25% ya wanawake waja wazito huavya mimba
- 12 Mei 2016
Watafiti wanakiri kuwa viwango hivyo vimeimarika katika nchi nyingi tajiri lakini wanaonya kuwa linaficha ukosefu wa mabadiliko katika maeneo maskini katika miaka 15 iliopita.
Wataalamu wanataka mbinu mpya ziidhinishwe za kuzuia mimba
Hatua mpyaWanasayansi wanasema idadi ya visa vya uavyaji mimba kila mwaka vimeongezeka kutoka milioni 50 kwa mwaka kati ya mwaka 1990-1994 hadi milioni 56 kwa mwaka kati ya 2010-2014.
Ongezeko hilo linashuhudiwa zaidi katika nchi zinazoendelea - chanzo kikuu kikiwa ni ongezeko la idadi ya watu na haja ya kuwa na familia ndogo.
Hesabu inaonyesha kwamba wakati visa vya uavyaji vinasalia kama vilivyo katika mataifa maskini, katika maenoe tajiri visa hivyo vimeshuka kutoka wanawake 25 hadi 14 kati ya wanawake 100 walio katika umri wa kuzaa.
Amerika kusini imetajwa kuwa kati ya wanawake 3 mmoja huavya mimba kiwango kilicho juu kuliko eneo lingine duniani.
Ulaya magharibi kuna ongezeko dogo la visa hivyo - ambavyo watafiti wanaashiria huedna ni kutokana na ongezeko la wanawake wanaohama kutoka Ulaya mashariki na maeneo mengine ya mbali zaidi.
'Unyanyapaa'Inawezekana kwamba baadhi hawatambui kwamba kuna huduma za kuzuia mimba au wanatoka nchi ambazo visa vya uavyaji vipo juu, watafiti wanasema
Dkt Bela Ganatra, kutoka WHO, anasema: "visa vingi yva uavyaji mimba katika utafiti wetu vinadhihirsha zaidi haja ya kuimarisha na kupanua huduma za kuzuia mimba.
"kuwekeza katika mbinu za kisasa kuzuia mimba sio ghali sana kwa wanawake na jamii kama kuwana mimba zisizohitajika na pia hatari za uavyji mimba."
Lakini utafiti huo umeashiria kwamba kupata suluhu sio jambo rahisi kama kuimarisha kufikiwa huduma za kuzuia mimba.
Wanawake wengi wanasema waliamua kututumia njia za kuzuia mimba kwa sababu walikuwa na wasiwasi wa madhara ya mbinu hizo, na pia walikabiliwa na unyanyapaa au waliona kuna hatari ndogo ya kushika mimba.
Katika ripoti nyingine, Dkt Diana Greene Foster, wa chuo kikuu cha California, San Francisco, amesema hakuna jibu litakalokuwa sawa kwa kila mtu.
Ameongeza: "wasiwasi wa afya na kutopendwa madhara ya mbinu za kuzuia uzazi ni kawaida katika nchi tofuati, na linaashiria haja ya kuidhinihsa mbinu mpya za kupanga uzazi na mitazamo inayolenga wanawake zaidi katika utoaji huduma hizo."
No comments:
Post a Comment