelea na huduma ya afya

JUMA LA AFYA KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KIMARA LAHITIMISHWA KWA BONANZA

Wiki iliyoanza jana  ilikuwa  ni ya mbaraka kwa washiriki wa Kimara Sda kwa semina za afya zilianza siku ya jumapili huku mada mbambali zikiwasilishwa na madakitari,ya kwanza ikihusisha umuhimu wa kujua ni magonjwa yatokanayo na lishe duni,ambapo mtoa mada Dr.Sabai alisisitiza lishe ni jambo muhimu sana kwa afya binadamu na semina hizi ziliendelea hadi jumamosi siku ya Sabato na siku hii watu waligawanyika katika makundi kulingana na rika lao ili iwe vyepesi kwa watoa mada waweze kujua ni nini rika husika linataka na hivyo kwa kupitia majibu ya  maswali mbalimbali toka kwa rika husika.
Jumapili baada ya semina kuisha kukawa na bonanza kubwa lilofanyika katika viwanza vya Shule ya Msingi Mavurunza Kimara Dar Es Salaam,bonanza hili lilihusisha michezo kama vile,kukimbia mbio za mita 100,mbio za kupokezana vijiti na kukimbiza kuku.
Zikianza mbio kwa namna hii hapo inahesabiwa moja,mbili,tatu jiandae ...kimbia
Inahitaji nguvu,jitahada na ubunifu na kwa mbio hizi za wanaume wa zaidi ya miaka 30 wakikimbia mbio moja kati ya michezo iliyoleta furaha na hamasa siku ya jana. 
Watoto nao hawakupenda kuachwa mbali,wako makini wasipitwe na mbio hizi zenye umbali wa mita 100 katika viwanja vya Mavurunza.
Wakina mama ni jeshi kubwa..hapa ni maandalizi ya mbio yakianza na wakisubiri mwamuzi wa mchezo ambaye ni mchungaji wa mtaa wa Kimara Rahisi Mande atoe ruksa na kufungilia mbio hizo.
Hili ni kundi la kwanza kwa mchezo wa kupokezana vijiti na hapa wakienda mbio kuwapa wenzao kundi namba mbili wakiwa mbele kabisa na katika mchezo huo Mzee Joshua Manyama ndiye aliibuka mshindi.
Mzee Manyama akiitimisha mbio hizi akiwa mbele kabisa kuwashinda wenzake na kushika nafasi ya kwanza kwa mchezo kwa kukimbia na kijiti hapo jana.
Mzee Ronard Manongi akikikimbia na kijiti katika uwanja wa Mavurunza ambapo Mzee Joshua Manyama ndiye alishinda mchezo huo.
Kushoto ni mshindi wa mbio za kukimbia na kijiti,Joshua Manyama anayefuata ni mchungaji wa mwamuzi wa michezo yote ya jana Rahisi Mande akimwelekeza mchukua taarifa za washindi na hapa wakiandika jina na Joshua Manyam.
Mama Manyama mke wa Joshua Manyama kushoto akikimbia kumkaribia kuku ambaye alifunguliwa ili wamkimbize wakina mama katika mchezo wa kukimbiza kuku lakini baadae ndiye alikuwa mshindi na kulia ni Mama Naetwe Manongi nae akikimbia kwa bidii katika mchezo huu.
Hapa ni Mama Mchungaji(kushoto) mwenye jezi ya blu anayefuata ni Diana Manyama,Asnati Ngakonda na mwisho ni Naetwe Manongi wakikimbiza kuku katika shindano la kukimbiza kuku lililofanyika jana.
Kulia ni Diana Manyama akifurahi mara baada ya kushinda katika shindano ya kuku hapo jana kushoto ni Asnati Ngakonda akimpongeza na kulia ni mtoto akishuhudia.


Furaha na bashasha zilitawala mara baada ya ushindi na Mama Diana Manyama akielekea kuhojiwa na mtangazji juu ya ushindi wake.
Kwa vijana huyu ndiye mbabe kupita wote kwa siku ya jana,kwani kijana John (kulia) alijipatia zawadi nono ya kuku aliyoshinda mara baada ya kuwashinda wenzake kwenye mchezo wa kukimbiza kuku hapo jana viwanja vya Mavurunza hapa akihojiwa juu ya ushindi wake na mtangazaji toka morning star redio Jackson Sekiete(kushoto).
Kulia ni Dr.Mathias Abuya(kulia) akiwa na kuku ambaye alimpata mara baada ya kushinda katika shindano la kukimbiza kuku na Dr.Abuya ndiye alikuwa mtoaji mada kwa juma lililopita la afya ambalo siku ya jana lilikamilishwa na bonanza la michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku,kukimbia na kijiti na mbio za mita 100 na hapa akiwa na Jackson Sekiete mtangazaji toka Morning star redio akieleza juma la afya lilivyokuwa na mwito wa washiriki wa kanisa katika maswala ya afya akigusia huduma za vipimo vya bure kwa uchunguzi kwa magonjwa na kina mama kama vile saratani ya matiti na kizazi.
Vuta nikuvute,hapa anatafutwa mashindi katika mchezo wa kuvuta kamba,na timu upande wa kulia walishinda.

