IRINGA yahitaji Bil1.5 kukarabati miundombinu
Halmashauri ya Wilaya ya IRINGA inahitaji zaidi ya shilingi Bilioni MOJA Na MILIONI MIA TANO kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji na barabara ambayo imeharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha
Halmashauri ya Wilaya ya IRINGA inahitaji zaidi ya shilingi Bilioni MOJA Na MILIONI MIA TANO kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji na barabara ambayo imeharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo STEVEN MUHAPA amesema kuwa tayari ombi la fedha hizo limepelekwa serikali kuu ili kunusuru wananchi na huduma za usafiri na umwagiliaji walizokuwa wanazitegemea hapo awali.
Ombi la fedha kwa Halmashauri hiyo limekuja siku chache baada ya mvua kubomoa kivuko cha umwagiliaji cha skimu ya LUGANGA kilichopo kata ya ILOLOMPYA.
Hali hiyo imesababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya RUAHA huko IDODI na kufurika kwa Mto MAPOGORO kufuatia mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kusababisha kaya zaidi ya 80 kuyahama makazi yao.
MUHAPA amesema maafa hayo huenda yakapunguza uzalishaji kwa wananchi na kuwataka madiwani kuwa karibu na wananchi wao katika kipindi hiki cha misukosuko.

No comments:
Post a Comment