TFF yatakiwa kusimamia ligi kwa ustadi
Dar es Salaam
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
salaam Issaya Mwita ameiomba shirikisho la Michezo wa mpira wa miguu
nchini (TFF) kuendelea kusimamia ligi kwa ustadi kulingana na ratibu na
taratibu za mpira wa miguu kama zililivyoanishwa na Shirikisho la Soka
Duniani( FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF).
Kwa mujibu wa taarifa kwa
vyombo vya habari iliyosainiwa Mstahiki Meya huyo inasema kuwa TFF
inatakiwa kusimamia ligi hiyo ili kuainisha, kubainisha, kutajirisha na
hatimae kutatua changamoto husika na kuwa na kiwango stahiki katika
msimu unaofuata ukilinganisha na changamoto zilizojitokeza katika msimu
uliopita.
Aidha, ameipongeza klabu ya
Yanga Africans Football Club kwa kunyakua ubingwa wa Tanzania bara kwa
mara ya ishirini na sita(26) tangu kuanzisha kwa mashindano ya ligi kuu
Tanzania yajulikanayo kama Vodacom Premier League.
Alifafanua kuwa Halmashauri ya
jiji la Dar es salaam inaiomba klabu hiyo kuthamini ubingwa wao kwa
kuonyesha viwango vya kimataifa ili kufanya jiji kuwa chuo cha mafunzo
ya michezo wa mpira miguu, bila kuridhika na kiwango walichonacho.
Mbali na hayo alitoa wito kwa
wadau wa mchezo wa mpira wa miguu kushirikiana ipasavyo ili kufanya
ligi ya Tanzania iwe miongoni mwa ligi bora Barani Afrika na duniani kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment