Arsenal 2 - 1 Leicester
- Saa moja iliyopita
Danni Welbeck ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu Aprili mwaka uliopita ameifungia Arsenal bao la pili na la ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester.
Welbeck alimhakikishia Wenger ushindi huo muhimu uliotamatisha msururu wa mechi 16 bila kushindwa wa kocha Claudio Ranieri.
Mchezaji mwengine wa akiba Theo Walcot ndiye aliyekuwa ameisawazishia Arsenal kunako dakika ya 70 ya kipindi cha pili.
Wageni hao ambao wamewatamausha wengi msimu huu kwa kufungua pengo la alama 4 kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya Uingereza walikuwa wamefunga bao la kwanza kupitia kwa mkwaju wa penalti.
Bao hilo lilitiwa kimiani na Jamie Vardy kunako dakika ya 45''.
Mpira umeisha.
GOOOOOOOL
90'Arsenal 2-1 Leicester
Danni Welbeck anaifungia Arsenal bao la pili
90'Arsenal 1-1 Leicester
Dakika nne za ziada zimeongezwa.
89' Aaron Ramsey (Arsenal) naye anapoteza nafasi nzuri baada ya kupiga nje pasi ya Alexis Sanchez
Olivier Giroud (Arsenal) anagonga pasi hafifu kipa wa Leicester anaudaka bila wasiwasi
87'Arsenal 1-1 Leicester
Per Mertesacker (Arsenal) anakosa nafasi nzuri mkwaju wa kichwa unatoka nje
85'Arsenal 1-1 Leicester
Alex Oxlade-Chamberlain anaondoka Danny Welbeck anaingia
Kocha Arsene wenge anamrejesha Danny Welbeck kwa mara ya kwanza tangu mwaka jana alipojeruhiwa
80'Arsenal 1-1 Leicester
77' N'Golo Kanté (Leicester City) anajaribu kutesa mabeki wa Arsenal lakini bila mafanikio
80' Aaron Ramsey (Arsenal) anafyatua kombora lakini wapi
76' Alexis Sánchez (Arsenal) anakosa mkwaju mzuri kutoka kwa Ozil
75'Arsenal 1-1 Leicester
Foul kuelekea lango la Leicester
Aaron Ramsey (Arsenal).
70' Arsenal 1-1 Leicester
GOOOOOOOOL
Theo Walcot anaisawazishia Arsenal
68' Arsenal 0-1 Leicester
Alexis Sánchez (Arsenal) anaongoza mashambulizi mbele ya lango la Leicester lakini wapi.
Mesut Özil naye anasaidia kufyatua makombora lakini safu ya ulinzi ya Leicester imeimarishwa Marcin Wasilewski
65' Arsenal 0-1 Leicester
Theo walcott anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya Francis Coquelin.
Danny Simpson aoneshwa kadi Nyekundu dakika mbili tu baada ya kurambishwa kadi ya njano ya kumchezea visivyo Olivier Giroud
51' Arsenal wanashambulia lango la Leicester
Olivier Giroud anagonga nje mpira wa kichwa
50' Arsenal 0-1 Leicester
Refarii Martin Atkinson anamuonesha Danny Simpson (Leicester City) kadi ya njano kwa kumwangusha Alexis Sanchez
47' Arsenal 0-1 Leicester
Mesut Özil (Arsenal) anashambulia lakini wapi.
Olivier Giroud amekosa makali mbele ya lango inakuwa ni Golkick.
46' Kipindi cha pili kimeanza .
Jamie Vardy aifungia Leicester bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti.
Na kipindi cha kwanza kimekamilika Foxes ama vijana wa Claudio Ranieri wanaenda mapumzikoni wakiongoza kwa bao muhimu dhidi ya washika bunduki wa Arsenal uwanjani Emirati.
Penalti
45 Arsenal 0-1 Leicester
Gooooooool!
Arsenal 0, Leicester City 1. Jamie Vardy (Leicester City)
Nacho Monreal (Arsenal)anaoneshwa kadi ya njano.
Arsenal waadhibiwa kwa penalti
39' Arsenal 0-0 Leicester
Francis Coquelin (Arsenal) anaoneshwa kadi ya njano kwa kucheza visivyo.
35' Arsenal 0-0 Leicester
Ikiwa matokeo yatasalia hivi hivi Arsenal ambao wamecheza mechi 26 wataipiku Tottenham hadi nafasi ya pili wakiwa na akama 49.
Itakumbukwa kuwa Tottenham wanamechi ngumu ya kukata na shoka dhidi ya Manchester City
Kona kuelekea lango la Leicester
32' Arsenal 0-0 Leicester
LOOOOOOOOO
Olivier Giroud anafunga bao lakini refarii anakataa anasema ameotea
26' Olivier Giroud (Arsenal) anakosa pasi safi kutoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain
26' Freekick
Riyad Mahrez (Leicester City)
25' Arsenal 0-0 Leicester
Kona ya , Arsenal.
Wes Morgan ameutoa nje mpira .
19'Offside Arsenal.
Olivier Giroud anachonga pasi muruwa lakini Mesut Özil ameotea
15' Je ameunawa ?
Alexis Sánchez (Arsenal) anadai Handbol lakini refarii anapuzilia mbali.
00:14 Arsenal 0-0 Leicester
Shinji Okazaki anapoteza nafasi pia katika lango la Arsenal akiwa amesalia na kipa Peter Cech
LOOOOO
Olivier Giroud (Arsenal) anapoteza nafasi ya wazi akiwa amesalia na kipa pekee yake.
00:12 Kona- Arsenal. Danny Simpson ameutoa nje.
00:08' Olivier Giroud (Arsenal) anacheza visivyo.
00:07 Arsenal 0-0 Leicester
Udhibiti wa mpira
Arsenal 72 %-28 %Leicester4. Riyad Mahrez ameifungia Leicester mabao 14 na kusaidia katika mabao mengine 10.
Yeye ndiye mchezaji wa kwanza kutimiza zaidi ya mabao kumi msimu huu.
00:03
Sanchez anakosa mkwaju wa kichwa na inakuwa ni Golkick kuelekea lango la Arsenal. LAAAAAAAAAKona kuelekea lango la LeicesterArsenal 0-0 Leicester (3:00 EAT) 00:01Mpira umeanza kwa kasi kubwa Arsenal wanafanya mashambulizi katika lango la Leicester Wachezaji wameingia uwanjani3.Iwapo Leicester watainyuka Arsenal watafungua pengo la alama 7 na itakuwa vigumu kwa timu yeyote kuwapokonya taji msimu huu. #Arslei
Mlinzi Per Mertesacker na kiungo Francis Coquelin wanarejea kikosini .
Danny Welbeck anarejea baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu mno takriban mwaka mmoja.Mara ya mwisho alipocheza ilikuwa ni Aprili 2015.Hii itakuwa mechi ya 100 kwa mchezaji Alex Ox-Chamberlain @Alex_OxChamboArsene Wenger amefanya mabadiliko mawili katika kikosi chakeArsenal v Leicester (3:00 EAT)Timu ya Arsenal : Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez, Giroud.
Leicester haijafanya mabadiliko yeyote kutoka kwa kile kikosi kilichoilaza Manchester City juma lililopita.
2.Kocha wa Leicester Claudio Ranieri amekihifadhi kikosi kilekile kwa mechi 6 sasa.
Je Kocha Arsene Wenger atakuwa kocha wa kwanza kuwazima Leicester ugeninini ?
- Leicester hawajapoteza hata mechi moja katika 16 walizocheza ugenini.
Mechi zitakazochezwa leo Jumapili baina ya timu 4 za kwanza zitaamua mwelekeo halisi wa ligi hii yenye wapenzi wengi duniani, Ligi Kuu ya Uingereza.
Arsenal itamenyana na Leicester City ambayo bado inaongoza ligi ikiizidi Arsenal alama 5.
Ushindi wa the Gunners utapunguza pengo baina yake na Leicester na kuipa matumaini zaidi ya kuendelea kupigana hadi mwisho.
Nayo Manchester City yenye nafasi ya 4 itaialika Tottenham iliyo kwenye nafasi ya pili.
Jumapili tarehe 14 Februari- Arsenal v Leicester 15:00
- Aston Villa v Liverpool 17:05
- Man City v Tottenham 19:15
No comments:
Post a Comment