JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA
UTUMISHI WA UMMA
TANGAZO LA KAZI YA MUDA
WAKUSANYA TAARIFA ZA TATHMINI YA KAZI –
(NAFASI 50)
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa
Umma ambayo imeanzishwa kwa Hati Maalum
iliyotolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 162 la tarehe
3 Juni, 2011. Majukumu ya Bodi ni kufanya mapitio
ya mara kwa mara ya viwango vya mishahara, posho
na mafao mengine na kumshauri Rais juu ya misingi
ya miundo ya mishahara katika utumishi wa umma.
Katika mwaka wa fedha 2015/16, Bodi inatarajia
kufanya Tathmini ya Kazi katika Utumishi wa Umma
kwa lengo la kuoanisha na kuwianisha mishahara.
Bodi inahitaji watumishi 50 watakaomsaidia Mtaalam
Mwelekezi kukusanya taarifa za awali:
a) Sifa za mwombaji
i) Mtumishi wa Umma;
ii) Elimu ni kuanzia shahada ya kwanza au
stashahada ya juu na kuendelea;
iii) Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha kwa Kiswahili na
Kiingereza;
iv) Mwenye maadili, uwezo wa kufanya kazi
inayozingatia matokeo, kujituma na kukamilisha
malengo kwa wakati; na
v) Uelewa wa kutumia kompyuta.
b) Kazi za kufanya
i) Kuwahoji watumishi wa Umma na kujaza dodoso
la kukusanyia taarifa;
ii) Kuingiza taarifa za madodoso kwenye mfumo wa
kompyuta; na
iii) Kazi nyingine zinazohusiana na Tathmini ya Kazi
kwa maelekezo ya msimamizi.
c) Mshahara
Waombaji watakaofanikiwa, kwa kuwa ni watumishi
wa umma, wataendelea kulipwa mishahara yao kama
ilivyo sasa. Aidha, Bodi itagharamia mafunzo na
posho za safari za kikazi kwa viwango vya Serikali.
d) Muda wa Kazi
Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa jumla ya miezi 15.
Hata hivyo, kazi ya mtumishi mmoja mmoja haitazidi
siku 100.
e) Namna ya kuwasilisha maombi.
i) Maombi yote yaambatanishwe na Maelezo binafsi
(CV), nakala za vyeti vya elimu ya juu na mafunzo ya
kompyuta;
ii) Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao
kwa kupitia anwani ya: es@psrb.go.tz ; na
iii) Maombi yote yapitishwe na waajiri wenyewe.
f) Mwisho wa kupokea maombi
Zoezi la kupokea maombi litafungwa tarehe
31/07/2015.
Tanbihi: Watumishi wanaofanyakazi katika Mamlaka
za Serikali za Mtaa wanahimizwa kuleta maombi yao.
IMETOLEWA NA KATIBU MTENDAJI
BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA
UTUMISHI WA
UMMA
Saturday, July 11, 2015
TANGAZO LA KAZI YA MUDA (BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA) MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAR 31/07/2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment