Libya kupewa silaha kupambana na IS
- Saa 5 zilizopita
Nchi 25 ikiwemo
Marekani zimekubaliana kuipa silaha serikali ya Libya kwa lengo la
kuiwezesha kukabiliana na wanamgambo wa IS wanaoendelea kuisumbua nchi
hiyo.
Muungano wa kimataifa umesema kuwa utalegeza vikwazo vya
silaha vya Umoja wa Mataifa juu ya Libya kutoa silaha kwa vikosi
vinavyounga mkono serikali mpya ya Tripoli.Waziri mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj, amesema kuwa IS wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwa nchi yake na msaada huo wa kimataifa utakuwa muhimu katika kupambana na ugaidi kwa mafanikio.
Nchi hizo tano ambazo ni wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa walifikia makubaliano hayo baada ya mazungumzo mjini Vienna.Libya imekumbwa na machafuko tokea kuangushwa kwa kanali Gaddafi mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment