Sunday, February 1, 2015

DIAMOND, J DEE, CHALI, MASANJA MKANDAMIZAJI JUU.

UTAJIRI wa komedi maarufu hapa nchini Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji au mchungaji kufuru! na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki mkwanja wa nguvu hapa bongo, Rorya maendeleo linakupa zaidi.
Emmanuel Mgaya mbele ya mali zake.
HABARI KAMILI
Habari hii ilitua mezani kwaenye blog hii kama kidokezo na ndipo mwandishi mmoja kulivalia njuga ili kuopata habari kwa kina juu ya mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni tishio kwa mastaa mbalmbali wa hapa bongo.
Masanja sio yule tena, an mpunga(fedha) mrefu sana hakuna msanii wa maigizo anayeweza kumfikia kwa sasa. Wengine hao ni mbwembwe tu ila pesa kwa Masanja imelala.
 MALI ZAKE
Kwanza ghorofa ambalo lipo Tabata na hapo ndiyo maskani pake anamoishi.Magari kibao ya kifahari pamoja na mashamba na kampuni ya ulinzi OK security.
Chanzo chetu kilibaini ukweli wa mali za msanii huyu na mambo mengine mengi yanayomwingizia kipato kama vyanzo vya mapato,
1. nyumba tatu bongo
2. magari sita
3. mashamba mawili Kigamboni na Mbeya.