Magufuli, Balozi Amina, Migiro wapenya
tatu bora
Details
Published on Sunday, 12 July 2015 00:30
Written by roryamaendeleo , Dodoma
Hits: 1162
WAJUMBE
wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM waliokutana
jana mjini hapa, walipigia kura majina matano ya
wawania urais kupitia chama hicho, ambapo Dk John
Magufuli, aliongoza na kufuatiwa na Balozi Amina Salum
Ali na Dk Asha-Rose Migiro.
Kwa matokeo hayo, viongozi hao walipelekwa katika
Mkutano Mkuu wa CCM kupigiwa kura na wajumbe wa
mkutano huo, ili kumpata mgombea urais wa chama
hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC,
Nape Nnauye, wagombea wengine walioshindwa katika
kura hizo, January Makamba na Bernard Membe,
waliridhia matokeo hayo.
Dk John Magufuli
Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 Chato (sasa Mkoa
wa Geita). Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 –
2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994 alisoma Shahada ya Uzamili
(Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988 alisoma Shahada ya Kwanza ya
Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua
masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982: alisoma diploma Chuo cha
Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981 alipata elimu ya juu ya sekondari
katika Shule ya Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978 alisoma elimu ya sekondari katika
Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. Mwaka 1975 – 1977
alisema Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani
Kagera. Mwaka 1967 – 1974 alisoma Shule ya Msingi,
Chato.
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni,
Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora,
Dodoma. Uzoefu wa kazi, siasa Mwaka 2010 – hadi
sasa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato. Mwaka
2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Samaki; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo
Mashariki (Chato). Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa
Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na
Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1989 – 1995:
Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative
Union (Ltd.) Mwanza.
Dk Asha-Rose Migiro
Dk Asha Rose Migiro alizaliwa Julai 9, 1956 katika
Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Migiro alianza
masomo katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es
Salaam mwaka 1963 hadi mwaka 1966.Akahamia shule
ya Msingi Korogwe, Tanga na kuendelea na elimu ya
msingi mwaka 1967–1969.
Baadaye akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne
katika Shule ya Sekondari Weruweru mkoani Kilimanjaro
mwaka 1970 mpaka 1973 na kidato cha tano na sita
katika Shule ya Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975.
Migiro alikuwa mmoja wa wasichana waliofaulu vizuri
Korogwe Sekondari na alipojiunga Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) mwaka 1977, alichukua Shahada ya
Kwanza ya Sheria (LLB) mwaka 1980.
Baada ya kukamilisha Shahada ya Kwanza, aliajiriwa
UDSM kusaidia kufundisha masomo ya sheria katika
nafasi ya Mhadhiri Msaidizi. Alifanya kazi hiyo kwa miaka
miwili, kabla ya kuendelea tena na masomo ya juu ya
sheria mwaka 1982–1984, alipohitimu Shahada ya
Uzamili ya Sheria (LLM).
Kati ya mwaka 1985–1988, aliendelea kufundisha
UDSM, ambapo mwaka 1988, alikwenda Chuo Kikuu cha
Konstanz, Ujerumani kusoma Shahada ya Uzamivu
(PHD) katika masuala ya sheria na kuhitimu mwaka
1992.
Dk Migiro alirejea Tanzania akiwa Mhadhiri Mwandamizi
na aliendelea kufundisha katika Kitivo cha Sheria cha
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo kati ya mwaka
1992 – 1994, alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Katiba
na Utawala na kati ya mwaka 1994 – 1997 aliongoza
Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai. Mwaka 2000, Dk
Migiro aliingia rasmi katika siasa.
Anaongea vizuri lugha nne za kimataifa, ikiwemo
Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani na ni mke
wa Profesa Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa
kike.
Ubunge, Uwaziri
Tofauti na wanasiasa wengi ambao hufikia ngazi za juu
za uongozi wa nchi kuanzia siasa katika nyadhifa za
vyama vyao, Dk Migiro amekuwa na historia tofauti
kidogo.
Yeye ameanza siasa za kujijenga akitokea katika
taaluma, akitazamwa na watu wengine kuwa ana uwezo
wa kulisaidia Taifa.
Mwaka 2000 aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa
Mbunge na baadaye akateuliwa kuwa Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005,
alimteua Dk Migiro kuwa Mbunge tena na Waziri wa
Mambo ya Nje, Januari 2006 na kuwa mwanamke wa
kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo.
Naibu Katibu Mkuu UN
Ilipotimu Januari 5, 2007, aliweka rekodi nyingine kubwa
kimataifa; alipoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN), Ban Ki-moon, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa
UN, akiwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo,
baada ya Louise Fréchette, Mwanadiplomasia wa
Canada.
Balozi Amina Salum
Ali Mwanadiplomasia Amina Salum Ali, alihitimu Chuo
Kikuu cha New Delhi , India - Shahada ya Uchumi (B.A),
mwaka 1979, pia alisomea masuala ya utawala wa fedha
na utafiti wa uendeshaji kwenye Taasisi ya Uongozi
(Institute of Management) Pune, India mwaka 1980.
Mwaka 1981 alihitimu Shahada ya Uzamili ya Masoko
katika Chuo Kikuu cha Pune, India - (Symbiosis College
of Management) na mwaka 1983 alijiunga na Chuo
Kikuu cha Helsinki, Finland, Kuchukua Diploma ya Utafiti
wa Masoko na Uuzaji wa Bidhaa za Nje.
Nyadhifa alizoshika Mwaka 1981 hadi 1982, Mchumi
Mwandamizi -Tume ya Mipango Zanzibar, mwaka 1982
hadi 1983, Mkurugenzi Biashara za Nje - Wizara ya
Biashara ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mwaka
1983 hadi 984, Katibu Bodi ya Biashara Zanzibar- Wizara
ya Biashara Zanzibar.
Nafasi nyingine ni, mwaka 1984 hadi 1985, Mchumi
Mwandamizi - Tume ya Mipango, Wizara ya Nchi Ofisi ya
Rais Zanzibar, mwaka 1985 hadi 1990- Mbunge Bunge
la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, mwaka 1985 hadi
1986- Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1986 hadi
1989- Waziri wa Nchi ,Wizara ya Mambo ya Nje.
Pia, mwaka 1989 hadi 1990- Waziri wa Fedha, Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1990
hadi 2000 – Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano Tanzania, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar, mwaka 2001 hadi 2005.
Amewahi pia kuwa Waziri wa Fedha, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar , Mjumbe wa Tume ya Mipango,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mwaka 2005 hadi 2006-
Mjumbe Baraza la Wawakilishi. Nyingine ni, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, mwaka 2006 - Mwakilishi wa Kudumu wa AU
kwenye Umoja wa Mataifa.
Saturday, July 11, 2015
Sifa za Magufuli, Migiro na Amina
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment