Friday, June 17, 2016

Mambo yanayoweza kutokea kwa mama katika kipindi cha ujauzito

Katika kipindi cha ujauzito athari hutokea nyingi ila kitu cha msingi mama mjamzito anatakiwa aanze kliniki mara moja pale anapokuwa tu mjauzito. Wakati wa ujauzito mabadiliko mbalimbali hutokea mara tu mimba inapotungwa.


Kipindi cha ujauzito hadi mama anajifungua tunaweza kukigawa katika vipindi vitatu,kwanza kuna miezi mitatu ya mawazo ambayo tunaiita
 “First tri-semister”, miezi mitatu ya pili
 “Second tri-semister” na miezi mitatu ya mwisho “
Third tri-semister”.
“Tri-semister” hizi ni miezi mitatu mitatu.Kuna mambo mengi yanayoweza kutokea katika kipindi hiki. Katika miezi mitatu ya kwanza au “first tri-semister”; wanawake wengi hupatwa na kichefuchefu na kutapika tunaita “Hyperemesi gravidarum”. Tatizo hili linaweza kusababisha mwanamke kutapika sana au kutema mate sana hadi kupungukiwa na maji mwilini. Wengine hushindwa kula kabisa chakula na mwili kudhoofika.Tatizo hili hutibika kabla au mama hupata nafuu endapo atawahi Hospitali kwa uchunguzi wa tiba.
[​IMG]Katika kipindi cha pili au “second tri-semister” mama huweza kuendelea na hali ya kichefuchefu na kutapika.Pia katika kipindi cha kwanza hadi hiki cha pili mama anaweza kupatwa na maumivu na kutokwa na damu ukeni.
Kutokwa na damu ukeni katika miezi mitatu ya mwanzo kunaweza kusababishwa na kukaza kwa mlango wa kizazi hivyo mishipa midogo ya damu “Capillaries” hupasuka na damu kutoka matone matone. Pia mimba inaweza kutoka endapo mimba hiyo itakuwa na matatizo ‘Congenital Abnormalities of the festus’ hivyo endapo kiumbe kitakuwa na kasoro hizo mwili utaitoa ‘Reject’. Katika hatua ya pili mimba pia inaweza kutoka ambapo mlango wa kizazi utalegea na tendo la ndoa litafanyika sana au mama kuwa na matatizo.
Tendo la ndoa halizuiliwi isipokuwa kama mama atakuwa hana hali nzuri kiafya kuanzia kipindi hiki cha pili hadi cha tatu ambacho ni cha mwisho.
Mama anaweza kutokwa na majimaji au damu ukeni ikiashilia mimba kutishia kutoka, hii ni kutokana na mlango wa kizazi kushindwa kubeba mimba ‘Cervical Incompetence’ au maambukizi na magonjwa mbalimbali kama vile malaria au maambukizi ya viungo vya uzazi.
Shinikizo la damu linaweza kuwa juu hasa katika kipindi cha pili hadi cha tatu ambapo hali hiyo inaweza kumsababishia mama akapata kifafa cha mimba ‘Eclampsia’.
Dalili za kifafa cha mimba ambacho mama anaweza kuzigundua mwenyewe ni shinikisho la damu kuwa juu ambapo akitembea kidogo anahisi moyo unaenda mbio na anaishiwa na pumzi, miguu inavimba, uke kuvimba au uso kuvimba baada ya kuamka asubuhi.
Kuanzia kipindi cha kwanza hadi cha tatu kuelekea kujifungua, mama anaweza kupatwa na tatizo la kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na muwasho, shinikizo la damu kushuka na maradhi ya mara kwa mara hasa katika njia ya mkojo na malaria.
Upungufu wa damu wakati wa ujauzito ‘Anemia in pregnancy’ ni tatizo kubwa ambalo husababishwa na ulaji usio mzuri hasa kutokula vyakula vyenye madini kama vile nyama, maini,dagaa na mboga za majani hasa matembele na mchicha.
Maambukizi kama tulivyoyaona na minyoo huchangia upungufu wa damu ambao athari zake ni pamoja na mtoto kufia tumboni, magonjwa ya moyo kwa mama na hata mama mwenyewe kupoteza maisha.
Imeandaliwa na Dkt. Chale

No comments:

Post a Comment