MTAA WA KIMARA SDA KUZINDUA PROGRAMU ZA UTUME KESHO, ZIKIPAMBWA NA TUKIO LA UGAWAJI WA VITABU VYA TUMAINI KUU & AFYA NA UZIMA

 Sabato ya kesho ni maalum kwa uzinduzi wa Programu za utume kwa mtaa wa Kimara wenye makanisa mawili, yaani Kimara na King'ongo.
Mgeni rasmi atakuwa ni Mwenyekiti wa Konferensi ya Mashariki Kati mwa Tanzania wa kanisa la Waadventista Wa Sabato (ECT) Mchungaji Joseph Mngwabi na leo ataweka jiwe la msingi la Kanisa la King'ongo.
Programu hizi zinaambatana na ugawaji wa vitabu vya Tumaini Kuu na Afya na Uzima.
Mahali: Viwanja vya Kanisa la Kimara King'ongo Dar Es Salaam
*****NYOTE MNAKARIBIHSWA****

WAIMBAJI WA FAMILY MUSIC WAMEKUSOGEZEA SINGLE YAO YA HIVI KARIBUNI, "SIFA ZAKO NITAIMBA"

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0768441610***

CHILDREN'S PRAYER BREAKFAS.

CHILDREN'S PRAYER BREAKFAS.

RORYAMAENDELEO 

 Hili ni tukio linalofanyika kwa mara ya pili hapa Mwenge Kanisani ikiwa ni mojawapo ya matakwa ya Idara ya Watoto. Tukio hili huandamana na kujifunza umuhimu wa maombi kwa watoto na vipindi vya kutosha vya kuomba pamoja kuimba na ushuhuda. Tukio hili lililoanza saa 12 alfajiri na kuhitimishwa saa 4 asubuhi, mara hii limesimamiwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo wa Konferensi (ETC) Bi Devotha Shimbe. Tukio hili lilihitimishwa na kushiriki kifungua kinywa cha pamoja. Hapa chini ni baadhi ya picha za tukio hilo.
Na Stephen Letta









TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MKATABA WA LUGUMI

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MKATABA WA LUGUMI

download (3)Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 Aprili, 2016 ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System).
Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo la kupotosha umma kutokana na kile kilicho amuliwa na kamati hiyo. Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 Aprili, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi la Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine ilibaini dosari katika utekelezaji wa mkataba huo.
Kutokana na dosari hizo, kamati iliomba Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.
Aidha, Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 12 Aprili, 2016 kuwasiilsha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprili 2016 kabla ya tarehe 18 Aprili, 2018 kama ilivyoshauriwa na kamati . Hivyo ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016. Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM 15 Aprili, 2016.

Wazee wa Zanzibar waanza kupokea Pensheni

Wazee wa Zanzibar waanza kupokea Pensheni

pe1
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na watu wenye ulemavu wa Tanzania Bara Dk. Abdallah Possi  alipofika katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
pe3
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na watoto Moudline Castico akielezea mikakati yao yakuwasaidia wazee katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa Wazee wa Zanzibar (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed.
pe4
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni ya Sh/= elfu 20 Mzee. Kombo Moh’d Kombo itakayokuwa ikitolewa kila mwezi, katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
pe5
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni Bi. Erestina Filex katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa leo April 15/2016.
pe6
Baadhi ya Wazee waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
………………………………………………………………………………………………………………
Na Miza Kona, Majda  Kasim -Maelezo Zanzibar.
Wazee 21,750 wameanza kunufaika na mpango wa serikali wa utoaji fedha za kujikimu yaani pensheni kwa wazee wote wanaoanzia umri wa miaka 70 ili kuimarisha maisha yao.
Wazee 13,150 ni kutoka Unguja na 8,600 wanatoka Pemba, katika mpango huo, kila mzee atapewa shilingi elfu ishirini kila mwisho wa mwezi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, katibu mkuu wizara ya uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto Asha Ali Abdallah, amesema hatua hiyo ni muhimu kwani nchi nyingi duniani zinao utaratibu kama huo.
Amesema, mbali ya kuwa kufanya hivyo ni wajibu, lakini kunahitaji maamuzi ya kijasiri na utashi wa kisiasa, ambapo serikali ya Zanzibar imeweza kuonesha dhamira yake kuimarisha maisha ya wazee.
Amesema msingi wa pensheni kwa wazee wote wa Zanzibar, ni sera ya hifadhi ya jamii iliyopitishwa mwaka 2014, ukiwa mpango mkuu wa taifa wa dira ya 2020 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umasikini nchini.
sambamba na hilo alisema kuwa wataendelea kuwa na jukumu kubwa katika kuwasajili wazee wapya watakaokuwa wanaingia katika mpango huo.
Waziri wa fedha Dk Khalid Salum Mohammed, alisema kuwa ili serikali iweze kupata maendeleo ni lazima wafanyakazi na wananchi kuwa wawajibikaji katika utendaji wa kazi zao.
Alisema katika kutekeleza mpango huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu na waaminifu ili kuhakikisha wazee wanaostahi wanapata pencheni zao kama inavyopaswa.
“hali halisi na uzoefu unaonesha kuwa kumekuwa na tabia za udanganyifu na wizi katika masuala mengi yanayohusiana na malipo….lakini nachukua nafasii hii kuwatanabahisha watendaji wote watakaohusika na utekelezaji wa mpango huu katika ngazi zote yoyote atakaebanika kufanya udanganyifu hatua kali zinatuchukuliwa dhidi yake”alisema.
Aidha aliwataka watendaji wa mpango huo kuwa na hekima,busara,uvumilivu,upole na huruma ni lazima zichukue nafasi yake katika kuwahudumia wazee.
Nae waziri wa Kazi,uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Moudline Castico ameahidi kwamba mpango huo utasimamiwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha wazee wote wanaostahiki wanapatiwa fedha zao kwa wakati na hakutakuwa na udanganyifu na upotevu wa fedha za serikali.
Mpango huo unatarajiwa kutumia shilingi miioni 435 kwa mwezi ambapo ni sawa na shilingi bilioni 5.220 kwa mwaka.
Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza Afrika mashariki kuanzisha mpango huo, nay a sita kwa Afrika baada ya Mauritius, Afrika Kusini, Lesotho, Namibia na Botswana.