Sunday, February 14, 2016

Raia Uganda kushiriki uchaguzi mkuu

Raia Uganda kushiriki uchaguzi mkuu

  • 11 Februari 2016
Uchaguzi
Image captionWapiga kura 15 milioni wanatarajiwa kushiriki
Wapiga kura nchini Uganda watashiriki kwenye uchaguzi mkuu 18 Februari, ambao ndio wa tatu tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi 2005.
Watachagua rais, wabunge na viongozi wa serikali za mitaa.
Rais Yoweri Museveni, aliyeongoza taifa hilo kwa miaka 30, anawania kuongoza kwa muhula wa tano, akikabiliana na wagombea wengine saba.
Kuna wapiga kura 15 milioni ambao wanatarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.
MuseveniImage copyrightAP
Image captionMuseveni ameongoza Uganda kwa miaka 30
Rais Museveni amekuwa uongozini tangu kuchukua uongozi kupitia vita 1986. Ana umri wa miaka 71 na ni mmoja wa viongozi walioongoza muda mrefu barani Afrika.
Alitarajiwa kumaliza kuhudumu muhula wake wa mwisho 2006 lakini mwaka 2005 katiba ilibadilishwa na kuondoa mipaka kwenye muhula wa rais.
Bw Museveni amekabiliwa na shutuma kutoka nchi za Magharibi zinazomtuhumu kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu. Ameyajibu mataifa hayo kwa kusema yanaingilia masuala ya ndani ya Uganda.
Kizza Besigye, ambaye wakati mmoja alikuwa rafiki mkuu wa Bw Museveni, amekabiliana naye uchaguzini mara tatu akitumia chama cha Forum for Democratic Change (FDC) bila kufanikiwa.
Amama Mbabazi pia alikuwa rafiki wa karibu wa Rais Museveni kabla yake kutangaza kwamba angewania urais.
Alihudumu kama waziri mkuu wa Uganda 2011-2014. Anawania kama mgombea huru kupitia vuguvugu la Go Forward.
Besigye
Image captionMbabazi (kushoto) na Besigye walikuwa wakati mmoja marafiki wakuu wa Museveni
Kuna wagombea wengine wanne ingawa hawatarajiwi kutoa ushindani mkubwa kwenye uchaguzi huo.
Nchini Uganda, rais huchaguliwa kuongoza kwa muhula wa miaka mitano.
Mgombea huhitajika kupata kura moja juu ya 50% ya kura zilizopigwa ndipo atangazwe mshindi la sivyo kufanyike duru ya pili cha uchaguzi kati ya aliyeongoza na mgombea wa pili katika kipindi cha siku 30.
Bunge la nchi hiyo lina vitu 418, kufuatia kuundwa kwa maeneo bunge 43 mapya 2015.
Masuala ambayo yamekuwa yakitawala kampeni ni ukosefu wa ajira, ufisadi na ubora wa huduma za serikali.
Wagombea watatu wakuu wameahidi kuimarisha miundo mbinu, kukabiliana na ufisadi, kubuni nafasi za kazi na kuboresha huduma bora ya afya miongoni mwa ahadi nyingine.
Suala ya mafuta pia limeangaziwa kwenye mikutano ya kampeni. Taifa hilo liligundua mafuta mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment