Serikali yakanusha kuhusu Mashine za kukoboa mpunga na mahindi Halmashauri ya Kahama kufanya kazi saa 24.
SERIKALI imekanusha madai
kuhusu mashine za kukoboa mpunga na mahindi katika Halmashauri ya Mji wa
Kahama kufanya kazi wakati wa usiku au saa 24.
Kauli hiyo imetolewa leo
Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa
Viti Maalum, Mhe. Salome Makamba ambaye alitaka kujua utayari wa
Serikali kuviruhusu Viwanda Wilayani Kahama kufanya kazi masaa 24 ili
kufidia uzalishaji uliokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokatika wakati
wa mchana.
Akijibu swali Mhe. Jafo amesema
kuwa, Serikali haijatoa zuio lolote kwa Halmashauri hiyo kwa mashine za
kukoboa nafaka kufanya kazi nyakati za usiku ambapo amefafanua kuwa
changamoto iliyopo ni kwamba viwanda hivyo vinatumia umeme wa jenereta
ambao umekuwa hautoshelezi kuendesha mashine wakati wote hali
iliyopelekea kuwepo kwa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
“Halamshauri imewasiliana na
Meneja wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) Kahama na yatari
tatizo hilo limeanza kushughulikiwa ili kupata umeme wa uhakika kutoka
Gridi ya Taifa ambapo tayari kituo cha usamabazaji kimeanza kujengwa
Kahama”, alisema Mhe. Jafo.
Ameongeza kuwa, Halmashauri
wilayani hapo inahamasisha Wawekezaji wa viwanda vidogo vikiwemo vya
kukoboa mpunga, mahindi pamoja na mazao mengine ili kupanua wigo wa
mapato kupitia ushuru wa huduma (Service Levy) na ajira kwa vijana.
“Hakuna sababu yoyote kwa
Serikali kuzuia wawekezaji katika viwanda vidogo na vikubwa, azma ya
serikali ni kupanua uwekezaji wa viwanda kadri iwezekanavyo kwa
kuzingatia fursa zilizopo, tunachofanya ni kuboresha mazingira
yatakayosaidia uwekezaji huo kufanyika kwa faida ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unakuwepo.
No comments:
Post a Comment