Habari wakuu,
Leo tunaendelea na bunge ambalo baadae litasitishwa na
Waziri Mkuu na kuhutubiwa na Rais wa Jamhuri majira ya
saa tisa mchana. Aliyekalia kiti ni spika wa bunge, mama
Anna Makinda akiendesha kipindi cha maswali na majibu.
Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri katika mojawapo ya siku
muhimu katika uhai wa miaka mitano wa bunge letu.
=======
Kwa sasa kamati ya bunge zima imekaa ili kupitisha
Muswada wa Sheria ya Tume ya Walimu wa Mwaka 2015
(The Teachers Service Commission Bill, 2015).
Kigwangala: Akidi haijatimia hivyo maamuzi ya kutunga hii
sheria yatakuwa batili na yanaweza yakapingwa kwenye
mamlaka nyingine hivyo naomba kikao hiki kiahirishwe
mpaka akidi itakapotimia.
Makinda: Tukifika kwenye kamati ya maamuzi ndio tutajua
Kamati ya bunge zima imemaliza kazi yake na bunge
linarejea
Makinda: Dr Kigwangala aliposimulia habari yake
hakuomba hoja ndio maana mimi nikaendelea na shughuli
zangu.
Kingwangala: Si kweli nimefata taratibu na bahati nzuri hii
imeandikwa Kiswahili na hata ingekua kiingereza
ningeelewa, lakini hapa nimesimama kwa ajili ya hoja
nyingine ya kusimamisha shughuli zote za bunge
zilizopangwa kwenye ratiba ya leo zisitishwe mpaka wakati
mwingine bunge litaona inafaa, naomba kutoa hoja.
Makinda: Hii sio hoja ya ratiba, haipo, hapa ni hoja ya
muswada na sasa ni matangazo. Naomba nisitishe
shughuli za bunge kwa muda wa nusu saa tutarudi tena.
========
Bunge limerejea na kwa sasa anaeongea nia waziri mkuu
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Pinda: Anaongelea bajeti na anasema kilichobaki ni
utekelezaji wake, anaongelea matukio ya vifo katika kikao
hiki cha bunge, kifo cha Mwaiposa mbunge wa Ukonga na
Donald Max mbunge wa Geita mjini pia kifo cha sheikh
mkuu wa Tanzania.
Muswada iliyopitishwa 2015: Muswada wa kuidhinisha
matumizi, one border stop bill, muswada wa benki ya
posta, muswada wa sheria wa masoko ya bidhaa 2015,
mswada wa sheria wa kuwalinda watoa taarifa, muswada
wa sheria ya petroli, mapato ya mafuta na gesi, uwazi na
uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji, marekebisho ya ajira
na kazi pia muswada wa tume ya walimu.
Kuna wabunge walitaka muswada wa mafuta na gesi
usijadiliwe, nakupongeza spika kwa busara zako.
Nawapongeza wabunge kwa kupitisha bajeti ya serikali kwa
kura nyingi za ndio takriban asilimia 85. Viaumbele vya
bajeti ni kugharamia shughuli za uchaguzi, pili kuweka
msukumo katika miradi inayoendelea, tatu kuweka
msukumo maalamu katika miradi ya kusambaza umeme na
maji vijijini.
Katika kipindi hiki cha 2010-15 na hasa hivi karibuni Rais
ameridhia kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na
wilaya za Tanganyika, Ubungo, Kigamboni, Songwe, Kibiti
na Malinyi. Halmashauri za wilaya ni 25 zikiwemo
Buchosha, Malinyi, Madaba, Manyoni Mpimbwe, Msimbo,
Mlele, Kakonko, Kyerwa, Uvinza, Chemba, Nyang'alwe
Busega, Itilima na Ikungi.
Halmashauri za manispaa ni pamoja na Chalinze, Ifakara,
Newala, Mbulu, Mbinga, Nzega Geita Kasulu Ilemela na
Kahama pia tarafa tano.
Waziri mkuu amemaliza na kwa sasa ni Jenista Mhagama
anaongelea baadhi ya kanuni zinatenguliwa ili kuruhusu
wageni ambao kanuni zilikuwa haziruhusu walioalikwa na
mheshimiwa spika ili kuketi ndani ya ukumbi wa bunge na
si sehemu waliyotengewa wageni. Makamu wa Rais, Rais
wa Zanzibar, Jaji mkuu na waheshimiwa majaji wote
atakaombata nao kwa ajili ya kusikiliza hotuba ya rais na
hoja imeungwa mkono.
Sasa ni hoja ya kuahirisha bunge mpaka litapoitwa tena na
hoja imepitishwa kwa kura nyingi za ndio. Kikao cha bunge
kimeahirishwa mpaka saa tisa mchana.
====
Bunge limerejea. Ratiba inaonyesha Mhe. Rais atahutubia
Bunge. Kwa sasa ameshawasili viwanja vya Bunge na
linapigwa Gwaride la kumpokea.
Viongozi mbalimbali wameshawasili, wakiwemo Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk Shein, Makamu wa Rais, Dk
Ghalib Bilal na viongozi wengine. Hawa wataingia kwa
mtindo wa msafara kuelekea ndani ya ukumbi wa Bunge..
Na sasa ni msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk Shein akiwa
ameambatana na Ally Zungu na makatibu wengine
wabunge kuelekea pahala pa kukaa.
Msafara unaofuata sasa ni wa makamu wa Rais akiwa
anaongozana na Mhe Job Ndugai, naibu Spika wa Bunge la
JMT pamoja na wapambe wa Bunge.
Ni zamu ya Mhe Rais, ambapo anasindikizwa na Mhe.
Spika, Mpambe wa Bunge na Makatibu wake wanaingia
sasa ukumbini kwa mtindo wa msafara, tayari kwa kuianza
shughuli hii.
Ukumbi wa Bunge unalipuka kwa shangwe huku wabunge
wengi wakisikika wakiimba 'CCM, CCM, CCM'..
Spika wa Bunge amesimama sasa na kutoa ukaribisho kwa
Mhe Rais.
Rais anaanza kuzungumza sasa;
JK: Mhe Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Hatimaye siku ya
kulivunja Bunge imewadia. Nakushukuru sana kwa
kunipatia nafasi ya kulihutubia bunge ili kutimiza wajibu
wangu huo wa kikatibu. Lakini shukrani yangu kubwa ni
kwako kwa kuliongoza bunge hili kwa uhodari mkubwa.
Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari. Wewe
ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu
kabisa katika muhimili huu wa kutunga sheria. Na
umethibitisha ya kuwa 'Wanawake wakipewa, wanaweza'.
Niwashukuru wabunge kwa kushiriki vema shughuli za
bunge na mmelitendea haki na kuliletea heshima na hadhi.
Nilipofungua Bunge la tisa, nilisema; 'Tutatelekeza wajibu
wetu kwa Ari mpya. Nguvu mpya na Kasi mpya'.
Thursday, July 9, 2015
Rais kuhutubia bungeni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment