Friday, June 17, 2016

Muwasho na kutokwa majimaji ukeni (Vaginal Discharge)



4a370b80f289545bd444292c5c61726aNi tatizo linalowapata zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa ingawa katika hali isiyo ya kawaida inaweza kuwatokea watoto ambao hawajavunja ungo au wanawake watu wazima waliofikia ukomo wa kuzaa.
Tatizo linaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono au likatokea tu kama fangasi.
Uchunguzi wa ugonjwa wa dalili hizi hauhusiani na maambukizi ya njia ya mkojo au yutiai. Ugonjwa umegawanyika katika makundi matano kama ifuatavyo;
Kwanza ni kutokwa na uchafu mwepesi na muwasho ukeni wenye harufu kama shombo ya samaki. Pili ni kutokwa na majimaji na muwasho mkali ukeni hasa sehemu ya nje ya uke na ukijisafisha na maji ya moto unapata nafuu.
Tatu ni kutokwa na usaha ukeni, nne ni kutokwa na majimaji mazito yasiyo na harufu wala muwasho ila yanakera yakiambatana na maumivu chini ya tumbo, tano ni kutokwa na uchafu mzito wenye muwasho.
Takriban magonjwa yote hayo huambukizwa kwa njia ya ngono isipokuwa fangasi ambayo hutokea kutokana na mabadiliko ya mazingira ya uke na hali ya mwili kwa ujumla.
Kwa hiyo hapa tutaanza kuyachambua magonjwa haya yenye dalili za aina moja. Kwa ujumla magonjwa haya ni sugu na hata tiba zake hutofautiana.Unaweza kudhani kwamba tatizo la kutokwa na uchafu ukeni halikuishi kumbe unaweza kutibiwa ugonjwa ambao siyo au kumbe una ugonjwa zaidi ya mmoja.
Kwa hiyo suala muhimu ni kuwaona madaktari kwa uchunguzi wa kina ili kujua una aina gani ya ugonjwa kati ya haya na upate tiba sahihi.
BACTERIAL VAGINOSIS
Ugonjwa huu kwa jina lingine unaitwa ‘Vaginitis’, mwanamke hutokwa na uchafu mweupe ukeni wenye harufu ya shombo la samaki. Kwa kawaida mazingira ya ukeni ni tindikali lakini katika hali hii mazingira hayo huwa Alkali na katika vipimo vya maabara kuna aina ya chembe chembe ziitwazo ‘Clue cells’ huwa zinaonekana.`
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Tatizo hili hutokea sana kwa wanawake wengi wenye hali ya kutokwa na majimaji ukeni. Katika hatua za awali takriban asilimia hamsini ya wanawake wenye tatizo hili hawaoneshi dalili.
Ugonjwa huu ni matokeo ya mabadiliko ukeni, ambapo bakteria wakazi hutoweka ambao ni walinzi hivyo husababisha pia tindikali hapo kutoweka na aina nyingine ya bakteria kuanza kuzaliwa. Bakteria hawa wapo wengi kama vile ‘Gardenella Vaginalis’, ‘Ureaplasma’, ‘Mycoplasma’ na wengineo. Kutokea shombo la samaki husababishwa na uwepo wa kundi la bakteria waitwao ‘Anaerobic’.
Ugonjwa huu wa ‘Bacterial Vaginosis’ husababishwa na mwanamke kushiriki ngono na mwanaume zaidi ya mmoja, kufanya ngono na mwanaume mpya au mpenzi mpya, kusafisha sana uke na kubadilika kwa mazingira ya ukeni.
Kwa hiyo yote, baadhi au mojawapo ya vyanzo hivyo vinaweza kukuathiri, cha msingi ni kufanyiwa uchunguzi hospitali kuthibitisha ugonjwa.
KINGA YA UGONJWA
Kujiepusha na ngono, epuka kusafisha uke sana na kutumia kemikali zitakazokusumbua ukeni. Ukitibiwa hakikisha na mpenzi wako anatibiwa au unafanyiwa uchunguzi wa kina.
Ugonjwa huu unafanana sana na ugonjwa wa Trikomonia ambao tutauona, kusinyaa kwa uke na tatizo linaloambatana na muwasho mkali wa ukeni.
MADHARA
Mama mjamzito mwenye tatizo hilo ana athari za kupata uchungu mapema kabla ya mtoto kukomaa, chupa ya uzazi kupasuka kabla ya mtoto kukomaa na mimba changa kutoka.
USHAURI
Tatizo hili kwa mwanamke au mjamzito au la, hutibiwa hospitali baada ya uchunguzi wa kina wa kuchunguza majimaji ya ukeni. Vipimo na matibabu hufanyika katika hospitali za mikoa kwa madaktari wa akina mama

No comments:

Post a Comment