Hongera –
Kwa Kupata Mimba!
Ujauzito ni mojawapo ya nyakati za ajabu na kufurahisha
sana, kumkamilisha mwanamke katika maisha yake. Unapokuwa
na kiumbe kidogo kunapoanza kutengenezwa ndani ya mwili wako
utaanza kupata mabadiliko mengi kimaumbile na kihisia. Unaweza
kujiandaa vema katika kuikabili hali hii ya kuvutia ukitambua kuwa
kipo kiumbe kinachokua ndani ya tumbo lako na jinsi unavyoweza
kukitunza. Ukijitunza vema kwa kufuata mwongozo wa lishe bora
wakati wa ujauzito, unaweza kumpa mtoto nafasi nzuri ya kuwa na
afya nzuri.
Kijitabu hiki kitakusaidia kufahamu mlolongo wa utatanishi
unaoendelea ndani ya mwili wako na kukuelezea utarajie nini
katika kila hatua wakati wa ujauzito. Utajifunza pia namna ya
kuchagua lishe iliyo bora na iletayo afya kwako na mtoto wako
mchanga kabla na baada ya kuzaliwa. Majedwali ya virutubisho
na vidokezo vyenye kukufaa vimetolewa katika kiambatisho ili
kukusaidia katika wakati huu muhimu sana.
Kijitabu hiki kimekusudiwa kuwa kama mwongozo na silaha
unayoweza kuitumia wakati wote wa ujauzito na ulezi. Lakini
kumbuka kwamba hakijakusudiwa au kuwa ukione cha maana
badala ya daktari. Daktari ni mtu muhimu sana katika matatizo
yako na kukupa ushauri.
Kuanza Kwa Maisha Mapya
Kila mwezi, vichocheo vya mwili wako vinafyatua mlolongo
wa matukio yanayosababisha kuruhusiwa kwa yai kutoka katika
‘ovari’ kiasi cha siku 14 kabla ya mzunguko wa hedhi yako. Yai
linaondoka kwenye ovari na kuanza safari yake mpaka kwenye mji
wa uzazi. Njiani linakutana na mbegu za baba zinazoingia wakati
wa kutana mwilini. Mojawapo ya mbegu inajiunga na yai, na
kuanzisha chembe mpya. Hii inagawa na kujiongezeka kwa upesi
wakati wa safari yake kufika tumbo la uzazi. Linapofika katika
tumbo la uzazi, na baada ya kuelea kwa siku tatu inajifungia na
tabaka ya tumbo la uzazi. Inachukua malisho yake kutoka kwa
mishipa ya damu ya mama inayopita, na inaanza kutengeneza
kondo. Ndani ya miezi mitatu kiinitete (embryo) huwa
kimeshakamilika – ni kazi ya kukua tu inayobaki. Mimba ya
kawaida hukua katika kipindi cha siku 280, au majuma 40 (miezi
tisa ya kalenda) kuanzia siku ya kwanza kilipomalizikia kipindi cha
siku za hedhi. Miezi tisa imegawanyika katika hatua, au vipindi
vitatu vya ukuaji.
Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ukuaji wa mimba kiumbe
kilichoko tumboni huitwa kiinitete (embryo). Katika awamu ya
kwanza ni muhimu kuwa makini na viungo muhimu. Katika hatua
hizi za awali, ingawaji ni kweli kuwa yaweza kuwa hivyo hivyo
katika muda wote wa ujauzito, mtoto aweza kudhurika kutokana na
mazingira na maumbile inayokuathiri wewe pia. Ni vizuri kuepuka
kila inapowezekana, kujilinda na magonjwa ya milipuko, X-rays na
dawa. Kama unahitaji matibabu, mwambie Daktari kwamba una
mimba. Hata hivyo, ni muhimu kutibu homa mapema usiathiri
mtoto.
Katika miezi mitatu ya awamu ya pili, kiinitete kinakua zaidi
na hapa huitwa kwa kitaalamu ‘fetus.’ Kuanzia mwezi wa sita,
mtoto aliyeko tumboni hukua haraka haraka zaidi kuliko nyakati
zilizotangulia, huhitaji chakula zaidi. Baadaye katika kijitabu hiki
utajifunza kwa nini lishe inahitajika kuboreshwa zaidi kwa mama na
mtoto katika kipindi hiki.
Wakati wa ujauzito, mwili wako hutengeneza viungo viwili
vya kushangaza ili kumbeba mtoto na kumlisha akiwa tumboni:
chupa (amniotic sac) na kondo la nyuma. Mtoto huishi na hukua
Mwongozo wa Kukupatia Viini Rishe - Unavyohitaji Mwilini
Mwongozo wa Vyakula Mwilini Faida Zake
Maziwa, siagi, mboga za kijani, spinachi
kabichi, mchicha, mhilile, kisanvu,
matembele, mlenda
Hutupatia
kalsiamu
Ini, nyama, kuku, mayai, mkate,
maharage na aina za mtama
Tunapata madini
ya chuma
Samaki, nyama ya ng’ombe, kuku, nyama
ya nguruwe, siagi, kumbikumbi, ndege,
nyama ya mbuzi, bata, kanga na kondoo
Tunajenga
mwili
Maziwa, samaki, maini, mboga za
majani
Tunapata
Vitamini A
Vyakula vya aina ya cha-chu, ngano,
mtama, ini
Tunapata
Vitamini B (B1hadi B12)
Machungwa, nyanya, ndizi, ubuyu,
Ukwata, ngwelu, ngukwe, mapapai,
malimau, ndimu, madansi, matango
Tunapata
Vitamini C
Jibini, maziwa ya mgando, mafuta ya
samaki, joto la jua
Tunapata
Vitamini D
Vyakula vya punje, mtama, mahindi,
karanga njugu mawe
Tunapata
Vitamini E
Nyama, ini, kuku, bata, maziwa, njugu
mawe mchele, mtama
Tunapata
vitamini ya
niacin
Mboga za majani, mchicha, kisanwu,
matembele, spinachi, kabichi, (mhilile)
majani ya maboga
Kuongeza
damu kusaidia
mifupa
Maumivu ya
Mgongo
Kaa mkao mzuri nyonga zikiwa zimekaa vema.
Unapokuwa umesimama mahali pamoja, kunja
magoti kiasi, badili uzito wako kutoka upande
mmoja kuelekea upande wa pili. Muone
daktari wako akushauri jinsi mnavyoweza
kufanya mazoezi madogo madogo kupunguza
maumivu ya mgongo.
Mkakamao
wa misuli ya
miguu
Nyanyua miguu. Wakati mwingine ongeza
kula vyakula vyenye kalisi na magadi ili
kuongeza nguvu ya mifupa. Kila mara
wasiliana na daktari wako.
Ngozi yenye
mafuta,
mabadiliko
ya ghafla
kwenye
ngozi, ngozi
kukauka.
Kunywa vinywaji vingi vya maji maji kwa ajili
ya ngozi inayo meremeta kwa mafuta; tumia
dawa ya kusababisha tishu laini kujikunyata na
kubana mishipa ya damu inayopendekezwa;
mwone daktari kama maumivu yakizidi. Kwa
ngozi iliyokauka: kunywa majimaji mengi na
utumie dawa iletayo unyevunyevu
iliyopendekezwa. Ili kupunguza mikunjo ya
ngozi, lainisha maeneo yote yaliyoathirika kwa
kupaka ‘cocoa butter’ (siagi ya kokoa) au
mafuta ya vaseline kila siku.
Matamanio
ya chakula
Tosheka kwa kujipatia vitafunwa vilivyorutubishwa.
akiwa ndani ya chupa, akielea huku na huku katika maji maji yenye
chumvi chumvi. Maji maji haya huzuia ukuta wa nyumba ya uzazi
usimbane mtoto, hivyo anakuwa na nafasi ya kukua. Chupa pia
huzuia mitikisiko yoyote -- iwapo utapigwa tumbo, mtoto atakingwa
na maji maji yaliyomzunguka ndani ya chupa.
Kondo la nyuma husaidia mfumo wa uhai wa mtoto. Likiwa
limeunganishwa katika ukuta wa nyumba ya uzazi, kondo hutumika
kupitisha chakula cha mtoto pia kama njia ya kutolea uchafu.
Mbadilishano wa Oksijeni (hewa safi), viini lishe na ulinzi dhidi ya
maambukizi ya magonjwa hufanywa na chembe chembe
zinazolinda mwili ambazo hupitia katika mkusanyiko wa seli za
kondo la nyuma na kitovu. Kondo hili kweli ni la ajabu sana kwa
maana linafanya kazi kama mapafu ya mtoto, figo, utumbo na ini.
Matukio ya Mimba Kila Wiki:
Tunahesabu mimba kuanzia siku ya kwanza ya kuingia
mwezini kwa mara ya mwisho. Kwahiyo, mimba yenyewe inaanza
wiki ya tatu baada ya kuona siku zako.
Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito
Wiki yaTatu
· Yai limeondoka kwenye ovary na kuanza safari yake
mpaka tumbo la uzazi. Njiani linakutana na mbegu za
baba zinazoingiza wakati wa kukutana mwilini.
Mojawapo ya mbegu inajiunga na yai, na kuanzisha
chembe mpya. Hii inagawa na kujiongezeka kwa haraka
wakati wa safari yake kufika tumbo la uzazi.
karibu kesho tutaendeleza sehemu ya pili
No comments:
Post a Comment