Wazee wa Zanzibar waanza kupokea Pensheni
Waziri wa Fedha na Mipango
Zanzibar Khalid Salim Mohammed akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na watu wenye ulemavu wa
Tanzania Bara Dk. Abdallah Possi alipofika katika uzinduzi wa mpango wa
pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya
Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,
Wazee, Vijana, Wanawake na watoto Moudline Castico akielezea mikakati
yao yakuwasaidia wazee katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni
kwa Wazee wa Zanzibar (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid
Salim Mohammed.
Waziri wa Fedha na Mipango
Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni ya Sh/= elfu 20
Mzee. Kombo Moh’d Kombo itakayokuwa ikitolewa kila mwezi, katika
uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli
ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango
Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni Bi. Erestina Filex
katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar
uliozinduliwa leo April 15/2016.
Baadhi ya Wazee waliofika kwenye
hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar
uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
………………………………………………………………………………………………………………
Na Miza Kona, Majda Kasim -Maelezo Zanzibar.
Wazee 21,750 wameanza kunufaika
na mpango wa serikali wa utoaji fedha za kujikimu yaani pensheni kwa
wazee wote wanaoanzia umri wa miaka 70 ili kuimarisha maisha yao.
Wazee 13,150 ni kutoka Unguja na
8,600 wanatoka Pemba, katika mpango huo, kila mzee atapewa shilingi elfu
ishirini kila mwisho wa mwezi.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa mpango huo, katibu mkuu wizara ya uwezeshaji, wazee, vijana,
wanawake na watoto Asha Ali Abdallah, amesema hatua hiyo ni muhimu
kwani nchi nyingi duniani zinao utaratibu kama huo.
Amesema, mbali ya kuwa kufanya
hivyo ni wajibu, lakini kunahitaji maamuzi ya kijasiri na utashi wa
kisiasa, ambapo serikali ya Zanzibar imeweza kuonesha dhamira yake
kuimarisha maisha ya wazee.
Amesema msingi wa pensheni kwa
wazee wote wa Zanzibar, ni sera ya hifadhi ya jamii iliyopitishwa mwaka
2014, ukiwa mpango mkuu wa taifa wa dira ya 2020 unaolenga kukuza uchumi
na kupunguza umasikini nchini.
sambamba na hilo alisema kuwa
wataendelea kuwa na jukumu kubwa katika kuwasajili wazee wapya
watakaokuwa wanaingia katika mpango huo.
Waziri wa fedha Dk Khalid Salum
Mohammed, alisema kuwa ili serikali iweze kupata maendeleo ni lazima
wafanyakazi na wananchi kuwa wawajibikaji katika utendaji wa kazi zao.
Alisema katika kutekeleza mpango
huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu na waaminifu ili kuhakikisha
wazee wanaostahi wanapata pencheni zao kama inavyopaswa.
“hali halisi na uzoefu unaonesha
kuwa kumekuwa na tabia za udanganyifu na wizi katika masuala mengi
yanayohusiana na malipo….lakini nachukua nafasii hii kuwatanabahisha
watendaji wote watakaohusika na utekelezaji wa mpango huu katika ngazi
zote yoyote atakaebanika kufanya udanganyifu hatua kali zinatuchukuliwa
dhidi yake”alisema.
Aidha aliwataka watendaji wa
mpango huo kuwa na hekima,busara,uvumilivu,upole na huruma ni lazima
zichukue nafasi yake katika kuwahudumia wazee.
Nae waziri wa
Kazi,uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Moudline Castico
ameahidi kwamba mpango huo utasimamiwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha
wazee wote wanaostahiki wanapatiwa fedha zao kwa wakati na hakutakuwa na
udanganyifu na upotevu wa fedha za serikali.
Mpango huo unatarajiwa kutumia shilingi miioni 435 kwa mwezi ambapo ni sawa na shilingi bilioni 5.220 kwa mwaka.
Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza
Afrika mashariki kuanzisha mpango huo, nay a sita kwa Afrika baada ya
Mauritius, Afrika Kusini, Lesotho, Namibia na Botswana.
No comments:
Post a Comment