Jumapili baada ya semina kuisha kukawa na bonanza kubwa lilofanyika katika viwanza vya Shule ya Msingi Mavurunza Kimara Dar Es Salaam,bonanza hili lilihusisha michezo kama vile,kukimbia mbio za mita 100,mbio za kupokezana vijiti na kukimbiza kuku.
Zikianza mbio kwa namna hii hapo inahesabiwa moja,mbili,tatu jiandae ...kimbia |
Inahitaji nguvu,jitahada na ubunifu na kwa mbio hizi za wanaume wa zaidi ya miaka 30 wakikimbia mbio moja kati ya michezo iliyoleta furaha na hamasa siku ya jana. |
Watoto nao hawakupenda kuachwa mbali,wako makini wasipitwe na mbio hizi zenye umbali wa mita 100 katika viwanja vya Mavurunza. |
Wakina mama ni jeshi kubwa..hapa ni maandalizi ya mbio yakianza na wakisubiri mwamuzi wa mchezo ambaye ni mchungaji wa mtaa wa Kimara Rahisi Mande atoe ruksa na kufungilia mbio hizo. |
Hili ni kundi la kwanza kwa mchezo wa kupokezana vijiti na hapa wakienda mbio kuwapa wenzao kundi namba mbili wakiwa mbele kabisa na katika mchezo huo Mzee Joshua Manyama ndiye aliibuka mshindi. |
Mzee Manyama akiitimisha mbio hizi akiwa mbele kabisa kuwashinda wenzake na kushika nafasi ya kwanza kwa mchezo kwa kukimbia na kijiti hapo jana. |
Mzee Ronard Manongi akikikimbia na kijiti katika uwanja wa Mavurunza ambapo Mzee Joshua Manyama ndiye alishinda mchezo huo. |
Hapa ni Mama Mchungaji(kushoto) mwenye jezi ya blu anayefuata ni Diana Manyama,Asnati Ngakonda na mwisho ni Naetwe Manongi wakikimbiza kuku katika shindano la kukimbiza kuku lililofanyika jana. |
Kulia ni Diana Manyama akifurahi mara baada ya kushinda katika shindano ya kuku hapo jana kushoto ni Asnati Ngakonda akimpongeza na kulia ni mtoto akishuhudia. |
Furaha na bashasha zilitawala mara baada ya ushindi na Mama Diana Manyama akielekea kuhojiwa na mtangazji juu ya ushindi wake. |
Vuta nikuvute,hapa anatafutwa mashindi katika mchezo wa kuvuta kamba,na timu upande wa kulia walishinda. |
No comments:
Post a Comment