Wakuu wa shule za msingi 10 wavuliwa madaraka na mkuu wa wilaya
MKUU wa wilaya ya URAMBO mkoani TABORA QUEEN MLOZI amewavua madaraka Walimu wakuu wa shule za msingi kumi ambao shule zao zimefanya vibaya katika matokea ya Darasa la saba mwaka jana
MKUU wa wilaya ya URAMBO mkoani TABORA QUEEN MLOZI amewavua madaraka Walimu wakuu wa shule za msingi kumi ambao shule zao zimefanya vibaya katika matokea ya Darasa la saba mwaka jana.
Sambamba na Walimu wakuu hao pia amemvua madaraka Mratibu elimu Kata wa ya KILOLENI MORIS MSHENGESHI ambaye shule tatu kati ya kumi zilizofanya vibaya zinatoka katika kata yake.
Uamuzi huo wa mkuu wa wilaya ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa mkoa wa TABORA kwa Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa wa TABORA la kuwataka kuwachukulia hatua za kinidhamu Walimu Wakuu wote watakaobainika shule zao zinzfanya vibaya kutokana na sababu mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya URAMBO ADAMU MALUNKWI amepongeza uamuzi huo wa mkuu wa wilaya na kumtaka kuendelea kuchukua hatua kwa Walimu wote watakaobainika kufanya uzembe mahali pa kazi.

No comments:
Post a Comment